lord atkin
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 257
- 922
Katika barua yake kwa umma Mhe Dk Emmanuel Nchimbi amesema kwamba nanukuu
"... nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mhe. Rais anatamani mabadiliko, hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu...."
Alipoona baadhi ya viongozi na wabunge wa ccm wanasimama hadharani na kumuita Yuda alidhani wanajituma wenyewe. Baadaye akapelekewa wito wa kumwita kwenye kamati ya maadili ya chama akaipokea. Siku ya kikao husika hakwenda kuhojiwa na kamati. Safari hii wakaandika barua kali zaidi wakimwita kwenye kamati kwa kikao kingine ambacho pia hakwenda.
Baadaye akapata taarifa kuwa wameitisha kikao cha kamati kuu cha dharura kwa ajili ya kumjadili na kumvua uanachama ili akose sifa za kuwa makamu wa Rais kwa mujibu wa katiba. Hapo ndipo sasa alipojiridhisha pasipo shaka kwamba Mhe. Rais anatamani mabadiliko. Akabaki na machaguo mawili, atimize ahadi yake ya kupisha makamu wa Rais mwingine ateuliwe au akomae wakamvue uanachama wao wenyewe.
Ama kwa hakika uamuzi aliochukua wa kuwawahi siku moja kabla ya kikao chao ni mzuri. Ni uamuzi ambao umemwacha na heshima kuliko angeondolewa na wao wenyewe. Kwa sasa sidhani kama wataendelea kumjadili na kumvua uanachama. Hata wakiamua wachukue kadi yao bado maamuzi yao yatakuwa overtaken by events kwa sababu ameshasema anastaafu siasa hivyo hata hiyo kadi haina kazi.