Jinsi Bikra Maria alivyompa mtihani kiongozi wa Kanisa, Nabii Zakaria..

Hivi nyie watu mnasoma Bible ipi hadi leo mnasema Bikra Maria! Basi Mama ngu ni Bikra bado kwani alinizaa na ka endelea kuzaa , upo wapi Ubikra wa Maria wakati aliendelea kuzaa na Joseph kwa kawaida tu hamjui kuwa YESU anao Ndugu wa Damu kwa Maria?
uwe unatoka nje ya box. ulishaambiwa Yusufu alikuwa mgane wa watoto saba kabla ya kuoa. kwanini unakuwa mvivu wa kutafuta taarifa? Yesu ana kaka zake na dada zake toka kwa mama mwingine. lakioni kwa Maria yupo mwenyewe.
 
Alichomaanisha zekaria nabii na zekaria babaye yohane ni watu wawili tofauti.zekaria babaye yohane hakuwa nabii bali kuhani yaani mwongoza ibada madhabahuni
Hapo sawa nimekusoma mkuu.

Yes walikuwepo Zekaria tofauti kwa nyakati tofauti. Huyu aliyetajwa kwenye Bible kama Nabii ndiye mwenye chapter yake ya Zekaria kwenye Agano Jipya.

Hata huyu mwongozo ibada naye inasemwa alikuwa Nabii na ndio maana mrithi wake (yaani mwanae Yohana - Mbatizaji) alirithi kazi za baba yake.

Nadhani imekaa sawa sasa!
 
Kwa maelezo yako uliyoandika unatuambia kwamba kumbe watu walikua wakiabudu kanisani kabla ya MARIA kupata mtoto?.
 
Kwa maelezo yako uliyoandika unatuambia kwamba kumbe watu walikua wakiabudu kanisani kabla ya MARIA kupata mtoto?.
Naona neno kanisa linaleta utata. Kimsingi nimelitumia kwa sababu za kimuktadha tu. Ni tafsiri ya kiistilahi wala isikubabaishe.

Halafu mbona nimefafanua vizuri hata kwenye matini ya uzi wenyewe? Au umesoma title tu?
 
Hapa inahitajika busara kubwa kukuelimisha mkuu.
as long as hakijaandikwa kwenye biblia na kinamuhusu Mungu is't Rubbish hata shetani anaweza kuandika vyakwake akasema ni vya Mungu .kwakuwa huna ujuzi wa maandiko ndiomaana unategemea maandiko nje ya biblia
 
Sipendi kuharibu hii mada nzuri ya muhusika pia najua lengo ni kuwa na uelewa mkubwa wa mambo kwa ujumla ikiwa pamoja na imani zetu

Lkn kwa sie ambao hatuamini hizi Hadith za Wayahudi na jamaa zao wa mashariki ya kati tunapita kimya hapa kwa huzuni kuu ya kwamba mtu mweusi itachukua muda sana kujisimamia

Kuna Mwanamalunde,Mkwawa , kinjekitile,Shaka , Nzinga mbandi, na kadhalika wanatakiwa kupewa heshima kubwa kuliko mtu mweupe mmoja eti ndo ‘muokozi’ wetu dah haya
 
as long as hakijaandikwa kwenye biblia na kinamuhusu Mungu is't Rubbish hata shetani anaweza kuandika vyakwake akasema ni vya Mungu .kwakuwa huna ujuzi wa maandiko ndiomaana unategemea maandiko nje ya biblia
Sawa mkuu. Uko sahihi!
 
Hawa jamaa uliowataja hapo mwishoni kuna vitabu vyao? Natamani kuwasoma vizuri wote, hasa falsafa zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni kweli mbona unashindwa kutoa sura na mstari husika kusapoti habari uliyotuletea? Usilete UTANI kwenye maandiko matakatifu. Toa ushaidi sura ipi na mstari upi kwenye Biblia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu wanataka kila kitu kiwe na reference kibiblia utafikiri ni kitabu cha historia na hata kingekuwa kitabu cha historia kisingeweza kubeba yote. Mafundisho yanarithishwa kwa maneno na maandishi. Kanisa limetunza hayo divinely hata sasa kwa msaada wa Roho Mtakatifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana mi nilikuwa najiulizaga kwa hapo.huyo yusuph anaishia kula kwa macho2 toka kwa mary mpaka anakufa.angekuwa kijana hii leo tungekuwa tunaongea mengine huenda angesha tembezaga miti bila kuangalia huyu ni mama wa roman catholic.
 
Basi ndiye huyo huyo. Baba yake alikuwa Zakaria na mama ni Elizabeth mkuu wangu.
Hapa si kweli. Yohana ambaye baba yake ni Zakaria na mama yake ni Elizabeth ndiye aliyekuja kumbatiza Yesu, yaani ni Yohana Mbatizaji, naye huyu aliuawa na Herode na kichwa chake kikatolewa kama zawadi kwa binti wa Herode siku ya birthday yake (Mathayo 14:1-12 na Marko 6:14-30). Kumbuka kuwa hata Yohana Mbatizaji alikuwa na wanafunzi wake (Luka 7:18-28) na hakuna popote katika Biblia ambako Yesu alimchukua Yohana Mbatizaji kama mwanafunzi wake.
Yohana aliyeandika Injili ya Yohana, zile nyaraka 3 na Ufunuo SIYO yule Yohana Mbatizaji mwana wa Zakaria na Elizabeth, kwani wakati hayo yanaandikwa Yohana Mbatizaji alishauawa na Herode. Yohana mwinjili na mwandishi wa nyaraka 3 na kitabu cha Ufunuo ni mwana wa Zebedayo (Luka 5:10). Yohana huyu alikuwa na nduguye aitwaye Yakobo. Vijana hawa wawili mama yao aliwaleta kwa Yesu akamwomba wakae mmoja kulia na mwingine kushoto kwa Yesu katika ufalme wake (Mathayo 20:20-28), na hawa walikuwa miongoni mwa mitume 12 wa Yesu kama walivyoorodheshwa katika Marko 3:13-18.
Tumsifu Yesu Kristo.
 
Reactions: IoT
Milele Amina.

Nilisahihisha mkuu. Awali wakati naandika nilishindwa kuwatofautisha.

Yanayobaki yapo kama yalivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eeh kwakweli, I wonder

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maria hakufa mkuu,, alipalizwa Binguni...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimebahatika kugika hapo na nipo mpaka sasa kiukweli namshukurubsana Mungu ninayo yaona na nikiisoma Bible huku naona live .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mara ya kwanza kusikia simulizi kama hili. Linahitaji sources ili kujiridhisha zaidi na kuamini uhalisiwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…