Ugwanzee
Senior Member
- Mar 7, 2024
- 137
- 225
si ww hapoAiseeee
Kumbe una dadako yupo hivyo!!! pole sana. Msaidie ujuavyo maana ni gangwe huyo dadaako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
si ww hapoAiseeee
Kumbe una dadako yupo hivyo!!! pole sana. Msaidie ujuavyo maana ni gangwe huyo dadaako
Watu Kama INSIDER MAN wanapaswa kupokea malipo kutoka jamiiforum.
Mods , Maxence Melo inakuaje hapa mtu kakamata hadhira zaidi ya mwaka na halipwi chochote kutoka kwenu?
Wengi tu hum tunaingia Jf mara Kwa mara Kwa ajili ya kuona Kama kuna mwendelezo.
Mtengeneza maudhui Kama huyu inafaa apewe chochote.
kwaio we.hapo shda nn aiseeKuna mmoja kaishi miaka mingi kdgo daslam anatupigisha stori mtaani vipande karibia vyote vya Insider Man afu anajifanya yeye aliyapitia haya namuenjoy tu kumtunzia heshima hahaha,
Kidogo kidogo nikinyataa nyataa,, ninatamaniiHuyu kichefuchefu 🤮🤮🤮🤮
Kosa kubwa unapenda kutoa ahadi hewa, acha kupromise kwa kutaka siku. Zinaumiza sana isipotokea wanawake ASILIMIA KUBWA na uwapunguzia mapenzi
Hajui kudanganya.. Though alijitahidi na eti wa zamani... Kosa zaidi.. Iryn sio mjinga Meneja
Hii kitu mwanamke alijua na kiuhakika deep ndaniiiii haisameheki kabisa, jua ipo imewekwa sehemu. Siku moja hatageuka so ujijue milele
Hongera tatizo haujakoma..
😂😂😂 Ukaona aibu kumbe unajua kubaunsi kei mbalimbali ila muogaaaaa
Jambo baya, bahati Iryn hakuweza wa 👂👁️ ila laweza semwa kistory na yoyote.. Ulitakiwe uwe smata kwenye hili
Wewe ni duh 🤣🤣🤣 maneno ya Sukari 😂😂😂
Mmmmh
Hapa umesahau!!!
Kumbe unajua kuweweseka 🤣🤣🤣🤣 hapo unakumbuka kukosa life anayokupatia.. Utafikiri unajiheshimu 😅😅😅
Haukomi na wewe ikija kei upo baba huruma sana.. Muhunwi
Sentensi hii ni muongo wewe.. Sema ndio hivyo Meneja una faida kubwa kwake. Ataendelea kujua juu ya Asmah. Wajanja wa chini hatusemi tunafanya nini kuyajua hata iwejeeeee..
Uongo
Muhunwi muhunwi tu damuni, ya A ingekushtua.
Oyooooo hii lazima 🤑🤑🤑 na Uzuri wake, ila haumpendi kutoka dipu moyoni.
Na Mary, Asmah na wengine haujawataja.
Hii 😂😂😂😂😂😂🤣🤣🤣🤣🥳🥳🥳🥳🥳🥳 Nimecheka sanaaaaa..
Uka nini? 😅😅😅😅 Si una wengine? Why haukupotezea. 🤣🤣🤣🤣🤣💃🏽💃🏽💃🏽💃🏽Ila ingekuwa labda amemumisi mchepuko hata wa kampani tu bila kwichi ningefurahia sana yaani business partner.
Iryn yupo smati sanaaa kupita unafikiri. Noti hili. Kuna mengi amepima akaamua maisha yaendelee.. Ila kuwa makini.. Na tulia.
Twasubiri ndoa zako tukupe Hongera.. Meneja. Mary Tamara, wivu.. atakuwa Prisca cha mtoto siku moja utatambua.
Haya maneno walisema wazee wazamani (ukiwa mjanja kuchapiwa ni Siri ya ndani )Na hata Insider akichapiwa mama J hawezi sema humu ndani ili mumcheke🤣🤣🤣 hiyo itabaki kuwa siri yake tuu, mtaona episode zijazo vile tiwst itakuja na mama J atabaki very clean hamtaamini.
Ndiyo nani?Cami halisi tumeshamjua now
Huwezi ku conclude au kumtumia insider kuwa Ndio maisha yalivyo. Insider Ana share experience yake na haiwezi kuwa hivyo kwa kila mtu, experience has to be lived.IRYN anaona Insider ndo mtu pekee wa kusimamia mali zake sababu jamaa ana
- Akili ya kusimamia biashara
- Hana Tamaa
- Intelligent
Vijana kuna vitu vingi sana vya kujifunza hapa, na wengi wetu tunasoma juujuu, jamaa ametupa code nyingi sana.
Insider ni mpambanaji, anzia pale alipoacha kazi na kuanza biashara ya Uber, ni wachache sana tungekuwa na huu uthubutu.
Amepitia ups & downs nyingi kwa Iryn, bado hakutaka kuwa mnyonge aliendelea na misimamo yake.
Yametokea matatizo kwenye kampuni, alikuwa na uwezo wa kuiba hela akasepa, lakini alikuwa mbele kuhakikisha kampuni inasimama. Jamaa kaenda Dodoma kuanzisha kampuni zake, hivi ungekuwa wewe ndo Iryn utamchukuliaje Jamaa?.
Mwanaume ukiweza kuwa na unique characteristics, hawa wanawake watakusumbua sana tena sana. Iryn ameona something unique kwa Insider hadi kamzalia mtoto. Mwanamke kwenye suala la kuzaa na mtu, huwa hawakurupuki asee, wako makini sana.
Rudi kwa suala la mama wawili, jamaa kasamehe kiroho safi na bado kampa zawadi binti yake. Yule dada yake Junior, anampango wa kumpeleka shule akasome.
Ni wangapi tuna moyo kama huu?,
Una maana gani hapa?Dada- Dada ❌
Kaka- Kaka ❌
Kaka- Dada ✅
Mama j,kaanza kuupiga mwingi,ila mwanangu insider muoe irene hapo ushaanza kuchitiwaSEASON 02
CHAPTER 37
“BY INSIDERMAN”
PART A
Siku ile nilipokutana na Asmah, nilimwambia kwamba afocus zaidi kwenye maisha yake. Nia yangu haikuwa kumuumiza au kumvunja moyo, bali nilihisi ni muhimu kukaa naye mbali kwa muda ili nirekebishe mambo kati yangu na Iryn. Pia, nilitamani Asmah apate nafasi ya kutafuta mtu ambaye atakuwa sahihi kwake, kwa maisha yake ya mbele.
Tangu siku ile tulipoonana, Asmah amekuwa akinipigia simu mara kwa mara na kuomba tukutane. Hata hivyo, mara zote nimekuwa nikimkatalia kwa visingizio vya kuwa na shughuli nyingi, nikimwambia nitamtafuta baadaye, lakini ukweli ni kwamba sijawahi kufanya hivyo.
Wakati nikiwa Tabora, tuliwasiliana na nikampa ahadi kwamba tutakutana Jumatatu mara tu nitakaporudi Dar ili tuzungumze na tuliweke sawa hili jambo. Niliporudi nyumbani, Asmah alinipigia simu mara nyingi, lakini sikujua kwa wakati huo kuwa alinitafuta sana. Kumbe, mama kijacho alikuwa anaziona simu na ujumbe wake kabla mimi sijapata nafasi ya kuona.
Katika kipindi hiki ambacho Iryn ni mjamzito, nilijitahidi kuepuka ugomvi wowote naye. Simu yangu kubwa mara nyingi nilikuwa namuachia kwa sababu sikuwa na chats zozote zenye utata. Mary, kwa upande mwingine, alikuwa anajua kinachoendelea, na tulikuwa tunawasiliana kwa kutumia namba mpya niliyokuwa natumia nikiwa Dodoma. Pia, Mary alishauri tuendelee kutumia namba hiyo mpya ili Prisca asigundue chochote kinachoendelea kati yetu.
Wakati nikiwa na Iryn pale sebuleni, simu ya Asmah ilipoita tena, Iryn alichoka na hali hiyo na akaamua kuipokea mwenyewe. Alionekana kushindwa kuvumilia zaidi, huku wivu ukiwa unamsumbua.
CONTINUE:
Mimi muda huu sikuwa na uwezo wowote wa kumzuia, hivyo niliamuacha aongee naye na aliweka loud speaker.
IRYN: “Asmah, habari yako.”
Asmah hakutegemea kwamba Iryn angekuwa ndiye anayepokea simu, na ghafla akawa mpole.
ASMAH: “Ooh! Bossy, habari yako.”
IRYN: “I'm good. What's your problem? You have been calling Insider nonstop."
ASMAH: “Alinambia yuko Tabora msibani, nilitaka kujua kama karudi.”
IRYN: “What is really going on between you and Insider? Please tell me the truth."
ASMAH: “Nothing is going on between us. He is one of my closest friends, and I really appreciate that."
IRYN: “Asmah, why are you doing this? I know you’re lying to me. Why are you disrespecting me like that? Fu**cking with my Man, and you know I’m pregnant with his child.”
ASMAH: "I didn't mean what I said."
IRYN: “You know I gave you all my respect, but you still sneak around and sleep with my Man. Usione nimenyamaza kimya, najua kila mchezo mnaocheza. Nilitegemea ungekuwa na heshima zaidi kwangu hasa baada ya mimi kuwa mjamzito, lakini hujali hata kidogo."
ASMAH: “What are you talking about.?”
IRYN: “Are you just pretending not to know what I’m talking about? You’re such a bad bitch, mpuuzi kabisa…..”
Nilipoona Iryn ameanza kupandisha hasira, ilibidi nimtulize na kumnyang’anya simu kwa sababu alikuwa amevuka mipaka. Alisimama kwa hasira, akaibamiza simu yangu kwa nguvu kwenye sakafu, na kisha akaelekea chumbani.
Nilishindwa kuelewa kwa nini Iryn alikuwa na hasira kubwa kiasi hiki, wakati Asmah hakuwa amesema chochote kibaya. Nilipoinama na kujaribu kuokota simu yangu, niligundua kwamba skrini ilikuwa imevunjika, betri ilikuwa imevimba, na sehemu nyingine zilikuwa zimeharibika. Nilimfata chumbani, lakini mlango ulikuwa umefungwa. Nilisikia sauti ya kilio kutoka ndani, na ilikuwa ni kilio cha maumivu makali.
“Baby, please fungua mlango.”
Nilianza kugonga mlango pale, lakini hakuonesha dalili za kufungua
“Baby, naomba tuongee. Tafadhali fungua mlango, mpenzi wangu."
Bado alibaki kimya na hakuzungumza chochote, aliendelea kulia kwa sauti kubwa. Hali hii ilinisababisha nijisikie vibaya sana, na niliona kama nimemkosea sana.
Niliamua kurudi seating room na kukaa kwenye sofa huku nikitafakari namna ya kutatua hali hii. Niliwaza kwa haraka nikaona ni busara niwe mpole na kumuomba msamaha ili kuepusha matatizo, ukizingatia hali aliyonayo kwasasa hatakiwa kuwa katika hali hii.
Ilipita nusu saa, lakini bado hakuonyesha dalili za kufungua mlango, na hapa nikaingiwa na wasiwasi kwa kuwa nilihisi anaweza kufanya jambo lolote baya. Nilimgongea tena, lakini hakutaka kufungua mlango. Hali hii iliponitatiza zaidi, nikaona ni bora nimtafute Claire kwa msaada, kwani sikuwa na jinsi nyingine ya kumsaidia Iryn.
Kumpata Claire ikawa ni shida maana simu yangu imezingua, nikaanza kuchanganyikiwa maana kuondoka na kumuacha peke yake mle chumbani ni jambo lisingewezekana kwanza ni hatari.
Baada ya kufikiri sana nikakumbuka home ninasimu nyingine ambayo inanamba ya Claire, hivyo nilimpigia simu mama J. Baada ya kumpigia alisema yuko chuo, hivyo ikabidi nimpigie Elena dada wa nyumbani na kumuelekeza.
Ndani ya dakika 5, Elena alinitumia namba ya Claire na bila kuchelewa nikampigia simu;.
MIMI: “Mambo, it’s me Insider.”
CLAIRE: “Hey! Insider mambo.”
MIMI: “Mambo mabaya shem wangu, naomba uje home haraka, please.”
CLAIRE: “Kuna nini? Iryn anataka kujifungua?”
MIMI: “Just come, please.”
CLAIRE: “I will be there soon”
Ndani ya dakika 15 Claire alifika na alikuwa akihema sana kama mtu ambaye alikuwa anakimbizwa, na alianza kuniuliza ni nini kinaendelea?
MIMI: “Claire, Iryn kajifungia ndani chumbani ni lisaa limepita, hataki kufungua mlango.”
CLAIRE: “Na hii simu vipi mbona imepasuka, mlikuwa mnagombana?”
MIMI: “Hapana, ni hasira zake ndo kaibamiza simu chini.”
CLAIRE: “Shem niambie ni nini kinaendelea ili nijue namna ya kuongea na Iryn, usinidanganye.”
MIMI: “Sikia Claire, huu sio muda wa kuanza kuulizana kinachoendelea, Iryn amejifungia na lisaa limepita, anaweza fanya jambo baya. Please, naomba unisaidie kuongea naye, ili afungue mlango, mengine tutaongea.”
CLAIRE: “Iryn, alikuwa analalamika sana, amekumiss, sasa umerudi mmegombana, mapenzi yenu siyawezi asee.”
Tuliongozana hadi mlango wa chumbani, na CLAIRE alianza kumuita Iryn kwa sauti ya upole. Baada ya kusikia sauti ya Cami, Iryn alijibu kwa hasira kwamba hataki kabisa kuniona mimi, na alitaka niondoke maeneo hayo.
CLAIRE: “Shem wewe ondoka, acha mimi niongee naye, akikaa sawa nitakupigia simu uje.”
Sikutaka kuwa mbishi juu ya hili, hivyo nilichukua funguo ya gari na kuondoka maeneo haya na akili yangu iliniambia nenda kwa Asmah. Saa yangu ilikuwa inasoma ni saa 10 jioni, nilihisi lazima Asmah atakuwa ofisini muda huu, nikaelekea moja kwa moja mpaka ofisini kwake.
Baada ya kufika nilipark gari parking ya nje kabisa na nikaingia ndani, nilikuwa niko spidi sana hata mapokezi sikusalimia. Nilimkuta Asmah yuko ofisini na moja ya mfanyakazi mwenzie na baada ya kuniona alisimama na kuja usawa wangu.
“Insider are you okay?.”
Sikutaka hata kuongea naye, nilimshika mkono na kuanza kuondoka naye pale ofisini, hata jamaa aliyekuwa naye alibaki akishangaa, kilikuwa ni kitendo cha haraka sana. ‘In a blink of an eye’.
Asmah alianza kulalamika pale,
“Wait, where are you taking me?”
Sikuwa hata nikimsikiliza muda huu, tulipofika nje ya geti nikampa ishara aingie ndani ya gari na akafanya hivyo, hata yeye alikuwa mpole na alianza kuogopa. Mlinzi alishuhudia lile tukio, lakini hakutaka kuingilia maana ananijua vizuri sana, hivyo alikuwa mpole.
Baada ya kuingia ndani ya gari tulianza kuangaliana na Asmah alionekana kuwa na wasiwasi sana;
MIMI: “Unajua kosa lako ni nini?”
ASMAH: “Insider, sikujua kama Iryn atapokea.”
Na nilimkatisha maongezi yake;
MIMI: “Umeniletea matatizo kwa mama kijacho wangu, unapiga simu wakati unajua fika naishi naye kwasasa na nilikupa taarifa mapema kuwa nitakucheki.”
ASMAH: “Insider, I’m really sorry, lakini haya yote wewe ndo sababu kaa ukijua hilo.”
MIMI: “Unamaanisha nini?”
ASMAH: “Umenichunia sana hadi najisikia vibaya, pale napokukumbuka.”
MIMI: “Mimi sijakuchunia kama unavyosema, ila nilikwambia kwasasa niache nifocus na maisha yangu. Kila siku nagombana na Iryn, juu yako, kwasasa sitaki haya yatokee ndomana nikakwambia vile. Pia, tambua natamani sana upate mwanaume atakayekupenda na kukuoa.”
ASMAH: “Stage niliyofikia, kukaa mbali na wewe ni ngumu. Insider nimekuzoea sana ujue, nawezaje kukaa mbali na wewe kwa yote uliyonifanyia?. Umejitoa sana kwangu, kipindi kile nimepata ajali, bado umenisaidia mambo mengi sana, najiona nina deni kwako.”
MIMI: “Huna haja ya kuwa na deni, sababu nilifanya toka moyoni na sihitaji unilipe. Asmah naomba utambue kwamba nakupenda sana, asingekuwa Iryn, huenda tungekuwa wapenzi na asingekuwa mama J, ningekuweka ndani kabisa.”
ASMAH: “Unataka kusema nini?.”
MIMI: “Upendo niliokuwa nao kwako, kwasasa umehamia kwa Iryn. Na sitaki kumpoteza kisa wewe, naomba uheshimu hili, yule ni mke wangu tayari na nitarajia kupata mtoto soon.”
ASMAH: “Hongera sana kwa kutarajia kupata mtoto soon.”
MIMI: “Please, move on kwa usalama wangu na wa kwako pia, tutaendelea kushirikiana kwenye mambo mengine, lakini tuwe na mipaka. Kwa mara ya kwanza leo Iryn, amepaniki live na ametoa maneno makali juu yako.”
ASMAH: “Hata mimi nimeogopa sana, kwa mara ya kwanza nazifeel hasira zake, na sikutoa neno lolote baya.”
MIMI: “Wasiwasi wake, mimi na wewe tuko kwenye mahusiano ya siri, kipindi hiki cha ujauzito amekuwa na wivu sana.”
ASMAH: “Sasa nafanyaje?
MIMI: “Mpigie simu, omba kuonana naye ili muongee juu ya hili, naamini atakubali muonane.”
ASMAH: “Insider mimi naogopa ujue.”
MIMI: “Mpigie simu sahivi, mwambie unataka kukutana naye, ukionana naye atatulia.”
Asmah alitoa simu yake mfukoni na akampigia Iryn, simu iliita bila kupokelewa, akapiga kwa mara ya pili, ndiyo kupokelewa na akamwambia dhumuni lake ni kuonana ili waongee na Iryn alimkubalia, akasema anamtumia location.
ASMAH: “Mimi naogopa siwezi kwenda.”
MIMI: “Sasa unaogopa nini?, nenda kajisafishe na unisafishe na mimi. Usikubali kitu chochote kile atakachokuuliza, wewe ni mtu mzima utajua utaongea nini.”
ASMAH: “What if kama anaushahidi kwamba we had sex.?”
MIMI: “I don’t think so, nafikiri kuna mtu kamjaza haya maneno, Iryn hana ushahidi juu ya hili.”
ASMAH: “Unajuaje kama hana evidence? Na ameongea vile mbele yangu.”
MIMI: “I know her, ingekuwa kweli anazo mimi ningejua tu, Asmah niamini mimi. You have to clean up the mess for me.”
ASMAH: “Sawa acha niende, kama kuna lolote nitakupigia simu.”
MIMI: “Nipigie kwa namba hii kama utapata shida, nitakuwa around.”
Baada ya kuachana na Asmah nilienda Cocobeach- Wavuvi kempu kutulia. Niliagiza heineken zangu mbili huku namsubiri Asmah. Muda huu nilitumia kuchat na Claire, nilimuuliza kuhusu maendeleo ya Iryn ana akasema yuko sawa, japo alilia sana. Nilimuuliza Iryn anafanya nini kwasasa, akasema amekaa kwa balconi na yuko na mgeni, nikajua ni Asmah wala si mwingine.
Kwa upande mwingine, Claire aliendelea kuniuliza shida ni nini, kwani hata Iryn hakuwa amemwambia sababu halisi ya ugomvi wetu. Nilimwambia aendelee kuwa mpole, na kwamba Iryn mwenyewe atamwambia tu chanzo cha ugomvi wetu.
Iryn ni mmoja wa wanawake ambao hawapendi kuweka maisha yao public, ni mtu ambaye anajali sana faragha ya mambo yetu ya ndani na hataki kuyaeleza kwa watu wengine. Hata kitendo kile cha kumpiga kule hotelin kilibaki kuwa siri yake pekee, hakuna mtu yeyote aliyemwambia kuhusu hilo.
Baada ya masaa mawili kupita na hakuna dalili za Asmah kunicheki, nilianza kuingiwa na wasiwasi. Nilijiuliza kwa nini anachelewa kutoka na nini kinaendelea?. Nilijaribu kufikiria kuhusu kumtumia ujumbe, lakini nikaona kwamba ilikuwa ni wazo baya.
Baada ya nusu saa, Asmah alipiga simu na kuniuliza nilipo. Nikamwambia aje Cocobeach tukutane. Ndani ya muda mfupi alifika Cocobeach na alisema yuko karibu na chupa ya Cocacola akinisubiri.
Nilitoka pale Wavuvi, nikamchukua Asmah, na nikaendesha gari kwa kasi hadi karibu na mitaa ya restaurant ya ‘Amigos’. Huko ndipo nilipokipaki gari na kuanza mazungumzo.
MIMI: “Nipe mrejesho wa mlichozungumza na mama kijacho.”
ASMAH: “Kila kitu kipo sawa kwasasa, nimeongea naye muda mrefu sana na amenielewa. Nimesema ukweli kwamba mimi na wewe tulikuwa kwenye mahusiano zamani wakati tumefahamiana, lakini tuliachana na kwasasa sisi ni marafiki.”
MIMI: “Una uhakika amekuelewa?”
ASMAH: “Trust me japo nimebanwa sana, juu yako. Alisema yeye yuko tayari kutuacha tuendelee na mahusiano, huenda yeye ndiye amedandia treni la watu. Nimemwambia Insider anakupenda sana na hayuko tayari kukupoteza na kila siku anajidai utamzalia mtoto wa kike.”
MIMI: “Umefanya jambo la muhimu sana, ahsante.”
ASMAH: “Nimekubali matokeo, japo nilikupenda sana naomba uendelee na Iryn, kwa heshima na wadhifa wake.
MIMI: “Leo ndo unakiri kuwa unanipenda sana?.”
ASMAH: “Ni kweli, kipindi umeanza mahusiano na Iryn nilikuwa naumia sana hujui tu.”
Simu yangu ilianza kuita na kuangalia ni Iryn alikuwa anapiga simu, nilimuonesha Asmah kuwa Iryn anapiga, naye akasema nipokee haraka. Baada ya kupokea aliniuliza niliko, nikamwambia niko Cocobeach, akasema nirudi home mapema.
Ilikuwa ni saa mbili usiku tayari, hivyo sikutaka kupoteza muda na nilimuaga Asmah kwa kumpa ahadi ya kuonana naye hivi karibuni na nikaondoka kurudi home.
Nilitumia muda mfupi sana kufika, kuingia ndani nawaona wamekaa sebleni, nami nikaketi pembeni ya mama kijacho. Wakati huu
Claire alikuwa akitabamu, kana kwamba kuna kitu anataka kuongea. Haikuchukua muda na aliaga anaondoka kurudi kwake, maana alikuwa na majukumu mengine ya kufanya.
Nilimpa kampani mpaka kwake na tukiwa njiani tulikuwa tunaongea na kubwa alisema, Iryn hajasema chanzo cha ugomvi wetu. Pia, aliendelea kusisitiza kwamba Iryn ananipenda sana. Baada ya kufika kwake, nilimshukuru sana kwa msaada wake na tukaagana pale, nami nikageuza kurudi home.
Baada ya kufika, Iryn alikuwa amekaa kwa balconi, hivyo nilienda na nikakaa pembeni yake. Palikuwa na hewa safi na upepo wa bahari ukipiga eneo hili kwa utulivu sana. Tulianza kuangaliana pale, nami niliamua kuvunja ukimya;
MIMI: “Nambie mke wangu, upo tayari tuongee?”
IRYN: “I’m listening.”
MIMI: “Mummy, mimi na Asmah hatuko kwenye mahusiano naku-apia kwa hili. Usipende kusikiliza maneno ya wabongo, hakuna anayependa kuona mimi niko na mwanamke mrembo kama wewe.”
IRYN: “Lazima niwe na maswali, kwanini Asmah tu, akupigie simu nonstop?. Mchana kabla ya kwenda lunch, alipiga simu mara 3 na bado akatuma message akilalamika sana kuwa unamtenga. Kwa haya yaliyotokea, na ninajua fika wewe na Asmah mlikuwa na historia unafikiri nitawaza nini?.”
MIMI: “Nakwambia ukweli, lastweek niliongea na Asmah akae mbali na mimi, na haya yote ni kwasababu yako, sikutaka uendelee kuwa na wasiwasi juu ya ukaribu wetu.
Ilibidi nimueleze ukweli kuhusu mipango yangu juu ya Asmah, ili aweze kuelewa na sikuona haja kumficha juu ya hili.
IRYN: “Unajielezea sana, nimekuelewa tuachane na haya.”
MIMI: “Baby, I don’t want another woman, and I”ll never disrepect you or my daughter like that.”
IRYN: “Unakumbuka tulikubaliana kwamba mtoto akiwa wa kike jina utampa wewe?”
MIMI: “Yes! Darling, unataka nikutajie jina kabisa?”
IRYN: “Don’t tell me hujaandaa jina bado.”
MIMI: “Niliandaa mummy, from today nitakuita ‘mama Ariana’, do you like the baby’s name?”
IRYN: “Yeah, it’s a beautiful name, and I like it. Thank you baba Aria.”
Furaha yetu ilirudi kama zamani na nilimwambia tuende chumbani tukalale maana muda ulikuwa umeyoyoma tayari.
Saa nne asubuhi nilitoka kwenda Mikocheni kuonana na Lucy, pia nilitamani sana tumalize tofauti zetu. Nilipofika pale ofisini niliweza kuonana na Lucy, bila kupoteza muda nilianza kumuomba radhi kwa kumkosea.
Lucy kwa upande wake alisema, aliumia sana kwa kitendo cha mimi kwenda Dodoma bila kumuaga wala kumtafuta, halafu nikawa nawasialiana na Hilda kwa siri, hiki ndo kilimuuma sana. Lucy, aliendelea kusema kwamba hakutegemea mimi ningemfanyia vile, ukizingatia sisi ni washikaji wa muda mrefu sana.
Ukweli nilikuwa nimemkosea sana, hivyo niliendelea kumuomba radhi na baada ya kumuelekeza sana dhumuni la mimi kufanya vile, hapa ndiyo aliweza kunielewa na kunisamehe.
Tulianza kuongea masuala mengine kwa ujumla na kubwa lilikuwa sakata la Asmah. Alinisisitiza sana kama nina mahusiano ya siri na Asmah, bhasi niache mara moja, kwani Iryn alimpigia simu na kulalamika kwamba anahisi kuna jambo linaendelea kati yangu na Asmah.
Baadae tulianza kuongea masuala ya ofisi maana landlord alikuwa ameanza kusumbua tuondoke, kwani alitoa taarifa mapema.
MIMI: “Iryn kaniachia hili suala nifanye maamuzi, wewe ndo manager wa hapa, unashaurije.?”
LUCY: “Hii location ilikuwa nzuri sana na imekaa kimkakati, tunapata wapi tena eneo zuri kama hili?”
MIMI: “Wateja wako wanaokuja hapa ni loyal customers?.”
LUCY: “Ndiyo na wageni wanakuja wengi sana.”
MIMI: “Nimewaza sana asubuhi nikaona ni bora ofisi ihamie Masaki. Tutaepusha cost nyingi sana, pia Masaki hatulipi pango bado pana nafasi kubwa ya kutosha.”
LUCY: “Kumbuka Mikocheni, tulitarget na wale wa kipato cha kati, tukihamia Masaki si tutawakosa hawa customers.?”
MIMI: “Bei zitabaki kuwa zilezile, na sikuzote mteja anafuata huduma bora, ukiwaambia tumehamia Masaki watakuja tu. Halafu, ijumaa tutakuwa na kikao asubuhi, fikiria hili vizuri na kesho unipe majibu ili tufanye maamuzi mapema.”
LUCY: “Sawa bossy, nipe muda nijifikirie juu ya hili.”
Baada ya maongezi marefu na Lucy, nilimuacha aendelee na majukumu yake huku mimi nikiendelea kukagua ofisi kwa ujumla.
Nilipigiwa simu na mama wawili, na wakati nilipoipokea, sauti ya Pili ilisikika. Alinisalimia na kusema kwamba nimewatenga sana, tofauti na zamani. Maneno haya yaliniuma sana, hivyo nikamuuliza yuko wapi. Alisema yupo ofisini kwa mama yake, na nikamwambia nitakuwa hapo baada ya lisaa.
Baada ya kumaliza ukaguzi, nilimuaga Lucy kisha nikaondoka kwenda ofisini kwa mama wawili. Nilipowapa taarifa kwamba nimefika, walikuja haraka, na Pili alinikumbatia mara tu alipoona.
Tulianza mazungumzo na mama wawili, ambapo habari kuu ilikuwa kuhusu mpango wa binti yake kusoma nje. Nilimuuliza Pili kama anaridhia kusoma nje, na alithibitisha. Baada ya hapo, nilimuomba Pili atupishe ili niweze kuzungumza na mama yake kwa faragha.
Mama wawili alifurahi sana kuniona na aliniuliza kuhusu agenda yangu Dodoma. Nikamwambia project nayoifanya kule na alinipongeza kwa hatua hii, kisha tukandelea na mazungumzo mengine kwa muda mrefu. Baada ya mazungumzo, niliomba niondoke na Pili na kumrudisha baadaye. Mama wawili hakuwa na tatizo na ombi hilo na aliniruhusu.
Niliondoka na Pili kwenda Mlimani na lengo langu lilikuwa kutimiza ahadi ya kumpa zawadi ya simu niliyomuahidi baada ya kumaliza shule. Pale Mlimani, nilionana na jamaa yangu, nikamwambia anipe bei ya iPhone 12, kisha nikampa nafasi Pili achague rangi ya simu anayoipenda. Ilikuwa ni surprise ambayo Pili hakutegemea, na alifurahi sana. Baada ya hapo, tukaenda kula pizza pamoja.
Jioni, nilimrudisha Pili kwa mama yake ofisini, ambapo mama wawili alifurahi sana na kunishukuru kwa zawadi niliyompa Pili. Baada ya hapo, nikaondoka kuelekea Masaki kuonana na Hilda ili nimpe taarifa kuhusu kikao kilichopangwa ijumaa.
Nilimshirikisha Hilda kuhusu mpango wa kufunga branch ya Mikocheni na kuwaleta Masaki, na yeye alikubaliana na wazo hili na kusema ni zuri. Nilimpa taarifa za kikao kilichopangwa na nikamwambia aandae ripoti zake vizuri ili aweze kujibu maswali pindi atakapoulizwa.
Muda ulikuwa umeenda, hivyo nikarudi nyumbani ili niwahi kumpikia mama kijacho. Mara tu baada ya kufika, aliniambia ana hamu ya kula chips na yai. Hapo hapo nikatoa simu na kumpigia Sele ili aandae sahani mbili na firigisi. Nikamuaga naenda kuzifuata, lakini akasema tuende wote, kwani amechoka kukaa ndani peke yake, hivyo tukaondoka kwenda kwa Sele.
Sele alishangaa sana kumuona Iryn akiwa mjamzito tena mimba kubwa, na alisema tuingie ndani tukae tusubiri kwani chips ziko jikoni. Iryn kwa upande wake, alisema anakulia palepale na aliagiza atengenezewe zingine za kuondoka nazo.
Baada ya Iryn kuingia ndani, nilibaki nikipiga story na sele;
SELE: “We mhuni unabalaa hujataka kuchelewesha, umemjaza upepo mrembo.”
MIMI: “Hata ile siku nakuuliza mahindi, yeye ndo alihitaji.”
SELE: “Bossy umetisha sana, unakojolea pazuri sana. Mwanamke kama huyu unapataje nguvu ya kuchepuka?.”
Tuliishia kucheka nami, nikaingia ndani kwa mama kijacho wangu ili tule.
Baada ya kumaliza kula, nilimlipa Sele pesa yake na alikata sahani mbili tu, moja alitoa offa kwa mama kijacho wangu, Iryn alifurahi na tukaondoka maeneo haya.
Baada ya kurudi nyumbani, Iryn alikwenda kulala, nami nilitumia nafasi hiyo kuwasiliana na Mary. Nilitamani kujua mpango wake wa kurudi Dar, na alisema kwamba anarudi kesho, Jumatano, pamoja na Jane. Alitamani sana tungeonana, lakini nilimkatalia na kumwambia avumilie hadi Jumamosi, kwani Iryn ataondoka hiyo siku.
PART B
Siku ya Alhamisi ile asubuhi, Iryn alinipa taarifa kuhusu ujio wa dada yake kutoka Ethiopia na alisema ataingia usiku sana. Nilimuuliza atafikia wapi? Akasema anafanya mpango ili afikie Sea cliff hotel.
Saa tano asubuhi, aliniaga kuwa anakwenda kwa mama Janeth kuonana na Jessie, hivyo nilimpa kampani ya ride hadi kwa mama, kisha nikaondoka kuelekea ofisini.
Nilikuwa nakazi ya kukagua hesabu za mauzo vizuri, kwani ni muda mrefu ulikuwa umepita pasipo kufanya ukaguzi. Niliweza kubaini matatizo madogo ambayo ambayo Hilda aliweza kuyajibia, hivyo nikaendelea kupitia ripoti na kuzicompile.
Saa 10 jioni, nilipigiwa simu na Iryn, kisha akaomba niende Mikocheni na alimpa simu jamaa ili anielekeze. Jamaa kunielekeza yalikuwa ni maeneo ya karibu na Shopperz, hivyo bila kupoteza muda niliondoka kuelekea huko.
Ndani ya muda mfupi nilikuwa nimewasili na jamaa alinielekeza hadi napark gari kwenye moja ya showroom ya magari. Sasa, baada ya kushuka ndiyo namuona Iryn na Jessie wamekaa na nikatembea mpaka usawa wao nikawasalimia.
Muda huu Jessie alikuwa ananiangalia tu, namimi nilikuwa namzingua pale;
IRYN: “Darling, follow me.”
Nilimfuata kwa nyuma, hadi ilikokuwa imepark Marcedes Benz.
IRYN: “Darling, hii gari ni nzuri? Unaionaje?”
MIMI: “Ni nzuri sana, halafu hii colour naona unique kwa benz.”
IRYN: “Mimi na Jessie wote tumeipenda.”
Alimuita jamaa ambaye ana asili ya uarabu na akamwambia aiotoe nje ili tuondoke nayo, na palepale aliomba account namba ili afanye malipo. Mimi nilikuwa sijui kinachoendelea kwakweli, nilihisi moja kwa moja gari ni ya Jessie.
Benz ilitolewa showroom mpaka nje kwaajili ya kuondoka, gari ilikuwa ni nzuri ikivutia sana. Aliniita akasema niache taarifa zangu kwaajili ya usajili, hapa sasa ndo nikahisi gari itakuwa yangu.
Sikutaka kubisha na nikafanya kama alivyosema. Jamaa aliahidi kwamba kesho kufikia saa 4 asubuhi kila kitu kitakuwa sawa, hivyo tukachukue plate namba. Baada ya malipo kufanyika, tuliondoka na Jessie akaondoka na ile Audi, wakati sisi tukaondoka na ile Benz. Uvumilivu ulinishinda na nikaanza kuuliza maswali;
MIMI: “Baby, bado sijui kinachoendelea kuhusu hii gari.”
IRYN: “Mimi kama MD, ofisi imekununulia gari ili iwe inakusaidia kwenye majukumu yako pamoja na ya ofisi.”
Niliishiwa hata niseme nini maana sikutarajia kuona Iryn akinifanyia surprise kama hii. Nilikuwa bado siamini kama kweli hii benz nayoendesha kweli ni yangu.
MIMI: “Baby nashukuru sana, hata sijui niseme nini kwahaya yote unayonifanyia. May God bless you.”
IRYN: “Kampuni ina imani kubwa sana na wewe, na hii ni moja ya shukrani yangu. Mimi bado sijakupa zawadi, ila nitaanza kwanza na nyumba mengine yatafuata.”
Tulienda mpaka kwenye apartment yetu, tukapark ile gari, kisha tukaondoka tena na Jessie kumrudisha kwa mama. Baada ya kurudi nilianza kuiangalia ile Benz kwa mara nyingine tena, jinsi ilivyo nzuri na kuvutia, na niliishia kutabasamu.
Kesho yake, ijumaa tulikutana kwaajili ya kikao kifupi ambacho kilihusisha viongozi tu, na tulifanyia pale Giraffe hotel, Mbezi Beach. Kikao kilianza saa 4 kamili asubuhi na kilihusisha watu sita tu, pamoja na Iryn.
Iryn alishukuru sana uongozi wa kampuni kwa kujitoa katika kipindi kigumu, hasa wakati ambapo hatukuwa na mawasiliano. Kama MD, aliahidi kuongeza mshahara kwa 30% kwa viongozi kutokana na kazi nzuri waliyofanya. Hakuishia hapo, aliongeza kuwa baada ya kikao, atatoa zawadi kwa wote.
Baada ya bossy kuongea, nilisimama kutoa taarifa ya mwenendo wa kampuni pamoja na kuifunga branch ya Mikocheni. Lucy na Hilda, walikuwa wanajua kinachoendelea kasoro wengine walikuwa hawajui, hivyo walibaki wakishangaa baada ya kuzisikia taarifa hizi;
IRYN: “Why? I didn’t expect you would come up with this bad idea.”
Nilianza kuwaeleza sababu ya kufanya maamuzi haya;
MIMI: “Tumejadili suala hili kwa undani pamoja na Hilda na Lucy. Tumeona kuwa gharama tunazolipa kwa pango ni kubwa sana, na kuongezeka kwa gharama za umeme, maji, vibali vya leseni na mamlaka nyingine ni mzigo mkubwa. Badala ya kutafuta ofisi mpya, ni bora wateja wetu wa Mikocheni waje Masaki. Hii itatusaidia kupunguza gharama nyingi na kuongeza faida kubwa. Kwa hivyo, tunataka ufahamu kuwa maamuzi haya tumeyachunguza kwa makini na hatuja kurupuka."
Baada ya kuwapa sababu ya kuifunga ofisi ya Mikocheni, kila mtu alinyamaza kimya akifikiria maana ni sababu ambayo ilimake sense vichwani mwao na baada ya dakika kupita, Iryn alianza kuongea.
IRYN: “Mnashaurije juu ya hili, lengo tupate maamuzi sahihi, kila mtu ajaribu ku-assess risks kabla ya kukubali haya maamuzi.”
Baada ya majadiliano ya dakika 20, kila mtu aliunga mkono wazo langu la kuhamishia branch Masaki. Bossy akatoa maelekezo tuanze taratibu mapema ili tusigombane na mwenye nyumba.
Ni kikao kilicho chukua masaa 2 na baada ya kumaliza, tulipata lunch ya pamoja bila kusahu kupiga picha za ukumbusho, nami nilitumia nafasi hii kupiga picha na mama kijacho wangu, kama ukumbusho wa ujauzito wake.
Baada ya kumaliza kila kitu, tuliwaaga na kuelekea Sea cliff hotel kuonana na dada yake ambaye aliingia Dar usiku sana, akitokea Ethiopia.
Tulipofika hotelini, tulimsubiri pale reception na haikuchukua muda alitoka na wakaishia kukumbatiana na Iryn. Dada yake yuko vizuri pia, sio wa kitoto ni mzuri kwelikweli, ila bado hafiki kwa Iryn.
IRYN: “This is Insider, my boyfriend. Do you recognise him?”
VIVIAN: “Of course I do. How are you, brother-in-law?”
MIMI: “I’m fine and happy to see you again."
Mkononi, Viviani alikuwa ameshika kimfuko kidogo na alimpa Iryn, naye akanikabidhi mimi na alinikonyeza, ile kuangalia ndani kuna nini, naona si simu, nikavunga.
Baada ya maongezi mafupi, tuliongozana mpaka parking ili tuondoke, njiani macho yote yalikuwa kwetu. Kwanza niliona ufahari sana kuongozana na wanawake warembo duniani, ni wanaume wachache sana wenye bahati kama hii.
Kwa upande mwingine Sister yangu alinipa taarifa kwamba yuko Airport na anatarajia kuingia Dar, jioni. Nilimpa taarifa Iryn na alisema tufanye booking ya room palepale Sea cliff hotel mapema.
Saa 10 jioni, tuliondoka kwenda JNIA kumpokea dada yangu. Iryn aligoma kabisa kubaki nyumbani na Vivian, alisema haitakuwa vizuri ikiwa nitakwenda peke yangu kumpokea dada yangu wakati yeye yupo
Baada ya kufika JNIA, tulikaa sehemu ya kusubiri abiria. Kama ilivyo kawaida, kila mtu aligeuka kumtizama Iryn kutokana na uzuri wake wa kipekee. Alikuwa kivutio maalum pale, akiwa na mimba yake.
Ndani ya nusu saa, sister aliwasili na waliishia kukumbatiana na wifi yake kisha tukapotea eneo hili. Tulianza kwanza kupitia Sea cliff hotel, ambapo tuliacha mabag yake, kisha tukaelekea home.
Apartment ilikuwa imechangamka sana maana walikuwa wanawake watatu wakipiga story, huku wakicheka. Mimi niliamua kuwapa space na nilienda kutulia chumbani nikipanga mambo yangu.
Nilitoa ile simu kwenye mfuko na ilikuwa ni Iphone 14 kama ileile aliyoivunja hadi rangi na niliweka laini yangu. Nilimpigia simu mama J kumpa taarifa kwamba kesho nitarudi, lakini ni kama aliipokea hii taarifa kwa kutojali.
Wakati huu, nilipata ujumbe kutoka kwa Asmah ambao ulisomeka anataka kuacha kazi, ilikuwa ni taarifa mbaya kwangu, hivyo nikampandia hewani. Nilimuuliza kwanini anataka kuacha kazi, akasema yeye ameamua hivyo kwani anataka kurudi shule kusoma. Nilifunga mazungumzo kwa kumpa ahadi ya kuonana kesho ili tuzungumze vizuri kuhusu suala hili, kwani ilikuwa ni ghafla sana.
Saa 2 usiku, tulitoka kwenda kupata dinner ya pamoja pale Karambezi Café. Wao waliendelea kuzungumza, na story zao nyingi zilikuwa zinahusu leba, wakati mimi nilikuwa nasikiliza kwa sikio la kuiba huku nikijifanya nipo bize na simu
Wakati naongea na dada yangu, nilimshukuru sana kwa kujitoa kwake na kukubali kwenda South Africa. Baada ya masaa mawili kupita, tuliagana ili wajiandae mapema kwa ajili ya safari ya kesho. Walielekea hotelini na sisi tukaelekea kwenye apartment yetu.
Usiku ulikuwa mrefu sana kwani nilikuwa nakazi ya mwisho kuhakikisha barabara inakuwa safi kwaajili ya mtoto kupita. Baada ya kazi ya muda mrefu, japo niliichafua sana, lakini mama kijacho aliridhika na kazi yangu na tukalala.
Asubuhi na mapema nilimuamsha ili tujiandae kwaajili ya safari. Baada ya hapo tuliondoka kuelekea Sea cliff hotel, ambapo tuliwachukua akina sister na tukaelekea Airport. Baada ya kuwasili pale JNIA tulipiga tena picha za mwisho kama ukumbusho, kisha tukachoma ndani.
Nilianza maongezi deep na Iryn na kubwa nilimtakia kila la kheri katika kuanza safari yake mpya ya kuwa mama na nilimpa ahadi ya kwenda South Africa kujumuika naye.
IRYN: “Baba Aria, nakupenda sana na naomba uheshimu hili. Kama nilivyokuahidi before, sitoweza kuwa na mwanaume mwingine zaidi yako, napenda sana nikuzalie mtoto mwingine baada ya huyu.”
Nilipenda sana kusikia akiniita Baba Aria na nilimshika mkono wake nikauweka pajani;
MIMI: “Wewe ni mke wangu tayari, nitaangalia namna ya kuwaoa wote, kuhusu watoto hata ukitaka dozen kwangu ni kazi ndogo.”
IRYN: “Promise me unakuja lini South?”
MIMI: “Mama Aria, ninaomba kwanza nikae na familia yangu, nime-mmiss sana mwanao Junior na mama J. Nitakuja before hujajifungua natamani niwe na wewe leba hadi unajifungua.”
Iryn alifurahi sana kusikia maneno matamu kutoka kwangu na tuliagana kwa kukumbatiana maana muda wa kucheck-in ulikuwa umewadia. Niliwaaga akina sister pamoja na Viviani na niliwaambia nitawaona soon, na kabla ya kuondoka Iryn alinikumbatia kwa mara nyingine tena.
Niliondoka pale JNIA nikiwa na furaha sana, na niliwasha gari kuondoka kurudi Masaki.
Baada ya kufika kwa apartment nilipark vizuri gari, Audi maana nilikuwa naiacha pale, kisha niliingia ndani kuchukua bag, pamoja na funguo za benz yangu, nikaanza safari ya kwenda home, Mbezi Beach.
Katika maisha yangu, hakuna siku niliwaza kama nitakuja kumiliki benz, lakini ndoto yangu ilitimia kwa kuendesha benzi kali. Barabarani nilikuwa mdogo mdogo sana, kama vile namuendesha bibi harusi. Baada ya kufika home, nilimpigia simu Elena akatoka kunifungulia gate.
Junior alikuwa amesimama kibarazani akishangaa gari, kwani anapenda sana magari na baada ya kuniona baba yake, alikuja spidi nikamnyanyua juu. Na alianza kulilia aingie ndani ya gari, bhasi nilimfungulia mlango akaanza kunyonga steering.
Kwa upande mwingine, nilishtuka kuona gari yangu nyingine siioni na baada ya kuuliza, Elena alisema mama J kaondoka nayo. Niliuliza kwani anajua kuendesha? Akanijibu ndio ni mwezi sasa anaiendesha, nilibaki nikishangaa.
Nilifurahi kusikia wife amejua kuendesha gari, kwani ilikuwa ni hatua nzuri kwa upande wetu. Nilikuwa nimechoka sana pamoja na usingizi, hivyo nilienda chumbani kulala. Kwa bahati mbaya sikuweza kulala mapema sababu Junior alikuwa akinisumbua sana.
Jioni, baada ya kuamka niligundua kwamba mama J karudi na nilienda seblen kukaa, lakini nilimsikia akiongea na simu huku akicheka kwa mbali. Nilitulia pale seblen nikishangaa TV na zilipita dakika tano, bado mama J anaongea na simu. Nilihisi haya si maongezi ya kawaida na nilisogea mpaka dirishani kusikiliza, maana alikuwa kasimama pale kibarazani.
Na aliendelea kuongea, tena kwa sauti ya chini, haya ni baadhi ya maneno aliyokuwa anajibu;
“Ndiyo, najua… ah, nimekumisi sana
Wewe pia unajua jinsi unavyonifanya nijisikie… usijali, nitakutafuta muda"
Tutaonana tena, usijali.
Baada ya kuona amemaliza kuongea na simu, nilirudi chumbani kwa spidi ya kunyata ili asinishtukie. Baada ya dakika 5 alirudi chumbani na nilijifanya nimelala, aliweka simu chaji akaondoka. Niliamka kwa lengo la kuikagua simu yake, kwa bahati mbaya alikuwa kabadilisha passcode, hivyo nikawa sina option nyingine.
Nilipata wazo nikague mkoba wake, na nikaona kuna risiti za Samakisamaki, Elements, KFC na nyinginezo. Nilianza kukagua za KFC zilionesha tarehe ya leo, za Elements zilionesha ni weekend iliyopita, lakini kilicho nishangaza zilionesha zimeprintiwa saa 4 usiku.
Nilibaki najiuliza mama J sio mtu wa marafiki wala kutoka out, huku Samakisamaki, Elements alikuwa na nani?. Huyu mtu waliokuwa wanaongea wote kwenye simu ni nani? Hapa sasa nikahisi kuna SOMETHING FISHY kinaendelea.
ITAENDELEA
Wanawake Hawaoni shida ku-share high value man.Unamsifu Mary ana akili ila naona ni bint mpumbavu hana akili kwa sababu kwanza mwanaume wa mdogo wake yaani X unaombwa vipi kuzaa na mwanaume ambae ana mwanamke kama mkewe wana mtoto bado ana mwingine ana mimba yake na wote hajaoa anaomba uzae ina maana atakuwa single mama malezi ya mama tu sio na baba kwa pamoja 😂ilitakiwa akatae hapo hapo ibaki anadinywa basi ila kwa alivyo mpumbavu atabeba mimba.
Insider ni kama wanaume wengi walivyo malaya sijui Mrangi sio kwa kupenda papa huko halafu roho mbaya ubinafsi kutaka kumzalisha bint wa watu unaharibu future yake huna mpango wa kuowa gonga tu upite sio uzalishe halafu hujifunzi kutokana na makosa.
Afanye hesabu aone asilimia ambazo wanawake wanafanya matukio Kama hayo na wanaume Ni ngapi kwa ngapi, wanawake mnaacha wanaume ama waume zenu mara ngapi kisa tu akatokea mwenye mbolea zaidi. Yaani nyie mnatufanyia haya Ila nyie mkifanyiwa mnaumia mno Mana unajua ladha ya mnachokifanya.Mfano wewe ndio ungekua dada yake mwandishi; kwa situation aliokua nayo kaka yako UNGEFANYAJE?
Dada yeyote anafanya hivyo kwa ajili ya kumlinda kaka yake. Wengine wamechukua watoto wa nje wa kaka zao wanawalea. Linapokuja swala la Kaka na dada au mama na mtoto hawa watu lao linakuwa moja. Wako tayari kubebeana dhambi.Dada yuko kwenye wakati mgumu sana, mwisho wa siku damu ni nzito kuliko maji. Na hii ndo maana ya ndugu wa shida na Raha.
Aiseeee
Kumbe una dadako yupo hivyo!!! pole sana. Msaidie ujuavyo maana ni gangwe huyo dadaako
We kiumbe umeshindikana ila najua kama una kaka wa baba mmoja na mama mmoja lazima utasimama na kaka yako kwenye matatizo yake.
As if story Iko present ni ishu inayoendlea SAS😂Nitafurahi sana siku nikiskia Mama J amepigwa mtungo.
INSIDER MAN aumie,alie