INSIDER MAN
JF-Expert Member
- Nov 7, 2018
- 2,005
- 19,579
- Thread starter
- #12,421
SEASON : 02
CHAPTER 8
“A TRUE STORY BY INSIDERMAN”CHAPTER 8
PREVIOUS
Baada ya game kuisha hatukukaa sana tukaondoka kurudi home na wife ndo alikuwa wakwanza kushuka kwa gari. Muda huu niliikumbuka ile voice ambayo nilikuwa nimerecord kule hotelini, hivyo niliona ndo muda sahihi wa kuisikiliza.
CONTINUE…
Niliangalia tena kama kuna usalama na nili-lock gari nikaanza kuisikiliza ile voice na ukweli nilikuwa nahamu sana ya kujua mazungumzo yao. Nilifanikiwa kuiplay na haya ndo yalikuwa maongezi yao na zaidi ya 90% yalikuwa kwa kiingereza,
CLAIRE: “Baby vipi kuhusu mimba yako, so unakwenda kuwa mama? You said you don’t trust him.”
IRYN: “Huyu mtoto nimempa zawadi Insider, kama atafanya ujinga ni juu yake.”
CLAIRE: “Ulikuwa unalalamika Insider ana mahusiano ya siri na moja ya wafanyakazi wako, mimi naona Insider atakusumbua tu best yangu. Hio mimba bado ni changa sana you can abort before it’s too late, Insider loves you because you are a rich and nothing more, listen to me."
IRYN: “No Claire Insider hana habari na Pesa zangu hakuna hata siku alishaomba pesa kutoka kwangu na juzi tu hapa amenambia hataki tumlipe mshahara maana ni dharau kwake. Kuhusu kunipenda hili naweza ku-agree Kuwa Insider huenda hana mapenzi kwangu lakini ana mapenzi kwa huyu mtoto tumboni.”
CLAIRE: “Mwanaume kama hana mapenzi kwa mama how come awe na mapenzi kwa mtoto? Acha kujidanganya, haimake sense kabisa na ukizingatia Insider ni mme wa mtu tayari, fanya maamuzi magumu kabla ya mambo kuharibika. Usipokuwa makini utaweza poteza familia yako pamoja na ndugu zote na bado Insider akakupiga na kitu kizito, ukajikuta unarudi ulikotoka na majuto juu.”
IRYN: “Remember, Insider is the only one who cared about me during that bad time, and now you're talking shit about him?"
CLAIRE: “I know you love him lakini kubali kupokea ushauri na kumbuka sisi ni marafiki tangu utotoni, sitapenda kuona best yangu unapata shida hapo baadae. Una miezi 9 ya kulea tumboni bado una miaka 3 ya kulea mtoto afu aje akufanyie ujinga unafikiri mimi nitajiskiaje?”
Iryn alinyamaza kimya kwa sekunde kadhaa na aliendelea kuongea,
IRYN: “Claire kama Insider atabadilika huyu mtoto atabaki kuwa furaha kwangu na siwezi ku abort kwahili sikuungi mkono dear. Pia nikwambie kama kuna lolote litatokea lawama zije kwangu maana mimi ndo niliyeamua kubeba hii mimba bila kumshirikisha.”
CLAIRE: “Anyway, umejipangaje huko Ethiopia? Nakumbuka uliniambia ndo jambo linalokupa stress kwasasa na hatukamaliza maongezi yetu.”
IRYN: “I don’t know maana nitakapotoa taarifa watataka kumjua Insider then lazima waseme suala la ndoa na hapa ndo utata utakuja maana Insider ana mke tayari.”
CLAIRE: “You told me bado hajafunga ndoa, hapo inaweza kuwa 50-50 anything can happen. Mimi cha kukushauri get him to marry you first.”
IRYN: “I don’t think it will work, he’s always smart and he knows what he is doing."
CLAIRE: “Nafikiri bado hujaamua na umekubali kuwa mchepuko, lakini kama utakubali ushauri wangu hakuna kisichowezekana.”
IRYN: “Claire we can stop here, he’s coming tutaongea haya.”
Baada ya kuisikiliza voice hapa ndo nilikuwa na uhakika wa 100% kuwa Claire ni snitch kwangu na niliona kama ana wivu wala sio kingine. Kwa upande mwingine nilijilaumu sana kuwahi kurudi maana maongezi yao yaliishia pazuri sana na Claire alikuwa ametema sumu kali sana.
Niliwaza kuhusu suala la kwenda Ethiopia na niliona kama nilifanya maamuzi ya haraka sana kumkubalia Iryn. Kwenda Ethiopia ni kama kutembea na kitanzi shingoni, niliwaza na kuona sina sababu ya kwenda huko.
“Nimeshampa ahadi ya kwenda huko tena kukaa week nzima, daah huu ni msala. Week ni kubwa sana kukaa kule lolote linaweza tokea, ikitokea Iryn akanitambulisha kwa familia yake kuwa mimi ndo mpenzi wake? Na wakija kujua mimi na mke tayari itakuaje?.”
Niliona naumiza kichwa kwa matatizo yaliyosababishwa na Iryn mwenyewe, tatizo langu mimi lilikuwa kwenye mtoto tu maana niliona lolote linaweza tokea, ukizingatia ile mimba bado ni ndogo. Niliona Claire bado ananguvu sana ya ushawishi kwa Iryn na lolote linaweza kutokea.
Niliona kuna umuhimu wa kutafuta wazee wa busara wa kunipa ushauri juu ya hili suala na kuna mzee wangu wangu tulikuwa tunapatana sana kipindi niko taasisi X, hivyo niliona kuna haja ya kwenda kuongea naye kuhusu hii ishu.
Suala la kuwaambia wazazi na ndugu zangu wa karibu niliona bado ni mapema sana na sitakiwi kuwa na haraka sana atleast mimba ifike miezi 6 kidogo naweza kuwa na ujasiri wa kumwambia hata dada yangu. Mimba ya mama J nilikaa miezi 6 ndo nilitoa taarifa kwa dada then nikampa taarifa mama, sikuona umuhimu wa kushirikisha familia yangu kwasasa.
Niliwaza mama anakuja jumamosi na atakaa na sisi mwezi mzima hapohapo nina safari ya kwenda Ethiopia na Iryn. Niliwaza hili jambo mbona linakuwa gumu sana? Na roho yangu kwenda Ethiopia ilikuwa inasitasita kwakweli. Kwa mbali nilimuona mama J katoka nje na amesimama kibarazani na akiangalia usawa wangu ni kama alikuwa anajiuliza mbona huyu mwanaume hatoki shida ni nini?.
Baada ya kuingia ndani nilikaa seblen nikicheza na Junior maana tulikuwa wawili tu pale sebleni na muda huu nilichukua simu yangu kuangalia kama Iryn amefika au laah. Hakukuwa na text yoyote kutoka kwake na mimi nilimtumia ujumbe kumuuliza kama amefika salama.
Nilianza kuview status za whatsapp maana na niliview status za Prisca nikaona kam-wish mama yake happy birthday. Nilireply kwa ujumbe uliosomeka “Happy birthday to our beautiful mama” na haikuchua muda Prisca alireply na tukaanza kuchati pale. Tuliendelea kuchat pale na kubwa alitaka nimpe majibu ya ile text yake ya mwisho kunitumia ya kuwa friends with benefits na mimi nilimwambia hilo halina shida kama karidhia.
Nilifikiri nikaona kuna haja ya kuendelea kuwa na Prsica kama mchepuko wangu ukizingatia tuna historia tayari. Niliona kama kaanza kujielewa hivi, hivyo hatonisumbua kama zamani na itakuwa rahisi sana kumcontroll.
******
Siku ya jumamosi mama yangu mzazi alikuja Dar es Salaam na alisema ataendelea kukaa na sisi mpaka Christmass ndio ataondoka kurudi mkoani. Asubuhi tulikuwa na usafi wa jumla pale home, kwa upande mwingine kila jumamosi ya mwisho wa mwezi huwa tunafanya usafi wa pamoja kwa wapangaji wote. Hii ni ratiba iliyowekwa na sisi tuliukuta huu utaratibu baada ya kuhamia.
Saa 10 jioni niliondoka na wife kwenda Magufuli bus terminal kwaajili ya kumpokea mama na aliwasili mida ya saa 11 jioni. Baada ya mama kuwasili tulikumbatiana na alimgeukia wife wakakumbatiana pia, ndo kuondoka kurudi home. Barabarani zilikuwa ni story za huko nyumbani na wife ndo alikuwa busy na mama mkwe wake, huku mimi nikiwa busy na usukani.
Baada ya kurudi home mama ombi lake la kwanza lilikuwa ni kumuona mjukuu wake na bahati nzuri Junior alikuwa pale seblen na furaha ya mama ilitimia baada ya kumuona. Mara ya mwisho mama kuja Dar ilikuwa ni baada ya wife kujifungua na kipindi hicho Junior alikuwa na miezi 2 tu. Kwa upande mwingine mama alifurahi sana kumuona dada bado tuko naye ukizingatia tumeishi naye toka Junior ni mdogo na kipindi kile mama anakuja Elena alikuwepo.
Baada ya kupata chakula cha usiku tulifanya ibada ya pamoja pale seblen na baada ya hapo mimi niliaga nakwenda kulala na niliwaacha wakiongea.
Jumapili asubuhi niliamka mapema kwenda kazini maana nilikuwa nina kazi ya kuanza kuandaa bonus za mwaka kwaajili ya wafanyakazi. Ni utaratibu wa kampuni kwa kila mwisho wa mwaka kutoa bonus na mshahara double, hivyo nilitaka nikamilishe hesabu mapema ili mishahara iwahi kutoka kwaajili ya sikukuu za Chtristmas na mwaka mpya.
Asubuhi wakati naondoka mama alikuwa bado kalala hivyo nilimuaga wife na kuondoka kwenda Masaki. Ilikuwa ni mida ya saa 2 asubuhi wakati nawasili pale ofisini kwa upande mwingine nilikuta wafanyakazi wako busy sana. Kwa siku za weekend kunakuwa na wateja wengi sana, hasa kuanzia ile asubuhi mpaka usiku.
Mimi niliendelea na majukumu yangu na baada ya nusu saa Hilda alikuwa kawasili na alikuja ofisini kunisalimia, tukapiga story mbili tatu akaondoka kwenda kuendelea na majukumu yake. Kwa upande mwingine stock ilikuwa umekata na tulikuwa na odda nyingi sana, hivyo niliona niwasiliane na Iryn maana toka tuongee kabla hajaondoka hakunipa ripoti.
Iryn yeye ndo huwa anaagiza mzigo pamoja na kulipia baada ya hapo ndo ananiachia mimi kwenye masuala ya kodi na clearing. Baada ya kumpigia simu alipokea na tukaanza mazungumzo na habari mbaya alisema anaumwa,
MIMI: “Mummy unasumbuliwa na nini?”
IRYN: “Nahisi mabadiliko ya mimba natapika sana.”
MIMI: “Pole mke wangu, nilitaka kukuliza kuhusu mzigo umefikia wapi? Tuna odda nyingi na stock hakuna kitu, mzigo wa mwisho uliagiza mdogo.”
IRYN: “Kuna mzigo uko njiani unakuja ni week tayari nilikuwa busy na wewe sikufuatilia mails, soon nakutumia details. Kuna mwingine nimefanya payment tayari lakini shida ni Meli niliyopata gharama za usafirishaji ziko juu sana kwa contena, supplier anaendelea kucheki meli nyingine.”
MIMI: “Ok sawa haina shida baby, mimi naomba nikuache maana nina kazi kibao hapa.”
IRYN: “Wait, ushaanza kufuatilia Passport?.”
Ukweli sikuwa nimenza process zozote na sikutaka kumdanganya hivyo nilimwambia ukweli,
MIMI: “Bado baby but kesho jumatatu nitaanza usiwe na wasiwasi.”
IRYN: “Why you’re not serious?. Tarehe 16 tutaondoka kwenda Ethiopia.”
MIMI: “Baby muda bado upo mwingi sana hili lisikupe mawazo.”
Baada ya kuachana na Iryn pale niliona tayari nishajiingiza kwenye kitanzi maana waswahili wanasema ahadi ni deni. Niliwaza hivi kama nitaghairi hii safari Iryn atachukua hatua gani? yani nilikuwa sina imani kabisa ya kwenda huko Ethiopia.
Muda huu Asmah aliingia ofisini amependeza sana na alikuwa ndo anafika na mimi kama kawaida yangi nilimpa sifa pale na nilimzingua kwanini kachelewa?”
MIMI: “HR unaingia saa 4 asubuhi serious?”
ASMAH: “Jana nimechelewa kulala na ulivyonambia utakuja ofisini mapema bhasi nikawa na amani. Insider stock haina kitu zimebaki wigi chache sana kwaajili ya wateja na unajua december hii customer ni wengi.”
MIMI: “Ni kweli, hizo pisi msitoe nje zibaki kwaajili ya sisi lakini kuna mzigo unakuja na soon utakuwa umewasili tayari.”
ASMAH: “Umeongea na Iryn mwenyewe?”
MIMI: “Yeah ameconfirm na mwingine bado anahangaika na meli analalamika gharama zimekuwa kubwa za usafirishaji.”
Baada ya mazungumza na Asmah, alitoka kwenda kuweka utaratibu na mimi muda huu nilianza kuyambuka yale mazungumzo ya Iryn na Claire na nilijisemea I have to do something.
Saa 9 za mchana niliondoka ofisini na lengo kubwa niende Mbweni kumsalimia Jane maana ilikuwa ni wiki imeisha bila kukanyaga pale kwake. Kipindi niko njiani nilimkumbuka yule dada ambaye tulibadilishana namba pale car wash lakini alikuwa hajanicheki, niliona dada ana dharau sana.
Baada ya kuwasili kwa Jane nilimkuta mama Pama pale seblen akiwa na wageni, nilimsalimia tukaendelea na maongezi na baadae Jane alitoka na alifurahi sana kuniona.
Pale kwa Jane ukweli ni wananiheshimu sana tena sana ilifika stage mpaka baadhi ya marafiki zake Jane walidhani mimi ni ndugu damu wa Pama. Jane alinipa ishara na mimi nilijua tu anataka tutoke nje tuongee na mimi ndo nilikuwa wa kwanza kutoka na yeye alifuata.
Tulikaa garden tukizungumza na kubwa ilikuwa ni suala la Mary maana Jane alitaka tuyamalize haya mambo haraka sana. Jane alionekana kuwa serious sana kwenye maongezi yake,
“Shem unajua wewe na Mary ndo watu wangu muhimu sana na nina waheshimu, sipendi jinsi mnavyoishi kwasasa kwanini msikae chini mkamaliza tofauti zenu?”
“Shem unajua fika Mary anahisia za kimapenzi kwangu na zile ni hasira ila atakaa sawa tu trust me. Mary namuheshimu sana ndomana sijataka kufanya ujinga wowote kwake maana najua italeta shida huko mbeleni, ni vizuri anichukie lakini kwa faida ya maisha yake kwasasa hawezi kuelewa.”
“I really appreciate naomba nikuulize jambo lakini kuwa honesty na mimi, yule dada (Iryn) ni nani kwako?.”
Niliona Jane anauliza maswali sensitive sana na niliona hata nikimwambia ukweli hakuna faida atakayopata, zaidi mahusiano yangu na Iryn yabaki kuwa ni siri,
“Shem yule ni bossy wangu kama nilivyokutambulisha na nina muheshimu sana, hatuna mahusiano zaidi ya hapa.”
“Sawa Insider mpaka nimekuuliza ujue ile siku kwenye lile sakata la Mary pale seblen niliona mabadiliko yake, na nikahisi mpo kwenye mahusiano”.
“Hiyo sio sababu lile suala alilofanya Mary ni la kitoto na alinikera sana, naamini Mary ndo anakupa hizi taarifa za uongo.”
“Insider naomba mkae na Mary myamalize na umwambie ukweli, sidhani Mary anakuchukia kwa hili kuna vitu unamfanyia ndomana.”
“Sawa shem haina shida nitakaa nae chini usiwe na wasiwasi.”
“Tuachane na haya ila Insider unabalaa sana shem wangu, yule dada alimtetemesha sana Mary afu she is very confident.”
Tulianza kucheka pale na Jane maana hata yeye alimkubali Iryn kuwa ni mrembo makini na kamkubali. Pia, Jane alinipa taarifa kuhusu 40 ya mtoto na alisema baada ya hapo ndo nitamkabidhi rasmi gari yake. Kwa upande mwingine alinipa taarifa ya kupewa zawadi ya gari kutoka kwa Umoja wa kikundi cha Pama na alisema hajui ni gari gani na itakuwa surprise siku hiyo ya 40 ya mtoto.
Saa 12 za jioni niliondoka kurudi nyumbani maana wife alikuwa kashaanza kupiga simu nonstop. Baada ya kuwasili home nilimkuta mama yuko seblen anacheza na mjukuu wake na tulisamiana pale nikakaaa kwenye coach.
Baadae tuliamua kutoka nje kukaa kibarazani kuendelea na maongezi maana niliona mama anakosa uhuru wa kuongea pale seblen,
MAMA: “Mpaka jumapili unakwenda kazini mwanangu?”
MIMI: “Hapana ila mara chache kama kuna jambo huwa nakwenda si unajua mimi ndo kila kitu?”
MAMA: “Bossy wako anaonekana ni mkarimu sana ile siku alinambia mama natamani sana nikujue siku maana Insider ni mchapakazi mzuri.”
MIMI: “Amesafiri mara moja kama atarudi bado upo atakuja kukusalimia na atafurahi sana kukufahamu.”
MAMA: “Yule binti mimba iliyoharibika anaendeleaje?
Nikajisemea mama kaanza kufukua makaburi kumbe hajasahau tu,
MIMI: “Yuko salama mama ila hatuna mawasiliano kwasasa niliamua kukaa naye mbali yale makosa yasijirudie tena.”
MAMA: “Vizuri lakini Roho inanambia bado anakupenda, naomba kuwa makini sana kwa hili mwanangu.”
Ilibidi nibadili mada niliona mama anakoenda siko kabisa,
MIMI: “Nambie harusi ni ya nani kwanza? Maana hatukuongea hili kabisa.”
MAMA: “Ni binti wa mama TUSI , si unamkumbuka yule bint yake wa kwanza?.”
MIMI: “Simkumbuki kabisa, bhasi tutakwenda wote na vipi kuhusu michango?
MAMA: “Tutakwenda na mama J, muwe mnahudhuria harusi za wenzenu ili mpate hamasa ya kuoana mapema. Na suala la harusi yenu mmefikia wapi? Haya ni maamuzi na mipango yenu, lakini siku zinakwenda.”
MIMI: “Harusi tutafunga mama ngoja amalize chuo kwanza nabado najipanga kiuchumi.”
MAMA: “Mwanangu unataka mjipangaje? Unajua kadri mnavyochelewa ndo mnampa nafasi shetani?”
MIMI: “Ndomana mama yangu upo najua unatuombea ili shetani asilete majanga.”
MAMA: “Biblia inasema mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate. Mimi nawaombea sana sana, lakini mnatakiwa na nyinyi mkumbuke kujiombea sawa mwanangu?”
Mama akishaanza masuala ya vifungu vya bible huwa nakuwa mpole sana, na muda huu wife alitoka na juice akatupa pamoja na mama. Tulikuwa na maongezi mengi sana na mama lakini cha ajabu lile jambo ambalo alisema kama ameoneshwa namficha hakuliongelea kabisa na mimi wasiwasi wangu ndo ulikuwa pale.
Mama aliniaga anakwenda kumsaidia wife kupika na mimi nilibaki pale kibarazani nikiwaza mambo mbalimbali ambayo yakinichanganya akili, likiwepo suala la Iryn la kwenda huko Ethiopia.
Jumatatu nilikuwa nina ratiba mbili muhimu ya kwanza ni kwenda kuonana na mzee wangu pale taasisi “X” na ratiba ya pili ni kwenda Uhamiaji kufuatilia suala la Passport.
Saa 3 za asubuhi nilikuwa nimewasili taasisi “X”, lakini nilikuta kuna mabadiliko makubwa sana pale, kwani asilimia kubwa ya watu nao fahamiana nao walikuwa hawapo, wamehamishwa. Kwa upande mwingine baadhi walikuwepo tunaofahamiana lakini sura nyingi zilikuwa ngeni. Idara niliyokuwa nafanyia kazi kulikuwa na watu wapya lakini ni watu wawili tu walikuwa wamebakishwa ambao ni kaka na dada yangu, ambao walipelekwa department zingine.
Baada ya kuelekezwa idara walizohamishiwa nilikwenda kwanza kuonana na dada yangu na tulipiga sana story na alinipa taarifa kuwa mzee wangu alikutana na panga kapelekwa mkoani, hivyo sikuwa na jinsi maana plan yangu ikawa imefeli. Namba yake nilikuwa nayo lakini kwa masuala kama haya niliona halina nguvu kuongea kwa simu na niliwaza nitafute plan B maana plan A ishafeli.
Baada ya kuachana na sister nilikwenda onana na brother angu na tulipiga story kadhaa kisha nikaenda msalimia manager wa ile taasisi. Manager baada ya kuniona alifurahi sana na tuliishia kupiga story nyingi sana za maisha maana toka tuachane hatuwahi onana wala hatukuwa na mawasiliano, licha ya kufanya kazi zake nyingi sana.
Habari kubwa manager alisema walikuwa na kikao na majina yetu yalipendekezwa kwaajili ya kupewa ajira maana tuna experience na tulichapa sana kazi kipindi kile. Manager alisisitiza sana hili suala kuwa ni serious na soon tutaanza pigiwa simu kwaajili ya kupewa mikataba. Mimi niliishia kumuitikia lakini nilijisemea hata kama nikweli siwezi kuikubali hio offer ya serikali ya kunilipa mshahara wa 1.5M, afu niache kazi yenye maslahi kwangu ambayo nalipwa mara 3 zaidi.
Kumkosa mzee wangu pale ofisini nilinyong’onyea sana na ukweli sikuwa na option kabisa na mzee aliyekuwa amebakia ni mmoja tu ambaye alinisaidia wakati natoa mahali ya mama J. Niliona kumshirikisha hili jambo italeta matatizo na nilijisemea sitakiwi kutumia nguvu sana kwenye hili suala, mambo yatakaa sawa tu.
Niliondoka kuelekea Kurasini pale Uhamiaji kwaajili ya kufuatilia Passport na nilikuwa tayari nimefanya mawasiliano na jamaa yangu ambaye anafanyia kazi pale na tulisoma Advance pamoja. Baada ya kuwasili pale tulionana na tuliongea kuhusu hili suala na alinihakikishia itatoka haraka nisiwe na wasiwasi kwa hili.
Niliondoka kuelekea Mikocheni na lengo langu nikaonane na Lucy maana toka Iryn aondoke hatukonana na niliwaza huenda ana jambo lolote la kunambia. Mchana nilikuwa nimewasili pale ofisini na nilimkuta anajisomea, baada ya kuniona alinambia anataka kwenda kula lunch, ikabidi na mimi niliunge.
Muda ambao tulikuwa tunapata lunch Lucy alinambia Iryn kamfungukia kuwa anamimba yangu na ananipenda sana. Lucy aliendelea kunisisitiza kwamba kwasasa nisimpe stress zisizo na msingi wala kumkera na nifocus na maendeleo ya kampuni. Kwa upande mwingine tuliendelea na mipango ya kiofisi na kubwa nilimwambia anisaidie kuandaa performance report ya kila mfanyakazi wa pale Mikocheni kwa mwaka mzima ili niweze kuandaa bonus zao zitoke mapema na mishahara.
Baada ya maongezi ya kiofisi tulianza maongezi mengine na nilishangaa kuona Lucy akiniulizia taarifa za Bob na mimi nikawaza huenda Bob kashamtongoza tayari. Japo Lucy hakutaka kuongea lolote nilihisi kuna kitu hakipo sawa na nilijisemea nitamcheki Bob anipe mkanda mzima wa kinachoendelea.
Saa 11 jioni niliamua kurudi home mapema maana niliona kurudi late na mama yupo pale home haiwezi leta picha nzuri ukizingatia mama anaonekana kuwa na maongezi mengi sana na mimi.
Baada ya kurudi home nilimkuta mama yuko nje na Junior akimwendesha kwa gari yake na nilimsalimia na tukaendelea na mazungumzo. Mama alishangaa sana kuona nina gari tatu pale home na mimi nilimwambia yakwangu ni moja tu ambayo ni ile Ist mpya na zingine sio zangu.
Tulianza kupanga mipango ya harusi na alisema harusi itafanyika Tabata na siku ya ijumaa itabidi twende Kariakoo kwaajili ya kununua zawadi za harusi. Mama alisema kama kikundi chao huko mkoani wamechanga kwaajili ya sherehe na yeye ndo mhasibu wa kikundi chao. Kwa upande wangu nilimwambia nitamfanyia shopping na nitampeleka saloon akang’arishwe na aliishia kufurahi.
Kwa upande mwingine mama alinisisitiza sana nitulie na kama nina wanawake wa nje bhasi niachane nao kwani Mungu amenipa mke bora na nimuheshimu sana mama J. Si unajua tena mambo ya wazazi, mama alinipa sana lectures na alikuwa hakosei sehemu za kupiga point.
Wakati nikiendelea kuongea na mama, Iryn alianza kupiga simu na mimi sikutaka kupokea simu zake muda huu maana nilikuwa na mazungumzo na mama. Baada ya kuona akiendelea kupiga simu kwa fujo nilimuaga mama mara moja nakwenda ndani kuoga then narudi.
Baada ya kupokea simu yake kama kawaida alianza kulalamika kwanini sipokei simu zake na ilibidi nimdanganye kuwa nilikuwa nadrive na simu ilikuwa silent. Sikutaka kumwambia Iryn kuwa mama yuko home maana nilijua angenisumbua sana kutaka kuongea naye na ingeleta tatizo.
Mimi na Iryn huwa tunakuwa na maongezi marefu sana, unakuta tunaweza ongea hata lisaa na bado hakuna dalili za kumaliza maongezi. Kwa upande mwingine aliuliza kuhusu progress za ufuatiliaji wa Passport na nilimwambia tayari nimeanza mchakato na soon nitakuwa nayo. Tangu Iryn arudi Dar na kuondoka niliona wivu kwangu umeongezeka sana na alikuwa akipiga sana simu mpaka kero na hapo anataka tuwe tunaongea tu ndo furaha yake.
*****
Ijumaa tulikwenda Kariakoo kununua hizo zawadi kwaajili ya harusi na tulianza kwanza kufanya shopping maduka ya Sinza, then tukamalizia Kariakoo. Zawadi ambazo mama alikuwa anataka kununua ni pamoja na fridge, Jiko na mazaga mengine. Kwa Kariakoo nina wadau wengi sana pale, hivyo haikuwa shida kwangu na tulipata fridge nzuri na bei kitonga.
Baada ya kumaliza shopping ilibidi twende Tabata kuzipeleka zawadi ili ziwe karibu na eneo la tukio. Break yetu ilikuwa Kinyerezi kwa mama TUSI na alikuwa kafikia kwa binti yake ambaye anaolewa na nilimsalimia pale na alifanya kunitambulisha binti yake maana tulikuwa hatujuani.
Jumamosi asubuhi mama alinipa ratiba kwamba tunatakiwa kuwahi kwenda ukumbini hivyo itabidi wawahi kwenda saloon ili kufikia saa 12 jioni tuwe amefika eneo la tukio. Saa 9 mchana wife na mama waliondoka kwenda Mikocheni na nilikuwa nishampanga tayari Lucy kuwa mama yangu anakuja hivyo asizingue.
Saa 12 jioni niliwapitia pale ofisini na nilikuta wamependeza sana kwakweli yaani ungemuona mama J wangu ungedata. Kwa upande mwingine Lucy aliniita pembeni na alianza umbeya wake na kubwa alifurahi sana kumuona mama yangu na aliishia kunimwagia sifa kuwa tumefanana sana.
Saa 1 usiku na madakika tulikuwa tumewasili Baracuda Highland hall na niliweza kuonana na mama zangu wa mkoani. Niliwasilimia pale na wao walifurahi sana kuniona na kama kawaida ya wamama waliishia kunichamba kwanini nakaa na mtoto wa watu bila kufunga ndoa?. Niliishia kujitetea pale na niliwapa ahadi kuwa soon na mimi nafunga ndoa, waliishia kumfurahia mama J na tukazama ndani eneo la tukio.
Tulikaa upande wa ndugu za Bibi-harusi na Kwenye meza yetu tulikuwa 10, mama alikuwa amekaa kati yangu na wife na muda huu tulikuwa tunapiga story wote watatu. Mama aliendelea kusisitiza tufunge ndoa mapema kwani muda unakwenda na sio lazima tufunge ndoa ya gharama, lawama zote zilikuwa zinakuja kwangu. Wakati story zimenoga kwa upande mwingine Iryn alianza kupiga simu na mimi nilikuwa nazimute maana sikuona sababu ya kuongea naye muda huu, na alipiga mara tatu.
Harusi ilikuwa nzuri sana kwakweli mpaka nikapata ka wivu na mimi nifunge harusi na mama J, lakini nikikumbuka suala la Iryn nikawa nakosa nguvu. Harusi iliisha saa 6 za usiku na tuliendelea kumsubiri mama maana alikuwa ana kikao na wamama wenzake na walitumia kama lisaa ndo tukarudi home kulala.
Jumapili nilichelewa sana kuamka na nilikutana na missed call nyingi tu, missed call 2 ilikuwa ni namba mpya, lakini nilipotezea na nilikwenda seblen kuangalia kama mama kaamka salama. Nilimkuta mama akicheza na mjukuu wake na nikamwambia jioni tutatoka wote kwenda kutembea na kupata dinna.
Nilitoka nje ili niweze kuongea na Iryn maana alikuwa kapiga sana simu pamoja na texts juu, nilimpigia simu na haikuchukua muda akapokea ila alionekana kuchukia sana,
IRYN: “Baby kwanini hupokei simu zangu toka jana?”
MIMI: “Sorry, sikuwa sehem nzuri ndomana.”
IRYN: “Unamaanisha nini kusema hukuwa sehemu nzuri? Na kwanini hujanambia kama mama amekuja Dar?”
Nikajisemea Lucy kashampa taarifa Iryn na nilisahau kumwambia asiseme hivyo sikuona sababu ya kum-mind Lucy,
MIMI: “Ningekwambia mummy kaja juzi na masuala ya harusi ndo yamemleta na ndo nilikuwa naye jana huko kwenye harusi.”
IRYN: “Sijapenda Kutonipa taarifa, four days remain before our trip to Ethiopia na nitakuja Dar ili tuondoke wote. Naomba nikija nimuone mama by any means, this is not for me, it's for your child."
MIMI: “Sawa no problem I’ll do my best”
Sikutaka kumkatalia maana ningeanzisha matatizo mengine hivyo nilikubali lakini nikijua hili jambo haliwezi tokea kwasasa. Muda wa kwenda Ethiopia ulikuwa unakuja kwa spidi sana na niliwaza pale nitatumia gia gani ya kuondokea pale home kwenda huko?. Niliwaza nimuache mama yangu mzazi home then niende na Iryn? Niliona kama haiwezekani.
Wakati nikiendelea kuwaza simu ya Prisca iliingia na baada ya kufanya nae maongezi alinipa taarifa kuwa kwasasa yuko Changanyikeni hivyo niwe nakwenda kumsalimia. Baada ya kuongea na Prisca nilifanya kumpigia simu dogo ripota wangu na nikamwambia aache kumfuatilia Prisca, amuache na maisha yake. Kwa upande wake dogo alishangaa sana na aliuliza kwanini nimeamua hivyo? Nilimwambia kwasasa hatuko kwa mahusiano, hivyo sioni sababu ya kumfuatilia .
Jioni tuliondoka familia nzima kwenda Karambezi cafe kwaajili ya kupata dinna ya pamoja na lengo langu kubwa mama afurahie kuja Dar. Baada ya kuwasili pale tuliagiza chakula lakini kwa mama ilikuwa shida kidogo kwani zile menu zilikuwa zinamshinda na nilifanya kumchagulia chips na beef.
Tuliendelea kupiga story pale na mama alionekana kulipenda sana eneo hili na muda huu simu yangu ilianza kuita na ilikuwa ni namba ambayo ilinitafuta asubuhi. Nilitoka na nikaenda kupokea simu,
ANONYMOUS: “Hello Insider za kwako?”
MIMI: “Salama habari yako pia.”
Wakati nataka kuuliza who’s this kwa haraka alijitambulisha,
ANONYMOUS: “Unaongea na Ghati tulikutana Carwash Mbweni.”
Hapa ndo kumkumbuka yule dada na ile siku tunakutana hakunambia jina lake,
MIMI: “Now nimekufaham mrembo, niliwaza umeamua kunipotezea maana kimya sana mpaka nimesahau.”
ANONYMOUS: “Sorry, nilipata emergence ya haraka, so nilikuwa bush kuna mradi nilienda simamia. Nimerudi sio muda na kitu cha kwanza nimeenda kwenye gari kutafuta business card yako ndo nimekupigia.”
MIMI: “Ooh thank you na pole na safari.”
ANONYMOUS: “Asante, upo pande zipi?”
MIMI: “Seems unataka tuonane.”
ANONYMOUS: “Yeah If possible maana niko tu, na sina pakwenda.”
MIMI: “Kwa leo ratiba ipo taiti mummy nitakucheki next week.”
ANONYMOUS: “No problem basi ngoja mimi nilale byee.”
Baada ya kuachana na dada nilisave namba yake na nikarudi mezani kujumuika na kina mama. Nakumbuka tulikaa pale mpaka saa 4 za usiku ndo kurudi home kulala na hii siku mama alisema atakuwa na kikao na sisi, kwani ana mazungumzo muhimu sana ya kuzungumza nasi.
*****
Tulikuwa tumeanza wiki mpya na zilikuwa zimebaki siku 3 tu za kwenda Ethiopia na ile asubuhi nilikwenda Kurasini kuchukua Passport yangu ilikuwa tayari imetoka. Baada ya kutoka pale Kurasini nilikwenda moja kwa moja mpaka Masaki lakini wakati niko njiani niliwaza nitafute sehemu nitulie kwanza.
Niliamua kwenda Cocobeach kutulia kwanza na kulifikiria hili jambo kwa makini sana before sijafanya mistake yoyote. Pale Coco nilitumia muda mwingi sana kulifiri hili suala na majibu niliyowaza nisiende huko Ethiopia na nilianza kuwaza nitatoa sababu gani?.
“Ok! Iryn anajua mama yuko Dar naweza mwambia tutakuwa na kikao cha familia ambacho ni muhimu niwepo, hivyo sitoweza kwenda Ethiopia. Sasa, Insider kama Iryn umempa ahadi ya kwenda ina maana hukujua mama anakuja? Kumbuka ana mimba yako tayari, kumpeleka Ethiopia kuna shida gani?”
Ni Roho mbili ambazo zilikuwa zinashindana ndani yangu, lakini hii ya kutokwenda ilikuwa na nguvu na nikajisemea potelea mbali kama atanichukia kwa hili, i’ts okay bado nitabaki kuwa baba mtoto ila kwenda huko sitathubutu Roho yangu imekataa.
Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana na nikaona kuna haja ya kwenda home kuongea na mama kuhusu hili suala la mimba ya Iryn. Niliona kwa stage niliyofikia ni ngumu sana kuwa na maamuzi sahihi, hivyo nahitaji msaada hata kwa mama yangu mzazi before mambo hayajaharibika.
Niliona sometimes kama mwanaume inatakiwa kuwa na maamuzi magumu, nibora mama ajue mapema kinachoendelea before it’s too late na maamuzi yafanyike mapema. Kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na kucheki ni Iryn alikuwa anapiga na nikajisemea leo namchana ukweli siendi Ethiopia.
CHAPTER 9
www.jamiiforums.com

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu
Insider ana tabia kama za ex wangu. Huyu ex ni so addictive... Ni ngumu kumuacha kimoja.. Hata kama ametoka kucheat ukim tait anakuwa mpoleee anakupeti nankukujaza na kukataa kata kata had unaamini hajafanya.. Wanawake washataka kupigana visu sababu yake. Mbingu ya wanaume kama hawa iko mbali...