Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

kwanza hongera kwa kupata mtoto, lakini fanya hivi
1. Usifanye siri hili jambo kwani ipo siku litajulikana tu.. mpeleke Iryn na mtoto nyumbani kwenu kumtambulisha wamjue damu yako.

2. Mwambie ukweli mama J kuwa una mtoto umezaa na Iryn na usimfiche chochote. mwache yeye aamue kuolewa au aache kuolewa na wewe..usimuoe bila yeye kufahamu hili jambo na aridhie mwenyewe kuwa kuna mke mwingine.

3. Mwambie mama J kuwa utafunga ndoa ya serikali na pale kuna option ya wewe kuwa na wake wawili au zaidi ili umlinde Iryn na watoto utakaozaa naye, watoto wote wana haki kwa baba yao.. Mama J anatakiwa ajue kabisa kuwa anaolewa na wewe lakini kuna mke mwingine ambaye naye utafunga naye ndoa..

4. Usithubutu kumuoa mama J bila ya kumpa taarifa ya mke mwenzake ambaye ni Iryn..yani ajue kuwa anaolewa kama mke wa kwanza na pia kuna mke wa pili. usisahau kuwa huyo mama J ni mchaga na mtusamehe tu wanawake wa kichaga wengi huwa wanabaki wajane jiulize kwa nini.. na hasa akigundua mume wake ana wanawake wengine na watoto huko nje mawazo yao yote huwa ni kwenye mali na kuwamaliza waume zao.. tusije tukaanza kuimba parapanda bado tunakupenda Insider..

5. Mama J akikataa kuolewa na wewe kwa sababu ya kufahamishwa kuhusu Iryn basi pambana na hali yako na umuoe huyo Iryn na ikibidi uchukue mwanao ulee wote pamoja..nakuusia usifanye siri kwa mama J kwani madhara yake ni makubwa huko mbele labda kama huwajui wachaga..
@INSIDER MAN wachaga ni wa kuwa nao makini sana, lakn pia nakuomba umtambukishe Irene kwa yule dada yako Mkubwa maana nahisi ndio atakuwa ni msiri wako, mwambie kila kitu usimfiche, usiache kumshirikisha plz. Wanaume wengi marafiki zao wanakuwaga dada zao na mama zao so anza na yule sister wako ambae mama yako alizaa na Muhindi
 
Ningekua mimi ndo mama J. Bora usiniambie mpaka mtoto atakavyokua mkubwa maybe miaka 10 huko tukiwa tushakuwa watu wazima zaidi tunafikiria majukumu zaidi.

My dad alimficha mama kwamba ana mtoto. Mama akaja kujua mtoto akiwa 20yrs, akamwambia tu baba amlete mtoto amuone.

Ila sasa hivi mapenzi bado ni moto moto, mimi nashauri usimwambie mama J. Kuhusu kuwaambia wazazi hapo labda wenzangu wakusahauri. Ila mzazi wako anaweza kukwambia mwambie mkeo na tunarudi pale pale.
Kwa baba yako ilikuwa hivyo nadhani kwa sababu mama yako hakuwa anaufahamu mchepuko wa baba. Kwa mama J ni tofauti anamfahamu Lyn na alishahisi kitambo kwamba hawa watu wana mahusiano but insider akakanusha.. mimi naungana na wale wanaosema before afunge ndoa na mama J ni vizuri swala la Lyn likawekwa wazi ili mama J achangue kuolewa au aendelee na maisha yake mengine
 
Hii story kwa hisia zangu ilikuwa na uwezo wa kuendelea zaidi ya hapa ,kwani Kuna mambo mengi muuhusika hajayaweka ,
Mf:mambo maendeleo ya mchepuko wa mzee Pama ,Maisha ya Ilyn huko SA na alivyoenda wakati wa kujifungua ,misukosuko aliyotuambia/pingamizi la ndugu ,Maendeleo ya kazi anazosimamia na mapokeo ya wafanyakazi kwa Iryn kuwa mama Mtoto rasmi na mengine mengi .

Tatizo lilianza kwa watu flani kuforce story iishe na wengine wakasema ingetakiwa imalizike episode ya 30 na watu kukosa uvumilivu wa kusubiri ,kila saa kejeli matusi na maneno mengi na lawama kwa msimuliaji
Mwisho akaona mambo yasiwe mengi ngoja aturidhishe .
Ndio maana akajitahidi kadri awezavyo akaandika ndefu na kubananisha mambo ndio maana anasema na amesha tekeleza atatupa Kama nyongeza ya namna mambo yalivyo endelea hivyo hii nyongeza ingewea kuwa Episode
Lingine angalia hii stori ni ya mwaka Jana mpaka mwezi wa tisa Kama sikosei Kuna zaidi ya Mwaka hapa hajatuwekea maisha yalisongeje .

Tutambue kuwa kwa Sasa majukumu ya Insardeman ni Mengi zaidi na siyo mtu wa kubweteka hivyo ndio maana story ilikuwa inachelewa na pia ndio sbb ya kufupisha ili amalizana nasi ,tofauti na hapo tungekuwa na subiri bado tungekuwa tunapata utamu[emoji2][emoji2][emoji2]
Yote kwa yote Asante mweshimiwa Insairdearman kwa story nzuri na kutokata taamaa kwani makwazo yalikuwa mengi ukitegemea kwa Sasa mambo ni [emoji91] na ulikuwa huna cha kupoteza Asante pia wasomaji na hasa waliokuwa na utulivu,na zidi Sana msimuliaji wetu, Asante Sana Sana ndugu
Niwatakie kila lililo jema wewe na Familia yako /zako pia katika miangaiko yako.
Pia kuna section moja alisema alikutana na mdada mmoja mzuri sana bahati mbaya hakuchukua namba. Yule dada akaj kurudi pale akamuuluzua Insiderma kwa muhudumu na muhudumu akaja akamwambia Insiderman ambaye aliamua kumuachia namba muhudumu ili aje ampatie huyo dada ( Sikumbuki kama ni kidimbwi, Samaki Samaki au wapi).

Hapa napo kwa namna walivyoivana na huyo dada siku ya kwanza tu kukutana nahisi kuna story nzuri napi! Basi tu INSIDER MAN
 
kabisaa cha muhimu maokoto ni kuwa one step ahead maana moyo wa mtu kichaka
Ila kama wanawake wa kichaga wanavyopenda maokoto na baadhi kuwatestisha in pisi waume zao kwa ajili hiyo. Sijui kama atashindwa ku compromise kwa hili huyo mama J
 
Maguire alifanya kosa kubwa moja la kimkakati. Kosa lenyewe ni kujidai sitaki-nataka kumla Iryn mapema mpaka Iryn akajenga urafiki na mama J. Kama Iryn angetafunwa mapema kipindi kile anamuita mwanetu chumbani kupanga nguo, basi sidhani kama Iryn angetaka kuweka ukaribu na mama J. Hii ingeweka mipaka mizuri na kuondoa dhana ya usaliti wa Iryn kwa mama J.

Maguire anataka kufanya kosa lingine kubwa sana la kimkakati. Kosa lenyewe ni kwenda kumtambulisha Iryn kwao, wakati akiendelea kumficha mama J. Hapa ndugu yetu anahamisha dhambi kutoka kwake mwenyewe, mpaka kua dhambi ya familia. Mama J akijua umezaa na Iryn itakua msala. Ila mama J akijua umezaa na Iryn, na familia yako ilikua inafahamu hili suala ila yeye akafichwa, inakua ni msala alafu msala tena. Beba mzigo wako mwenyewe chief, haina haja ya kuibebesha familia nzima!

Kwakua umepanga kufunga ndoa na mama J, kuna options mbili za maana unazoweza kuchagua: mfiche mama J mpaka watoto wa Iryn watakapokua wakubwa, au umwambie mama J kabla ya ndoa kwamba Iryn ni mke mwenzie then umshawishi akubali kua mke mkubwa. Option ya pili italeta msala, lakini sio msala mkubwa kama ambavyo mama J atakuja kugundua miaka miwili baada ya kufunga ndoa. Kuna maumivu ya talaka, mgawanyo wa mali na visasi mpaka kwa mtoto ambayo utayapitia mpaka ushangae!

Mwisho kabisa, jiandae kisaikolojia kuachana na mama J, ili ikitokea ikawa hivyo basi usiumie sana. Wasomaji wako tunajua umekufa na kuoza kwa Iryn zaidi ya unavyompenda mama J. Japo unatuzuga ila maandishi yako yanakukataa;

  • unapoteza hisia za kumkaza mama J, ila Iryn show kila siku.
  • Kwa Iryn hadi jikoni ulikua unaingia kupika, ila kwa mama J hata kurudi nyumbani ni utata.

Ilikua story nzuri sana, ila mwisho nimekuhurumia kwa huo mtihani unaokukabili. Inawezekana wewe unauchukulia poa, ila sio mdogo. Kua makini sana na mama J. Hakuna kiumbe hatari kama mwanamke alieumizwa moyo na akaamua kulipa kisasi!
 
Ukweli kwa mama J kabla ya ndoa utanuweka huru ili mama J aamue kusuka au kunyoa. Kwa vyovyote vile mama J atajua, ni Bora amuwahi kabla
 
Ila kama wanawake wa kichaga wanavyopenda maokoto na baadhi kuwatestisha in pisi waume zao kwa ajili hiyo. Sijui kama atashindwa ku compromise kwa hili huyo mama J
inategemea ni mtu wa type gani kama ni mtu yule anae mfatilia mwanaume kila hatua na wivu juuu hapo lazima pachimbike na anaweza kuachia ngazi labda INSIDER MAN na iryn wafanye kummpooza na tako la nyani au duallis kisha apewe taarifa kwamba ndoa yake itakuwa ya mitara 😂
 
Amchane mama J kabla hawajaanza process za kubariki ndoa au akaushe mpaka watakapofunga ndoa aje agundue tu mwenyewe
Msichoelewa hiyo process ilishaisha,
Mama J aligundua kwamba baba mtoto wake ana michepuko si mchepuko tu.
Na jamaa alikua anasema ni wateja tu.
Mama watoto kajiongeza leo yuko Kwao kesho kaenda Moshi safari zikawa nyingi tu
Na huku huyu ndugu yetu (jf si ni ndugu)
Akikamata pisikali,mama inakua mwalo mwalo.
Usiweke miguu kushoto mmoja ,kulia mmoja ramani itasomaje?
Uko na Iryn deal nae
Uko na mama J deal nae.
 
Sasa ninaweza kuchangia baada ya kumaliza kusoma kipande cha ziada...

Kwenye ibara zetu za katiba huwa tunasimama na wahenga ya kwamba "kitanda hakizai haramu"...

Lakini kwenye situation ya bazazi mwenzetu INSIDER MAN aliboronga mahali pamoja hapo nyuma kwa kuwafanya Mama J na Iryn kuwa marafiki kwa kiwango cha kuwafanya wajione ni mtu na dadaye, hata uwe bazazi sugu kiasi gani usiruhusu mchepuko ukawa rafiki na 'maza hausi'...

Ushauri:
1. Suala la mahusiano yake na Iryn liendelee kuwa siri kwa sasa, la sivyo hiyo ndoa anayotarajia na Mama J haitakuja kutokea, kama ni kumpa taarifa iwe ni miaka ijayo huko...

2. Nimeona kuna mahali jamaa kaandika ana mpango wa kumpeleka mtoto na Iryn nyumbani kwa wazazi, hii naona haitakuwa busara kwamba wazazi wajue lakini mwanamke aliyesalitiwa hajui chochote, itakuwa kama 'zereu' fulani hivi...

3. Aendelee kumjali Mama J na kumuhudumia kama mke kwa kiwango kisichomithilika, hii itafanya siku atayovunja habari kwa Mama J huenda moyo wa mwanamke huyu wa kichaga utakubali matokeo...
Asante sana Speaker wa mabazazi 😀😀😀😀 mabazazi wote mpite na kusoma hapa jamani mkiongozwa na insider....

Bro asante japo daahhh najaribu kuvaa viatu vya mama J vinanibana maumivu ya usaliti ni makali hasa kwa mtu unaemjua kwamba kumbe all those days alikua anaanila kisogo (nimewaza kama mama J) any way ni fikra zetu tu wana nzengo huwenda mambo yakawa rahisi tu kwa mama J...

Thanks in advance bro Watu8
 
Sasa ninaweza kuchangia baada ya kumaliza kusoma kipande cha ziada...

Kwenye ibara zetu za katiba huwa tunasimama na wahenga ya kwamba "kitanda hakizai haramu"...

Lakini kwenye situation ya bazazi mwenzetu INSIDER MAN aliboronga mahali pamoja hapo nyuma kwa kuwafanya Mama J na Iryn kuwa marafiki kwa kiwango cha kuwafanya wajione ni mtu na dadaye, hata uwe bazazi sugu kiasi gani usiruhusu mchepuko ukawa rafiki na 'maza hausi'...

Ushauri:
1. Suala la mahusiano yake na Iryn liendelee kuwa siri kwa sasa, la sivyo hiyo ndoa anayotarajia na Mama J haitakuja kutokea, kama ni kumpa taarifa iwe ni miaka ijayo huko...

2. Nimeona kuna mahali jamaa kaandika ana mpango wa kumpeleka mtoto na Iryn nyumbani kwa wazazi, hii naona haitakuwa busara kwamba wazazi wajue lakini mwanamke aliyesalitiwa hajui chochote, itakuwa kama 'zereu' fulani hivi...

3. Aendelee kumjali Mama J na kumuhudumia kama mke kwa kiwango kisichomithilika, hii itafanya siku atayovunja habari kwa Mama J huenda moyo wa mwanamke huyu wa kichaga utakubali matokeo...

Nakuongezea miaka mitano Tena ya uenyekiti, ombi lako la kuomba upumzike tumelikataa.

Mtu akishakua Rafiki na wife ndio tayari ticketi ya kumkwepa kwenye tasnia yetu. Hapo ukishupaza shingo inakugharimu.
 
EXTRA EPISODE 07

BY INSIDER MAN

Biashara ya Uber ni moja ya biashara nzuri sana maana inakukutanisha na watu wengi sana wenye hadhi “status” tofauti, foreigners, matajiri na maskini nknk.

Hii biashara niliiacha baada ya kifo cha Mzee Pama kwasababu ya kumuenzi kifo chake, Pama nilikutana naye kupitia hiihii Uber. Kwasasa hii biashara naifanya kwa kuajiri vijana na ninazo Uber mbili na dereva zangu wanafanya vizuri sana hakuna ujinga wanaofanya na wale wateja zangu wote nimewaunganisha nao.

Hii biashara imenikutanisha na watu wengi sana niwe mkweli, wengi sijawaandika kabisa kwenye hii story na wengi wao bado tuna wasiliana sana maana walikuwa wateja zangu na wana niamini. Nimekutana na watu wengi sana kupitia Uber kama watu maarufu, celebrities, wanasiasa nk, kipindi nafanya hii biashara na ndo iliyonipa connections na kutoboa maisha.

Just imagine bila Uber nisingekutana na Iryn, Mzee pama, Jane, Mzee Juma, Mama wa2, Mama Janeth, Sumaiya, Lucy, Prisca na Mary nknk. Kupitia Iryn ndo niliwajua hao wengine wote, kupitia Pama nilimjua mzee Juma na Jane. Hapo unaona connection moja inafungua au inaongeza connection zingine.

Dunia hii jinsi inavyokwenda tajiri rafiki zake ni matajiri, maskini rafiki zake ni maskini, dereva rafiki zake ni madereva, mfanyabiashara rafiki zake ni wafanyabiashara, vivyohivyo kwa mkulima, mwalimu, mwanafunzi, mlevi nknk.
Sasa kama wewe maskini ufanye nini ili uweze kukutana na matajiri? kwa mtizamo wa haraka utaona ni ngumu but ni very simple, the question is how?.

Ukifuatilia kwa makini utagundua matajiri wanaingia sehemu expensive na zenye thamani kama hadhi yao, ni ngumu sana kumkuta tajiri anakula kwa mama ntilie ni kitu ambacho hakiwezekani. Matajiri wengi utawakuta wakienda kupata lunch/dinner kwenye mahotel makubwa kama Serena, Hyatt, au kwenye migahawa mikubwa na ya kisasa.

Siku mojamoja jenga utaratibu wa kutembelea haya maeneo hata sio ghali kuingia kupata dinner au lunch ni vile uoga wetu. Nenda viwanja vikubwa kama Samakisamaki nknk huko utakutana na watu wenye hadhi tofauti, mtu anayeingia Samakisamaki actually hata kipato chake si kidogo. Na ukienda maeneo kama haya kuwa mtu wa kujichanganya usipende kukaa kivyako vyako hii itakusaidia kupata watu wapya. Kwa upande wangu toka nianze kwenda haya maeneo nakutana na watu wengi sana tofauti na wana status nzuri sana.

Maeneo ya hadhi kama haya ukiingia, ukakutana na mtu yoyote kwanza atakuheshimu ataona wewe si mtu wa kawaida. Ukijenga tabia ya kutembelea haya maeneo naamini utapata connections nyingi sana na utakutana na watu wenye hadhi.

Biashara ya Uber pia ni sehemu ambayo ni rahisi sana kukutana na matajiri sababu asilimia kubwa ndo usafiri wao, mtu kama anatoka point A to B ni ngumu kutumia usafiri wake ataishia kurequest. Kama Dereva uwe unapiga nao story hawa watu acha kujikuta kauzu msome kwanza mteja ukiona ni talkative anza kupiga naye story, hii itasaidia kufungua milango mingine.

Kwa upande wa Posta/Masaki kuna ofisi nyingi sana na utawabeba Ma-Hr, Managers, C.E.O’s nknk, jitahidi uwe unafanya engagement nao usiwaogope, tengeneza connection. Mimi Insider ningekuwa nataka kuajiriwa kipindi kile bhasi ningekuwa nilipata kazi muda sana.

Cheki conversations yangu na moja ya mteja niliyekutana naye Posta,

INSIDER: “Bossy wangu naona umependeza sana na pigo za Ki-HR.”

CUSTOMER: “Mhh kaka naonekana kama HR?”

INSIDER: “Exactly nambie kama nimekosea.”

CUSTOMER: “Hahaha hamna bhana, mimi ni mtu wa kawaida tu mbona.”

INSIDER: “Ooh sawa kama kweli wewe ni HR naomba connection ya mchongo, napambana na Uber angalau mkono uende kinywani, lakini huku ni kugumu sana.”

CUSTOMER: “Jamani lakini sio mbaya Mungu atakusaidia, una elimu gani kaka?”

INSIDER: “Nina degree ya Uchumi naweza kuisaidia kampuni kwenye mambo mengi sana, kama itatokea chance naomba nikumbuke bossy wangu.”

CUSTOMER: “Kaka usijali utanipa namba yako afu utanitumia na CV kabisa incase imetokea nafasi nikupambanie.”

Sasa ukituma CV kwa watu 20 hapo unakuwa na Probability kubwa ya kupata mchongo na ukiwa na qualifications nzuri, kutoboa ni haraka sana. Hawa watu wamenitafuta sana honestly, na last week kuna dada kanipigia simu nilimtumiaga CV mwakajana nilikuwa nimemsahau, sasa kanipigia simu ili anipe connection lakini nilimwambia nimerudi shule kusoma. Unaona ni muda mrefu lakini still alikuwa na CV yangu akanikumbuka, mimi nilikuwa nimesahau kabisa.

Suala la kupata wateja Private ni juhudi zako za kupambana na kuwa mbunifu, kumbuka Uber ni biashara na mpo wengi na wengi gari zao ni nzuri, inabidi uwe mjanja sana kuwapata hawa wateja wa Private.

Ukiwa smart unajiweka vizuri, gari yako ni safi nje na ndani, gari full AC na inanukia vizuri. Naamini huwezi kosa wateja wa private na asilimia kubwa ya wateja utakao wapata ni wanawake, kingine cha muhimu mtangulize Mungu pale unavyotaka kwenda mzigoni, just pray.

Mteja mpaka anaamua kukutumia private anaangalia vitu vingi sana kutoka kwako ukiachana nakuwa na gari kali, pia customer care nayo ni muhimu sana ili kuwavutia. Wanaume hawana shida ila kwa dada zetu wanapenda sana ukiwapa customer care nzuri sana, pamoja na kuwasifia sifia yaani wanapenda sana.

Kitu kingine ambacho Uber wanafeli sana, unakuta umemchukua mteja kutoka Posta kwenda Masaki. Baada ya kumdrop unamwacha aende badala ya kumuuliza kama anarudi tena Posta ili umrudishe wewe unamuacha aende kwa hapa mnafeli sana, wengi wenu mnapishana na hela.

INSIDER: “Dada samahani unarudi tena Posta? ili nikusubiri?”

CUSTOMER: “Yes narudi ila nitachelewa kidogo, kuna customer namuattend.”

INSIDER: “Unaweza tumia muda gani maximum.”

CUSTOMER: “30 minutes maybe.”

INSIDER: “Mimi nitakuwa around kama utakaribia kumaliza just text me nianze kusogea.”

CUSTOMER: “Sawa usijali.”

30 minutes sio nyingi kwa kumsubiri customer maana kuna muda request zinakuwa shida afu biashara ni ushindani sana, lazima uwe mjanja na mbunifu. Kumbuka pia sio kila mteja atakwambia umsubiri ni wewe ujiongeze tu, sasa mteja kama huyu ukimrudisha Posta lazima atasave namba yako na ataanza kukutumia.

Kingine ukimshusha mteja kwa destination ongea naye kama atakuwa na kazi Private awe anakutumia, tengeneza na Business card zako unakuwa unawapa wateja. Ukiwapa wateja 30 business card yako kuna ambao watakutafuta tu mfanye kazi, na kumbuka ukifanya kazi na mmoja anafungua baraka ya kukuunganisha na wengine, circle yako inazidi kutanuka inafika stage unawateja wengi.

Mimi binafsi kuna stage ilifika hata Uber nikawa siwashi, yaani ile asubuhi nikiwa drop akina mama wa2 na Maggy, unakuta nina booking ya kufanya kazi na loan officers na hapo inakuwa kazi ya siku nzima.

Nilifanya kazi na hawa loan officers wa CRDB, NMB, EXIM, KCB nknk ni wengi mno nimefanya nao sana kazi, na wao kwa wao ndo walikuwa wanapeana connection wananitafuta. Malipo yanakuwaga kwa card ila sasa ikitokea wamepiga mshindo walikuwa wananipa sana hela.

Ukija kwa mtaani wengi walikuwa wananitafuta si unajua wanawake hawapendagi shida? Kama anasherehe bhasi atanitafuta tunakubaliana bei ya siku nzima afu tunafanya kazi, Dullah nilimpa connection ya mtoto wa bank na baadae kaja kuwa mke wake halali.

Nimefanya kazi nyingi sana yaani kuna muda nilikuwa napiga pesa mpaka ukiniletea story za kuajiriwa nakuona mchawi. Narudia tena kama upo smart ukifanya uber unapata kazi kwa haraka sana na maana utakutana na watu wengi wenye status tofauti.

Kitu kingine cha muhimu kwenye Uber ni uaminifu hata ukiona kitu cha thamani mteja amekisahau wewe mrudishie itakupa sifa nzuri sana. Nimekutana na simu nyingi sana kwenye gari wateja wamesahau, wallets, pochi nknk lakini nilikuwa nawarudishia kwa uaminifu na sikuwahi kuwa na tamaa.

Kitu kingine usikatae request hata kama mteja anakwenda sehemu ya mbali kama upo kazini wewe nenda cha muhimu ongea na mteja muone mnasaidianaje maana yeye anataka usafiri wewe unataka Pesa. Kama ni usiku na mteja anaingia ndani ndani sana, mchukulie bodaboda kwaajili ya usalama wako na uwe makini sana hasa kwa nyakati za usiku.

Huwa nawashangaa sana madereva wa Uber wanaolalamika kuwa biashara ni ngumu kwakweli huwa siwaelewi kabisa, kwa mwaka jana wakati Vita ya Russia/Ukraine imeanza kupamba moto kweli biashara ilikuwa ngumu sababu nauli zilipaa sana, ila kwa dereva wa Uber kutegemea request ni umaskini wa akili. Tumia Uber kukupa connections za kupata wateja wa private na sio kutegemea requests hapa utafeli tu na kuishia kulalamika biashara ni ngumu.

Jambo lingine madereva wa Uber 80% hawajatulia ni malaya, sasa ukiendekeza pussy hesabu maumivu, utaishia kuwapakia mademu bure kila wanakokwenda. Mademu wa Dar wajanja sana they know hot to manipulate a Man, hapo akikupata ana uhakika wa free Uber ya kumpeleka kwenye mishe zake. Hii tabia mpaka madem waliojariwa wanayo maana akikupata ana uhakika wa usafiri wa asubuhi, hakuna dem anayependa kupanda daladala asubuhi na kubanana hakuna.

Utakutana na mademu wengi sana kwenye hii biashara ila ukikosa self control utaishia kutembea nao na kuwagongea kwenye gari. Asilimia kubwa ya madereva wa Uber gari zao ni guest, nyie mnaotumia huu usafiri kuweni makini sana. Hawa jamaa wanagongea mademu au mashoga humo humo ya gari, usipendelee kukaa seat za nyuma ni hatari sana.

Umaskini ni mbaya sana ndugu zangu maana utakuwa unakubali kushawishika kwa vitu vidogo, sahivi mashoga asilimia kubwa wanaliwa na madereva wa Uber sababu ya njaa. Hawa watu sijui wanatoa wapi pesa kwakweli, lakini ndo kwanza wanakaa sehemu nzuri kama mbezi Beach, Mikocheni nknk.

Ukiwapakia hawa watu ni wasumbufu sana wata kutongoza sana, nimekutana nao sana hawa watu na wengi wamenisumbua sana mpaka kero, kukuwekea offa ya laki 5, million kwao ni kawaida. Sasa kwa dereva ambaye ana njaa hapa hatoboi ataishia kuwala tu, bad news mpaka mastar nao hamna kitu, kuna msanii huwa siamini kama na yeye ni chakula yaani daah! hali ni mbaya sana. Kuna presenter maarufu kanisumbua sana na niliishia kumblock lakini bado akaendelea kunitafuta kwa namba nyingine, mpaka nikamwambia nitaavujisha chats zako ndo akatulia ila hali ni mbaya sana Mungu atusaidie.

Ukiwa HB na unajipenda hawa wanawake watakutongoza sana na hasahasa wamama wanasumbua sana “mashangazi”. Mademu watakusumbua sana, nyakati za usiku utapakia mademu ambao hawajielewi wamelewa na kama unatamaa utaishia kuwala.

Dar ni mkoa mchafu sana hasa kwa nyakati za usiku, ukitaka kuamini hili wewe jaribu kutembelea maeneo ya Sinza, Masaki ndo utaona ushenzi unaofanyika. Nyakati za usiku kwa Sinza mashoga kibao wanazagaa, Masaki kuna Malaya wengi sana. Kwa Mbweni ukisikia illegal issues ndo ziko huko kama sembe, utapeli bhasi huko ndo HQ yake kwa hapa mjini. Hii Dar ione hivihivi lakini ni chafu sana, mimi Dar naijua yote hakuna kitu utakacho nidanganya na ninazifahamu chocho zote.

Mimi nilikuwa natafuta hela na sikuzote pesa utazipata kwenye mambo ya hovyo, mfano mimi nilikuwa na connection za kuwapata madem wa kizungu, kichina, kihindi nknk, kupitia Masai-Ellias na pia kuna chocho ziko Posta unawapata wazungu ni hela yako tu. Mfano madem wa kizungu minimum Price wanacharge kuanzia $300 mpaka $1,000 inadepend na quality ya mwanamke, hapo ukimuanganisha kwa tajiri hukosi hata $100-200 ya kuweka mfukoni. Mimi nashida gani? kwenda kumchukulia foreigner demu na kumplelekea hotelini na kujipatia $100 kuna kazi hapo?.

Ukiwa kwenye hio biashara utakutana na vishawishi vingi sana ukiachana na mademu, pia kuna vishawishi vya kuingia kwenye dili za kikubwa kama sembe, kusafirisha wazamiaji nknk, point hapa kuacha tamaa maana unaweza ambiwa kila kichwa cha mzamiaji ni 2M afu uwapeleke Bagamoyo hapo ukipiga hesabu una 10M, ni wachache ambao wanaweza kuikataa hii offa.

Ishu ya mwisho na muhimu kwa Dereva wa Uber ni kuzingatia usafi wako binafsi, vaa pendeza chomekea kama vile unakwenda ofisini, pulizia na unyunyu wako freshy. Kwa weekend mimi nilikuwa nakula pamba safi nimetupia jeans na t-shirt afu chini nina raba yangu kali freshy.

Usishangae haya mambo kazi ya Uber ni ngumu sana na inataka moyo, wapo watakao kudharau, kupewa kejeli ni jambo la kawaida sana, muhimu hapa wewe mind your business usipende kubishana au kugombana na wateja itakucost, kubali kuonekana mjinga ila kwa faida yako.

Katika vitu ambavyo nilijitahidi sana kuvizuia ni pamoja na wife kupanda ile Ist, maana niliona natengeneza mikosi kwa mke na mtoto. Ndomana nilikuwa nikirudi break ya kwanza ni bafuni kuoga kutoa nuksi ndo mambo mengine yaendelee, lingine nilikuwa najitahidi sana kufanya usafi wa gari.

Biashara ya Uber ni rahisi sana kukutana na watu wapya na kupata Connection nyingi sana kama utakuwa smart. Maana huku ni easy kukutana na foreigners, Celebrities , pisi kali nknk. Just assume wastani kwa siku unabeba abiria 10 mara 30= 300, zidisha mara miezi 12= 3,600. Huu ni wastani tu nimetumia, sasa kwenye hawa watu 3,600 utakosa connection hapa???.

Dereva wa Uber ukilalamika Biashara ngumu bhasi jua wewe upo kundi hili,

1. Unategemea request tu
2. Umeendekeza Mademu/Starehe
3. Hujiongezi.

Wewe utaishia kulalamika Biashara ngumu.

insiderman1@yahoo.com
 
Maguire alifanya kosa kubwa moja la kimkakati. Kosa lenyewe ni kujidai sitaki-nataka kumla Iryn mapema mpaka Iryn akajenga urafiki na mama J. Kama Iryn angetafunwa mapema kipindi kile anamuita mwanetu chumbani kupanga nguo, basi sidhani kama Iryn angetaka kuweka ukaribu na mama J. Hii ingeweka mipaka mizuri na kuondoa dhana ya usaliti wa Iryn kwa mama J.

Maguire anataka kufanya kosa lingine kubwa sana la kimkakati. Kosa lenyewe ni kwenda kumtambulisha Iryn kwao, wakati akiendelea kumficha mama J. Hapa ndugu yetu anahamisha dhambi kutoka kwake mwenyewe, mpaka kua dhambi ya familia. Mama J akijua umezaa na Iryn itakua msala. Ila mama J akijua umezaa na Iryn, na familia yako ilikua inafahamu hili suala ila yeye akafichwa, inakua ni msala alafu msala tena. Beba mzigo wako mwenyewe chief, haina haja ya kuibebesha familia nzima!

Kwakua umepanga kufunga ndoa na mama J, kuna options mbili za maana unazoweza kuchagua: mfiche mama J mpaka watoto wa Iryn watakapokua wakubwa, au umwambie mama J kabla ya ndoa kwamba Iryn ni mke mwenzie then umshawishi akubali kua mke mkubwa. Option ya pili italeta msala, lakini sio msala mkubwa kama ambavyo mama J atakuja kugundua miaka miwili baada ya kufunga ndoa. Kuna maumivu ya talaka, mgawanyo wa mali na visasi mpaka kwa mtoto ambayo utayapitia mpaka ushangae!

Mwisho kabisa, jiandae kisaikolojia kuachana na mama J, ili ikitokea ikawa hivyo basi usiumie sana. Wasomaji wako tunajua umekufa na kuoza kwa Iryn zaidi ya unavyompenda mama J. Japo unatuzuga ila maandishi yako yanakukataa;

  • unapoteza hisia za kumkaza mama J, ila Iryn show kila siku.
  • Kwa Iryn hadi jikoni ulikua unaingia kupika, ila kwa mama J hata kurudi nyumbani ni utata.

Ilikua story nzuri sana, ila mwisho nimekuhurumia kwa huo mtihani unaokukabili. Inawezekana wewe unauchukulia poa, ila sio mdogo. Kua makini sana na mama J. Hakuna kiumbe hatari kama mwanamke alieumizwa moyo na akaamua kulipa kisasi!
Watu wanachambua mapenzi Kama mpira. Formation, mifumo na njia zote za kupita na vichochoro zake ndani.
 
Huu msala nitausovu, 2033 nitakuwa na majibu tuombe uzima. [emoji120]
 
INSIDER MAN kuna story humu something like wema ni akiba jamaa alikuwa na demu bongo then akaokota dodo la kupendwa na demu wa kizungu mtoto wa kishua , mademu wote wapata mimba ila akaamua kuoa mbongo kwasababu ya mama yake ndo alimchagua mbongo, alijaribu kuachana na yule mzungu ikashindikana na walifanikiwa kupata mapacha, mwisho wa siku mkewe huyu mbongo aligundua wakazungumza yakaisha na mke akabariki yule mzungu akawa bi mdogo, na mzungu akawachukuwa watoto wa mke wa jamaa akaenda kuwalea huko nje so watoto bi mkubwa na bi mdogo walilelewa pamoja ..
Twaibu nami nilikuwa ninawaza hivyo kwamba asitishe kufunga ndoa na mama J kwanza ili amweleze ukweli kwamba ana mtoto wa nje na Iryne na jinsi ninavyowajua wamama wa kichaga baadhi yao lakini anaweza kuchukulia positively kwamba hii ni fursa kwa kumpata mwenza mwenye pesa nani ajuaye anaweza asikasirike bali huenda akakubaliana na hali.Lau akilichukulia kwa ukali na kuonyesha kutokubaliana nalo achukue ustaarabu wake Insider ataamua kujikita kwa Iryne.
 
kwanza siku hizi hilo jambo ni la kawaida huko duniani,eti unakuta mke na mume wapo busy kutafuta girlfriend 🤣 kweli bhangi sio chai imeharibu sana watu hasa hao waliohalalisha matumizi yake.
 
I’m done with extras, Email napokea ujumbe mwingi kutoka kwa wadau mbalimbali ni messages nyingi sana na nyingi watu wanaomba muendelezo wa matukio mpaka Iryn anajifungua. Nimepokea mails nyingi sana kutoka kwa watu tofauti, niseme nashukuru kwa feedback zenu na kuna wale ambao mna appreciate niseme ahsante, nitazipitia mails zote na kuzijibu taratibu.

Kutokana na wingi wa watu kuomba Season 2 ya matukio yote yaliyoendelea nitawapa muendelezo mwakani na nitaishia pale Iryn alivyojifungua. Ndugu zangu nimebanwa na shule kwasasa na majukumu ya kutafuta mkate wa Junior na Ariana (CODE).

Nimepitia ushauri wenu kuhusu hili sakata la Iryn na Mama J, kuna watu mmetoa ushauri mzuri sana, ahsanteni sana nitaufanyia kazi. Kwa upande wangu kuna hatua ambazo nilianza kuzichukua nafikiri mtaona Season 2, maana nahitaji kutuliza sana akili kwenye hili Jambo.

Kuna msemo unasema “Mtaka yote kwa Pupa hukosa vyote.” Kwa upande wangu nataka vyote.

Tukutane mwakani panapo majaliwa naamini tutakuwa pamoja.
 
Wishing You All The Best Bro...lakini Mary mliishia wapi?
 
Insider na mama J hawajafunga ndoa bado, ndio wapo ktk mchakato. Ndio nikamshauri kabla ya kufika mbali aweke wazi kuhusu Iryn na mtoto.

Huyo mama J ndio ataamua kuendelea na mchakato wa ndoa ama la.
Sio kwamba ata kataliwa kumuoa mama j hapana. Ila kwenye ukristo hakuna wake wawili so ndoa itafungwa vizuri ila shida inaanza wewe kutaka kulazimisha uhalali wa wake wawili.

Kibinadamu tupo sawa mana ni nature ya wanaume kuwa na watot wengi toka enzi ila utashindana na imani yako mpk kufa kwako, unless uwe muslim.
 
Nakuelewa Mkuu, kumbuka akishaliweka wazi jambo la mtoto kwao litapokelewaje na litaishia wapi, ndio maana nashauri akamilishe kwanza zoezi la kubariki ndoa hayo mengine yatafuata baadae.

Mama Jr machale yalishamcheza, anaweza kuvumilia mtoto Kwa mwanamke mwingine lakini sio Iryn, itamtafuna sana akiwaza jinsi mambo yalivyokua yanaenda. Itakua ngumu sana kwake kuamini kwamba safari za awali Zanzibar hapakua na mahusiano. Kila mara jamaa alipochelewa kurudi nyumbani atandindoshewa jumba Bovu Iryn.

Hata Iryn alivyokua anaenda nyumbani kuwasalimia Junior na Mama yake itaonekana alikua anawakebehi tu.
Hasira zake usipime, weka mbali kabisa.
Ndio amwambie ukweli mama J aamue.
 
Back
Top Bottom