Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Mwanaume mchepukaji hawezi kufanya makosa kama hayo ya kujirudiarudia tena kwa kuyapanga wewe mwenyewe,

kuwatoa Hilda na Asmah kwa pamoja kwa wakati aliokua nao wa kutokua kwenye maelewano na mke wake pamoja na Irene, tena kwa Asmah kuonyesha mahaba mbele ya Hilda uo ni ujinga na kutokujitambua
Jamaa amekuwa muwazi uzembe ambao wanaume tunaweza jikuta tunafanya bila kutarajia. Mwanamke analewa anafanya matukio ambayo hukutarajia huenda hata kwa makusudi kama ilivyokuwa kwa Irene kwenda kwa mama J. Nafikiri hujawahi kutana na visa vya wanawake. Huwezi fikiri kuwa Asmah aliona Hilda anampenda Insider akaona atapoteza mechi ni bora kuua move mapema. Defensive mechanism za wanawake ni za kujilipua mno
 
Tatizo la kuwajua madem ukubwani, alishasema alichelewa kuanza kwichi kwichi. Umri nao ni mdogo afu kazishika hela mapema.
Kuwa smart, kuwa na pesa pendwa na wanawake wazuri wenye status. Nakwambia kila mmoja atatamani kukuonja waone una nini cha ziada. Ukiwa wa mishangazi utafuatwa na mishangazi tu. Ukianza na mashoga watakuja wengi tu wa aina hiyo utajiona una nuksi. Utawakwepa 100 ila kumi wataanguka mikononi mwako ili kujenga heshima na ulijali utashika hatamu. Ni ngumu kuwakwepa wote.
 
SEASON 02
EPISODE :27

“BY INSIDER MAN”

PREVIOUS:
Tuliongea mambo mengi sana na dada huku tukipanga vitu kwaajili ya safari ya kesho kurudi Tanzania.

CONTINUE:

Wakati tukiendelea kupanga nguo, simu ya dada yangu iliita. Nilipoangalia, niliona ni jamaa akipiga, na nikampa dada. Jamaa alimjulisha dada kuwa amefika salama, na kwamba amefurahi sana kuwa naye. Pia, alimtakia usiku mwema. Dada alimjibu kwa kumtakia usiku mwema pia, na akamwambia kuwa tutaonana kesho, kwa kuwa ilikuwa lazima tuonane

Baada ya jamaa kukata simu, tuliishia kucheka, kisha tukaendelea na mipango yetu kwaajili ya safari.

Asubuhi na mapema, tuliamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya safari. Wakati huo huo, jamaa alipiga simu na kutujulisha kwamba tutakutana airport akitusubiri.

Tax ilipofika kutuchukua, mmoja wa dada waliokuwa wakituhudumia hotelini alitusaidia kubeba mabegi yetu kuyapeleka nje. Nilimuita na kumshukuru kwa huduma nzuri aliyotupa kwa kumpa Rand 200 kama zawadi ya shukrani.

Nilipompa pesa, nilimwambia 'see you next time.' Sister aliishia kunipiga ngumi ya mgongo na dada mhudumu alifurahi sana na kutuaga, kisha akaondoka. Nilijikuta nikiangalia umbile lake kwa matamanio ya juu sana, wanawake wa South Africa wamebarikiwa kujazia nyuma kwa namna ya kipekee.

Tulianza safari ya kwenda airport na ndani ya muda mfupi tuliwasili. Sister alimpigia simu jamaa kumpa taarifa kuwa tumefika airport na tupo upande wa ‘Departure’. Baada ya dakika tano kupita Jamaa alikuja mpaka tuliko na tukaendelea na story za mwishomwisho.

Kwa upande wetu, tulimshukuru sana kwa msaada aliotupa tangu tulipofika Afrika Kusini. Baada ya hapo, tukaagana naye kwani muda wa kucheck-in kwaajili ya safari yetu ulikuwa umewadia.

Safari yetu ilianza saa 3 asubuhi. Kwanza, tulipitia Johannesburg na tukakaa huko kwa takriban saa moja kabla ya kuendelea na safari. Wakati tukiwa njiani, sister alisema kuwa akishuka, ataunganisha tena safari ya kwenda Arusha kwani hawezi kulala nyumbani kwa sababu ya wife.

Saa 10 za jioni tuliwasili JNIA, dada Tyna alitupokea maana alikuwa around akitusubiri.
Tyna alifurahi sana kutuona na alituuliza kuhusu mafanikio yetu kwenye jambo lililotupeleka South Africa. Hata hivyo, sister alibadilisha mada kwa kumwambia afungue bag aone kilichotupeleka kule.

Sister alikuwa kamnunulia zawadi Tyna za vipodozi na baadhi ya nguo, zilikuwa ni zawadi nyingi tofauti, na swali lake likawa limejibiwa kwa namna hii. Sister alimuuliza kuhusu ticket yake ya kwenda Arusha, Tyna alisema ataondoka na ndege ya jioni sana, ila ni ya Kilimanjaro.

Tulikwenda kwenye cafe kupata chakula kwa sababu tulikuwa na njaa sana. Tulipofika, tuliketi na kuzungumza kuhusu mambo mbalimbali huku tukipiga stori. Kwa upande wangu, niliendelea kumsubiri dada hadi alipoondoka kuelekea Arusha, ili niweze kurudi nyumbani. Sikutaka kumwacha dada peke yake katika mazingira haya.

Baada ya lisaa sister alipaswa kucheck-in kwaajili ya kuanza safari yake ya kwenda Arusha, na tuliagana kwa kupiga picha za mwisho pamoja na dada Tyna. Nilimsisitiza sana dada asije akajisahau akapost status sababu itatuletea shida kubwa sana. sister alisema yuko makini, kisha tukaagana kwa kumbatiana pale.

Nilipata wazo la kuonana na Dullah kabla ya kurudi home ili nimuombe radhi ya kutokuwepo kwenye harusi yake. Tulipowasiliana, tulikubaliana tukutane Mlimani city, ambapo aliniambia soon atakuwa amefika, nami nilimwambia natoka airport.

Niliondoka na Uber kuelekea Mlimani city mapema sana nilifika eneo la tukio tayari. Nilifanya mawasiliano na Dullah ili aje parking afungue gari yake ili niweke bag langu, kisha tukaenda kukaa samaki samaki.

Mhudumu alikuja kutusikiliza pale, nami niliishia kuagiza heinekeni nilitaka kupunguza stress za South Africa;

MIMI: “Brother kabla ya yote nikupe hongera kwa ndoa.“

DULLAH: “Ahsante sana, jambo lilikwenda vizuri na honey moon ilikuwa nzuri sana.”

MIMI: “Mseng** honey moon ya nini wakati mlianza kulana kabla ya ndoa?.”

DULLAH: “Tulia kijana, mapenzi ya honey moon ni matamu sana.”

MIMI: “Nisamehe sana kwa kutohudhuria maana sipo sawa toka ile siku tuoanane.”

DULLAH: “Usijali senior naelewa, ulikuwa wapi? nakuona na bag na ulinambia upo airport.”

MIMI: “Acha tu senior, nimepigwa na kitu kizito sana, kwasasa sina hamu na kiumbe anayeitwa mwanamke, sahivi nawaona takataka.”

DULLAH: “Nini tena kaka umekutwa na jambo gani?.”

Nilimsimulia Dullah mkasa mzima mpaka naenda South Africa na sister yangu;

MIMI: “Hapa ndo narudi kaka huwezi amini, hustle zote lakini nimeambilia patupu.”

DULLAH: “Najiuliza kwanini afunge simu? Si akwambie ukweli tu! kuliko kukupa stress zisizo na sababu?.”

MIMI: “Sijui mzee baba atajua mwenyewe na maisha yake, mimi sina habari naye kwasasa aendelee na maisha yake.”

DULLAH: “Bro mimi kama refa wa match VAR inaniambia wewe ndo umeachwa, pole sana asee. Na wasiwasi asijekuwa ameondoka na nyota yako maana hawa madem sometimes miyeyusho.”

MIMI: “I believe in God, I don’t care.”

DULLAH: “Ufanye mchakato uoe sasa utulie na familia yako. Si unakumbuka kipindi kile nilikwambia ukianza Uber utakutana na pisi nyingi kali utapagawa, ulinibishia.”

MIMI: “Mwanamke niliyekutana naye na kuanza mahusiano ni Iryn mzee, mimi sichomeki kila sehemu najitambua.”

DULLAH: “Fala nini na yule demu wa mbezi beach uliyempangia nyumba Makongo?”

MIMI: “Huyo tumesha achana kitambo sana.”

DULLAH: “Angalia sasa wote umewatia mimba na zimeharibika, madem wa Uber ni nuksi.”

MIMI: “Fala umeanza kulewa unatalk shit, nishukuru kwa kukupa Latifah bila mimi ungekuwa hujaoa.”

DULLAH: “Kwahili ulitisha sana Senior, sema mzee una kismart na wanawake, wewe ni mwanaume ambaye hata ukiachana na manzi leo, kesho unapata mwingine wa maana. Njoo sasa kwa akina sisi, kupata dem anayejielewa ni kipengele, wengi ni wanyonya damu. Soko lilikuwa gumu, lakini sasa nina latifah wangu mambo shwari.”

MIMI: “Sawa bhana naona umeanza kujisifia.”

Tulikaa pale mpaka saa 3 za usiku, kisha tukaagana, nami nilirequest uber ya kunirudisha home. Kipindi niko njiani nilifuta picha zote za Iryn mpaka namba za simu, na nilijiapia kwamba pindi nikifika home nitaendelea kufuta picha zote kwenye simu yangu nyingine ya zamani.

Baada ya kuwasili home Elena alitoka kunipokea na tulisalimiana pale, na alinipa pole ya safari. Kuingia seblen namuona wife anamnywesha uji Junior, nikamsalimia na kumuuliza maendeleo ya home kwa ujumla, lakini alikuwa akinijibu kwa sauti ya chini sana, kama kuna kitu hakipo sawa, nikaachana naye.

Niliamua kuingia chumbani ili nioge nipumzike maana nilikuwa nimechoka sana. Sasa baada ya kuingia ndani naona bag lake kubwa limekaa mkao wa safari. Nilibaki najiuliza hili bag hapa namna gani? Mbona kama kuna kitu hakipo sawa humu ndani?.

Nilijisemea labda anataka kwenda home kupumzika ukizingatia chuo kimefungwa tayari. Sikutaka kuanza kujipa stress za bure, hivyo niliingia bafuni kuoga ili nilale.

Baada ya kutoka bafuni, mama J aliingia chumbani na kuketi kitandani huku akinitizama kwa umakini kama mtu anayepanga kusema kitu. Nilipomuona, nikajua kuwa kuna jambo fulani ambalo anataka kuzungumza.

MIMI: “Swahiba upo sawa? Nimekuletea zawadi mke wangu.”

WIFE: “Baba J, leo naona ni mwisho wa mahusiano yetu. Tumejaribu sana, lakini nadhani unataka hivi toka muda mrefu na sina uwezo wa kuendelea kuumizwa. Nimekuvumilia sana, lakini sasa ni bora tuishi kwa amani na kumlea mtoto kwa ushirikiano. Nia yangu ni kutafuta amani na furaha kwa wote, na siwezi tena kuvumilia hii hali, tuangalie mustakabali wa mtoto wetu kwa umakini.”

Na alianza kutoa chozi pale, lakini mimi nilikuwa hata sielewi anacholilia na tatizo ni nini?

MIMI: “Unashida gani Swahiba?”

WIFE: “Nashukuru kwa yote, Baba J. Nadhani malipo ni hapa hapa duniani, hivyo naona ni bora tuachane. Nakuacha na maisha yako, na kwetu sijafukuzwa."

MIMI: “Unanichanganya hata sijui unatatizo gani, niambie shida ni nini?”

WIFE: “Unanidanganya unakwenda Zanzibar Kikazi kumbe unaenda na Iryn kula bata, hivi unawezaje kufanya hivi?. Sawa Iryn ni mzuri kushinda mimi, anapesa unaweza kumuoa, naomba niwape space ili muwe huru, imeniuma sana.”

MIMI: “Wewe haya yote kakwambia nani?”

WIFE: “Nilikwambia kama kuna something fishy kinaendelea kati yako na yeye nitajua, ushahidi wote upo kwenye simu yako mwenyewe.”

Hapa sasa nilikuwa na uhakika kwamba wife alikagua simu yangu na kuona picha za Iryn na mimi tulipokuwa Zanzibar. Sikujua hata nimjibu nini kwa wakati huu kwani nilikuwa nimekamatika kabisa na sina cha kujitetea.

MIMI: “Naomba nisikilize mke wangu, hakuna chochote kinachoendelea, kesho tutaongea vizuri sahivi nimechoka sana.”

WIFE: “Haina haja ya kuzungumza ushahidi wote upo clear hata mtoto mdogo akiona atajua kinachoendelea bila kuambiwa. Kesho asubuhi mimi naondoka pamoja na mtoto, nakuachia nyumba yako uwe huru kufanya umalaya wako.”

Alinifyonza na akaondoka kwenda Sebleni. Ukweli sikujua hata najitetea nini maana ushahidi wote anao, na ukizingatia picha zipo kimahaba sana, ni ngumu sana kumuaminisha mtu nyinyi sio wapenzi.

Nilianza kujilaumu pale, huyu mwanamke kazidi sana, kwenye simu yangu alikuwa anatafuta nini mpaka anafungua na hidden files?.”

Kwajinsi ambavyo nilizificha picha za Iryn, sikutegemea kama wife angekuja kuziona, mpaka anaziona ina maana kwamba alifanya msako wa uhakika, yani wa folder to folder.

Nilijilaumu sana kwa kushindwa kubadili passcode kwa wakati mpaka naingia kwenye matatizo. Niliyakumbuka maneno ya Iryn kipindi kile aliyoniambia kwamba mimi ni mzembe hasa linapokuja suala la simu.

Asubuhi baada ya kuamka nilimwambia wife nikirudi jioni tutaongea, lakini asifanye jambo lolote la kipumbavu. Niliingia kuoga ili niende Mbweni kumsalimia Jane pamoja na kujua maendeleo yake kwa ujumla, maana toka niko South alikuwa amenitafuta sana kwa whatsapp.

Wakati niko njiani nilipata wazo nipitie kwanza dukani ili niangalie na maendeleo ya duka. Dukani alikuwepo dada baada ya kuniona aliishia kufurahi na tukaendelea kupiga story kuhusu biashara kwa ujumla na alisema inaenda vizuri.

Niliwaza kuna haja ya Jane kumuajiri kijana wa kumsaidia dada dukani hasa kwenye kubeba mizigo ya wateja na kazi ngumu za dukani. Niliona dada anateseka sana kwa hili, hivyo nikapanga kuzungumza na Jane kuhusu hili jambo na nikaondoka kwenda Mbweni.

Kwa upande wa Mbweni wakati nina wasili Jane alikuwa nje na mdogo wake Vicky wakifua nguo na baada ya kushuka kwa gari niliwasalimia na nikaingia ndani kuangalia kama kuna chai.

Baada ya kumaliza kunywa chai nilikuwa na mtoto pale seblen namuendesha kwenye gari yake. Baada ya lisaa Vicky ndo alikuwa wa kwanza kuingia ndani na tukaanza story, na kubwa alisema chuo kimefungwa yuko likizo.

Wakati nikiendelea kuongea na Vicky, wakala wetu wa clearing alinipigia simu na kubwa alinipa taarifa za mzigo;

AGENT: “Bossy habari yako, nimekutumia control number kwenye email kwaajili ya malipo since last week, lakini hamjafanya malipo mpaka sasa.”

MIMI: “Malipo ya nini tena?.”

AGENT: “Hujui kwamba kuna mzigo uliagizwa na bossy wako?”

MIMI: “Sijui sina taarifa kabisa aliagiza mzigo?”

AGENT: “Alinipa taarifa toka january, mbaya zaidi wote simu zenu hazipatikani, soon meli itawasili Dar es Salaam fanyeni malipo haraka.”

MIMI: “Ahsante kwa taarifa wacha nilifanyie kazi nitakurudia.”

AGENT: “Sawa.”

Sikuamini kuzisikia hizi taarifa kutoka kwa agent na bila kuchelewa nilimpigia simu Hilda kumpa taarifa naye aliishia kufurahi, tukakubaliana kesho tuonane kwa maongezi zaidi.

Baada ya kupata chakula cha mchana nilianza mazungumzo na Jane na kubwa nilimuaga ninaondoka kwenda Dodoma kwaajili ya mambo yangu na nitakawia kurudi.

Jane kwa upande wake hakufurahishwa na hizi taarifa maana aliona dizaini kama nazingua;

JANE: “Unakwenda lini huko Dodoma?”

MIMI: “Jumapili hii naondoka kwenda huko.”

JANE: “Kazini je? Sikuelewi au umeacha?”

MIMI: “Sijaacha ila nimechukua likizo ndefu kidogo.”

JANE: “Nahitaji wigi kama ya Mary naipataje kama wewe unaondoka?”

MIMI: “Ondoa wasiwasi kuna dada nitakupa namba yake mtawasiliana pale ofisini.”

JANE: “Nami kuhusu dukani, nani atanisaidia mahesabu?”

MIMI: “Kila mwisho wa week uwe unanitumia mauzo na gharama zote halafu mimi nitazifanyia kazi.”

JANE: “Hapo sawa leo nitakupa ahsante yangu ambayo nimeahidi kwa muda mrefu sana.”

MIMI: “Nitashukuru sana kwa hili.”

Jane aliingia ndani na hakuchukua muda mrefu alitoka ameshika bahasha iliyotuna vizuri na alinikabidhi pale;

JANE: “Shem pokea hii, unanisaidia mambo mengi sana, wewe ni moja ya mtu muhimu sana kwangu.”

MIMI: “Ahsante sana shem wangu, zawadi huwa haikataliwi.”

JANE: “Na unaanzaje kukataa kwa mfano?”

Jioni niliondoka kwa Jane na kipindi niko njiani nilipata wazo la kupitia site ili niangalie na maendeleo ya mradi wa mzee Juma. Baada ya kuwasili pale site, mradi ulikuwa umefikia hatua ya kunyanyua nguzo.

Nilifanya mawasiliano na Cami kumpa taarifa kuwa niko site nakagua mradi, naye aliishia kuniomba nipige picha za kutosha, kisha nimtumie kwa whatsapp. Nilitumia nusu saa kufanya ukaguzi kisha nikaondoka kurudi home.

Baada ya kufika nyumbani niliweza gundua kwamba hakuna mtu maeneo haya maana palikuwa kimya sana, hivyo nilitoa funguo zangu kwenye gari, nikafungua geti na kuingia ndani.

Nilienda straight chumbani na hapa ndo kujua mama J kaondoka kama alivyosema maana bag lake halikuonekana. Nilijikuta naanza kumlaumu wife kwa maamuzi ya haraka aliyochukua.

Sikuwa na mudi ya kukaa home bali niliondoka kwenda Upanga kwa Asmah, lakini nilimpigia kwanza akanambia yuko ofisini. Nilipitia Orysterbay nikachukua funguo na kuondoka kwenda kwake na ile kufika niliingia chumbani nikalala.

Usiku nilisikia Asmah akiniamsha kwaajili ya kula dinner aliketi pembeni yangu;

“Insider upo sawa kweli? Nimerudi muda mrefu sana, nimeoga, nimepika bado umelala, unaumwa?”

“Niko sawa sema kuchoka sijapata muda wa kupumzika vizuri kama leo.”

“Pole sana! Macho yangu yanaona haupo sawa kama umeamua kunificha haya.”

“Hamna Asmah wangu twende tukale, umepika nini?”

“Tambi na Kuku, wewe twende nimepika vingi tu.”

“Tangulia nakuja mummy.”

Wakati tunakula nilianza kumdadisi Asmah kama amefanya mawasiliano na Iryn hivi karibuni, lakini alisema hapana ni muda hawajawasiliana.

Baada ya kumaliza kula nilimshukuru kwa chakula, kisha nikarudi chumbani kuoga. Baada ya dakika 20 Asmah alikuja chumbani akapanda kitandani, kisha akakaa juu yangu. Alianza kunipa kashikashi pale, ila sasa mimi sikuwa na mizuka hata silaha iligoma kusimama.

Asmah alijitahidi kufanya kila mbinu ,lakini wapi sikuwa na hamu kabisa na nilimwambia aniache tulale.

“Is something wrong with you?, leo hii wewe wa kunikatalia?. Insider umepatwa na matatizo gani? mbona sikuelewi?”

“Asmah kuna mambo yananiumiza sana akili naomba kwa leo tulale kesho tutaongea sawa mummy?, sina hamu na sex kabisa.”

Asmah alimind kimtindo na aliendelea kuchezea silaha yangu wakati tumelala, lakini wapi fimbo iligoma kusimama sikuwa na hisia kabisa.

Kesho yake baada ya kuamka, Asmah alikuwa ameondoka tayari kwenda kazini. Niliwaza pale kitandani nikaona ratiba yangu ya leo nionane na Lucy na Hilda, halafu niende kuonana na kaka Allen maana kuna masuala ya kiofisi nilihitaji msaada kutoka kwake.

Niliondoka kwenda Mikocheni kuonana na Lucy ili tuzungumze vizuri, mara ya mwisho alisema anataka kuacha kazi, hivyo nilitaka kumsihi asifanye ujinga kama huu.

Baada ya kuwasili Mikocheni nilienda straight ofisini na Lucy kuniona alikuja speed akanikumbatia;

LUCY: “Oooh! Insider I have missed you so much.”

MIMI: “I miss you too! Pole na kazi.”

LUCY: “Sina hata hamu na kazi kwasasa, nakuwazia wewe tu. Najua kipindi unachopitia ni kigumu sana, but you will be stronger than before.”

MIMI: “Ahsante kwa kunipa moyo, lakini naomba usiache kaze Lucy, wewe endelea kuisimamia hii ofisi.”

LUCY: “Iryn mwenyewe hapatikani kwenye simu, mzigo umekata, Hilda naye analalamika stock imekata, landlord anatuhesabia siku hapa hata sielewi.”

MIMI: “Usiache kazi kwenye kipindi kigumu kama hiki, ujue tulienda na sister mpaka south Africa kumtafuta?.”

Lucy alinikatisha,

LUCY: “Mlienda South Africa na Sister? Na imekuaje?”

MIMI: “Huwezi amini tulimkosa na inaonekana amekwenda Dubai. Tulipishana kidogo sana, sisi tunaingia na yeye ndo alikuwa anatoka.”

LUCY: “Dubai kaenda kufanya nini na kwa nani? Asijekuwa ameenda kwa Muajemi.”

MIMI: “Hapo sasa ndo hatujui mshikaji wangu na kwanini Dubai?”

LUCY: “Iryn hajawahi kuikubali Dubai na mara nyingi huwa analalamika na hali ya hewa ya kule. What the f*ck ameenda huko? Ni kula bata hakuna kingine.”

MIMI: “Point yako unataka kusema hana mimba.”

LUCY: “Ndo maana yake, nakumbuka alinambia baada ya kumaliza mitihani atakwenda Ufaransa kupumzika, kusika Dubai naanza kuwa na wasiwasi.”

MIMI: “Halafu, amepostpone masomo yake.”

LUCY: “What? Hapa sasa naanza kuunganisha dots, nahisi amefanya hivo ili wasimshtukie chuo. Anaogopa kuulizwa maswali, nafikiri ameamua kuficha aibu kwa wanafunzi wenzake.”

Maneno ya Lucy yalianza kumake sense kwenye akili yangu, niliona Lucy ameongea ukweli mtupu. Niliwaza pale nimwambie kuhusu safari yangu ya Dodoma?, nikaona nipotezee nisimwambie.

MIMI: “Mummy naomba sana uisimamie hii ofisi na usiache bila kuwasiliana na Iryn sawa. Kuhusu stock, agent amenipa taarifa kuna meli soon itawasili Dar na mzigo. Naomba uendelee kuwahimiza wateja walipe cash ili ziendelee kusaidia kurun office sawa?.”

LUCY: “Insider mazingira ya kazi yamekuwa magumu sana. Just imagine umeandika barua ya kwenda likizo lakini mpaka sasa hakuna aliyezungumzia hili.”

MIMI: “I know! Kwasasa wote ni kama wameisusia kampuni kutokana na mambo yanayoendelea uzuri wewe unafahamu kiini cha tatizo. Ombi langu naomba uvumilie maana una andaa mazingira ya kuja kuwa manager bora hapo baadae.”

LUCY: “Sawa Insider nimekuelewa mshikaji wangu, but I hate Iryn for this.”

MIMI: “Don’t hate her, we both don’t know what is going on, but time will tell.”

Niliaga pale na kabla ya kuondoka Lucy alinikumbatia kwa mara nyingine tena kwa muda mrefu, kisha nikaanza safari ya kwenda Masaki kuonana na Hilda. Njiani nilipata wazo la kuonana kwanza na Allen na kuhusu Hilda nimtafute baadae baada ya kumalizana na Allen.

Kaka Allen alikuwepo ofisini na baada ya kufika alinikaribisha, kisha tukaanza maongezi pale. Kubwa alitaka kufahamu kinachoendelea kuhusu Iryn maana ni siku wiki zimekata pasipo kuwasiliana.

Nilimpa story nzima mpaka kwenda Afrika Kusini na sister yangu juu ya hili na baada ya kumaliza aliishia kushangaa na kunionea huruma;

ALLEN: “Bro! Huyu mwanamke ni wa tofauti sana, ni aina ya wanawake wanaopenda kupetiwa ana udiva sana. Mimi bado naamimi dada anamimba na atakutafuta wewe sahivi fanya mambo yako hata usimuwazie.”

MIMI: “Ndo jambo lililo nileta hapa kwako. Naondoka kwenda Dodoma kufanya harakati zangu, sasa nahitaji msaada wako.”

ALLEN: “Nakusikiliza wewe ongea nione kama naweza kukusaidia.”

MIMI: “Kampuni inapitia kipindi kigumu sana kwasasa. Sister alinishauri nisiache kazi kwenye hiki kipindi mpaka wao wafanye maamuzi. Kama nilivyokwambia awali kwamba mama na binti hawako kwenye maelewano na hawapatikani kwa simu.”

ALLEN: “Sister amekushauri vizuri sana hata mimi ningesema hivo, nikusaidiaje?”

MIMI: “Naomba msaada wa kunisaidia kutuma ritani za kodi kwenda TRA maana nitakuwa busy sana huko.”

ALLEN: “Hili usijali nitakusaidia wewe cha msingi utanipa mawasiliano ya unaemuachia ofisi ili niwe namkumbusha kwa hili.”

MIMI: “Ahsante sana bro! Na kuhusu malipo?”

ALLEN: “Wewe nenda Dodoma pindi ukirudi tutamaliza, usiwe na wasiwasi.”

MIMI: “Nashukuru sana kaka kwa hili.”

Tuliendelea kuongea masuala mengine na yeye aliendelea kunitia moyo na kuniaminisha Iryn hajatoa mimba niondoe wasiwasi kwenye hili. Tulikubaliana kwa badae tukutane pale Samakisamaki kabla sijaondoka ukizingatia na weekend ndo ilikuwa imeanza.

Kwa upande mwingine Hilda alikuwa akipiga simu kwa fujo maana nilimwambia niko njiani, lakini nikawa nimepitia kwanza kuonana na Allen.

Baada ya kumalizana na Allen niliondoka kwenda kuonana na Hilda. Nilimpa taarifa tukutane mgahawa wa Salty kwaajili ya kufanya maongezi. Mimi nilikuwa wa kwanza kuwasili eneo la tukio, hivyo niliagiza msosi kabisa huku nikiendelea kumsubiri Hilda.

Baada ya dakika 15 Hilda aliwasili eneo la tukio na baada ya kusalimiana, naye aliagiza chakula kisha tukaanza mazungumzo;

MIMI: “Naona unazidi kuwa mrembo manager wangu.”

Hilda alipatwa na aibu maana hakutegemea kusifiwa muda huu.

HILDA: “Ooh! Thank you Insider. Hupatikani kwa simu unanipa wasiwasi sana.”

MIMI: “Huna haja ya kuwa na wasiwasi mimi nipo na wewe.”

HILDA: “Mpaka sasa hujanipa feedback, stock iliyobaki week inaweza isimalize.”

MIMI: “Good news agent kanitafuta leo na kanitumia control number nifanye malipo ya mzigo, soon meli itakuwa Dar.”

HILDA: “Waow! Good news hapa sasa ninaanza kuwa na amani.”

MIMI: “Changamoto iliyopo ni pesa za kulipia hizo kodi za clearing maana kampuni haina pesa.”

HILDA: “Tunafanya nini sasa juu ya hili?”

MIMI: “Bado sijajua ni kiasi gani tunatakiwa kulipia huko, nikirudi home nitaangalia. Embu niambie ule mpango wetu ulifanikiwa wa cash?”

HILDA: “Asilimia kubwa umesaidia sio mbaya. Vipi wewe kuhusu wale tunaowadai ulisema utaongea nao.”

MIMI: “Walisema twende tukachukue lakini tuwe na evidence ya kuandikishiana kuwa wamelipa. Sasa nitadraft barua badae nitakutumia, kisha utaigonga mhuri na kwenda nayo kesho. Nipigie hesabu cash in hand uliyonayo halafu badae utanipa mrejesho.”

HILDA: “Hili ondoa shaka nikifika ofisini nakutumia hesabu.”

MIMI: “Jambo jingine mimi nitaondoka jumapili kwenda Dodoma sijajua nitakaa kwa muda gani huko.”

HILDA: “Najua umeacha kazi lakini hutaki kuwa muwazi kwangu, please usifanye hivo.”

MIMI: “Siwezi kuacha kwasasa mpaka wahusika waseme neno.”

HILDA: “Pole sana najua unapitia magumu sana, naamini yataisha.”

MIMI: “Ni kweli, labda nikwambie kuwa sipo kwenye mahusiano mazuri na Iryn, na hata na mama pia. Nakuomba sana uangalie hii kampuni, ninakuamini sana, sitaki kuona kampuni ikifia kwenye mikono yetu. Muda wowote ukikwama, nipigie nikupe msaada. Pia, kuna mtu nitakupa namba zake atakayenisaidia kutuma ritani TRA na kushughulikia mahesabu mengine. Jambo lingine, jitahidi sana kutuma ripoti kwa wakati; tuma kwangu na usisahau kuwa-CC mama na Iryn."

HILDA: “Nimekuelewa, mpaka sasa naona umeacha kazi ila unajiondoa taratibu….”

MIMI: “Hilda listen to me. Sijaacha kazi hata usifikirie kuhusu hili sawa?”

Tulikuwa tumekaa kwa kuangaliana na nilimshika mikono yake miwili na tuliishia kuangaliana kwa sekunde kadhaa bila kuongea;

“Umenielewa?” Na alikubali kwa kutingisha kichwa chake.

“Sasa nitakupa namba yangu mpya ambayo tutakuwa tukiwasiliana nayo. Sitaki usumbufu wa aina yoyote nikiwa Dodoma. Hii namba nitakayokupa ndiyo utaitumia kuwasiliana nami, sawa? Tafadhali, usimpe mtu mwingine yeyote."

HILDA: “Nimekuelewa Insider, nitakumiss sana ujue.”

MIMI: “Nitakuwa nakuja Dar pia hata wewe unaweza kuja Dodoma. Badae tutatoka out au unaratiba zingine?”

HILDA: “Hapana badae lazima tuwe wote maana sijui kama nitakuona tena.”

Tuliondoka cafe kwenda parking na pale tuliagana kwa kumbatiana na nikaondoka kwenda Upanga.

Nilianza kwanza kupitia Shoppers supermarket, nikanunua mahitaji muhimu ya home, kisha nikaendelea na safari yangu ya upanga. Baada ya kuwasili nilienda kuoga na nilipanda kitandani ili nipumzishe akili maana nilikuwa na mambo mengi sana kichwani yakiumiza akili yangu.

Suala la mama J kuondoka home kwenda kwao lilinipa sana mawazo maana sikutaka kuona tukikaa vikao vingine ambavyo havina sababu. Asubuhi mama yangu alinipigia simu, lakini sikupokea sababu nilijua lazima amepata taarifa kutoka kwa mama J, halafu sikuwa na majibu ya kueleweka.

Jioni Asmah alirudi kutoka ofisini na tulianza kusaidiana kupika jikoni. Alionesha kufurahia sana kampani yangu na alikuwa akishangaa kuona mwanaume naingia jikoni. Muda huu nami nilikuwa nampa masifa kedekede pamoja na matani ya hapa na pale.

Nilimpa taarifa ya kutoka out naye aliishia kufurahia taarifa hii, na kuhusu suala la kwenda Dodoma sikutaka kumshirikisha kabisa na nilivunga ili kuepusha maswali.

Saa 2 usiku tuliondoka kwenda Masaki na tulifanya kurequest Uber ya kutupeleka Samakisamaki. Allen alikuwa amefika tayari eneo la tukio na alinielekeza alikokaa na sisi baada ya kuwasili tulienda usawa alionielekeza.

Tulikuta anakunywa, hivyo na sisi tukaagiza vinywaji, kwa upande wangu niliagiza heineken na Asmah nilimuagizia wine 4 cousin. Baada ya nusuu saa Hilda naye aliwasili, kwahiyo jumla tukawa wanne.

Nilimtambulisha Hilda kwa Allen kuwa ndiye ambaye namuachia ofisi kwa kipindi hiki na watakuwa wakiwasiliana. Allen aliendelea kuongea na Hilda kuhusu hili suala na baadae wakabadilishana namba za simu.

Mida ya saa 7 za usiku, Asmah alisema amechoka na akapendekeza tuondoke tukalale. Asmah siyo mnywaji, yeye huwa anaonja tu. Chupa yake ya wine ilikuwa nusu, nikamwambia aimalize ndipo tuondoke, lakini alishindwa kuimalizia.

Muda huu Asmah alikuwa haelewi kabisa na alionesha kudeka sana mbele yangu na kina Hilda. Ilinilazimu kuaga na tukawaacha wao wakiendelea kunywa maana walisema bado wapo sana.

Baada ya kurudi Upanga sikuwa na jinsi zaidi ya kumshughulikia Asmah kisawasawa, hivyo nilikuwa nikimpa mapigo ya mwisho mwisho ya kuagana. Nilimpa mapigo mawili ya nguvu, naye kwa upande wake alionesha kuyafurahia sana, baada ya hapo tukalala.

Asubuhi mimi ndio nilikuwa wa kwanza kuamka, Asmah alikuwa amelala hajitambui, hivyo nikaingia jikoni kutengeneza soup na baada ya kukamilika nilimuasha ili tunywe pamoja.

Baada ya kumuamsha alianza kunilaumu pale;

“Insider unaharibu sana maisha yangu, wewe ndo umefanya mimi nianze kutumia alcohol.”

“Wine ni alcohol? Unazingua.”

“Mwili unauma balaa najihisi kuchoka tu.”

“Twende tukale kwanza, then utaoga halafu nikufanyie massage.”

“You can’t be serious.”

Tulikwenda kupata soup na Asmah aliendelea kuniuliza ni nini kinaendelea kati yangu na Iryn?. Sikuwa tayari kumwambia kinachoendelea, hivyo niliishia kumdanganya tu. Hakuishia hapo bali aliendelea kuniuliza kwanini pia hapatikani kwenye simu? Niliishia kumdanganya yuko likizo.

Baada ya kupata soup tulienda kuoga, kisha nikamuaga naondoka kwenda home, lengo langu nikajiandae na safari. Asmah alikuwa amelala kitandani sababu ya uchovu na kabla ya kuondoka nilimkiss shavuni.

“Umelala kwangu siku mbili, mke wako utamwambia nini?”

Asmah ni kama alinitonesha kidonda maana nilikuwa nimeanza kusahau;

“Amesafiri ndomana unaniona kwako.”

“Najikuta natamani sana kuwa na mtoto.”

“Kwahiyo unataka kunizalia mtoto?”

“I don’t know”

“Sawa! Mimi naondoka tutawasiliana mummy.”

“Si unarudi lakini.”

Sikumjibu bali nilimkonyeza kisha nikaondoka maeneo haya. Nikiwa njiani kuelekea home niliwaza nisajili line ya simu nyingine ambayo nitakuwa naitumia Dodoma lengo nisipatikane hewani kwa kipindi chote nitakachokuwa huko. Pia, sikutaka usumbufu kutoka kwa wazazi kuhusu sakata la mama J ndomana nikaona dawa ni kutopatikana tu.

Niliplan kumpanga sister mapema kuhusu hili suala kabla mambo hayaharibika, niliona yeye ndo mtu sahihi wa kulimaliza mapema ukizingatia wanapatana sana na wife. Nifikiri pindi nitakavyo fika home bhasi, jambo la kwanza niongee naye, japo atanimind sana, lakini sina jinsi.

Baada ya kurudi home nilipumzika kwanza maana nilikuwa na uchovu sana. Mchana mama wawili alinipigia simu, na alianza kwa kulalamika kwamba ni muda mrefu amekuwa akinipigia halafu sipatikani.

Baada ya maongezi mafupi aliomba niende kwake Madale tukaonane ili tuongee mambo muhimu. Sababu nilikuwa nina safari niliona busara niende ili nimuage kabisa, na nilimpa ahadi ya kwenda kwake jioni.

Saa 11 jioni nilitoka nyumbani kuelekea Madale kwa mama wawili, ilinichukua kama nusu saa kufika nyumbani kwake. Nilipaki gari, kisha nikaanza kuelekea ndani. Nilipofika kibarazani, baba wawili walitoka na kusema kwamba nipo chini ya ulinzi.

“Chini ya ulinzi? Acheni utani nina shida na mama Pili yupo?”

“Dogo tunavyokwambia upo chini ya ulinzi unakuwa unatuletea dharau sindio?”

Hapa walikuwa wa kali nami nikaanza kuona hawa jamaa wapo serious, binafsi nilijua ni utani na mmoja alikuja akanishika mkono.

“Nimefanya kosa gani mpaka mseme hivo?”

“Tukifika kituo cha Polisi utajua kosa lako.

Muda huu mama wa2 alitoka nje kibarazani huku mkononi kashika funguo ya gari na alitoa ishara ya kuondoka. Nilikuwa nahisi kama niko ndotoni, nilikuwa siamini kama ni kweli mimi Insider napelekwa Polisi.

ITAENDELEA KESHO
Pole ndugu wanaume tunapitia mengi
 
Kwakweli tuamini hivo tu af jmn jokes aside mtu gani pesa kwake zinamiminika yani gafla mume wa sista anaagwa juu kwa juu na mkewe wanaenda sauz anakubali fasta na milioni juu ha ha we insaida wewe unatudharau sana aisee
Kwakweli tuamini hivo tu af jmn jokes aside mtu gani pesa kwake zinamiminika yani gafla mume wa sista anaagwa juu kwa juu na mkewe wanaenda sauz anakubali fasta na milioni juu ha ha we insaida wewe unatudharau sana aisee
Kinachonishangaza ni huko kupewa pesa nyingi kila wakati ,tena bila kuvuja jasho
 
Back
Top Bottom