Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

Jinsi biashara ya Uber ilivyonikutanisha na dada huyu mrembo wa ajabu

SEASON 02:
A TRUE STORY BY INSIDER MAN

CHAPTER 01:

CONTINUE ……….
Simu yangu ilianza kuita pale na alikuwa ni Mama J akipiga na nilitabasamu kuona simu yake na niliipokea.

MIMI: “Baby nakuja kukuchukua turudi home na tukapate dinner ya pamoja.”

MAMA J: “Mbona ghafla sana na hujanipa taarifa mapema? na vipi kuhusu Junior atakaa na nani?”

MIMI: “Hutakiwi kuyakimbia matatizo inatakiwa ujue namna ya kuyakabili, siku kama bibi yake hayupo utafanyaje?.”

MAMA J: “Si unajua kesho natakiwa kureport chuo?“

MIMI: “Tutaongea haya” na nikakata simu.

Muda huu nilikuwa nawaza vitu vingi sana kichwani pale parking, ukweli moyo wangu ulianza kuumia kuona Iryn ananiacha na niliingiwa na wivu mkubwa sana juu yake, yaani nilitamani sana aendelee kubaki Dar. Nilikuwa siamini kama kweli Iryn anaondoka na ananiacha, nilihisi kama ndoto.

Wakati niko kwenye dimbwi la mawazo ujumbe uliingia kwenye simu yangu na ulitoka CRDB Bank ukionesha kiasi cha pesa kimeingizwa kwenye account yangu. Ni Iryn alikuwa kafanya muhamala, nilitabasamu na niliwasha gari nikaondoka kwa fujo sana pale JNIA.

Niliendesha gari kwa kasi sana barabarani kuelekea Boko kwa mama J, sasa wakati niko mwenge mataa, simu yangu ilianza kuita na ilikuwa ni namba mpya lakini haikuonekana kuwa ngeni kwangu na sikutaka kujiuliza sana na nikapokea simu.

“Hi Insider”

“Prisca”?

“Yes ni mimi, usinambie ushafuta namba yangu.”

“Hapana, nakusikiliza unashida gani?”

“Insider naomba kuonana na wewe please! please!.”

“Kuna nini Prisca, huwezi ongea kwa simu?”

“Ndio, ndomana nikaomba tuonane nakuomba sana.”

“Ok, nitakujulisha when and where.”

“Thank you, msalimie Junior.”

“Sawa zitafika usijali.”

Baada ya kuzungumza na Prisca nilijua fika huyu anaomba appointment na mimi lakini lazima litakuwa suala la mahusiano wala sio jambo lingine. Kwa upande wangu nilijisemea msimamo wangu utabaki ni uleule sitaki kujihusisha naye tena kwenye mahusiano ya aina yoyote ile.

Saa 1 usiku nilikuwa nimewasili pale ukweni na nilifungua gate nikaingiza gari ndani na bahati nzuri Junior alikuwa kibarazani anacheza peke yake. Baada ya kushuka kwa gari nilikwenda moja kwa moja nikambeba na yeye aliishia kufurahi na tukazunguka upande wa mbele.

Upande wa mbele kulikuwa na shemeji zangu wawili (Dada yake wife pamoja na mamdogo wake) wanakaanga maandazi. Ilikuwa ni muda sana toka tuonane na dada yake hata yeye alivyoniona aliishia kutabasamu, niliwasalimia wote na nilichukua andazi moja nikaanza kulila taratibu.

SHEM: ”Shem karibu…”

MIMI: “ Leo kama zari nimekuotea maana ni kitambo hatuonani.”

SHEM: ”Nipo sema tunapishana, naona unazidi kunawiri nipe siri ya mafanikio shem.”

MIMI: “Siri ya mafanikio muulize mdogo wako atakwambia.”

Na muda huu mama J alikuwa katoka nje,

SHEM: “Haya bhana karibu ndani shem, usiishie nje.”

MIMI: “Hapahapa nje panatosha tuendelee kupiga story, kwanza sikai sana maana nimekuja kuwabeba hawa warudi kwao.”

SHEM: “Mbona haraka hivyo na huyu mtoto mtafanyaje?”

MIMI: “Shem wewe usiwe na wasiwasi mama J anajua kila kitu.”

MAMA J: “Kwani ndo tunaondoka sahivi?”

MIMI: “Nimekwambia muda sana niko njiani ila hujawahi kuwa serious, anza kutoa vitu mimi nikusaidie kupeleka kwa gari tuondoke.”

SHEM: “Shem uko moto sana sijakuzoea hivi.”

MIMI: “Hahahaa sitaki wenye nyumba wanikute na hii ndo mida yao ndomana unaona niko moto, kwanza unakuja lini kwetu?”

SHEM: “Nitakuja shem kuwasalimia niyaone na makazi mapya.”

Tuliendelea kupiga story mbalimbali pale na utani mwingi mpaka mama J alivyomaliza kutoa vitu vyote na kuweka kwa gari ndo nikawaaga pale na sisi tukaondoka.

Wakati tumeingia kwa gari Mama J alianza kuniangalia sana na alionesha mtu ambaye anakitu cha kuongea na alikuwa anatabasamu, kwa upande wangu sikuwa hata nataka kumwangalia kabisa na yeye alianza kuongea,

WIFE: “Bae mke mwenza ameshaondoka tayari?”

Nilishtuka kusikia wife akiongea haya maneno ilibidi nimwangalie muda huu,

MIMI: “Mke mwenza kivipi? Sio bossy wangu tena?”

WIFE: “Hujanijibu swali kaondoka?”

MIMI: “Mama J maswali yako sometimes kama mtoto hata Junior atakuja kukuzidi, angekuwa hajaondoka ungeniona hapa? ndio ameondoka si alikuaga lakini?.”

WIFE: “Ndio aliniaga ndo kakuachia na gari?”

MIMI: “Hapana gari ya mama yake hii nitairudisha.”

Muda huu niliwasha gari na tukaanza safari,

WIFE: “Sawa na huyu Junior tunamfanyaje?”

MIMI:?“Junior asikupe shida twende kwanza sehemu tukae then tuanze maongezi.”

Niliendesha gari mpaka Whitesands hotel na tukaenda moja kwa moja mpaka restaurant kwaajili ya kupata Dinner, tuliagiza chakula na maongezi yakaendelea.

Tuliongea mambo mengi sana na kubwa nilimwambia sitaki kuona anakwenda kwao hovyohovyo bila sababu ya msingi maana haileti picha nzuri. Na kuhusu mtoto tulikubaliana nitakuwa ninakwenda naye kazini huku tukiendelea kufanya mawasiliano na Elena. Tulikubaliana kama Elena atarudi itabidi tuangalie namna ya kumpeleka shule hata akasomee fani yoyote ili iwe kama shukrani yetu kwake.

Hatukutumia muda mwingi sana hivyo tuliamua kuondoka kurudi home kulala na baada ya kuwasili home Asmah alinipigia simu kunijulia hali na nilimwambia itabidi tukae kikao next saturday na team kutoka salon zote. Baada ya kuzungumza na Asmah nilimtafuta Iryn ili kujua kama amefika salama lakini hakuwa online, hivyo nikajisemea atanitafuta akiwa online na mimi nikalala.

Jumanne tulikuwa tumeanza mwezi novemba ile asubuhi kama kawaida mapema niliamka na nilikwenda tizi baada ya kurudi nilikuta mam J akimwandaa mtoto ili tuondoke maana yeye alikuwa anakwenda chuo. Baada ya kupata breakfast tuliondoka na safari ilikuwa kumpeleka kwanza Mama J chuo na baada ya kumdrop mimi na Junior tuliamua kwenda ofisini Mikocheni.

Ndani ya dakika chache tulikuwa tumewasili pale ofisini na nilikwenda ndani kuendelea na ratiba zangu. Muda huu nilijikuta nam-miss Iryn hivyo nilitoa simu mfukoni nikampigia lakini hakuwa online. Nilianza kupatwa na wasiwasi why toka aondoke jana hajanitafuta wala kunipa taarifa yoyote? What’s really going on? na nikamtumia ujumbe ukisomeka,

"Hey baby, just wanted to check in and see how your journey to South Africa is going. I have been thinking about you and hope everything is going well. Let me know when you have a chance. Miss you!"

Haikuchukua muda Lucy akaingia ofisini na baada ya kumuona Junior aliishia kufurahi na alimbeba.

LUCY: “Insider mambo umekuja na mchumba wangu leo.”

MIMI: “Fresh tu, sikujua kama utakuwepo hapa nilijua utakuwa chuo.”

LUCY: “Nishakamilisha taratibu zote nasubiri timetable tu na lecture zianze kuchanganya.”

MIMI: “Vizuri, this weekend tutakuwa na kikao sijui unaratiba?”

LUCY: “Ndo unaniambia hapa now but haina shida na kitafanyikia wapi?”

MIMI: “Asmah atakucheki juu ya hili mtapanga nyie.”

LUCY: “Siamini Iryn kama kweli kaondoka.”

MIMI: “Bado unaota sindio?

LUCY: “No nakuonea huruma wewe utakuwa lonely.”

Ilibidi nicheke afu nikanyamaza na nikapotezea hii mada maana Lucy alianza kuvuka redline

MIMI: “Lucy chuo utakuwa unakwenda muda gani?”

LUCY: “Jioni saa 11, hakuna kitakachokuwa kinaharibika bossy.”

MIMI: “Sawa nakubali manager wangu.”

Hii siku nilishinda pale Mikocheni kwa upande wa Junior aliishia kuzurura mle ndani na nje na uzuri alikuwa anacheza na dada zake hivyo ilikuwa burudani maana walitokea kumpenda.

Mchana Iryn alinipigia simu kupitia whatsapp video na tuliongea kwa muda mrefu sana, kubwa aliniahidi mwezi huu mwishoni atakuja Dar kwa ajili yangu maana hawezi kukaa muda mrefu bila kuniona. Tuliongea mambo mengi sana likiwemo suala la yeye kuanza clinic pamoja na kuwapa taarifa wazazi wake kuhusu suala hili la mimba.

Baada ya kuongea na Iryn sikutaka kuendelea kupoteza muda pale ofisini, hivyo nilimuaga Lucy na sisi tuliondoka kwenda Mlimani city kupoteza muda huku tukiendelea kumsubiri mama yake atoke chuo. Junior hakuwa msumbufu kabisa kwanza ndo alikuwa anaona raha kuzurura na baba yake, haya mambo yeye ndo anatakaga unaweza kaa naye siku nzima na huwezi msikia akiulizia mama wala kulia.

Usiku mida ya saa mbili Hilda alinipigia simu na muda huu nilikuwa nimekaa nje kibarazani na nilivyoiona simu yake nilishangaa sana maana ndo ilikuwa mara yake ya kwanza ananipigia simu usiku. Nilihisi atakuwa na shida hivyo niliipokea simu yake,

MIMI: “Hi Hilda za wewe.”

HILDA: “Safi Bossy, umepotea sana.”

MIMI: “Hapana nipo something wrong?”

HILDA: “Hapana nikasema nikusalimie pia nashukuru kwa kunichagua kuwa moja wa ambao tutapewa mafunzo.”

MIMI: “Usijali dear, tuko pamoja bado unakaa na Asmah?”

HILDA: “Ndio but nishapata kwangu tayari.”

MIMI: “Ooh hongera sana, umepata wapi?”

HILDA: “Morocco hapo by next week nitahamia.”

Baada ya kuona hana jambo la muhimu niliamua kukatisha maongezi,

MIMI: “Hongera sana kesho tutaongea vizuri, bye uwe na usiku mwema.”

Niliamua kukatisha maongezi maana muda ulikuwa ni usiku japo alionekana kuwa na maongezi zaidi na mimi.
*****
Asubuhi nilikwenda ofisini Masaki nikiwa na Junior kama kawaida na baada ya kufika pale ofisini team ilikuwa imewasili na baadhi walioniona waliishia kushangaa sana kuniona na mtoto. Kwa upande mwingine Hilda alikuwa pale reception na tukaanza story hata yeye alishangaa sana kuniona na mtoto uvumilivu ulimshinda ilibidi aniulize,

HILDA: “Bossy huyu ni mwanao? yaani mmefanana balaa huwezi kubisha hili.”

MIMI: “Hahaha mwanangu ndio, Junior kamsalimie mamdogo.”

HILDA: “Hongera sana so HB.”

MIMI: “Asmah kafika?”

HILDA: “Yeah yuko ndani.”

MIMI: “Sawa ngoja nikamuone afu nitarudi, pia jana kuna jambo ulitaka kuongea dizaini kama ulikuwa unaogopa kusema, leo utasema.”

HILDA: “Hahahaha sawa wewe nenda kwanza ukirudi tutaongea, utanikuta na dogo hapa.”

MIMI: “Angalia ni mtundu sana huyu, hachelewi kuchafua hali ya hewa.”

HILDA: “Nitam-mudu.”

Niliingia ndani na nilimkuta Asmah akionekana kuwa busy sana na baada ya kuniona alikunja laptop yake na tukasalimiana, nikakaa kwenye coach. Haikuchukua muda Asmah naye akaja akakaa kwenye coach na tukaanza story pale.

MIMI: “Nambie Bossy wangu.”

ASMAH: “Safi nimefurahi kukuona Insider, Iryn mzima?

MIMI: “Acha unafiki unataka kusema hajawasiliama na Iryn?”

ASMAH: “I did.”

MIMI: “So unanichora tu hapa. Aya niambie kikao cha weekend umepanga kifanyike lini? na wapi?”

ASMAH: “Siku iwe jumamosi ila place bado sija confirm but soon nitakupa update.”

MIMI: “Sawa mummy, nilitamani sana leo kuja kulala na wewe sema unaishi na Hilda.”

ASMAH: “Wewe Insider? akili yako iko sawa kweli?”

MIMI: “Kinachofanya uone akili yangu haiko sawa ni nini?”

ASMAH: “Insider yaani navyokuogopa kwasasa hivi naanzaje kulala na wewe?”

MIMI: “Ooh vizuri kama kweli umeanza kuniogopa na bado utaendelea kuniogopa zaidi, ngoja niwasalimie akina Rebby.”

Nilianza kuondoka pale na nilisikia akiniita

ASMAH: “Insider….umechukia?”

Nilitabasamu nikamkonyeza na nikafungua mlango nikatoka kwenda reception kwa Hilda lakini sikumkuta na niliamua kwenda kuwasalimia akina Rebby na niliwakuta wanacheza na Junior.

MIMI: “Hilda nilikuwa nakutafuta wewe kumbe umekuja huku.”

HILDA: “Mwanao ni mtundu sana hataki kushikwa kumuachia kaja huku.”

REBBY: “Insider kuanzia leo mimi nitakuwa mkwe wako, una mtoto mzuri hivi asee.”

MIMI: “Naona unaweka odda mapema ya kuwa lishangazi kwa mwanangu ausio.”

Kila mtu aliishia kucheka baada ya mimi kuongea hivi,

REBBY: “Jamani mbona mapovu?”

MIMI: “Thubutu.”

Nilimuacha Rebby akinisikitikia na niliondoka reception na tuliendelea mazungumzo yetu na Hilda.

MIMI: “Ongea sasa nataka kuondoka kama unaona aibu niandikie text.”

HILDA: “Hamna kuna kitu nilitaka kuomba but naona mapema sana.”

MIMI: “Ongea tu, usiwe na wasiwasi.”

ASMAH: “Nilikuwa nataka kuomba mkopo ili ninunue baadhi ya vitu nikahamie kwangu.”

MIMI: “Uko sahihi ni mapema sana kwakweli, ulitaka mkopo wa kiasi gani?”

HILDA: “Million 1 tu.”

MIMI: “Fanya hivi ongea na Asmah mshikaji wako akudhamini, hili litawezekana. Kama atakubali bhasi utanijulisha sawa?.”

HILDA: “Sawa haina shida nitaongea naye badae.”

MIMI: “Ok see you then.”

Niliondoka na Junior na safari yetu ilikuwa ni kuelekea kwenye apartment ambayo tulikuwa tunakaa na Iryn kabla hajaondoka na nilitakiwa kuikakabidhi apartment. Baada ya kuwasili maeneo yale nilikwenda moja kwa moja ndani na nilifungua makabati ya chumbani na kulikuwa na vitu ambavyo aliviacha kama viatu, nguo skin jeans, mikoba handbags na vitu vingine kibao.

Wakati nikiendelea kumsubiri Dalali kwa upande mwingine simu yangu ilianza kuita na ile kucheki ni mama Janeth alikuwa akinipigia simu. Nilipokea na tuliongea mambo mengi sana pamoja na utani mwingi, dizaini kama alikuwa anajua mimi ni mkwe wake tayari. Mama alinambia tuonane badae kuna mambo anataka tukazungumze nikiwa pamoja na Asmah.

Baada ya kuongea na Mama Janeth nilimpigia video call Iryn na uzuri alikuwa online na alipokea kwa haraka sana,

“Hi baba mtoto, I was thinking about you.”

“Unaendeleaje na mwanangu?”

“We good, nakuona upo na mwanangu Junior na nishaanza kuwa-miss”

“We miss you too, niko hapa kwa apartment naona kuna vitu ulisahau nikuwekee au?”

“No afu nilisahau kukwambia, hivyo viatu baadhi utampa Sumaiya, hizo skin mpe Hilda na Jack niliwapa ahadi, hizo handbags juu yako kama utampelekea mke mwenza au utazigawa.”

“Sawa baby.”

“Okay darling bye.”

Baada ya kuagana na Iryn kwa upande mwingine Dalali alikuwa kafika tayari hivyo tulifanya makabidhiano ya apartment na tukaagana pale na sisi tukaanza safari ya kurudi home.

Niliwasili home mapema sana na nilikuwa nimekaa kibarazani na muda huu nilikuwa nawaza namna ya kuzitumia pesa alizonipa Iryn. Nilikuwa nahitaji umakini wa hali ya juu sana kwenye hili jambo, niliwaza kumpa mtaji mama J kwenye biashara yake ya M-pesa na Tigopesa ili aanze kufanya na miamala ya Bank. Pia nilipata wazo kabla sijafanya haya maamuzi lazima kwanza nijue mipango yake ili nione kama naweza mpa pesa au laah.

Niliingia jikoni kwaajili ya kupika chakula cha mtoto pamoja na cha kwetu maana wife alikuwa hajarudi bado. Kwa upande mwingine Junior alikuwa nje anacheza na mtoto wa jirani yetu ni wa kike na mkubwa kidogo kwa Junior.

Saa moja usiku ndo muda ambao tulikwenda kwa mama Janeth pamoja na Asmah kuitikia wito. Baada ya kuwasili kwake tulikaribishwa ndani lakini tulikuta mama ana wageni hivyo ilitubidi tumsubiri kwa pale nje kibarazani mpaka amalize. Mimi sikuwa na story kabisa na Asmah muda huu na yeye alianzisha story,

ASMAH: “Insider are you okay?”

INSIDER: “Yeah kuna tatizo?”

ASMAH: “Seem hauko sawa, sorry kama nilikukwaza ile asubuhi ulikuwa utani tu.”

INSIDER: “Wasiwasi wako tu, mimi niko sawa.”

Akanisogelea karibu,

ASMAH: “Insider bado una deni kwangu.”

INSIDER: “Deni gani tena?”

ASMAH: “Kutoka out bado sijasahau ile siku uliyonizingua.”

INSIDER: “Hahahaa unawezaje kutoka out na mtu unayemwogopa?”

Maongezi yetu yalikatishwa baada ya mama Janeth kutokea,

“Wanangu poleni nafikiri tukae hapa wote na mazungumzo yetu tufanyie hapa au mnaonaje mtakuwa comfortable?”

“Hakuna shida mama hapa pametulia sana.”

Tulianza maongezi yetu pale kuhusu kuongeza mishahara kama alivyoahidi pamoja na suala la mafunzo. Mama alisema mtu atakayetoa mafunzo anatarajia kuwasili Dar jumapili hii na mafunzo yataanza jumatatu as planned.

Tuliongea masuala mengine mengine kuhusu kampuni pamoja na safari zake anazotarajia kuzianza soon za kwenda huko Ukraine na US. Kwa upande wake alisema atakuwa busy sana hivyo anatutegemea sana kwenye kusimamia hii kampuni.

Nilimwambia mama nimeleta na gari yake ambayo niliachiwa na Iryn lakini mama alisema ile gari sio yake bali yeye alimkabidhi Iryn kuwa mali yake hivyo niendelee kuitumia.

MAMA: “Mwanangu hio gari mimi nilimpa Iryn kuwa na amani endelea kuitumia nafikiri hata yeye anapenda ukiendelea kuitumia.”

MIMI: “Mhh hapana mama hakuwahi nambia hili, hii gari kwangu ni gharama siwezi kuimudu naomba niiache hapa.”

MAMA: “Kama ni gharama za mafuta hili ondoa shaka, sipendi haya magari yaendelee kukaa hapa yanaharibika bila sababu ndomana niliamua kumpa hio gari Iryn.”

MIMI: “Sawa mama nimekuelewa kama ni hivyo basi nitakuwa nakuja kuichukua mara moja moja lakini sio kukaa nayo, hapa kwako usalama upo.”

MAMA: “Nitaongea na Iryn akiridhia sawa ila kwasasa endelea kuitumia.”

Tuliagana na mama Janeth pale kwake na sisi tukaondoka na wakati tunatoka Asmah alisema tukapate dinner ya pamoja na atalipia.

MIMI: “Muda umekwenda Asmah tutatoka next time.”

ASMAH: “Unanipa lift mpaka home au niliquest uber?”

MIMI: “Fanya kurequest nataka niwahi home leo nimechoka sana.”

Japo alionesha kutofurahishwa na majibu yangu lakini sikuwa na jinsi. Nilipark gari pembeni tukiendelea na story na yeye alikuwa akisubiri usafiri.

ASMAH: “Insider una bahati sana yaani mpaka unalazimishwa kubaki na gari, mbona hii nyota wengine hatuna.?”

INSIDER: “Unataka kuwa na nyota ya aina gani? na huu uzuri wote ulionao huoni kama Mungu alikupendelea?”

Asmah ilibidi acheke maana hakutegemea kama ningempa jibu la namna hii,

ASMAH: “Kama mimi ni mzuri na Iryn aseme nini?”

INSIDER: “Seems hujiamini na hujikubali, ngoja leo nikwambie ukweli Asmah. Ukianza kujikubali hutakuwa unalalamika kwangu hutongozwi, sometimes unajiweka local sana mpaka uzuri na thamani yako inapotea. Embu mcheki mtoto Hilda anavyotupia viskin jeans na zinavyomkaa, mtoto kiuno huko, inshort anajipenda.”

Asmah alikuwa kimya kwa muda ni kama nilikuwa nimemchana ukweli, na dizanini alianza kuwa na aibu.

ASMAH: “Ushaanza kumtamani Hilda?”

INSIDER: “Nimekupa mfano namna anavyojipenda but you can do better than her you’re so beautiful.”

Asmah alinyamaza kimya ni kama alipatwa na aibu ghafla, na muda huu simu yake ilianza kuita na alikuwa ni dereva wa uber, alimuelekeza tulipo na baada ya uber kuwasili tuliagana na mimi nikaondoka kuelekea home.

Wakati niko njiani nilikumbuka suala la Prisca kuomba tuoanane na nikakumbuka kumpigia simu dogo ili anipe report ya upelelezi aliofikia mpaka sasa. Nilifanya mawasiliano na majibu niliyopata ni kwamba kwasasa hakuna taarifa yoyote maana vyuo vilikuwa vimefungwa na hajamuona Prisca kwa muda sana maeneo ya kule. Nilimsisitiza dogo aendelee na uchunguzi wake na pindi atakapopata taarifa mpya bhasi anijulishe na nilimwambia nitamtumia muamala sio muda mrefu.

*********
Jumamosi ya week ya kwanza ya mwezi November ilikuwa ndo siku ya kikao chetu na kubwa ilikuwa ni kwaajili ya kupeana majukumu mapya na kutambulishana management mpya ya kampuni.

Niliamka asubuhi na mapema kama kawaida nilikwenda jogging na baada ya kurudi na kujiandaa niliamua kwenda Mbweni kumsalimia Jane. Baada ya kuwasili pale home nilimkuta Jane na mama yake wako seblen na wageni. Niliwasalimia na mimi nilitoka nje kwenda kuangalia maendeleo ya mbwa wangu na walionekana kukua kwa kasi sana.

Baada ya dakika 10 nilisikia Jane akiniita na aliomba tukae garden ili tuongee, Jane akiniona huwa anafurahi sana na mimi kama kawaida yangu matani huwa siachi.

“Nakuona shem wangu unazidi kuwa mzuri.”

“Hahaha jamani huoni nilivyojichokea hapa shem.”

“Naona mambo si muda mrefu yatakuwa hadharani, na wanasemaje maendeleo.?”

“Yaani doctor anasema muda wowote tu naweza kushusha, nikianza kusikia dalili niwahi kwenda hospital.”

“Na wewe unampango wa kujifungulia wapi?”

“Rabininsia palepale naona ni pazuri.”

“Ukianza kuona dalili nijulishe mapema ili nije nikupeleke, sawa shem?”

“Usijali Insider, nashukuru sana kwa kunijali najua huyu mtoto atakupenda sana.”

“Hilo halina ubishi, mimi nilikuja kukujulia hali, pia nimekuja na vyakula vya mbwa na kama utahitaji kitu kingine nambie nikuletee.”

“Usiwe na wasiwasi kama kuna lolote nitakujulisha shem wangu.”

Niliendelea maongezi na Jane kuhusu masuala mbalimbali ya maisha na yeye alisisitiza sana akijifungua lazima afungue biashara kama tulivyokuwa tumepanga before. Jane alikuwa yuko hoi sana yaani alikuwa ni mtu ambaye anahesabu siku za kujifungua cha ajabu alikuwa anazidi kung’aa.

Niliagana na Jane na mimi niliamua kurudi kwanza home kupumzika na wakati nimefika home nilistaajabu sana kuona pale uwanjani nina park gari 3 (Audi, Dualis na ist). Nikajisemea Jane akijifungua tu nitamkabidhi gari yake na hii audi jumatatu lazima niirudishe kwa mama Janeth.

Wakati bado niko nje kibarazani nikiendelea kuwaza ghafla nilisikia Junior akiniita akitokea kwa jirani na akaja kwangu ameshika remote ya gari yake na alikuwa ananipa huku ananivuta. Mimi nilishamsoma anataka nikamwendeshe na nilikwenda mpaka kwa gari yake nikaanza kumwendesha pale, baada ya dakika kadhaa akaja rafiki yake wa kike naye akakaa pembeni nikaendelea kuwaendesha.

Baada ya muda nilisikia mtu akiniita “Jirani” na ile kugeuka alikuwa ni dada na tukasalimiana pale,

“Jirani habari yako.”

“Salama sana jirani, karibu niko na madogo hapa.”

“Nilikuja kumchukua huyu binti yangu ili akale ila kwasasa hawezi kubali.”

“Hapa itabidi uwe mpole hawezi kukuelewa, hongera una bint mzuri kama wewe.”

“Hahaa ahsante sana jirani hata wewe una kijana mzuri, si unaona bint yangu kila muda anamtaka Junior hahahaa. Toka uhamie hapa nakuonaga kwa mbali pia huonekaniki, karibu sana.”

“Ahsante sana jirani, nimekuwa na mambo mengi sana toka nihamie hapa lakini tuko pamoja, bila shaka mama yake Junior mmeonana.”

“Mama J tunaonana daily maana haipiti siku sijaja kwenu au yeye kuja kwangu kumuilizia mtoto.”

“Binti yako anaitwa nani?”

“Joana”

“Bhasi kuanzia leo nitakuwa nakuita Mama Joana.”

Tulishia kucheka wote pale na kila mmoja aliondoka na mtoto wake kuingia ndani maana nilikuwa nataka nipumzike before ya kwenda kwenye kikao Mikocheni.

Saa 12 jioni niliondoka kuelekea Regency hotel mikocheni kikao chetu ndo kilikuwa kinafanyika pale na nilikuwa nje na muda. Baada ya kuwasili na kuingia ndani, timu yote ilikuwa imewasili tayari nilikuwa ni mimi tu nasubiriwa ili kikao kianze.

Kikao kilianza na ni Asmah aliyeinuka na kuanza kuongea maana yeye alikuwa ndo katibu wa hiki kikao.

“Team habari za jioni kabla ya kuendelea naomba tufungue kikao chetu kwa sala.”

Baada ya sala Asmah aliendelea kuongea,

kama mnavyofahamu leo ndo kikao chetu na Agenda zote za kuhusu hiki kikao zinajulikana, hivyo mimi nitazungumza machache na mengine atazungumza manager wetu.”

Baada ya Asmah kumaliza kuongea alinikaribisha ili niweze kuzungumza na mimi sikutaka kupoteza muda nilianza kuongea.

Team habari yenu, nafurahi kuwaona kwa mara nyingine mkiwa mmependeza sana. Julieth hongera umependeza kushinda wote humu ndani.”

Waliishia kucheka na wote walifurahi baada ya kuongea haya maneno..

Guys sitaki tupoteze muda hapa ila dhumuni kubwa la hiki kikao ni kujadili kuhusu kubadilika kwa uongozi kama mlivyosikia kikao kilichopita bossy wetu Iryn kaenda masomoni, mama yetu pia atakuwa busy sana. Agenda ya pili itakuwa kuzungumzia suala la kuanza kwa mafunzo jumatatu na mafunzo yatakuwa pale kwa mama Janeth kwake hivyo wale mliochaguliwa zingatieni hili. Agenda yetu yetu ya tatu itakuwa ni kuhusu Sacoss yetu pamoja na kutoa maoni, ushauri na mapendekezo mbalimbali kuhusu kampuni yetu.”

Baada ya ukimya kadhaa niliendelea kuongea,

Ninaanza kutaja majina ya viongozi wenu na utaratibu uliotumika, tumezingatia uzoefu pamoja na elimu. Kuanzia leo Asmah ni HR wa kampuni matatizo yote ya kiofisi pamoja na yale binafsi mtakuwa mnamwona yeye na msaidizi wake atakuwa Hilda. Lucy atabaki kuwa manager wa branch ya Mikocheni na msaidizi wake atakuwa Julieth. Mimi Insider nitakuwa top manager hasa kwenye masuala ya fedha na maendeleo yote yanayohusu kampuni kwa ujumla.”

Niliongea masuala mengine mengi sana kuhusu maendeleo ya Saccos yetu bila kusahau mikakati na malengo ya kampuni. Baada ya kumaliza kuongea tulikaribisha maswali, maoni na ushauri na kila mmoja alifunguka kwa upande wake.

JULIETH: “Manager muda wa kumaliza mafunzo ni saa ngapi? na je tutatakiwa kwenda na nini? na kwa mama Janeth tunafikaje maana wengine hatukujui.”

ASMAH: “Muda wa kumaliza mafunzo ni saa 12 jioni na suala la chakula liko chini ya ofisi, pia tunaandaa bajeti ya nauli kwa ajili yenu lakini bado hatujafikia muhafaka na mama, baada ya hiki kikao tutakwenda kujadiliana naye na nitawapa mrejesho.”

MIMI: “Afu kuhusu vitu ya kwenda navyo, msiwe na wasiwasi mtavipata kulekule. Naona tumalize kikao chetu na tusubiri dinna ya pamoja then tutaondoka kurudi makwetu.“

Wakati tukisubiri dinna pale story za hapa na pale zilikuwa zikiendelea pamoja na kupiga picha za pamoja kwa upande mwingine Iryn alikuwa akinipigia sana simu lakini sikutaka kupokea simu zake muda huu maana haikuwa sehemu sahihi ya kufanya maongezi.

Nilianza kupiga story na Hilda pale na mimi kama kawaida yangu nilianza kumzingua.

MIMI: “You look great today kama Kim K.”

HILDA: “Thank you bossy, hata wewe pia.”

MIMI: “Ushahamia kwako? nataka nije nilale kwako.”

HILDA: “Tayari, wewe karibu tu muda wowote.”

MIMI: “Unanihakikishia usalama wangu lakini?”

Hilda alianza kucheka,

HILDA: “Yeah why not?”

Baada ya dakika 10 chakula kilikuwa tayari na baada ya kumaliza kula mimi na Asmah ilibidi tuage team na tuliondoka kwenda kwa mama Masaki.

Ilituchukua muda mfupi sana kuwasili Masaki kwa mama na baada ya kukaribishwa ndani seblen ilimchukua dakika 5 mama kutoka ndani na tukaanza maongezi. Mama alisema trainer atawasili kesho akitokea Canada na mafunzo yatafanyikia palepale kwake floor ya juu ya nyumba yake. Suala lingine tulilojadili ni kuhusu nauli na posho kwa watakao hudhuria hii training na tuliona 50,000/= kwa siku ingependeza zaidi.

Yalikuwa ni mazungumzo ya kama lisaa kasoro na tuliagana na mama pale tukaondoka maeneo yale. Asmah hakuwa na mood ya kurudi home mapema hivyo alianza kunishawishi tutoke out na muda ulikuwa unasoma saa 3 usiku tayari.

ASMAH: “Insider si tunatoka out? Sijisikii kabisa kurudi home mapema hivi.”

INSIDER: “Si kuna Hilda kule home? atajiskiaje ukimwacha alone na umetoka out.”

ASMAH: “Hilda kashahamia kwake toka juzi.”

Wakati nikiendelea kujifikiria hili ukweli sikuwa na mood na mzuka wa kutoka out, na nilikuwa najifikiria kwa hili. Kwa upande wake simu yake ilianza kuita,

“Insider Iryn anapiga simu.”

MIMI: “Pokea ongea naye.”

Na mimi nilihisi tu Iryn anapiga simu kwa Asmah sababu mimi sipokei simu zake na nilimwambia Asmah aweke loudspeaker.

ASMAH: “Hi bossy.”

IRYN: “Fine, za wewe?”

ASMAH: “Safi dear.”

IRYN: “Sound great, upo ofisini?”

ASMAH: “Hapana tumetoka mapema sana leo maana tulikuwa na kikao.”

IRYN: “meeting? mbona sina hizi information?”

ASMAH: “Insider atakuambia nafikiri.”

IRYN: “Okay! na mmeshamaliza kikao chenu?”

ASMAH: “Yeah ni 30mns zimepita na mimi narudi home hapa. Nambie bossy wangu ushaanza masomo?”

IRYN: “Ndio kipenzi nakujulia hali mpenzi.”

ASMAH: “Thank you bossy mimi niko poa.”

Baada ya kumaliza mazungumzo Iryn alikata simu na Asmah alinigeukia akaanza kuongea,

ASMAH: “Insider nipeleke home nikalale.”

MIMI: “Umeghairi kutoka tena?”

ASMAH: “Wewe nipeleke tu sina hamu tena ya kutoka.”

Ilibidi nicheke kinafiki maana simu ya Iryn ni kama ilimpa warning juu ya next move aliyokuwa anaitaka kuifanya.

Tulielekea na usawa wa Toure road mpaka tunafika kwake cha ajabu njiani kila mtu alikuwa kimya na hakuna aliyekuwa anamwongelesha mwenzie. Asmah alishuka kwenye gari akaniaga na mimi nikaondoka kurudi home sikutaka kupoteza muda kabisa na saa yangu ilikuwa inasoma nne kasoro za usiku.

Nilirudi na Mwaikibaki road na baada ya kufika Nakiete pharmacy ilibidi nishuke ili ninue dawa ya mafua kwaajili ya Junior. Wakati niko mle ndani pharmacy simu ilianza kuita na alikuwa ni bossy lady akipiga sababu nilikuwa natoa maelezo kwa doctor sikutaka kuipokea simu yake, nikajisemea huyu nitaongea naye kwenye gari. Simu iliendelea kuita na kukata na aliendelea kupiga kwa fujo sana lakini sikuwa na nguvu ya kupokea simu yake maeneo haya.

Baada ya dakika 3 doctor alirudi na dawa na akawa ananipa maelekezo pale namna ya kutumia dawa kwa mtoto. Wakati natoka mle ndani kwenda parking kwaajili ya kuondoka simu yangu iliita tena na mara hii alikuwa anapiga kwa simu ya kawaida na baada ya kuingia kwa gari niliipokea simu yake.

IRYN: "Darling, why didn't you pick up my phone?"

MIMI: “I'm sorry, I was in a meeting and couldn't answer at the time.”

IRYN: “Why didn't you tell me?”

MIMI: “I apologize for not informing you earlier but everything is going well.”

IRYN: “Whenever I need to talk to you, you don't answer my calls on time. What’s wrong with you?”

Mpaka nafika home alikuwa analalamika sana na mimi niliendelea kumbembeleza na kuwa mpole maana sikupenda awe vile ukizingatia ana ujauzito. Baada ya kufika home nilipark gari pembeni maana sikutaka kuingia ndani ili niendelee kuyajenga na Iryn na tulikuwa tumeanza maongezi mengine.

MIMI: “So, baby mimba inazidi kukua na huwezi kuendelea kuhide ni bora ukawaambia wazee mapema before it’s too late.”

IRYN: “Mama yangu mdogo nimesha mpa taarifa tayari ila mzee bado hajui soon nitaongea naye, but kuna jambo nilitaka kukwambia ila ni busara tuongee tukionana.”

Muda huu simu ya Mary ilianza kuingia na mimi baada ya kuona Mary akipiga nilipoteza kabisa network.

MIMI: “Sawa baby.”

IRYN: “Baby good night see you tomorrow I love you”

Baada ya Iryn kukata simu ndo napata akili na kuanza kujiuliza hivi Iryn amesema kuna jambo la kuongea, hivi kwanini sijamuuliza ni jambo gani?. Nilianza kujilaumu lakini ikabidi niwe mpole na muda huu simu ilianza kuita tena ni Mary alikuwa akipiga. Ukweli niliona aibu hata kuipokea simu yake maana toka aondoke sikuwahi kuongea naye wala kumpigia simu na text zake sikuwa na jibu.

MIMI: “Mary..”

MARY: “Hi Insider, finally leo umepokea simu yangu.”

MIMI: “Nisamehe rafiki yangu, toka uondoke nimekuwa busy sana then nasahau kukurudia, umesharudi tayari?”

MARY: “Yeah nimerudi jana dear.”

MIMI: “Umerudi na zawadi yangu?”

MARY: “Yeah you know I do care about you.”

MIMI: “Thank you ukisema hivyo utafanya nijisikie vibaya mummy.”

MARY: “Kesho unaratiba gani? maana niliwishi sana nikuone maana nimekumiss sana.”

MIMI: “Sure kesho tutaonana usiwe na wasiwasi.”

MARY: “Nimefurahi kusikia hivyo byee Insider kesho tutaongea mengi tukionana. Angalia whatsapp kuna ujumbe wako.”

Baada ya kuagana na Mary na mimi nilifungua haraka whatsapp kuangalia Mary katuma nini?, damn alikuwa kanitumia picha zake akiwa amewaka sana na nikagundua Mary nje na kuwa Kenya pia alikwenda Europe. Niliishia kuziangalia zile picha kwa tamaa za kifisi na nikaingia ndani maana nilikuwa nimekaa pale nje kwa zaidi ya lisaa.

Baada ya kuingia ndani niliingia kuoga kwanza na nilirudi sebleni kuongea na mama J kuhusu suala la dada wa kazi wamefikia wapi? maana alisema kufikia jumatano Elena angekuwa amerudi lakini haikuwa hivyo.

Kutembea na Junior kila angle nilianza kuona ni mtihani maana Junior ni mtundu sana ukizubaa sekunde tu humwoni machoni pako, hivyo alikuwa anahitaji uangalizi wa karibu sana. Na pia sakala la kuanza kwa mafunzo jumatatu nilikuwa nahitajika kuwa karibu sana na mazingira ya ofisini, kuwa na Junior ingekuwa tatizo.

“Baby vipi kuhusu suala la dada umefanikiwa kuwapigia simu?”

“Nimetoka kupiga simu sio muda hapa lakini hazipatikani zote mpaka baba yake.”

“Aisee sasa hii hatari so tunafanyaje? maana kumpeleka shule huyu ni mdogo sana kwa umri wake.”

“Mama ananitafutia dada mwingine so tuwe na subira maana tukiharakisha tunaweza pata dada mbaya ikawa tatizo.”

“Jumatatu nitakuwa busy sana afu siwezi kwenda na Junior na wewe unakwenda chuo.”

“Nitaongea na bibi yake asubuhi nitakuwa nampeleka afu jioni navyotoka chuo nitakuwa napitia kumchukua.”

“Sipendi tumsumbue mama anashinda pia kwenye biashara zake huu mzigo ni wetu.”

“Dada yangu pia yuko home so hakuna tatizo hata yeye alikuwa tayari kukaa naye uzuri Junior sio mtoto wa kulialia.”

“Pia maendeleo ya biashara zako yakoje?”

“Maendeleo mazuri baba J, dogo wa bajaji hana shida kule dukani nako hakuna shida.”

“Una mpango gani na biashara zako

Baada ya kumsikiliza niliona anamipango mizuri sana na nikaona kuna haja ya kumpa pesa ili aongezee na uwakala wa bank hasa CRDB na NMB, japo sikumwambia chochote.

Mama J aliondoka kwenda chumbani na mimi nilibaki pale seblen nikiangalia match ya Barcelona. Baada ya dakika 15 nilisikia mlango ukigongwa na nikasimama kwenda kufungua, nilijua lazima atakuwa jirani. Baada ya kufungua mlango nilipigwa na butwaa kubwa sana na sikuamini nayemuona mbele yangu muda huu,

CHAPTER 02[emoji116]
Aisee
 
SEASON 02
CHAPTER 41

“BY INSIDER MAN”

CONTINUE:

Kwa upande wangu, sikutarajia hata kidogo kukutana na mama mkubwa. Niliposogea, nilimsalimia kwa heshima. Alinijibu kwa upole, kisha akaniangalia kwa makini, macho yake yakitua pia kwa Aria aliyekuwa kamshika. Sekunde chache zilivyopita, alinitazama tena na kusema kwa sauti tulivu, “Umefanana sana na mtoto.” Kabla sijapata nafasi ya kujibu, Mama Janeth naye alidakia, akinitazama kwa tabasamu na kusema, “Ni kweli kabisa, mnafanana sana wewe na Aria.”

Niliishia kutabasamu baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa mama mkubwa, kisha nikatafuta sehemu ya kuketi. Sebleni palikuwa na wageni wengi sana, hali iliyonifanya nijisikie kutokuwa na utulivu, lakini sikuwa na namna. Nilibaki pale, nikijaribu kuzoea hali ile, huku nikionesha utulivu ambao sikuwa nao ndani yangu.

Baada ya dakika nyingi kupita, niliamua kwenda chumbani kwa Iryn ili kumsalimia na kumjulia hali. Nilipofika, niligundua hakuwa peke yake, alikuwa na wageni wawili. Niliwasalimia wote kwa heshima, na bila kusita, Iryn alinitambulisha kwa marafiki zake akisema, “Hawa ni marafiki zangu, tumesoma nao chuo Ufaransa.”

Nilimuuliza Iryn kuhusu maendeleo ya kidonda chake, na aliniambia kuwa anaendelea vizuri kabisa. Tulipokuwa tunaendelea kuzungumza, ghafla Jimmy aliingia chumbani. Mara tu Iryn alipomuona, uso wake ulibadilika kabisa.

JIMMY: “Hata ukininunia, freshy tu."

IRYN: “Jimmy, nakuchukia sana!"

JIMMY: “Hujaanza leo, na sishangai kabisa.”

IRYN: “Jana ulimpeleka wapi Insider?”

Jimmy alinitazama kwa wasiwasi, akihisi labda nimemueleza Iryn kuhusu tulikokuwa usiku huo. Nilimpa ishara kuwa sina ufahamu wowote juu ya jambo hilo.

JIMMY: “Sawa, tulienda Soho kuburudika, na tulirudi salama."

Iryn, akiwa amekasirika, alitazama pembeni na kuona bakuli karibu yake. Alilichukua kisha akamrushia Jimmy kwa hasira, huku akimfyonza kwa dhihaka.

Na wakati huu, Amara aliingia chumbani na kuanza kuuliza, “Shida ni nini?" Jimmy, kwa haraka, alimnyanyua juu juu na kutoka naye hadi sebleni. Lilikuwa tukio la ghafla na la kufurahisha, kiasi kwamba kila mtu aliishia kucheka, hata wageni.

Niliamua kuondoka chumbani ili kumpa Iryn nafasi na wageni wake. Hata hivyo, wakati nilipokuwa natoka, ghafla nilisikia akiniita kwa sauti ya upole, “Subiri kidogo...”

IRYN: “Darling, where are you going?”

MIMI: “Nipo mke wangu, huna haja ya kuwa na wasiwasi.”

IRYN: “Usije ukanitoroka kama jana ulivyofanya.”

MIMI: “ Leo nipo na wewe baby.”

Baada ya kurudi sebleni, nilitambua kuwa watu watatu hawakuwepo, nao ni dada yangu, Vivian, na Samantha. Nilipouliza, niliambiwa kuwa walitoka kwenda supermarket kununua vitu kwa ajili ya mama mtoto.

Baada ya takriban saa moja, mzee Virgil aliwasili na familia yake yote. Ilikuwa siku ya kipekee kwani niliweza kuwafahamu wadogo zake wote kupitia mama mdogo, kasoro kaka yake ambaye mzee alimzaa na mwanamke mwingine.

Mchana tulikula chakula cha pamoja, ambacho kiliagizwa kutoka kwa wapishi wa nje. Baada ya lunch, mama Janeth alitusalimu na kutuaga, akituambia kwamba anaondoka kwa safari ya kwenda Tanzania, kisha ataendelea na safari yake kwenda Marekani (USA).

Kabla ya mama Janeth kuondoka, tulipata nafasi ya kuzungumza. Nilimshukuru sana kwa kujitoa kwake na kuhakikisha Iryn anajifungua salama. Mama Janeth alinituliza, akisema kwa upole, “Iryn ni binti yangu, huna haja ya kunishukuru kwa hili.”Maneno yake yalikuwa ya faraja, yakiniondolea wasiwasi.

Jioni nilikutana na dada yangu, na tukatafuta sehemu tulivu kwa ajili ya mazungumzo yetu. Mara tu baada ya kuketi, dada alianza kuzungumza kwa hisia, akilalamika kuhusu tabia zangu mpya ambazo nimeanza kuonesha waziwazi mbele ya mama J. Aliuliza kwa upole lakini kwa msisitizo, “Kipindi kile ulipolala nje, ulikuwa wapi?” Akiongeza kwa tahadhari, alisema, “Na kama utathubutu kunidanganya, itakuwa ndio mwisho wa maongezi yetu.” Maneno yake yalikuwa na uzito, yakinifanya nifikirie kwa makini kuhusu majibu yangu.

Niliwaza pale na kuamua ni bora niwe mkweli ili tuweze kumaliza mambo haya.

MIMI: “Nilikuwa na mwanamke mwingine.”

SISTER: “Una matatizo gani? Tuliongea vizuri kabisa kuhusu haya, lakini bado unaendelea kuyafanya. Je, unanidharau mimi dada yako? Nilitegemea utaanza kufocus na watoto wako, lakini unazidi kuhangaika na wanawake wengine?”

MIMI: “Dada yangu, najua nimezingua. Mwanamke huyu alinifata Dodoma mwenyewe, na kipindi kile nilikuwa nimegombana na mama J, na Iryn alikuwa hana dalili za kurudi.”

Majibu yangu yalimfanya dada yangu aonekane mwenye wasiwasi zaidi, lakini pia nilijua ni muhimu kuwa mkweli ili kuweza kuendelea mbele.

SISTER: “Nisikilize kwa makini, bro. Usinione kama mjinga kukusaidia na kesi zako za kila siku ambazo unafanya kwa makusudi. Leo nakupa onyo la mwisho, kama una wanawake nje na hawa mama watoto wako, nikaja kupata kesi, utakuwa umefunga kufuli la mimi kukusaidia.”

MIMI: “Dada yangu, usifike huko, nimekuelewa na sitokuangusha.”

SISTER: “Na kilichofanya uondoke bila kumuaga mama J ni nini? Unaonesha dharau kama hizi kwa mke wako.”

MIMI: “Mimi naondoka tumegombana kwa sababu alimpigia mama yangu simu na kumwambia nililala nje. Niliona ananichonganisha na mama yetu, kwa kitu ambacho hana ushahidi nacho.”

SISTER: “Unataka kuachana na mama J, kisa Iryn?. Ukitaka mambo yako yaanze kuharibika tena, bhasi jichanganye ufanye huo ujinga unaotaka kuufanya, utayakumbuka maneno yangu.”

MIMI: “Siwezi kumuacha mama J, hili nakuapia dada yangu.”

Baada ya kumaliza tofauti zetu, dada aliniahidi kunisaidia kuliweka sawa suala la Iryn. Alinishauri nisubiri mtoto afike miezi sita ndipo nianze hatua za kuwaambia wazazi. Alisema ni bora nianze kumshirikisha mzee, na kisha yeye ndiye atakayemwambia mama. Maneno yake yaliniweka katika hali ya matumaini, kwani nilijua kwamba kwa msaada wake, naweza kupata njia sahihi ya kukabiliana na hali hii.

Dada alinionyesha mbinu ya kuanza kumuandaa kisaikolojia mama J, akisema kwamba nianze kufanya hivi taratibu ili aanze kuhisi mapema kuwa nina mtoto nje. Hata hivyo, nilishindwa kumuelewa alimaanisha nini, hivyo ilibidi nimuulize.

MIMI: “Mbinu gani natakiwa kuanza kuitumia?”

SISTER: “Katika maongezi yenu, unaweza kumuuliza, 'Hivi, ukija kufahamu kuwa nina mtoto nje, utafanyaje?' Inatakiwa uwe unamuuliza mara kwa mara hadi pale atakapozoea na kuona ni jambo la kawaida.”

MIMI: “Dada yangu, sio kwa mama J, hachelewi kulianzisha.”

SISTER: “Hawezi kufanya chochote kwa sababu atakuwa hana ushahidi. Kwa mara ya kwanza atapata shida kadri anavyozidi kusikia kutoka kwako, lakini atazoea na kuona ni jambo la kawaida. Wewe cha kuzingatia ni kuwa unachukua note ya majibu anayotoa, na utakuwa unanitumia.”

Maneno yake yalikuwa na maana, lakini nilihisi bado kuna changamoto kubwa katika kutekeleza mbinu hiyo. Lakini dada alizidi kukazia kwamba mbinu hii itaanza kumuandaa kisaikolojia, na baada ya muda atazoea hali hiyo. Alisisitiza kwamba hata nitakapokuja kumpa taarifa rasmi, haitaleta shida sana na atakuwa na uwezo wa kuelewa vizuri. Maneno yake yalinipa matumaini, kwani niliweza kuona uwezekano wa kumfikia mama J kwa njia ambayo ingekuwa rahisi na ya busara.

Kuhusu suala la kumpa taarifa rasmi, dada alishauri ni bora nisubiri hadi nitakapomalizana na wazee na kila kitu kipo sawa. Alisema kwamba ni hapo ndipo nianze hatua za kumwambia mama J. Dada alinihakikishia kwamba atanisaidia kadri anavyoweza kwa kutumia uwezo wake wote hadi mambo yawe sawa. Maneno yake yalijenga imani ndani yangu, na nilihisi kuwa na msaada wa dada yangu kutanisaidia kukabiliana na changamoto hii.

Baada ya kumaliza maongezi yetu muhimu, dada aliniaga na kuniambia kwamba kesho, Jumapili, ataondoka kurudi Tanzania. Alisisitiza kwamba pindi nitakaporudi Dar es Salaam, nimtaarifu ili aje tuyaweke sawa na mama J.

Nilimuuliza dada kama amelipia tiketi ya ndege, naye akasema kwamba wifi yake, Iryn, alikuwa amelipia tayari na amemwingizia pesa nyingi kwenye akaunti yake, ingawa hakutaka pesa hizo. Dada alifungua app ya benki na kunionesha kiasi ambacho aliingiziwa, na nilibaki nikishangaa.

Mwishoni, dada alinipongeza kwa kuwa baba, akisema kuwa Aria ni damu yetu halali. Maneno yake yalinipa furaha kubwa na kunitia moyo zaidi. Tuliagana kwa kukumbatiana, kisha tukarudi ndani kuendelea na mambo mengine, kwani tulikuwa tumetumia muda mwingi sana kwenye maongezi yetu.

Kibarazani, akina Jimmy walikuwa wanacheza last card, na mimi nilijiunga nao, tukawa jumla wanne: Mimi, Jimmy, Vivian, na Samantha. Mchezo ulikuwa mzuri sana, maana tulianza hadi kuweka hela kwa mshindi, na hali hiyo ilifanya ushindani uwe mkali. Baadaye, dada alikuja na tukawa jumla watano, na mchezo ukawa na ladha mpya, huku kila mmoja akijaribu kushinda kwa njia yake. Kicheko na furaha vilijaza hewa, na ilikuwa ni fursa nzuri ya kuondoa mawazo na kufurahia muda pamoja.

Ninataka niwaambie kuhusu undugu wa Jimmy, Iryn, Vivian, na Samantha. Ninarudisha hadi chapter 9, siku ambayo nilifika Ethiopia kwa mara ya kwanza. Katika siku hiyo, dada watatu walikuja kumpokea Iryn, ambapo alinitambulisha. Yule dada mkubwa ndiye alikuwa Vivian, mtoto wa Pili wa mama mkubwa, huku Jimmy akiwa mtoto wa kwanza akifuatiwa na mdogo wake katika wale wawili waliokuwa wamekuja kumpokea Iryn.

Hawa watatu wa kwanza, Vivian, Jimmy, na mdogo wao, wanatoka kwenye tumbo moja, wakiwa na mama na baba mmoja, ingawa baba yao alishatangulia mbele za haki. Mama mkubwa alizaa watoto wengine wawili na mume mwingine, Samantha na mdogo wake wa mwisho. Huyu mdogo wa mwisho ndiye mmoja kati ya wale dada wawili wadogo ambao Iryn alinifahamisha kama wadogo zake.

Mama mkubwa ana jumla ya watoto watano. Watatu wa kwanza wanashiriki baba mmoja, wakati hawa wawili wa mwisho wanashiriki baba mwingine. Kati ya watoto hao watano, Jimmy pekee ndiye mtoto wa kiume. Kwa Iryn, watoto hawa ni kama binamu zake (cousins), ingawa yeye hupenda kuwaita dada na kaka.


Nilikaa sana pale nyumbani, na hatimaye mimi na Jimmy tuliondoka saa 6 usiku kurudi hotelini. Nilipitia mapokezi kuchukua kadi yangu, na dada wa mapokezi akaniambia kuwa kuna ujumbe wangu. Alinipa kadi na kikaratasi kidogo. Nilielewa kinachoendelea mara moja, na Jimmy aliona yote hayo, akabaki kutabasamu.

Baada ya kuingia chumbani, nilifungua kile kinote na kugundua kuwa ilikuwa ni namba ya simu ya Nala. Niliweka pembeni na kuelekea bafuni kuoga. Baada ya kumaliza kuoga, nilijilaza kitandani, nikiwa nimechoka lakini mawazo yakiwa hayajakaa sawa. Nilianza kuyapitia kwa kina yale mazungumzo yangu na sister, nikitafakari maana yake na mwelekeo wa mambo.

Ukweli ni kwamba, Sister alizungumza mambo mengi sana, lakini kubwa kuliko yote, aliniapia kwamba nikifanya makosa tena, basi atajiondoa kabisa kwenye huu msala, na niachwe nipambane peke yangu. Sister ndiye kiungo muhimu katika kufanikisha hili jambo, hivyo niliona ni busara kutulia na kuwekeza nguvu zangu kwa umakini kwenye familia zangu.

Niliwaza sana kuhusu wazo la kumuacha Mary, lakini kila nilipofikiria, nilijikuta nikipoteza nguvu kwa sababu bado nampenda. Hata hivyo, kutokana na ushauri wa Sister, niliona sina budi kufanya hivyo. Ni bora nimuache mapema kuliko kusubiri na kuleta matatizo makubwa zaidi huko mbeleni.

Niliwaza sana na hatimaye nikaamua kwamba nitakaporudi Dar es Salaam, nitamtafuta Mary ili tuzungumze wazi kuhusu hili suala. Kilichonipa faraja kidogo ni kwamba Mary tayari alikuwa anafahamu kinachoendelea kuhusu mahusiano yangu na Iryn, hivyo nilihisi mazungumzo yetu yangeweza kuwa ya uwazi zaidi.

Jambo lingine lililoanza kunisumbua kichwani ni jinsi wazazi wangu watakavyopokea taarifa za mimi kuzaa na Iryn. Swali kubwa lililozunguka mawazoni mwangu lilikuwa, je, watalichukuliaje suala hili? Nilijua kuwa na mtihani mgumu mbele yangu, lakini kwa sababu Sister aliahidi kunisaidia, nilijisemea kwamba kila kitu kitakuwa sawa. Hata hivyo, sikupuuza uzito wa hali hiyo.

Kwa upande wangu, nilitamani sana kuona Junior na Aria wakifahamiana tangu utotoni ili waweze kujenga uhusiano wa karibu na bond nzuri. Kuhusu hili suala, nilihisi mzee ndiye anayeweza kunipa ushauri mzuri zaidi. Hivyo, nilianza kupata hamasa ya kumtafuta mapema ili tuweze kuzungumza na kupanga namna bora ya kufanikisha hili.
*****

Asubuhi, baada ya kuamka, nilimpigia simu mama J ili kumsalimia, lakini hakupokea, hivyo nilihisi labda alikuwa ameenda kanisani. Niliingia bafuni haraka kuoga na kujiandaa ili tuweze kwenda kwa mama mtoto. Ilikuwa saa mbili asubuhi, na nilihisi muda ulikuwa unayoyoma. Nilimpigia simu Jimmy kumjulisha kuwa tuanze safari, lakini naye hakuwa akipokea. Hatimaye, nikaamua kwenda kumgongea chumbani kwake.

Baada ya kufika kwenye chumba chake, maana yeye alikuwa floor ya juu, niligonga mlango na alitoka kufungua. Alikuwa haja jiandaa, hivyo nilipompa taarifa ya kuondoka, aliniambia nimsubiri ajiandae haraka. Nikamwambia atanikuta kwenye restaurant nikimsubiri.

Nilielekea kwenye restaurant kupata kifungua kinywa, na wakati huo nilikuwa nawasiliana na Iryn, ambaye alikuwa akinisisitizia nianze safari mapema ili niweze kucheza na mtoto. Baada ya nusu saa, nilimuona Jimmy akiwa ameongozana na mwanamke mwenye asili ya kizungu, na nikahisi huenda alikuwa amelala naye. Hali hii iliniacha na maswali mengi kichwani mwangu.

Walipofika, waliketi pamoja nami, na Jimmy alifanya utambulisho wa kawaida, na mimi pia nilimsalimia yule dada. Waliagiza kifungua kinywa, na baada ya kumaliza, tuliondoka kwenye eneo hilo, tukimwacha dada akisubiri usafiri wa kumpeleka kwake.

Wakati tuko kwenye Uber, nilianza kumuuliza Jimmy maswali kuhusu yule mwanamke. Nilikuwa na hamu ya kujua zaidi kuhusu mahusiano yao, na jinsi alivyomjua.

MIMI: “Bro, yule ni nani tena?”

JIMMY: “Tulikutana juzi Soho club, tukabadilishana namba, jana baada ya kuchat naye, nilimpanga aje hotelini akakubali.”

MIMI: “She’s a hoe?”

JIMMY: “I don’t think so, anafanyia kazi kwenye moja ya ubalozi hapa South Africa.”

Nilibaki kimya, nikitafakari kwa undani. Jimmy alikuwa amenishinda kabisa kwa tabia zake. Nilijiuliza mara ngapi ameweza kukutana na wanawake kama yule, na ni wangapi mpaka sasa? Spidi yake ilikuwa ya kutisha, na ilinifanya nishindwe kuelewa vizuri mwelekeo wake. Nilijikuta nawaza kama angeweza kudhibiti hali hii, au kama ilikuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku.

Baada ya kuwasili, mazingira yalionekana kuwa kimya na tulivu sana. Tulipofika kibarazani, mtoto wa Jimmy alionekana akicheza peke yake. Jimmy alimnyanyua kwa furaha, kisha tukaingia ndani kuzungumza na mama mtoto ili tupate kujua ratiba ya siku ile.

Pale sebuleni, dada yangu alikuwa amemshika mtoto, na tukaingia kwenye mazungumzo kuhusu safari yake. Alisema anatarajia kuanza safari saa 11 jioni. Wakati huo, Iryn alitoka sebuleni na kuja kukaa pembeni yangu. Alionekana kuzidi kuimarika kadri siku zilivyokuwa zinaenda, jambo lililonipa faraja. Mazungumzo yetu yaliendelea kwa utulivu, na hali ilikuwa ya amani.

Baada ya kula chakula cha mchana, mimi, dada yangu, na mama mkubwa tuliamua kuwa na kikao chetu binafsi. Tulitafuta utulivu nje kwenye bustani, mbali na kelele na muingiliano wa watu wengine. Hapa tuliweza kuzungumza kwa uwazi na utulivu, tukijadili mambo muhimu bila usumbufu wowote. Mazingira yalikuwa tulivu, na kikao kilikuwa na uzito wa kipekee.

Mama alianza kwa kumshukuru sana sister kwa kujitolea kwake kwa kipindi chote hadi Iryn alipojifungua. Sister alisaidia sana, hasa kwenye mazoezi na mbinu mbalimbali za kuhakikisha Iryn anajifungua salama. Kwa kuwa sister yangu tayari alikuwa na watoto wawili, alikuwa na uzoefu mwingi ambao ulimsaidia kumwelekeza Iryn vyema wakati wa ujauzito na hadi wakati wa kujifungua. Mama alionyesha shukrani za dhati kwa mchango wake mkubwa.

Ukiachana na yote, Sister aliweza pia kutengeneza mahusiano mazuri sana na wifi zake, kama Vivian na Samantha. Wote walionekana kumpenda sana dada yangu kwa jinsi alivyojitoa na kujali. Uhusiano wao ulijengeka kwa upendo na uelewa, na hilo lilifanya familia kuwa karibu zaidi.

Kuhusu suala la mimi kumpa mimba binti yake, mama alisema hawezi kusema lolote kwa sababu Iryn mwenyewe alifanya maamuzi yake, na ni mtu mzima ambaye anaelewa vyema anachokifanya. Alionyesha kutambua kwamba Iryn alikuwa na uwezo wa kuchukua maamuzi yake binafsi, na hakutaka kuingilia zaidi. Hii ilileta hali ya unafuu kidogo, ingawa suala hilo bado lilikuwa na uzito wake.

Mama aliniuliza swali ambalo lilikuwa zito kulijibu:

“Una mpango na malengo gani juu ya Iryn?"

Nilihisi uzito wa swali hilo, lakini nilijua dhumuni la mama kuuliza ni nini. Nikajua kwamba ni muhimu kufikiri kwa umakini na kuepuka kutoa ahadi ambazo huenda nisitekeleze. Kwa kutumia busara na tahadhari, nilimjibu hivi:

MIMI: “Asante mama kwa kuniuliza swali hili muhimu. Ninamuheshimu sana Iryn na ninatambua nafasi yake katika maisha yangu. Nimeliona hili suala kwa uzito wake, na ninataka kuhakikisha kwamba mimi na Iryn tunajenga msingi mzuri wa ushirikiano, hasa kwa ajili ya ustawi wa mtoto wetu. Nataka tuchukue mambo hatua kwa hatua, huku tukijadiliana na kupanga vizuri mustakabali wa familia yetu. Ninaendelea kutafakari juu ya mpango mzuri na utakaokuwa bora kwa wote, na nataka kuhakikisha kwamba kila kitu kinawekwa wazi na kwa manufaa ya pande zote mbili.”

Mama na Sister waliniangalia kimya kwa muda, wakitafakari majibu yangu. Mama, hasa, alionekana kutotarajia jibu langu. Niliona machoni mwake kwamba alitarajia kitu tofauti, labda ahadi thabiti au mpango ulio wazi zaidi kuhusu mustakabali wangu na Iryn.

MAMA: “Naona umejibu kwa hekima, lakini bado sijapata uhakika. Wewe na Iryn, mna mpango wa kuwa pamoja au hili ni suala tu la mtoto?”

MIMI: “Naelewa unavyohisi mama, na ni swali lenye uzito. Kwa sasa, mimi na Iryn tunaendelea kuzungumza juu ya mstakabali wetu. Kipaumbele chetu kikubwa ni kuhakikisha mtoto anakua katika mazingira bora, lakini bado tupo kwenye hatua ya kufikiria kwa kina jinsi ya kutatua hali yetu ya kibinafsi. Siwezi kusema kwa hakika wakati huu, ila nataka iwe wazi kwamba sitamtelekeza Iryn wala mtoto wetu.”

MAMA: “Hilo ni jambo jema kusikia, lakini ningependa kuona mnapanga mustakabali wenye utulivu zaidi, hasa kwa ajili ya binti yangu. Matarajio yangu ni kwamba, kama kuna upendo na nia njema, basi mtachukua hatua ya kusonga mbele pamoja.”

MIMI: “Ninakubaliana na wewe kabisa mama, Iryn ni mtu muhimu kwangu na sina mpango wa kufanya maamuzi ya haraka bila kufikiria kila mtu aliyehusika. Ni muhimu kwangu kwamba wote tunakuwa na maelewano mazuri kwa ajili ya mtoto na hatimae, kwa Iryn pia.”

MAMA: “Nashukuru kwa uwazi wako, ningependa tu kuona unachukua hatua thabiti, maana Iryn anastahili uhakika. Si kwamba nakuwekea shinikizo, lakini ningependa kuona binti yangu akiwa kwenye mikono salama.”

MIMI: “Naelewa mama, na ninakuhakikishia kwamba natilia maanani kila kitu unachosema. Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha mambo yanaenda vizuri kwa Iryn na mtoto wetu.”

Mama aliniangalia kwa makini, na nilihisi alikua akiwaza, labda akijiuliza, “Huyu jamaa ana akili sana.” Nilijua kuwa niliyajibu maswali yake yote kwa umakini na hekima. Hata dada yangu alionesha tabasamu, akionyesha kushangazwa na jinsi nilivyoweza kujibu maswali ya mama kwa njia ambayo haikuniingiza kwenye mtego.

Mama aliendelea na mazungumzo, akasema angependa kuwajua wazazi wetu, akisisitiza kuwa ni muhimu kwa mustakabali wa mtoto. Aliongeza kwamba sasa sisi tumeshakuwa muunganiko wa familia, na ni muhimu kuimarisha uhusiano huu kwa kuhakikisha kila mmoja anajua historia na asili ya mwingine. Mama alionyesha kuwa na hamu ya kujenga mshikamano ndani ya familia yetu, ili mtoto apate msingi mzuri wa malezi na urithi wa kihisia.

Baada ya kumaliza mazungumzo yetu, Sister alijiandaa kwa ajili ya safari yake ya kurudi Tanzania. Hali ilikuwa ya huzuni kidogo, lakini pia ya furaha kwa sababu tulikuwa tumepata muda mzuri wa kuzungumza na kujenga uhusiano wetu zaidi.

Saa 9 mchana, Sister alitoka na begi lake na kutuaga pale sebuleni. Tulitoka nje na kupiga picha za pamoja kama kumbukumbu ya wakati wetu mzuri pamoja. Baada ya hapo, mimi na Vivian tulimpa kampani hadi uwanja wa ndege. Safari hiyo ilikuwa ya furaha, ingawa tulihisi huzuni kidogo kwa sababu ya kuachana. Tulizungumza mengi katika gari, tukijadili mipango ya baadaye na sister kuahidi kukutana tena na kina Vivian hivi karibuni.

Tukiwa airport, tulizungumza mambo mengi sana, na Sister aliendelea kunisitiza kwamba nitakaporudi Dar es Salaam, nimpe taarifa ili aje nyumbani kuweka sawa masuala yangu na mama J. Kabla ya kucheck in, aligana na Vivian kwa kukumbatiana kwa upendo, na niliona jinsi walivyokuwa na uhusiano mzuri. Baada ya hapo, tuliondoka maeneo hayo, tukielekea nyumbani, tukiwa njiani story na Vivian ziliendelea na niseme hawa mashem zangu wananikubali na tunapatana sana.

Usiku, niliwasiliana na mama J pamoja na mwanangu Junior. Nilimdanganya kwamba nipo China nikifuatilia mzigo, na baada ya hapo nitatoka kwenda South Africa kumuona Iryn, ambaye amejifungua mtoto. Mama J hakutoa maoni mengi kuhusu hilo, zaidi alisema atawasiliana na Iryn kumpa hongera. Ingawa alionekana kutokuwa sawa na hali hiyo, nilijua ujumbe wangu ulikuwa umemfikia.
*****

Wiki inayofuata, ambayo ilikuwa ni wiki ya kwanza ya mwezi wa 7, idadi ya wageni iliongezeka sana pale kwa Iryn. Ndugu zake kutoka Ethiopia walifika, na pia marafiki zake wa chuo waliosoma pamoja Ufaransa walikuwa wakija na kuondoka. Sebuleni, kila kona ilikuwa imejaa zawadi za mtoto, na hapo ndipo nilipogundua kwa kweli kwamba Iryn alikuwa na mtandao mpana wa watu. Hali hiyo ilionyesha jinsi alivyokuwa akipendwa na kuungwa mkono na watu wengi, na ilifanya moyo wangu ujaze faraja na kujivunia kuwa sehemu ya maisha yake.

Siku ya Jumatano, mama mkubwa aliondoka kurudi Ethiopia ili kuendelea na majukumu yake. Pia, dada wa kazi kutoka Ethiopia alifika nyumbani kusaidia katika kazi mbalimbali. Iryn alieleza kuwa hakutaka dada wa kazi mwenyeji kwa sababu ya tabia zao, hivyo alihitaji mtu ambaye wangeweza kuendana kiutamaduni. Hali hiyo ilionyesha umuhimu wa mazingira yanayofanana na utamaduni wao, na niliona ni busara kwa Iryn kuchagua mtu ambaye angeweza kuleta utulivu na uelewano katika familia.

Siku ya Jumapili, Jimmy pamoja na familia yake waliondoka kurudi Ethiopia, hivyo aliyebaki ni dada Vivian. Baada ya kuondoka kwa Jimmy, nilienda kukaa na Iryn, maana idadi ya watu ilikuwa imepungua, na mle ndani tulikuwa jumla watano. Hali hiyo ilituletea fursa nzuri ya kuzungumza kwa undani zaidi na kujenga uhusiano wetu.

Wiki ya pili ya mwezi wa 7, Jumatatu, bibi yao ‘Momo’ alifika South Africa kumuona kitukuu chake. Aliwasili jioni, na mimi na Samantha tulikwenda kumpokea pale airport. Momo, ambaye sasa ana umri wa miaka 70, ni bibi mwenye uzoefu wa maisha, lakini bado ana nguvu za kujiendesha. Momo ana tabia ya kutabasamu na kuwa na nishati, na nilijua kwamba uwepo wake ungeongeza furaha na umoja katika familia yetu.

Tangu tupo kwenye gari hadi tulipofika nyumbani, Bibi alikuwa na furaha sana na alionyesha hamu kubwa ya kumuona kitukuu wake. Alikuwa akizungumza kwa lugha yao ya nyumbani, lakini Samantha alikuwa ananiambia kila kilichokuwa kinaendelea, akitafsiri maneno ya bibi kwa urahisi. Ilikuwa ni furaha kubwa kusikia shauku ya bibi, na niliweza kuhisi upendo wake wa dhati kwa familia.

Baada ya kufika nyumbani, Iryn hakuwa mbali kumpokea bibi yake, na walikumbatiana kwa furaha na kumkaribisha ndani. Kitu cha kwanza bibi alichomba ni kumuona kitukuu wake, na alifurahi sana baada ya kumuona. Uso wake ulijawa na tabasamu la furaha, na Iryn alionekana pia akifurahia moment hiyo. Nilijua kuwa bibi alikuwa na matumaini makubwa kwa ajili ya kitukuu chake, na nilihisi furaha kuona jinsi familia ilivyokuwa ikijenga uhusiano mzuri katika kizazi tofauti.

Baada ya bibi kurudi nyumbani, mazingira yalichangamka sana, kwani bibi ni mwongeaji sana, na wajukuu zake wanampenda sana. Bibi alisema ataendelea kukaa na Iryn na hafikirii kurudi Ethiopia mapema, jambo lililomfanya Iryn ajisikie vizuri. Iryn ni mjukuu ambaye bibi yake anampenda sana, na hii ni kwa sababu Iryn humjali sana bibi yake, akimpa huduma na kumuhudumia kwa upendo.

Kwa upande wangu, tangu nilipofika South Africa, tayari wiki mbili zilikuwa zimepita, na nilipanga kuondoka Jumapili ya weekend. Niliangalia hali yangu na kugundua kwamba kuendelea kukaa huku kungeweza kuathiri mambo yangu mengi, kuanzia kampuni hadi biashara zangu. Nilijua ni muhimu kurejea nyumbani ili kusimamia masuala yangu na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa. Ingawa nilifurahia wakati niliokuwa pamoja na Iryn na familia, nilihisi ni lazima nitafute njia ya kuleta uwiano kati ya majukumu yangu ya kifamilia na biashara zangu.

Kesho yake asubuhi, nilimfata Iryn chumbani ili niweze kuzungumza naye kuhusu suala langu la kuondoka. Pembeni yake kulikuwa na diary, hivyo niliichukua na kuanza kuisoma. Niliona alikuwa akiandika mipango yake, na nilicheka baada ya kuona ameandika mpango wa kuanza gym.

Of course, alikuwa ameanza kunenepa sana kutokana na kuwa mama na vyakula anavyokula, lakini bado haikufanya apoteze uzuri na shape yake. Kinyume chake, niliona kuwa mabadiliko hayo yaliongeza mvuto wake, na alikuwa akionekana kuwa na uzuri wa kipekee ambao unakuja na umama.

MAMA ARIA: “Darling, unacheka nini?”

MIMI: “Nimefurahi kuona una mpango wa kuanza Gym, lakini bado mapema sana.”

MAMA ARIA: “I know, baada ya miezi 3 nitaanza mazoezi ya kupunguza huu mwili.”

Nami, nikasogea kukaa pembeni yake;

MIMI: “Nimekumiss baby mama.”

Iryn alianza kuangalia usawa wa bunduki yangu na akanishika kidevu changu na tukaanza kuangaliana pale;

MAMA ARIA: “Are you horny?”

MIMI: “Ofcourse yes.”

MAMA ARIA: “Pole! nadhani unakumbuka siwezi kusex kwasasa hadi nipone vizuri, doctor alishauri baada ya miezi 3, ila mwezi ujao nitaenda kuangalia maendeleo.”

MIMI: “Naelewa usijali, mimi nitavumilia kwa hili.”

Usawa wa matiti yake ulionekana kulowa maziwa, kwani chuchu zake zilikuwa bado zimesimama. Baada ya kumuona vile, ilibidi nimwambie kwamba analowa, akicheka kidogo kwa aibu. Alijua kwamba hali hiyo ni ya kawaida kwa mama anapokuwa katika kipindi hiki, lakini nilijua kwamba ilikuwa ni muhimu kwake kujisikia vizuri kuhusu mwili wake.

MAMA ARIA: “Mwanao hataki kunyonya, halafu mama yake nina maziwa mengi sana. Uwe unamsaidia mwanao kunyonya, kwani naishia kuyakamua na kuyamwaga. Nikupe unyonye? Yatakusaidia kiafya.”

Nilihisi aibu baada ya kusikia haya maneno kutoka kwa Iryn. Aliponigeukia na kunipa ishara ya kunyonya, sikuona sababu ya kukataa, kwani alikuwa anayamwaga. Nilijisemea, si afadhali nikanywa mimi kuliko yamwagwe. Nilianza kuyanyonya taratibu hadi aliposema basi, ndio kuacha na yalikuwa ni matamu sana.

MAMA ARIA: “Vipi matamu?”

MIMI: “Yeah! Aria anafaidi sana.”

MAMA ARIA: “Mwanao mpole kama wewe, naona huyu atarithi tabia zako.”

MIMI: “Bado mtoto, akikua ndio tutajua tabia zake, hata Junior alikuwa mpole kama Aria, ila sasahivi ni balaa.”

Tulipoanza mazungumzo yetu, alizungumzia suala lake la kurudi shule na akaniambia kuwa analiwazia kwa umakini. Nami nikamshirikisha mpango wangu wa kurudi shule mwezi wa kumi, ambapo alinisisitiza kwa upendo kuwa ni vema nisomee masomo yangu ya masters nchini Afrika Kusini ili tuwe karibu na mtoto wetu.

Ingawa wazo hilo lilikuwa zuri, nilijua kuwa kulikuwa na changamoto nyingi zinazoweza kufanya isiwezekane. Hivyo, nilimpatia jibu lililofikiriwa vizuri, ambalo alielewa kwa upole na busara.

Nilimwambia kwa upole,

Baby mama, nikisomea huku, kumbuka kuwa mambo mengi yanaweza kuyumba, kuanzia kampuni yako hadi miradi yangu. Ufuatiliaji wa karibu ni muhimu sana. Acha mimi nisomee Dar ili niwe karibu na biashara zetu. Kuhusu Aria, nitakuwa nakuja mara kwa mara kuwasalimu, siwezi kukaa muda mrefu bila kumuona binti yangu. Kama vile wakati wa ujauzito wako ulivyokuwa ukija Dar es Salaam mara kwa mara, sasa ni zamu yangu kuja Cape Town. Tutaendelea kuwa karibu, hata kama nitakuwa huku.”

Mama Aria alifurahi sana kusikia maneno yangu, na hakuwa na la kusema zaidi. Baadaye, nilimueleza kuhusu mpango wangu wa kuondoka Jumapili. Hata hivyo, kwenye suala la kuondoka, alionekana kulipokea tofauti na aliniomba niondoke mwisho wa mwezi. Nilijaribu kumsihi kwa upole, na kumuomba aniruhusu niondoke wiki ijayo, huku nikiahidi kuwa nitarudi mapema kwa ajili ya sherehe ya "Simchat Bat" ya mtoto wetu.

Baada ya kumaliza mazungumzo yetu, aliamua kwenda kuoga. Wakati huo, Aria alikuwa ameamka, hivyo nilimbeba na kutoka naye sebleni ili tupate muda wa kukaa pamoja. Sikuwa na shughuli nyingi za kufanya kipindi hicho nikiwa Afrika Kusini, zaidi ya kutumia muda wangu mwingi kucheza na Aria. Sikutoka kwenda sehemu yoyote mara kwa mara, isipokuwa tu kwenda supermarket pale panapohitajika.

Haikupita muda mrefu kabla mama Aria hajarudi kwenye seating room, na kunijulisha kuhusu ujio wa mgeni. Aliniambia kuwa anayekuja ni kaka yake, ambaye ni wa kwanza kwa upande wa mama mwingine. Nilikuwa nimeshaongelea kidogo kuhusu huyu kaka yake, katika Season 1: EP10.

Mchana ule, kaka yake alifika nyumbani kumsalimia Iryn pamoja na mtoto, akiwa ameongozana na mpenzi wake. Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona kaka yake kwa upande wa baba. Ni kijana mwenye haiba fulani ya "manton," kwa mbali anataka kuendana na rappa AKA.

Tulisalimiana pale, kisha tukaingia kwenye mazungumzo ambapo alinikaribisha sana Afrika Kusini kwa ukarimu. Iryn akaanza kumuuliza kaka yake kuhusu maisha na kazi kwa ujumla. Ingawa kaka yake Iryn yuko vizuri kiuchumi, tatizo lake kubwa ni matumizi ya madawa, jambo ambalo limemuharibu sana. Niliwahi kugusia kuhusu hili hapo awali.

Baada ya kupata chakula cha mchana kwa pamoja, kaka yake na mpenzi wake waliondoka. Mama Aria kisha alinipa taarifa nyingine kwamba siku ya Jumamosi tungeenda nyumbani kwa baba yake. Aliongeza kuwa kuna mambo kadhaa watakayokwenda kuyapanga na mzee wake, na akaniambia atanishirikisha katika hayo mazungumzo siku hiyo.

*****

Hatimaye, siku ya Jumamosi ilifika, siku ambayo ilikuwa ni ya kwenda kwa mzee Virgil, baba mkwe wangu. Mzee Virgil alikuwa akija mara kwa mara nyumbani kumuona mjukuu wake, na kitendo cha Iryn kujifungua kilimfurahisha sana. Hakuwa na maswali mengi kuhusu malengo yangu kwa binti yake, wala hakujishughulisha na hilo. Kile kilichomgusa zaidi kilikuwa ni upendo mkubwa aliokuwa nao kwa mjukuu wake. Ilionekana kana kwamba alikuwa akitamani kwa muda mrefu sana kupata mjukuu, na sasa alikuwa akifurahia kila muda aliokuwa naye.

Saa nne asubuhi, gari lilikuja kutuchukua kwa ajili ya safari ya kwenda nyumbani kwa mzee Virgil. Tuliondoka watatu tu, mimi, Iryn, na Samantha. Safari yetu ilikuwa na umbali wa takriban kilomita 45 hadi kufika nyumbani kwa mzee, Somerset West, ambayo iko pembezoni mwa Cape Town. Huu ni sawa na umbali wa kutoka Mwenge hadi Bagamoyo. Njia ilikuwa nzuri, na tulikuwa na mazungumzo mazuri kwenye gari, tukiwa na hamu ya kufika na kumtembelea mzee.

Mzee aliamua kujenga na kuishi nje kidogo ya mji wa Cape Town, na tulivyoanza kuingia katika maeneo haya, nilikuwa nikiona majumba ya kifahari ambayo yalivutia sana macho yangu. Mazingira ya hapa ni kama Ulaya, ni masafi, na kote ni lami, hakuna vumbi. Nyumba zimepangiliwa kwa ustadi wa hali ya juu, mandhari yake ikiwa ya kijani kibichi. Wakati tunaingia Somerset, tulikuwa tukipishana na magari ya kifahari, hali iliyoongeza uzuri wa eneo hili.

Gari lilipaki nje ya geti kubwa, na haikuchukua muda mrefu likafunguliwa, ingawa pale getini hakuonekana mtu yeyote aliyefungua. Tulipofika ndani, gari lilitembea kwa mwendo wa takriban mita 100, na njiani tulipishana na bustani nzuri ya kuvutia.

Baada ya kufika usawa wa nyumba, tulishuka na mbele yangu nikaona bonge la mjengo wa kifahari, aina ya villa. Ilikuwa nyumba kubwa ya kisasa ya ghorofa moja, na kila kipengele chake kilionekana kuwa kimepangwa kwa umaridadi. Ujenzi wa nyumba hiyo ulikuwa wa kisasa na wa kuvutia, ukionyesha ushawishi wa hali ya juu wa usanifu. Ilionekana kama ni mahali pazuri pa kuishi, ambapo mandhari ya karibu iliongeza uzuri na raha ya mazingira.

Wakati huu, mama yake mdogo alitoka kutupokea akiwa na wanae, na haikuchukua muda mzee Virgil akatoka kumkaribisha binti yake. Alikuwa na furaha kubwa sana kutuona na aliomba kumbeba Aria, Mzee Virgil alionyesha upendo mkubwa kwa mjukuu wake.

Nilisikia sauti ya upole kutoka kwa Iryn ikinikaribisha kwa furaha:

“Baba Aria, hapa ndiyo nyumbani, karibu sana.”

Tulipokuwa tunaingia ndani, nilikutana na bonge la msebule uliojaa mapambo ya thamani kubwa kama crystals na marbles. Nimeingia katika nyumba nyingi za kifahari, lakini sebule ya kwa Mzee Virgil ilikuwa ya kipekee kabisa. Ukarabati wa ndani ulikuwa wa kiwango cha juu, na kila kipande cha samani na mapambo kilionyesha umaridadi na mtindo wa kipekee, ikifanya iwe mahali pa kuvutia.

Iryn alianza kunitambulisha kwa wadogo zake wa pale nyumbani kwa upande wa mama mdogo. Mama mdogo ana watoto watatu tu; mtoto wa kwanza ni wa kike, ambaye nilimfahamu nikiwa hospitalini, alikuwa akitarajia kuanza chuo mwaka huo na wawili ni wa kiume, wenye umri wa miaka 13 na 8. Walionekana kufurahia kuniona na walikuwa na shauku ya kujua kuhusu mimi, hali ambayo ilileta maongezi yawe mengi zaidi.

Baada ya lisaa, wageni watano walifika, na kati yao, mmoja tu alikuwa na asili ya Afrika; wengine wote walikuwa wazungu. Kati ya wageni hao, mmoja alikuwa ni babu, na aliomba amshike Aria. Mzee Virgil alifanya utambulisho pale, akimwambia Iryn kwamba wale ni ndugu zake. Iryn alifurahi sana kusikia hivyo, kwani kwa upande wake alikuwa kwenye mission ya kuwasogeza karibu ndugu wote wa upande wa baba yake. Hali hiyo ilileta hisia za umoja na furaha, na ilikuwa ni fursa nzuri kwa familia kukutana na kuimarisha uhusiano wao.

Tulipata chakula cha mchana pamoja, na baada ya wageni kuondoka, Iryn alitoka nje na mzee wake kufanya mazungumzo. Walionekana kuwa na mazungumzo ya karibu na ya kina, hii ilikuwa ni nafasi nzuri kwao kujadili mambo ya familia na kujenga msingi mzuri wa ushirikiano.

Wakati huu, nilikuwa na mama mdogo tukifanya mazungumzo, ambapo aliendelea kunikaribisha kwa ukarimu. Alizungumza kwa upole, akielezea furaha yake kuwa na familia pamoja na jinsi alivyovutiwa na ujio wangu.

Baada ya lisaa, Iryn aliniita nitoke nje ili tuweze kuzungumza na mzee wake. Alimweleza baba yake jinsi ambavyo nimekuwa msaada mkubwa sana katika biashara zake. Mzee wake alishukuru kwa dhati na kusema niendelee kuwa na moyo huo huo. Alionyesha furaha kubwa kwa mimi kuwa sehemu ya familia yake.

Kuhusu suala la kumzalisha binti yake, mzee hakuwa na neno lolote la kukatisha tamaa. Badala yake, alitutakia mafanikio mema na kusema angetamani kuona tukifika mbali zaidi katika maisha yetu.

Mzee aliondoka pamoja na mjukuu wake, na kutuacha mimi na Iryn tukiendelea na mazungumzo yetu. Iryn alianza kunishirikisha kuhusu kazi kubwa aliyonayo katika kuzisimamia kampuni za baba yake. Aliniambia kuhusu mali mbalimbali anazomiliki baba yake hapa Afrika Kusini, ikiwa ni pamoja na apartments, mashamba ya zabibu, na kampuni ambayo ni miongoni mwa waexporter wakubwa wa wines.

Alielezea jinsi alivyohusika katika kusimamia shughuli hizi na jinsi anavyopanga mipango ya kuziendeleza zaidi. Hali hiyo ilionyesha kiwango cha juu cha kujitolea kwake na uelewa wa biashara, na ilinipa mtazamo mzuri kuhusu familia yao na malengo yao ya kifamilia.

Tangu siku ile tulipokutana na Iryn na kuanza mahusiano yetu, hakujawahi kuwa na wakati ambapo alitaja utajiri wa baba yake. Badala yake, alijikita zaidi katika kunieleza kuhusu majukumu aliyokabidhiwa ya kuwa msimamizi wa kampuni za baba yake. (SEASON 1: EP40)

Hii ndiyo siku nilipogundua kwamba mzee Virgil si mtu wa kawaida, kwani ana utajiri wa kutisha. Lakini ukimwona, unaweza kumchukulia kuwa mtu wa kawaida sana. Kama mnavyojua, wazungu hawana tabia ya kujionesha kama wana fedha, tofauti na sisi Waafrika, ambao mara nyingi tunapenda maonyesho ya kifahari.

Iryn aliendelea kunieleza jinsi mzee wake alivyotokea kunikubali sana. Aliniambia kwamba amemshauri atulie nami, kwani kwa sasa wanaume wengi hawaaminiki. Maneno hayo yalikuwa ya faraja kutoka kwa Iryn, yakiwa na uzito wa maana. Nilimuhakikishia kuwa nitajitahidi kumsaidia kadri ya uwezo wangu, kwa sababu uaminifu ni msingi wa mahusiano yetu.

Nilimuuliza Iryn kuhusu mgawanyo wa mali za mzee na jinsi anavyowaangalia watoto wengine, wakiwemo Smith na kaka yake mkubwa, ambapo jumla yao ni watoto sita wa mzee Virgil. Iryn alijibu kwamba hadi sasa, watoto wanne tu wanatambulika rasmi, ambao ni yeye pamoja na wadogo zake watatu kwa upande wa mamdogo. Aliongeza kuwa kuhusu kaka yake na Smith, bado hawajazungumza na mzee wao kuhusu suala hilo, lakini wanatarajia kuangalia namna nyingine ya kufanikisha mambo yao.

MIMI: “Na vipi kuhusu mama mdogo?”

IRYN: “Mama mdogo si mmoja wa mrithi wa hizi mali. Alifunga ndoa ya mkataba na mzee, na moja ya makubaliano ni kwamba hatahusika kwenye urithi wa mali zaidi ya watoto tu.”

MIMI: “Baba yako ni genius sana.”

IRYN: “Mali nyingi sana mzee kazipata akiwa na mama yangu. Ndiyo maana unaona mimi nikiwa kipaumbele cha kwanza, hata wakati ambapo hatuko kwenye maelewano na mzee. Kwa upande wake, alikuwa anapata tabu sana kuhusu hili.”

Iryn alikuwa huru kunifungukia mambo mengi sana. Alisema kwamba hata kitendo cha kuzaa na mimi si kwamba alikurupuka tu kufanya maamuzi hayo, bali alifikiria kuhusu mustakabali wake na mali za baba yake. Alieleza kwamba kipindi kile baada ya kurudi kutoka South Africa kumwona mzee wake, aliona kuna umuhimu wa kuwa na watoto ambao wataweza kurithi mali hizo, kwani hata yeye atakufa.

Iryn alifikiria kwa kina na kugundua kwamba hakuna mtu anayemuamini zaidi yangu kwa sasa. Alijisemea atafanya kila mbinu ili anizalie mtoto, lakini lengo lake kubwa ni kuhakikisha urithi wa mali za baba yake unakuwa salama. Aliendelea kueleza kwamba, mama mkubwa wake na ndugu zake wanamuona kama mjinga sana, lakini hawajui mipango yake ya siri. Hakuwa na nia ya kuona mali ambazo mama yake alizichuma na baba yake zikipotea kwa watoto wengine. Kwa hiyo, alichukua maamuzi haya magumu, lakini yaliyojikita katika manufaa ya kizazi chake.

Nilishusha pumzi ndefu sana, nikijisemea kwamba kumbe Iryn yuko very calculated na alikuwa na mipango mikubwa ambayo sikuwa na habari nayo. Nilikuwa bado siamini kwamba Iryn anaweza kubeba mimba kwa sababu ya kijinga kama aliyokuwa akinambia, lakini leo ndiyo nimeelewa kuwa alikuwa anawaza extra miles. Iryn alikuwa na malengo ya dhati, na sasa nilianza kuelewa uzito wa maamuzi yake.

IRYN: “Baba Aria, naomba nisamehe sana kwa kutokushirikisha hili mapema, nilijua ipo siku ungekuja kujua ukweli. Nilikuwa nauwezo wa kuzaa na mwanaume yoyote yule ninayemtaka hata kwa kumlipa na nikapata mtoto, lakini niliona wewe ndio unafaa.”

MIMI: “Naomba tuachane na haya, Aria ni mtoto wetu tuangalie namna gani ya kumlea na kumtunza ili tuje tujisifu kuwa naye.”

IRYN: “Babu yake kafurahi sana kumuona, ndio mjukuu wake wa kwanza. Pia unakumbuka nilikwambia kuhusu afya ya mzee wangu? Hana maisha marefu sana hapa duniani ni pesa tu zinafanya anaendelea kuishi.”

MIMI: “Nakumbuka baby, naamini ataishi muda mrefu zaidi hapa duniani, tusichoke kumuombea.”

IRYN: “Natamani kupata mtoto mwingine, hata nikiwa natembea barabarani, kushoto nina Aria na kulia nina mdogo wake nakuwa na bodyguards wangu.”

MIMI: “Naona unanipa greenlight ya kukupa mimba ya pili.”

IRYN: “Yes! Why not, unafikiri atakuwa nani zaidi yako?”

MIMI: “Sawa baby subiri kwanza Aria akue mengine tutapanga.”

Baada ya mazungumzo marefu, tulianza kutembea na kutalii mazingira ya nyumba yao. Aisee, nyumba yao imezungukwa na bustani nzuri, huku ukubwa wa kiwanja ukiwa kama ekari tano. Tuliposhuka chini, tulikuta mizabibu mingi imepandwa, kuzunguka upande wa nyuma nakutana na swimming pool mbili, moja ya wakubwa na nyingine kwa ajili ya watoto. Nyumba hiyo ilikuwa na mvuto wa kipekee, na mbele zaidi kulikuwa na nyumba ndogo ya wafanyakazi ambao kazi yao ni kutengeneza zile bustani na kumwagilia mimea.

Nilishindwa kuelewa kwanini Iryn ameshindwa kukaa na baba yake na ameamua kupanga aishi peke yake. Sikutaka kumuuliza kuhusu hili, kwani nilijua Iryn ana akili sana na huwa hafanyi jambo lolote bila sababu. Nilihisi kuwa kuna mambo mengi nyuma ya uamuzi wake, lakini kwa heshima yake, niliona bora nisubiri hadi atakapojisikia kuzungumzia.

Saa mbili usiku, tulipata dinner ya pamoja, na baada ya hapo tuliagana kuwa tunaondoka. Walitusindikiza hadi nje, ambapo dereva alikuwa amekuja kutufuata tayari. Tukiwa pale nje, mzee aliendelea kuongea na binti yake, na nilipata fursa ya kubaini upendo mkubwa sana alionao kwa Iryn. Mazungumzo yao yalionyesha uhusiano wa karibu na wa kipekee kati yao, na ilikuwa wazi kwamba Iryn alikuwa na nafasi maalum katika moyo wa baba yake.

Dereva aliyekuwa amekuja kutufuata ni ameajiriwa na mzee na kazi yake ni kwaajili ya kuwapeleka watoto shule na kuwarudisha, au kuwapeleka matembezini.

*****

Wiki ya tatu, nilipanga kuondoka Cape Town siku ya Ijumaa, nikijitayarisha kurudi Dar es Salaam na kuendelea na ratiba zangu za kila siku. Hata hivyo, nikiwa South sikuwa na kazi yoyote ya kufanya zaidi, nilijikuta nikicheza sana na Aria, kwani hiyo ndiyo ilikuwa shughuli pekee iliyonipa furaha na kunifanya nijisikie hai.

Kwa upande wa Mary, mawasiliano yetu yalikuwa yanaendelea vizuri, na yeye kwa upande wake alionyesha wazi hamu ya kuniona na alitaka anione mapema iwezekanavyo. Alikuwa akiendelea kuniambia kwa kusisitiza ni kwa sababu ya kutamani kuungana tena na mimi, na alilalamika kidogo kuhusu kuchelewa kwangu kurudi.

Siku ya Jumatano, nilitoka na Iryn kwenda kukagua biashara yake ya saloon, ambayo ni kubwa sana na ina wafanyakazi wengi. Iryn alionekana kuguswa sana na hali ya wafanyakazi, akilalamika kuhusu jinsi watoto wa South walivyo wavivu katika kazi zao. Alisema anafikiria kuandaa mpango wa kuajiri watu kutoka nchi za jirani ili kuongeza ufanisi na kuleta mabadiliko chanya katika biashara yake.

Ijumaa usiku, kabla ya safari yangu, nilikuwa na mazungumzo ya mwisho na baby mama yangu. Katika mazungumzo yetu, habari kubwa aliyonipa ilikuwa kuhusu kufuatilia kampuni ya mzee wake, ambayo alidhulumiwa na wabongo. Alionyesha wasiwasi kuhusu jinsi anavyoweza kusaidia katika kurejesha haki na kuleta uwazi katika mambo haya.

Nakumbuka niliwagusia kidogo kuhusu kampuni za ujenzi na umeme ambazo baba yake alikuwa anazimiliki hapa Dar es Salaam, mwanzoni mwa Season 1: EP 10. Baada ya Rais JPM kuingia madarakani mambo yalibadilika kwa kiasi kikubwa, hasa katika masuala ya tenda na kuamua kufunga kampuni na kurejea South ili kuendeleza kampuni zake zingine, huku akikabiliana na changamoto nyingi kutokana na mabadiliko hayo.

Kuna kampuni moja ya masuala ya electronics ambayo baba yake aliiacha, lakini wabongo wazee wa fursa walicheza na umiliki wake. Ingawa mzee wake alionekana kupotezea suala hilo, Iryn alisisitiza kwamba hali hii haiwezekani na alitaka kuchukua hatua dhidi ya watu waliofanya uhuni huo. Alijua kuwa alikuwa na hati zote zinazohitajika, na hivyo alikusudia kudeal na wahusika ili kurejesha haki na kumaliza tatizo hilo.

Iryn alinikabidhi hati zote na kuniagiza nianze kufuatilia suala hili pamoja na mwanasheria. Alinisihi sana kuhakikisha tunafanikiwa katika juhudi hizi. Aliongeza kuwa atarudi Tanzania mwezi Desemba kuangalia maendeleo ya kesi hiyo, na pia tutajadili kuhusu mradi wa kufanya Dodoma. Alionekana kuwa na matumaini kwamba kwa pamoja tunaweza kupata suluhisho na kuendeleza mipango yetu ya baadaye.

Niliingia chumbani kujiandaa, na Iryn alinifuatia kwa nyuma, akinikumbatia huku akizungusha mikono yake mbele yangu. Tulianza kukumbatiana kwa mahaba mazito, na hisia zangu zilianza kuwa na nguvu sana, kwani ilikuwa muda mrefu sijaonja ile furaha. Hali yangu ilizidi kuwa mbaya, nikijua jinsi nilivyokuwa na tamaa ya kuwa karibu naye. Tulianza kupigana makisi ya mwisho mwisho lakini sikuwa na uwezo wa kufanya chochote, sababu ya afya yake. Alichokifanya mama mtoto, alikoki RPG kwa mkono wake laini, hadi pale ambapo risasi za moto zilipotoka kwa kasi.

Nilihisi mabadiliko katika mwili wangu, na nikapata wepesi wa haraka. Tulikwenda kuoga pamoja, na nilijiandaa kwa haraka ili niweze kuongea kidogo na Momo na kumuaga kabisa. Nilitaka kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa kabla ya kuondoka.

Nilimshukuru Momo kwa uwepo wake nyumbani, kwani alikuwa anatusaidia sana kucheza na mtoto. Nilimuaga kwa kumkiss shavuni, na kisha tukaanza safari yetu kwenda airport. Niliongozana na Iryn pamoja na Samantha, ambao walinipa kampani na njiani tulikuwa tunapiga story za mwisho.

Baada ya kufika uwanja wa ndege, niliagana na mama Aria, kwani sikutaka aanze kunisubiri hadi nimalize mchakato wa kucheck-in. Sikuona haja ya wao kufanya hivyo. Nilianza kwa kumkumbatia Samantha, na nikamalizia kwa kumkumbatia mama mtoto. Cha ajabu, alinionyesha upendo kwa kunipa na ulimi, na hiyo ilileta hisia mpya za mshangao na furaha.

Saa 7 usiku, safari yangu ya kurudi Dar es Salaam ilianza, na njiani kote nilikuwa na furaha sana. Nikiwa kwenye ndege, mawazo yangu yalizunguka kuhusiana na watoto wangu, Junior na Aria. Nilitamani sana kuona wanangu wakianza kujuana mapema na kutembeleana, kwani ni damu zangu. Nikaona kuna umuhimu wa kumtafuta mzee wangu na kumshirikisha kuhusu jambo hili mapema ili kila kitu kiwe wazi. Nilijisemea, "I'm running out of time; let me do this." Hali hiyo ilinipa msukumo wa kutenda haraka ili kuhakikisha familia yangu inakuwa na muungano mzuri.

THE END OF SEASON 2

Thank you for your time!
Waiting for SEASON 3
 
For me,this is the best episode ever.

To all hard workers and hustlers out there,this financial consultation has worth more than 100M tsh. And also,this episode has unlocked the codes for those who are struggling in online taxing.

Bro,

You have my respect,big time!!
Supported
 
EXTRA EPISODE 07

BY INSIDER MAN

Biashara ya Uber ni moja ya biashara nzuri sana maana inakukutanisha na watu wengi sana wenye hadhi “status” tofauti, foreigners, matajiri na maskini nknk.

Hii biashara niliiacha baada ya kifo cha Mzee Pama kwasababu ya kumuenzi kifo chake, Pama nilikutana naye kupitia hiihii Uber. Kwasasa hii biashara naifanya kwa kuajiri vijana na ninazo Uber mbili na dereva zangu wanafanya vizuri sana hakuna ujinga wanaofanya na wale wateja zangu wote nimewaunganisha nao.

Hii biashara imenikutanisha na watu wengi sana niwe mkweli, wengi sijawaandika kabisa kwenye hii story na wengi wao bado tuna wasiliana sana maana walikuwa wateja zangu na wana niamini. Nimekutana na watu wengi sana kupitia Uber kama watu maarufu, celebrities, wanasiasa nk, kipindi nafanya hii biashara na ndo iliyonipa connections na kutoboa maisha.

Just imagine bila Uber nisingekutana na Iryn, Mzee pama, Jane, Mzee Juma, Mama wa2, Mama Janeth, Sumaiya, Lucy, Prisca na Mary nknk. Kupitia Iryn ndo niliwajua hao wengine wote, kupitia Pama nilimjua mzee Juma na Jane. Hapo unaona connection moja inafungua au inaongeza connection zingine.

Dunia hii jinsi inavyokwenda tajiri rafiki zake ni matajiri, maskini rafiki zake ni maskini, dereva rafiki zake ni madereva, mfanyabiashara rafiki zake ni wafanyabiashara, vivyohivyo kwa mkulima, mwalimu, mwanafunzi, mlevi nknk.
Sasa kama wewe maskini ufanye nini ili uweze kukutana na matajiri? kwa mtizamo wa haraka utaona ni ngumu but ni very simple, the question is how?.

Ukifuatilia kwa makini utagundua matajiri wanaingia sehemu expensive na zenye thamani kama hadhi yao, ni ngumu sana kumkuta tajiri anakula kwa mama ntilie ni kitu ambacho hakiwezekani. Matajiri wengi utawakuta wakienda kupata lunch/dinner kwenye mahotel makubwa kama Serena, Hyatt, au kwenye migahawa mikubwa na ya kisasa.

Siku mojamoja jenga utaratibu wa kutembelea haya maeneo hata sio ghali kuingia kupata dinner au lunch ni vile uoga wetu. Nenda viwanja vikubwa kama Samakisamaki nknk huko utakutana na watu wenye hadhi tofauti, mtu anayeingia Samakisamaki actually hata kipato chake si kidogo. Na ukienda maeneo kama haya kuwa mtu wa kujichanganya usipende kukaa kivyako vyako hii itakusaidia kupata watu wapya. Kwa upande wangu toka nianze kwenda haya maeneo nakutana na watu wengi sana tofauti na wana status nzuri sana.

Maeneo ya hadhi kama haya ukiingia, ukakutana na mtu yoyote kwanza atakuheshimu ataona wewe si mtu wa kawaida. Ukijenga tabia ya kutembelea haya maeneo naamini utapata connections nyingi sana na utakutana na watu wenye hadhi.

Biashara ya Uber pia ni sehemu ambayo ni rahisi sana kukutana na matajiri sababu asilimia kubwa ndo usafiri wao, mtu kama anatoka point A to B ni ngumu kutumia usafiri wake ataishia kurequest. Kama Dereva uwe unapiga nao story hawa watu acha kujikuta kauzu msome kwanza mteja ukiona ni talkative anza kupiga naye story, hii itasaidia kufungua milango mingine.

Kwa upande wa Posta/Masaki kuna ofisi nyingi sana na utawabeba Ma-Hr, Managers, C.E.O’s nknk, jitahidi uwe unafanya engagement nao usiwaogope, tengeneza connection. Mimi Insider ningekuwa nataka kuajiriwa kipindi kile bhasi ningekuwa nilipata kazi muda sana.

Cheki conversations yangu na moja ya mteja niliyekutana naye Posta,

INSIDER: “Bossy wangu naona umependeza sana na pigo za Ki-HR.”

CUSTOMER: “Mhh kaka naonekana kama HR?”

INSIDER: “Exactly nambie kama nimekosea.”

CUSTOMER: “Hahaha hamna bhana, mimi ni mtu wa kawaida tu mbona.”

INSIDER: “Ooh sawa kama kweli wewe ni HR naomba connection ya mchongo, napambana na Uber angalau mkono uende kinywani, lakini huku ni kugumu sana.”

CUSTOMER: “Jamani lakini sio mbaya Mungu atakusaidia, una elimu gani kaka?”

INSIDER: “Nina degree ya Uchumi naweza kuisaidia kampuni kwenye mambo mengi sana, kama itatokea chance naomba nikumbuke bossy wangu.”

CUSTOMER: “Kaka usijali utanipa namba yako afu utanitumia na CV kabisa incase imetokea nafasi nikupambanie.”


Sasa ukituma CV kwa watu 20 hapo unakuwa na Probability kubwa ya kupata mchongo na ukiwa na qualifications nzuri, kutoboa ni haraka sana. Hawa watu wamenitafuta sana honestly, na last week kuna dada kanipigia simu nilimtumiaga CV mwakajana nilikuwa nimemsahau, sasa kanipigia simu ili anipe connection lakini nilimwambia nimerudi shule kusoma. Unaona ni muda mrefu lakini still alikuwa na CV yangu akanikumbuka, mimi nilikuwa nimesahau kabisa.

Suala la kupata wateja Private ni juhudi zako za kupambana na kuwa mbunifu, kumbuka Uber ni biashara na mpo wengi na wengi gari zao ni nzuri, inabidi uwe mjanja sana kuwapata hawa wateja wa Private.

Ukiwa smart unajiweka vizuri, gari yako ni safi nje na ndani, gari full AC na inanukia vizuri. Naamini huwezi kosa wateja wa private na asilimia kubwa ya wateja utakao wapata ni wanawake, kingine cha muhimu mtangulize Mungu pale unavyotaka kwenda mzigoni, just pray.

Mteja mpaka anaamua kukutumia private anaangalia vitu vingi sana kutoka kwako ukiachana nakuwa na gari kali, pia customer care nayo ni muhimu sana ili kuwavutia. Wanaume hawana shida ila kwa dada zetu wanapenda sana ukiwapa customer care nzuri sana, pamoja na kuwasifia sifia yaani wanapenda sana.

Kitu kingine ambacho Uber wanafeli sana, unakuta umemchukua mteja kutoka Posta kwenda Masaki. Baada ya kumdrop unamwacha aende badala ya kumuuliza kama anarudi tena Posta ili umrudishe wewe unamuacha aende kwa hapa mnafeli sana, wengi wenu mnapishana na hela.

INSIDER: “Dada samahani unarudi tena Posta? ili nikusubiri?”

CUSTOMER: “Yes narudi ila nitachelewa kidogo, kuna customer namuattend.”

INSIDER: “Unaweza tumia muda gani maximum.”

CUSTOMER: “30 minutes maybe.”

INSIDER: “Mimi nitakuwa around kama utakaribia kumaliza just text me nianze kusogea.”

CUSTOMER: “Sawa usijali.”


30 minutes sio nyingi kwa kumsubiri customer maana kuna muda request zinakuwa shida afu biashara ni ushindani sana, lazima uwe mjanja na mbunifu. Kumbuka pia sio kila mteja atakwambia umsubiri ni wewe ujiongeze tu, sasa mteja kama huyu ukimrudisha Posta lazima atasave namba yako na ataanza kukutumia.

Kingine ukimshusha mteja kwa destination ongea naye kama atakuwa na kazi Private awe anakutumia, tengeneza na Business card zako unakuwa unawapa wateja. Ukiwapa wateja 30 business card yako kuna ambao watakutafuta tu mfanye kazi, na kumbuka ukifanya kazi na mmoja anafungua baraka ya kukuunganisha na wengine, circle yako inazidi kutanuka inafika stage unawateja wengi.

Mimi binafsi kuna stage ilifika hata Uber nikawa siwashi, yaani ile asubuhi nikiwa drop akina mama wa2 na Maggy, unakuta nina booking ya kufanya kazi na loan officers na hapo inakuwa kazi ya siku nzima.

Nilifanya kazi na hawa loan officers wa CRDB, NMB, EXIM, KCB nknk ni wengi mno nimefanya nao sana kazi, na wao kwa wao ndo walikuwa wanapeana connection wananitafuta. Malipo yanakuwaga kwa card ila sasa ikitokea wamepiga mshindo walikuwa wananipa sana hela.

Ukija kwa mtaani wengi walikuwa wananitafuta si unajua wanawake hawapendagi shida? Kama anasherehe bhasi atanitafuta tunakubaliana bei ya siku nzima afu tunafanya kazi, Dullah nilimpa connection ya mtoto wa bank na baadae kaja kuwa mke wake halali.

Nimefanya kazi nyingi sana yaani kuna muda nilikuwa napiga pesa mpaka ukiniletea story za kuajiriwa nakuona mchawi. Narudia tena kama upo smart ukifanya uber unapata kazi kwa haraka sana na maana utakutana na watu wengi wenye status tofauti.

Kitu kingine cha muhimu kwenye Uber ni uaminifu hata ukiona kitu cha thamani mteja amekisahau wewe mrudishie itakupa sifa nzuri sana. Nimekutana na simu nyingi sana kwenye gari wateja wamesahau, wallets, pochi nknk lakini nilikuwa nawarudishia kwa uaminifu na sikuwahi kuwa na tamaa.

Kitu kingine usikatae request hata kama mteja anakwenda sehemu ya mbali kama upo kazini wewe nenda cha muhimu ongea na mteja muone mnasaidianaje maana yeye anataka usafiri wewe unataka Pesa. Kama ni usiku na mteja anaingia ndani ndani sana, mchukulie bodaboda kwaajili ya usalama wako na uwe makini sana hasa kwa nyakati za usiku.

Huwa nawashangaa sana madereva wa Uber wanaolalamika kuwa biashara ni ngumu kwakweli huwa siwaelewi kabisa, kwa mwaka jana wakati Vita ya Russia/Ukraine imeanza kupamba moto kweli biashara ilikuwa ngumu sababu nauli zilipaa sana, ila kwa dereva wa Uber kutegemea request ni umaskini wa akili. Tumia Uber kukupa connections za kupata wateja wa private na sio kutegemea requests hapa utafeli tu na kuishia kulalamika biashara ni ngumu.

Jambo lingine madereva wa Uber 80% hawajatulia ni malaya, sasa ukiendekeza pussy hesabu maumivu, utaishia kuwapakia mademu bure kila wanakokwenda. Mademu wa Dar wajanja sana they know hot to manipulate a Man, hapo akikupata ana uhakika wa free Uber ya kumpeleka kwenye mishe zake. Hii tabia mpaka madem waliojariwa wanayo maana akikupata ana uhakika wa usafiri wa asubuhi, hakuna dem anayependa kupanda daladala asubuhi na kubanana hakuna.

Utakutana na mademu wengi sana kwenye hii biashara ila ukikosa self control utaishia kutembea nao na kuwagongea kwenye gari. Asilimia kubwa ya madereva wa Uber gari zao ni guest, nyie mnaotumia huu usafiri kuweni makini sana. Hawa jamaa wanagongea mademu au mashoga humo humo ya gari, usipendelee kukaa seat za nyuma ni hatari sana.

Umaskini ni mbaya sana ndugu zangu maana utakuwa unakubali kushawishika kwa vitu vidogo, sahivi mashoga asilimia kubwa wanaliwa na madereva wa Uber sababu ya njaa. Hawa watu sijui wanatoa wapi pesa kwakweli, lakini ndo kwanza wanakaa sehemu nzuri kama mbezi Beach, Mikocheni nknk.

Ukiwapakia hawa watu ni wasumbufu sana wata kutongoza sana, nimekutana nao sana hawa watu na wengi wamenisumbua sana mpaka kero, kukuwekea offa ya laki 5, million kwao ni kawaida. Sasa kwa dereva ambaye ana njaa hapa hatoboi ataishia kuwala tu, bad news mpaka mastar nao hamna kitu, kuna msanii huwa siamini kama na yeye ni chakula yaani daah! hali ni mbaya sana. Kuna presenter maarufu kanisumbua sana na niliishia kumblock lakini bado akaendelea kunitafuta kwa namba nyingine, mpaka nikamwambia nitaavujisha chats zako ndo akatulia ila hali ni mbaya sana Mungu atusaidie.

Ukiwa HB na unajipenda hawa wanawake watakutongoza sana na hasahasa wamama wanasumbua sana “mashangazi”. Mademu watakusumbua sana, nyakati za usiku utapakia mademu ambao hawajielewi wamelewa na kama unatamaa utaishia kuwala.

Dar ni mkoa mchafu sana hasa kwa nyakati za usiku, ukitaka kuamini hili wewe jaribu kutembelea maeneo ya Sinza, Masaki ndo utaona ushenzi unaofanyika. Nyakati za usiku kwa Sinza mashoga kibao wanazagaa, Masaki kuna Malaya wengi sana. Kwa Mbweni ukisikia illegal issues ndo ziko huko kama sembe, utapeli bhasi huko ndo HQ yake kwa hapa mjini. Hii Dar ione hivihivi lakini ni chafu sana, mimi Dar naijua yote hakuna kitu utakacho nidanganya na ninazifahamu chocho zote.

Mimi nilikuwa natafuta hela na sikuzote pesa utazipata kwenye mambo ya hovyo, mfano mimi nilikuwa na connection za kuwapata madem wa kizungu, kichina, kihindi nknk, kupitia Masai-Ellias na pia kuna chocho ziko Posta unawapata wazungu ni hela yako tu. Mfano madem wa kizungu minimum Price wanacharge kuanzia $300 mpaka $1,000 inadepend na quality ya mwanamke, hapo ukimuanganisha kwa tajiri hukosi hata $100-200 ya kuweka mfukoni. Mimi nashida gani? kwenda kumchukulia foreigner demu na kumplelekea hotelini na kujipatia $100 kuna kazi hapo?.

Ukiwa kwenye hio biashara utakutana na vishawishi vingi sana ukiachana na mademu, pia kuna vishawishi vya kuingia kwenye dili za kikubwa kama sembe, kusafirisha wazamiaji nknk, point hapa kuacha tamaa maana unaweza ambiwa kila kichwa cha mzamiaji ni 2M afu uwapeleke Bagamoyo hapo ukipiga hesabu una 10M, ni wachache ambao wanaweza kuikataa hii offa.

Ishu ya mwisho na muhimu kwa Dereva wa Uber ni kuzingatia usafi wako binafsi, vaa pendeza chomekea kama vile unakwenda ofisini, pulizia na unyunyu wako freshy. Kwa weekend mimi nilikuwa nakula pamba safi nimetupia jeans na t-shirt afu chini nina raba yangu kali freshy.

Usishangae haya mambo kazi ya Uber ni ngumu sana na inataka moyo, wapo watakao kudharau, kupewa kejeli ni jambo la kawaida sana, muhimu hapa wewe mind your business usipende kubishana au kugombana na wateja itakucost, kubali kuonekana mjinga ila kwa faida yako.

Katika vitu ambavyo nilijitahidi sana kuvizuia ni pamoja na wife kupanda ile Ist, maana niliona natengeneza mikosi kwa mke na mtoto. Ndomana nilikuwa nikirudi break ya kwanza ni bafuni kuoga kutoa nuksi ndo mambo mengine yaendelee, lingine nilikuwa najitahidi sana kufanya usafi wa gari.

Biashara ya Uber ni rahisi sana kukutana na watu wapya na kupata Connection nyingi sana kama utakuwa smart. Maana huku ni easy kukutana na foreigners, Celebrities , pisi kali nknk. Just assume wastani kwa siku unabeba abiria 10 mara 30= 300, zidisha mara miezi 12= 3,600. Huu ni wastani tu nimetumia, sasa kwenye hawa watu 3,600 utakosa connection hapa???.

Dereva wa Uber ukilalamika Biashara ngumu bhasi jua wewe upo kundi hili,

1. Unategemea request tu
2. Umeendekeza Mademu/Starehe
3. Hujiongezi.

Wewe utaishia kulalamika Biashara ngumu.

insiderman1@yahoo.com
Ushauri wa Gharama tumepewa BURE
 
Noted👍

Noted 👍

Noted 👍..... Lara1 bado sijasoma thread zake ila kwa Analyse haina kubisha, huyu ni 💥💥

Ndani ya Kipindi kifupi nimesoma Threads nyingi sana baada ya hio comment 👆👆 hapo juu. Aisee nimekuja kukutana na visa na Mikasa ni hatari ndugu zangu. Haya maisha yana vingi vya kujifunza yani si masiara ndugu zangu.
HAWA JAMAA HESHIMA SANA KWENU
1. leadermoe R. I. P
2. UMUGHAKA
3. LwandaMagere
4. JBourne59 Salute Sana Mzee wetu🙋🙋🤚
5. KigaKoyo
6. INSIDER MAN
7. Analyse
8. BM X6
9. konda msafi

Bado naendelea Kuzisoma kwa kasi sana nitazidi kuiongeza List. Very Inspiring Live Life Stories, Salute Sana!!!
Hata mimi nimsoma zote hizo
 
Back
Top Bottom