Inaendelea......
Simu yangu ilianza kuita, kucheki alikuwa camilla binti wa mzee juma.
"mambo insider vipi utakuwa na nafasi leo jioni tukapate dinner? Alafu kuna mzigo wako kutoka kwa dady"
Niliwaambia camilla anapenda sana kudeka na uzungu mwingi, ile sauti yake tu nikashindwa hata kumkatalia.....
Baada ya kumaliza dinner camilla alinikabidhi bahasha na kuniambia "huo mzigo wako insider, dady amesema utakusaidia na kukusogeza mpaka wiki ijayo atakaporudi......nilimrudisha camilla kwao na kabla sijaondoka nikafungua ile bahasha ya A4 ndani nikakuta burungutu la elfu kumi kumi zimefungwa kwa haraka haraka nikahesabu ni kama million saba hivi mzee juma alinipa ya matumizi, nikasema hii nitaanza kumlipa mama wa2 mkopo wake.....