Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

ADDITION

IN LOVING MEMORY OF MR. PAMA

Mzee Pama alikuwa na sumbuliwa na ugonjwa uliomtesa kwa zaidi ya miaka 12, mpaka kifo chake kinatokea ilikuwa ni tayari muda umefika. Hata kusurvive kwa kipindi chote hicho ni sababu ya Pesa tu, la sivyo angekuwa alikufa muda sana.

Mzee Pama aliandika waraka toka May na aliandika barua ya Mirathi June week moja kabla ya kifo chake, ni kama alikiona kifo chake mapema.

Mzee Pama alikufa akiwa na watoto watano (5) ambao wote ni mabinti na aliacha mjamzito ambaye ni Jane ambaye alikuwa anatarajia kupata mtoto wa kiume. Hata waraka ulivyosomwa kuwa Jane atapata mtoto wa kiume watu walionekana kufurahishwa sana na zile taarifa.

Mzee pia aliacha Jina la kuitwa mtoto wake wa kiume akizaliwa na baada ya Jane kujifungua alipewa hilo jina X.

Mzee Pama alikuwa ni mstaafu wa Kampuni moja kubwa tu ya kimataifa inadeal na uchimbaji wa madini hapa nchini. Licha ya kustaafu bado walikuwa wanamtumia kwenye Project zao kwenye nchi nyingi hapa Africa. Pia mzee Pama alikuwa ana kampuni zake za kununua na kuuza madini na alikuwa na vitalu pia so alikuwa ana Pesa balaa.

Siku ambayo alikuwa anaagwa pale kwake Ununio mimi na Mary si tulikwenda kujiandikisha kwenye daftari la mahudhurio?. Kimbembe ni kwamba ulikuwa unaandika Majina yako, unakotokea, namba ya simu, Mahusiano yako na Marehemu, kiasi chako cha mchango wako na mwisho kabisa ulikuwa una sign.

Mary ndo alikuwa wa kwanza kuanza kuandika na mimi sikuwa siriazi muda ule sasa baada ya kumaliza nilifata mimi. Nilivyofika kwenye mchango nikasema ngoja niangalie wengine wameandikaje kwakweli nilidata maana watu walikuwa wanatoa michango mikubwa balaa.

Niliona watu wameandika michango mikubwa sana hizi milioni 5, 10 zilikuwa kibao kwenye ile page, wa laki walikuwa wakuhesabika. Kabla ya Mary Pesa ndogo ilikuwa ni laki 5 sasa baada ya kuona Mary kaandika laki 2 ilibidi nicheke kimoyomoyo. Mimi ukweli nilichangia laki 5 maana pesa yenyewe nilitoa kwa zile ambazo alikuwa kanitumia Mzee Pama.

Niliwaza muda ule kutoa pesa yote iliyokuwa imebaki milion 4 kwa account maana milion 2 nilikuwa nishaiutoa tayari kule Mbweni. Lakini nikakumbuka Mzee alisema ananipa Pesa kwaajili ya Shukran na kunipa assist nilikokwama niliamua kuchangia laki 5. Na niliwaza pesa itakayobaki nitafanya jambo kwaajili ya ukumbusho wake.

Malipo yalikuwa yanafanyika kwa bank au Lipa namba na zilikuwa palepale kwa daftari. Nilishangaa sana kuona watu wakichanga pesa nyingi vile hapo watu Karibu 500 kasoro walikuwa washajiandikisha tayari.

Mary alishangaa sana alinambia “Insider hata nilikuwa sijui niweke kiasi gani maana niliona watu wanatoa michango mikubwa balaa ikabidi nijivute na mimi sio mbaya”.

Nilicheka sana kwakweli, hapa ndo nikawaza ukiwa maskini utazikwa na maskini ukiwa Tajir utazikwa na matajiri.

Kitu kingine msiba ulisimamiwa na Kikundi cha Mzee Pama ambacho huwa wanasaidiana kwenye shida na Raha. Walisimamia kila kitu mpaka mazishi na bado walitoa rambirambi kwa wafiwa. Yaani ile michango ilikuwa sio kitu tuseme haikutumika kabisa.

Mzee Pama nilifanya naye kazi nyingi na alinisaidia sana kiuchumi kielimu nk. Bado tumetoka sana out kama Samaki Samaki tumekwenda sana. Ni mambo mengi sana ambayo sikuyandika humu, alikuwa ni rafiki, Mzazi na mshauri kwangu.

Mzee Pama alinifundisha sana maisha na jinsi ya kuishi na watu, pia mzee aliniamini na alinipenda sana kama kijana wake. Kitu ambacho kilimkosesha raha Mzee Pama ni kukosa mtoto wa kiume tu.

R.I.P mzee Pama kila June nitaendelelea kukumbuka na kukuenzi kwa yote. Uliniachia task ya kuwa karibu na Jane na sasa ana mtoto wako wa Kiume wa miezi 9 na ana afya tele.

Ni vitu vingi sana vilitokea kwenye huu msiba ikiwemo watoto zake wote kusomeshwa mpaka chuo, siwezi kumbuka vyote.

Kingine June hii tulikwenda Tabora na Jane kulitembelea kaburi lake na kuweka maua. Niliteseka sana baada ya kifo chake nilikuwa na stress sana na nilikuwa nikimwota sana usiku Mzee na ndotoni nilikuwa naona akicheza na mwanae.

Baada ya kifo cha Mzee Pama niliamua
kuachana na Biashara ya Uber/Bolt kama heshima yangu kwake.

Hii ni moja ya kumbukumbu kubwa na mbaya sana ambayo biashara ya Uber iliniachia kwenye historia ya maisha yangu. Kumbukumbu ingine tutaikuta huko mbele kidogo.

R.I.P MZEE PAMA MUNGU AENDELEE KUKULAZA MAHALI PEMA PEPONI.

Romans 14:8
"If we live, we live for the Lord, and if we die, we die for the Lord. So, whether we live or die, we belong to the Lord."

Warumi 14:8
"Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana"

AMEN [emoji120]
Aminaaa....!
 
Mkuu vumilia soon nitafungua CODE zote ili ufanikiwe kwenye hii Biashara na jinsi ya kukutana na hawa watu.

Nimefunga PM sababu kuna watu nilikuwa nawapa namba zangu, ila wajinga wachache wameanza kuexpose privacy zangu humu ndani. Kuna watu wanakuja PM kwa mambo yao na sio msaada.

Kuna wale ambao ni serious nitatoa email kwaajili ya nawasiliano na sio namba tena.
Insider, nahitaji email yako plz, njoo PM unipe, kuna mambo nahitaji tuwasiliane ya kunijenga zaidi
 
Mkuu vumilia soon nitafungua CODE zote ili ufanikiwe kwenye hii Biashara na jinsi ya kukutana na hawa watu.

Nimefunga PM sababu kuna watu nilikuwa nawapa namba zangu, ila wajinga wachache wameanza kuexpose privacy zangu humu ndani. Kuna watu wanakuja PM kwa mambo yao na sio msaada.

Kuna wale ambao ni serious nitatoa email kwaajili ya nawasiliano na sio namba tena.

Kuna swali nimetaka kukuuliza tangu Iryn aliporudi tena..

Je, wahusika wakisoma hawatakitambua?

Mke wako haswa na Iryn hawatakujua ni wewe?

Hao wengine hata sijali zaidi ya hao wawili.

Na je, ulimuomba Iryn ruhusa ya kurusha haya yote maana lazima Kuna watu watamtambua tu wakisoma haswa yake ya biashara yake.

Natumaini majina ya wenzao haswa wa karibu ni ya uongo na yeye. Nakumbuka ulisema Prisca na Mary ndio umeyabadili.. wadogo zao je?

Story nzuri, tunasubiri muendelezo... Kujua pia kama Prisca kajifungua mtoto wa kike au?

R.I.P. Mzee Pama nae wamjuao watamtambua. Bora kwako hayupo tena.
 
Acha kucomplicate mambo mkuu. Kila kitu unachosoma kwenye huu uzi kipo kwa Code sio rahisi mhusika kujua niko makini sana.

Kingine Hao wote hata JF hawaijui kabisa.
 
Mkuu vumilia soon nitafungua CODE zote ili ufanikiwe kwenye hii Biashara na jinsi ya kukutana na hawa watu.

Nimefunga PM sababu kuna watu nilikuwa nawapa namba zangu, ila wajinga wachache wameanza kuexpose privacy zangu humu ndani. Kuna watu wanakuja PM kwa mambo yao na sio msaada.

Kuna wale ambao ni serious nitatoa email kwaajili ya nawasiliano na sio namba tena.
Pole sana. Ubinadamu kazi
 
hivi mtu ukimuexpose mwenzio humu bila ridhaa yake unapata faida gani?

yani kuna baadhi ya watanzania wana roho za kichawi, yaani mtu roho inakuambia tu ngoja nimchunguze huyu mtu nimueke hadharani

hata chuki huanza hvi hivi kwa wema then wakifanya wao malipizi wanaonekana wabaya. hivi insider akasema haendelei na story si mtamuona mbaya.
[emoji867]
Dunia hii unavyoiona sivyo ilivyo. Kuna watu ukiwaona unaweza kudhani umepata watu,lakini watu ni wachawi,sio kabisa kushare nao kwa uwazi
 
Mkuu vumilia soon nitafungua CODE zote ili ufanikiwe kwenye hii Biashara na jinsi ya kukutana na hawa watu.

Nimefunga PM sababu kuna watu nilikuwa nawapa namba zangu, ila wajinga wachache wameanza kuexpose privacy zangu humu ndani. Kuna watu wanakuja PM kwa mambo yao na sio msaada.

Kuna wale ambao ni serious nitatoa email kwaajili ya nawasiliano na sio namba tena.
Wabongo ni wajinga sana yaani huu ujinga waliniletea hadi mm . Yaani unafanya kitu kwa ajiri yao alafu wao ndio wanakua wa kwanza kuzingua
 
Back
Top Bottom