Jinsi DC Sabaya alivyomnasa Afisa Ugani na mtandao wa kitapeli wa Q NET alivyochota mamilioni ya watu

Good morning business partner!

Siku nitakupeleka makumbusho & posta ukawasikilize kwa mtu asiye makini nguvu yao ya ushawishi wanaangukia humo.

Ila sitokuacha kule pekee yako honey !
Morning my Business partner/hubby, hivi makumbusho na posta ndiyo centre za mambo ya network marketing?, nakumbuka kuna mtu alinipeleka "Forever living " makumbusho huko huko waliongeaa wakaongea nikawa nawasikiliza ila inakuja inakataa yani + nilikua broke vibaya at the end nikawaambia sina mtaji na bidhaa zao ni ghali mno dawa ya meno 40,000/= sijui 25,000/= hivi Buza kwetu huko ningemuuzia nani jamani watu tunanunua whitedent letu kubwaa 2500/= tu😀😀
 
Walimu ni wahanga wakubwa wa matapeli, sielewi ni kwanini!
Juzi juzi mwl mmoja mstaafu kule Kahama amesaidiwa na TAKUKURU kunasuliwa kutoka ktk mkataba wa kitapeliwa wa riba ya 200%!
 
Walimu ni wahanga wakubwa wa matapeli, sielewi ni kwanini!
Juzi juzi mwl mmoja mstaafu kule Kahama amesaidiwa na TAKUKURU kunasuliwa kutoka ktk mkataba wa kitapeliwa wa riba ya 200%!
Sasa si kama ambavyo una sikia serikal ya magu inachelewesha kuwalipa wastaafu mafao yao ss hapo tayar ni changamoto
 
Hao wazee wa good morning asubuhi, mchana good morning, jioni good morning, usiku good morning ni matapeli tu mbona. Halafu watu wenyewe wanaokwambia eti utapata mamilioni wao wenyewe wamechoka kinoma kimaisha ila wana ushawishi wa hatari kama madalali. Pale Mwanza wanazo ofisi zao Nyegezi nyuma ya stand inayojengwa na ofisi zao kwa nje hakuna bango lolote la kuonyesha ni shughuli gani inaendelea humo ndani. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza au Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana fanyieni kazi jambo hilo.
 
huyu DC Sabaya napenda sana nmana yake ya utendaji, nadhani kwa style yake ya kupiga kazi kwa haraka na kwa wakati ange fiti sana DAR.
 
Hamna lolote hapo huyo Pimbi atavuta hela na jamaa watamwachia kiki zinatafutwa .
 
Hawa Q-net wametapakaa karibu kila Mkoa. Wakifanikiwa kumtapeli mmoja wenu katika eneo lenu, huyo sasa atakuja kuwatapeli ninyi akiwa anajua au hajui kuwa yeye mwenyewe katapeliwa na hivyo hata ninyi anawatapeli. Anayekuja kwako kukushawishi kuingia kwenye mtego huo ni yule anayekufahamu na mnafahamiana vilivyo na pengine ni rafiki au ndugu yako kabisa.
 
Jamaa yangu alinipeleka pale Moshi mitaa ya soko la meimoria, akitaka nijiunge. Sikurudi tena. Cha kushangaza walikuwa na leseni na watu walishakalamika lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Nilienda pale nikiwa na kumbukumbu ya rafiki yangu aliyetapeliwa sh. milion 5 na pyramid scheme ingine iliyokuwa inajulikana km D9. So nikajua ni wale wale.
 
GOOD MORNING!! Alafu ni saa 10 jioni. Ndio salamu yao ukienda ofisini kwao. Kama hujitambui na hufikiri nje ya box jamaa wana ushawishi, ulaghai mwingi sana. Watu wamepigwa kwelikweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…