Jinsi carryover ya mwaka wa kwanza ilivyotaka kunisababisha nisi-graduate chuo

Ungekuwa Muhimbili wangekuwa washakula kichwa.
 
Yess ndo nilitakaa kuelezea hii hapa.
 
Yess ndo nlitakaa kuelezeaa hii hapa.
Watu wanaona noma miaka ya nyuma kwa hizi college coursework ya 16 ilikuwa ina matter watu wakawa wanadisco sana. Imeondokewa lakini bado mambo hayajabadilika bado watu wanaliwa vichwa tu ukisema uweke 16 watakaofaulu hawatozidi 10 CONAS na COET
 
Mi naona sio ugumu wa course ila ni ugumu wa malecturer. Kozi kama hizohizo za coet & conas vyuo vingine mbona wanapata coursework 40% kawaida tuu.

Lecturers wa public universities za bongo ni wazinguzi sana. Halafu unakuta anafundisha na vyuo vya private ambako hazingui kama huku public. Hakuna chuo cha private kitakuchekea endapo utasubmit matokeo ambayo nusu ya wanafunzi wamefeli.
 
Umeongea ukweli malecturer wa public unis wanaona sifa kufelisha wanafunzi
 
Hata Udom kuna college kama Earth Science and Engineering, miaka ile course work ya 16 ilikuwa haizingatiwi sana make mziki ni "mziki mnene" kama wa EFM
 
yaani unacarry mara mbili na bado unaendelea kuwa mwanafunzi?hicho chuo wanatumia system ama inakuaje make mi najua ukicarry mara mbili system inakukataa
Humu ndani mnatiana pressure za bure ku carry mara mbili sio shida wala mtu hawezi disco labda kama GPA yake iwe ndogo sana ndio anaweza disco tofauti na hapo ni uongo vijana someni vizuri hizo prospectus za vyuo vyenu
 
Humu ndani mnatiana pressure za bure ku carry mara mbili sio shida wala mtu hawezi disco labda kama GPA yake iwe ndogo sana ndio anaweza disco tofauti na hapo ni uongo vijana someni vizuri hizo prospectus za vyuo vyenu
Si ndio hapo mkuu mimi japo nilicarry mara 2 ila sijawahi kupata sup ya somo lingine na GPA haikuwahi kushuka chini ya 3.5
 
Sio tu uki carry zaidi ya mara moja.
Hata hiyo course work yako ya under 16 usingefanya UE.
Kuna vyuo kwenye hii nchi, ni kama wako vitani
Hata sisi chuo course work chini ya 10 kwa masomo mengine na 15 kwa core subject ni technical sup. Hata UE upate 100% bado utakua umesup tu.

Nimeshangaa jamaa ana coursework ya 8 na bado anapambana UE eti atatoboa.

Vyuo vinatofautiana sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…