Pre GE2025 Jinsi Freeman Mbowe anavyoenda kumfuta Lissu kwenye siasa za Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mpaka Leo wapo baadhi hawajakubali yale matokeo.

Lusungo Retired Fundi Mchundo Quinine
Sijamsikia hata mtu mmoja akisema kuwa Tundu Lissu sio Mwenyekiti wa Chadema. Lakini kukubali matokeo hakumaanishi tukubali kila kitu anachosema au anachofanya Tundu Lissu. Kwa wengine wetu Tundu Lissu ni mwanasiasa kama mwanasiasa mwingine Tanzania. Na kwa sababu hiyo anastahili kukosolewa hata kupingwa pale inapobidi. Kufanya tofauti ya hiyo ni kumuabudu na hiyo haitakuwa kumtendea haki.

Tulimpinga kwa sababu ya kampeni chafu aliyoifanya. Kushinda kwake uchaguzi hakubadili msimamo wetu. Ni yeye ndie anayetakiwa kututhibitishia kuwa Lissu wa kampeni sio Lissu Mwenyekiti.

Amandla...
 
Aibu yako hii
 
Mpaka Leo wapo baadhi hawajakubali yale matokeo.

Lusungo Retired Fundi Mchundo Quinine
Mimi unielewe. Sina shida na Lisu na wala sina uswahiba na Mbowe hata kidogo. Sijawahi kumshabikia Mbowe hata mara moja. Niliisuport chadema kwa vile malengo yake yanaoana na matamanio yangu kuibadiri Tanzania kutoaka kwa unyangau wa CCM.

TATIZO LANGU NA LISU:Ni namna Lisu and team walivyomdhalilisha/mbagaza Mbowe kwa uongo wakasahau kuwa wanakigawa chama! Nikamuona Lisu aliyekuwa my favorite politician kumbe hovyo...mroho wa madaraka, anaweza akafanya lolote apate madaraka!

akasahau kuwa kama siyo Mbowe kusema Muhimbili katu simpeleki Lisu, angelimalizwa Muhimbili maana waliompiga rrisasi wangelimfuata Muhimbili kwa njia nyingine!
 

Attachments

  • MBOWE.mp4
    36.7 MB
Mi nimeamua kuwaponda vichwa kwasababu nimegundua hawa wapambe wana akili ndogo sana na wengi wao ni wanywa visungura!
 
Ukweli wengi wenu mnatamani Sana kumuona mwenyekiti mpya akikwama/akishindwa Ili mpate hoja za kumkosoa.
 
Ukweli wengi wenu mnatamani Sana kumuona mwenyekiti mpya akikwama/akishindwa Ili mpate hoja za kumkosoa.
Sisi hoja yetu ni kwamba alifanya kampeni chafu. Sisi tunachotaka ni akiletee mafanikio chama chake ambayo mnasema Mbowe alishindwa kwa sababu alilambisha asali na alipokea mshiko wa mama Abduli. Akikwama au akishindwa hana wa kumsingizia ingawa tayari mmeishaanza juhudi za kumtafuta mtu wa kumuangushia jumba bovu. Mara mbona Freeman haonekani, mara Aidan hana mchango wowote kwa CDM.
Akifanikisha jambo tutamsifia, na akishindwa tutamkosoa.

Amandla...
 
Tayari mwamba wako kashabwagwa.
Ila ukweli lissu hajui siasa wala uchumi. Anajua sheria tu tena zile za kiwakili. Sasa siasa na uwakili wapi na wapi. Ndio maana yeye issues zake ni za kisheria tu. Utasikia katiba mpya, no reforms no election, watu kupotea, haki za binadamu etc etc. Kwamba nini sera yake kiuchumi na kijamii hajui wala husikii kitu kutoka kwake. Alichowahi kusema yeye ni muomini wa demokrasia ya kiliberali. Ile ya uhuru wa kila kitu. Kuanzia uhuru wa kudhulumu maskini hadi uhuru wa ushoga.
 
Uchafu mnauleta ninyi wazushi!

Uchaguzi wa mwenyekiti ulikuwa huru na wa haki, mpaka Mbowe akashindwa kwa kuridhika na kumuunga mkono mshindi.

Kungelikuwa na rough yoyote, Mbowe angesema.

Sasa ninyi ni nani wa kusema Lisu alitumia kampeni chafu?

Neno hilo la uchafu mnalisema kwa kulirudia bila kufafanua ni uchafu gani Lisu alioufanya kwenye kampeni hizo?
 
Naona Mbowe aliposema kuwa kuna character assassination wewe ulielewa kuwa anasifia kampeni iliyokuwa ikiendeshwa na Lissu.

Hata mjaribu kujisafisha vipi lakini kampeni yenu ilijitahidi sana kumchafua Mwenyekiti Mbowe.

Mbowe ni muungwana ndio maana hakupinga matokeo na sasa hivi anaendelea na biashara zake kama alivyo ahidi.

Amandla...
 
umemaliza kila kitu! Lisu ni shetani wa madaraka, anaweza kufanya /kusaliti lolote apate madaaraka. ka amemsaliti Mbowe aliyeokoa maisha yake kwa kusema Muhimbili haendi maana watammaliza, leo angelimtukana/kumdhalilisha/kumbagaza Mbowe? Lisu hafai kabisa....mroho wa madaraka. Hii ni kasoro kubwa sana tena sana amejipaka
 
Sidhani kama ni shetani lakini mengi nakubaliana na wewe. Kwa mawazo yangu yeye na wafuasi wake ndio wanapaswa kutuonyesha kuwa hatumtendei haki na yale yalikuwa ni mambo ya kampeni tu.

Amandla...
 
MH! MAMBO YA KAMPENI KUMSEMEA MTU CHARACTER ASSASSINATION? HAPANA. WATU WANAAMINI KUWA MBOOWE ALIKULA RUSHWA YA ABDUL....HII SIYO SAWA
Kwa kweli ule ulikuwa uovu uliopitiliza. Hapa suala sio kusamehe au kusahau bali ni kujaribu kusonga mbele. Kusahau au kupuuzia haiwezekani.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…