ADDITION
IN LOVING MEMORY OF MR. PAMA
Mzee Pama alikuwa na sumbuliwa na ugonjwa uliomtesa kwa zaidi ya miaka 12, mpaka kifo chake kinatokea ilikuwa ni tayari muda umefika. Hata kusurvive kwa kipindi chote hicho ni sababu ya Pesa tu, la sivyo angekuwa alikufa muda sana.
Mzee Pama aliandika waraka toka May na aliandika barua ya Mirathi June week moja kabla ya kifo chake, ni kama alikiona kifo chake mapema.
Mzee Pama alikufa akiwa na watoto watano (5) ambao wote ni mabinti na aliacha mjamzito ambaye ni Jane ambaye alikuwa anatarajia kupata mtoto wa kiume. Hata waraka ulivyosomwa kuwa Jane atapata mtoto wa kiume watu walionekana kufurahishwa sana na zile taarifa.
Mzee pia aliacha Jina la kuitwa mtoto wake wa kiume akizaliwa na baada ya Jane kujifungua alipewa hilo jina X.
Mzee Pama alikuwa ni mstaafu wa Kampuni moja kubwa tu ya kimataifa inadeal na uchimbaji wa madini hapa nchini. Licha ya kustaafu bado walikuwa wanamtumia kwenye Project zao kwenye nchi nyingi hapa Africa. Pia mzee Pama alikuwa ana kampuni zake za kununua na kuuza madini na alikuwa na vitalu pia so alikuwa ana Pesa balaa.
Siku ambayo alikuwa anaagwa pale kwake Ununio mimi na Mary si tulikwenda kujiandikisha kwenye daftari la mahudhurio?. Kimbembe ni kwamba ulikuwa unaandika Majina yako, unakotokea, namba ya simu, Mahusiano yako na Marehemu, kiasi chako cha mchango wako na mwisho kabisa ulikuwa una sign.
Mary ndo alikuwa wa kwanza kuanza kuandika na mimi sikuwa siriazi muda ule sasa baada ya kumaliza nilifata mimi. Nilivyofika kwenye mchango nikasema ngoja niangalie wengine wameandikaje kwakweli nilidata maana watu walikuwa wanatoa michango mikubwa balaa.
Niliona watu wameandika michango mikubwa sana hizi milioni 5, 10 zilikuwa kibao kwenye ile page, wa laki walikuwa wakuhesabika. Kabla ya Mary Pesa ndogo ilikuwa ni laki 5 sasa baada ya kuona Mary kaandika laki 2 ilibidi nicheke kimoyomoyo. Mimi ukweli nilichangia laki 5 maana pesa yenyewe nilitoa kwa zile ambazo alikuwa kanitumia Mzee Pama.
Niliwaza muda ule kutoa pesa yote iliyokuwa imebaki milion 4 kwa account maana milion 2 nilikuwa nishaiutoa tayari kule Mbweni. Lakini nikakumbuka Mzee alisema ananipa Pesa kwaajili ya Shukran na kunipa assist nilikokwama niliamua kuchangia laki 5. Na niliwaza pesa itakayobaki nitafanya jambo kwaajili ya ukumbusho wake.
Malipo yalikuwa yanafanyika kwa bank au Lipa namba na zilikuwa palepale kwa daftari. Nilishangaa sana kuona watu wakichanga pesa nyingi vile hapo watu Karibu 500 kasoro walikuwa washajiandikisha tayari.
Mary alishangaa sana alinambia “Insider hata nilikuwa sijui niweke kiasi gani maana niliona watu wanatoa michango mikubwa balaa ikabidi nijivute na mimi sio mbaya”.
Nilicheka sana kwakweli, hapa ndo nikawaza ukiwa maskini utazikwa na maskini ukiwa Tajir utazikwa na matajiri.
Kitu kingine msiba ulisimamiwa na Kikundi cha Mzee Pama ambacho huwa wanasaidiana kwenye shida na Raha. Walisimamia kila kitu mpaka mazishi na bado walitoa rambirambi kwa wafiwa. Yaani ile michango ilikuwa sio kitu tuseme haikutumika kabisa.
Mzee Pama nilifanya naye kazi nyingi na alinisaidia sana kiuchumi kielimu nk. Bado tumetoka sana out kama Samaki Samaki tumekwenda sana. Ni mambo mengi sana ambayo sikuyandika humu, alikuwa ni rafiki, Mzazi na mshauri kwangu.
Mzee Pama alinifundisha sana maisha na jinsi ya kuishi na watu, pia mzee aliniamini na alinipenda sana kama kijana wake. Kitu ambacho kilimkosesha raha Mzee Pama ni kukosa mtoto wa kiume tu.
R.I.P mzee Pama kila June nitaendelelea kukumbuka na kukuenzi kwa yote. Uliniachia task ya kuwa karibu na Jane na sasa ana mtoto wako wa Kiume wa miezi 9 na ana afya tele.
Ni vitu vingi sana vilitokea kwenye huu msiba ikiwemo watoto zake wote kusomeshwa mpaka chuo, siwezi kumbuka vyote.
Kingine June hii tulikwenda Tabora na Jane kulitembelea kaburi lake na kuweka maua. Niliteseka sana baada ya kifo chake nilikuwa na stress sana na nilikuwa nikimwota sana usiku Mzee na ndotoni nilikuwa naona akicheza na mwanae.
Baada ya kifo cha Mzee Pama niliamua
kuachana na Biashara ya Uber/Bolt kama heshima yangu kwake.
Hii ni moja ya kumbukumbu kubwa na mbaya sana ambayo biashara ya Uber iliniachia kwenye historia ya maisha yangu. Kumbukumbu ingine tutaikuta huko mbele kidogo.
R.I.P MZEE PAMA MUNGU AENDELEE KUKULAZA MAHALI PEMA PEPONI.
Romans 14:8
"If we live, we live for the Lord, and if we die, we die for the Lord. So, whether we live or die, we belong to the Lord."
Warumi 14:8
"Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana"
AMEN [emoji120]