King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Qnet, Forever ni Matapeli.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Morning my Business partner/hubby, hivi makumbusho na posta ndiyo centre za mambo ya network marketing?, nakumbuka kuna mtu alinipeleka "Forever living " makumbusho huko huko waliongeaa wakaongea nikawa nawasikiliza ila inakuja inakataa yani + nilikua broke vibaya at the end nikawaambia sina mtaji na bidhaa zao ni ghali mno dawa ya meno 40,000/= sijui 25,000/= hivi Buza kwetu huko ningemuuzia nani jamani watu tunanunua whitedent letu kubwaa 2500/= tu😀😀Good morning business partner!
Siku nitakupeleka makumbusho & posta ukawasikilize kwa mtu asiye makini nguvu yao ya ushawishi wanaangukia humo.
Ila sitokuacha kule pekee yako honey !
Ndugu, kazi ya kufundisha na yeye mwalimu kuingizwa chaka ni vitu viwili tofauti.Sasa kama Mwalim anaingizwa chaka namna hii je hao anaowafundisha wanajifunza nn kutoka kwake?
Hakika mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Kwa kitendo alicho kifanya DC wa Hai kuwaokoa walimu walio ingizwa mkenge na wajanja wa mjin ni kitendo cha pongezi .
Haiwezekani biashara izi za chain market ziwe njia ya kuwalalia walala hoi kwa mzunguko wake usiokuwa na faida yenye mashiko na kuendeshwa kinyume na utaratibu wa nchi
Sasa si kama ambavyo una sikia serikal ya magu inachelewesha kuwalipa wastaafu mafao yao ss hapo tayar ni changamotoWalimu ni wahanga wakubwa wa matapeli, sielewi ni kwanini!
Juzi juzi mwl mmoja mstaafu kule Kahama amesaidiwa na TAKUKURU kunasuliwa kutoka ktk mkataba wa kitapeliwa wa riba ya 200%!
Hahah nasema uongo ndg zanguuuuuuuuuuuuuuuuuuu?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Umenikumbusha mbali, kweli picha hazifutiki mitandaoni
Hao wazee wa good morning asubuhi, mchana good morning, jioni good morning, usiku good morning ni matapeli tu mbona. Halafu watu wenyewe wanaokwambia eti utapata mamilioni wao wenyewe wamechoka kinoma kimaisha ila wana ushawishi wa hatari kama madalali. Pale Mwanza wanazo ofisi zao Nyegezi nyuma ya stand inayojengwa na ofisi zao kwa nje hakuna bango lolote la kuonyesha ni shughuli gani inaendelea humo ndani. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza au Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana fanyieni kazi jambo hilo.HAI, KILIMANJARO
Mkuu wa wilaya ya HAI, Mkoani Kilimanjaro Lengai ole Sabaya amemsweka ndani mtumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Dominica Mwapombe kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa kitapeli na kufanikiwa kujipatia mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu kwa njia ya udanganyifu.
Aidha ameiagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru wilayani humo, kufanya uchunguzi wa kina juu tukio hilo na kuchukua hatua za kisheria.
Sabaya amefikia uamuzi huo Mara baada ya kupokea malalamiko ya watu mbalimbali wakiweno walimu waliofika ofisini kwake wakidai kutapeliwa na Mwapombe
Kupitia taasisi ya biashara ya Qnet Marketing ambapo yeye ni mwakilishi wake.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, Mwapombe ambaye ni afisa ugavi wa halmashauri hiyo amefanikiwa kuchota mamilioni ya fedha kutoka kwa walimu na wafanyabiashara (majina yamehifadhiwa) waliopo katika wilaya hiyo baada ya kuwashawishi na kufanikiwa kuwaunganisha na mtandao wa kibiashara wa Qnet.
Walimu wanne na mfanyabiashara mmoja waliohojiwa na mkuu huyo wa wilaya katika mkutano wa walimu uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo, walidai kumpatia mtuhumiwa mamilioni ya fedha kwa makubaliano kwamba watapokea kiasi cha dola 200 kila mwezi na kwamba ili upate kiasi hicho lazima ulete mwanachama wawili ama watatu wa kujiunga na mtandao huo.
"Kuna walimu na wafanyabiashara wamefika ofisini kwangu kulalamika kutapeliwa na taasisi ya Qnet kupitia Mwampombe na wenzake kuna mwalimu amelipa kiingilio cha Sh. milioni 4.2, kuna aliyetoa Sh. milioni 4.3, mwingine amelipa Sh. million 3.5 na mwingine ametoa Sh. milion 1.6 "
"Hawa wote waliahidiwa kupokea sh, laki NNE kwa mwezi lakini tangu wametoa fedha hizo kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu hawajawali kupokea chochote kwa sababu hawajaleta wanachama, sasa huu ni utapeli kama matapeli wengine" alisema Sabaya.
Aliongeza kuwa mtandao huo wa Qnet haujasajiriwa kupitia wakala wa usajiri wa makampuni (BRELA), hii ni baada ya kupiga simu kwa mkurugenzi wa Brela, David Nyaisa ambaye kupitia simu ya mkuu huyo wa wilaya iliyokuwa imewekwa sauti alithibitisha kuwa kampuni hiyo haina usajiri.
Mmoja ya walimu hao(Jina limehifadhiwa) akiongea katika mkutano huo,alisema alishawishiwa na rafiki yake kujiunga na mtandao huo na kutoa kiasi cha sh milioni 4.3 kwa mtuhumiwa ,akiahidiwa kupokea dola 200 kila mwezi baada ya kuwa ameleta wanachama wengine huku akipewa zawadi ya saa na cheni.
"Tangu nimetoa hii hela tarehe 5mwezi wa kwanza mwaka huu sijaona hela yoyote nimeingiziwa kwenye akaunti yangu na kila nikiwafuata kuwaomba hata lisiti wanadai nitaingiziwa kwenye mtandao ,nakuomba mheshimiwa unisaidie maana ndoa yangu ipo mashakani" Alisema mmoja ya wahanga wa tukio hilo.
Kwa upande wa mtuhumiwa ambaye ni mwakilishi wa Qnet alisema kuwa kampuni hiyo ni ya kibiashara na imesajiriwa kwa ajili ya kufanya biashara kwenye mtandao.
"Kwanza Mimi sio mwajiriwa wa Qnet ni mwakilishi huru na hii biashara niyakwenye mtandao hata kwenye ilani ya 61 ya ccm inaeleza mkakati wa kuimarisha biashara ya kwenye mtandao" alisema Mwapombe.
Ends...
Picha 1 ,DC Sabaya
Picha 2,Mtuhumiwa wa utapeli wakati akihojiwa.
Picha 3,Mhanga wa utapeli akielezea jinsi alivyotapeliwa.
View attachment 1646957View attachment 1646958View attachment 1646961
Kuna ukweli fulani naona haujawekwa wazi. Qnet ni mojawapo wa sponsors wa timu tajiri Manchester City.Hii video Ole Sabaya kampigia simu Mkuregenzi Brela kasema haijasajiliwa na walisha toa tahadhari kwa bahadhi ya taasisi ya serekali zilipo omba kujua uhakika wake : DC SABAYA AINGILIA KATI SAKATA LA WANANCHI KUTAPELIWA