Jinsi gani ya kukabiliana na wizi/utapeli unaotokana na kusemeshwa na kupumbazwa na mtu usiyemjua?

Sio Wote ni Kutapeliwa Mkuu! Wengine ni kupumbazwa TU! Shukuru Mungu TU Wewe hayajakufika. Usiwaona Wote Wajina na Waliponzwa na Tamaa zao!!
Mkuu kupumbazwa na dawa hilo nitalikataa kata kata. Kungekuwa na 'utaalam'' huo ni watu wengi wangelizwa.
 
Mkuu kupumbazwa na dawa hilo nitalikataa kata kata. Kungekuwa na 'utaalam'' huo ni watu wengi wangelizwa.
Kuna mama mmoja alikua mpangaji wetu mda kidogo, alikua wale mama(asili ya upemba) flani wapenda mikufu na urembo urembo wa ghali,
Siku baada ya tukio mfanyakazi kazi alisema alitumwa na watu ambao alikutana nao barabarani akapewa maelekezo akafanya kama alivoambiwa aliingia ndani akachuku mikufu yote, simu na pesa akawapeleka kwa majama
 
Huyo ''alileweshwa'' kwa maneno tu. Tapeli yoyote anachota akili za windo lake na kuaminisha kuwa lile jambo ni la kweli. Kwa mfano unapoambiwa utapata fedha nyingi za chap chap basi akili zako zote zinakuwa kwenye kupata na hutakumbukuka tena vitu vingine.
 
Jamaa ni mafundi balaaa sijui mumewe atamwambia nini[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Dadeki yani wale wahuni sioo nimetoka zangu home naenda kazini kwa mama mwaka 2011 hiyo nina visimu vile kinokia kile obama sijui na hela kama elfu 10 hivi... Mmoja akaja akaniuliza samahani unajua sehemu flani wanauza madini nataka nikauze madini yangu sema ukinionesha tutagawan hela alikuwa mbabu hivi.. nkasema sipajui ghafla akatokea mbaba kwa nyuma yule mzee akamuuliza pia yule baba akasema anapajua so akaniomba na mimi nimsaidie tumsindikize hela tutagawana mamaee laiti ningejua ambacho kingenikuta nisingeingia tamaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yani nikaanza kuwafata ila kuna saa nikawa nasita yule mbabu akafika point akasema nimechoka kutembea wajukuu zangu mnaonaje mkauze hela mniletee aisee yule mbaba akasema sawa mzee tuamini yule mzee akasema bhasi mniachie hata Hela au kama hamna niachieni simu maana nawapa madini je msiporudi?? Aiseee sikujua sikujuaaa nikatoa simu na yule baba akampa yake tukachukua madini tukaanza kutembea tukakatisha kona kama mbili yule Baba akasema nisubiri hapa nihakikishe yule babu asijetutoroka shika haya madini nakuja yani Nkajiona bonge la mjanjaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] likapita nusu saa mtu harudi ndo akili ikaja nifungue kikaratasi dadeki udongoo tu na maweee pale nlipomuacha babu nimerudi kweupee nyie nyiee Kulia nksashindwa kucheka nkashindwa nikabaki nimeduwaa kama dak 10 siamini kisimu changu na hela vimeenda[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] Nkaanza safari ya kurudi home huku kama akili imeniruka ndo nkaanza kuliaa huku naendaa mbwaa wale walinifundisha uhuni mapema hadi leo Simuelekezi mtu yani hata iweje.
 
Hata wewe oooops nigga.
 
Pole sana [emoji23][emoji23]
 
Home maza nikashindwa kumelezea imekuwaje ila mzee alielewa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Adhabu sikununuliwa kisimu tena
Tunajifunza kupitia makosa [emoji16][emoji16]
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dah ukakaa zako unahisi una madini ya mamilioni
 

Afu jamaa wakishakuibia hata ipite miezi mingapi huwaoni ng’o
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dah ukakaa zako unahisi una madini ya mamilioni
Yani kuna saa nikajisemea huyu boya sijui nimtoroke[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nyie nyie sasa ningeenda kufungulia nyumbani ndo ningezimia kabisa
 
Vuta ganja ukomaze akili ili uepushe matatizo madogo kama hayo...kwanza ni wachache watakaopata ujasiri hata wa kukusogelea🐒
Katikati ya hii comment kuna jibu -Ukomaze akili

Nb: sio lazima utumie ganja lakini, ila fanya ukomaze akili itasaidia kwa kiasi kikubwa sana.
 
Hao uliowataja wengine wameibiwa kwa ujinga wa kutaka kupata faida haraka haraka. Wewe unakutana na mtu usiyemjua anakwambia mambo ya nyota sijui anakuuliza akiba ya pesa bado unamjibu tu? Huo ni ujinga tu hamna ulozi hapo. Ngoja niwape visa vyangu viwili nilivyokutana na wapumbavu kama hao nikawatoa nishai.
Wa kwanza nilikutana naye Dodoma nikiwa na mishe za biashara. Tulipokutana akanisalimia kwa bashasha na kujitambulisha kuwa yeye ni polisi. Akaendelea kusema kuna pesa imeibuwa na wao wanazitafuta kwa kukagua pesa kwa watu wanaowahisi. Akiwa bado anaongea akatokea mwenzake akajifanya katoka kuuza karanga na pia amekubali hela zake zikaguliwe. Basi nikawa nishausoma mchezo.
Nikamuuliza mnakagulia wapi akasema kule (kuonyesha kwa kidole). Moyoni nikasema ngoja niende ila kama ni uchochoroni nagoma. Tulipofika tukakaa sehemu ya wazi. Akaanza mwenzangu akawapa walet wakaenda uchochoroni na kujifanya wamekagua wakarudi. Wakasema yeye hana shida. Zamu ikawa yangu niwapatie wallet. Hahaa niliwapa za uso hawakuamini macho yao. Niligoma na kuondoka kwa dharau sana kuonyesha nimewajua nia yao.
Kisa cha pili ni dar es salaam posta pale baharini. Mwaka 2006 askofu Gamanywa akiwa na kanisa lake limeanza pale viwanja vya sabasaba alikua maarufu sana nchi nzima. Basi nikiwa napunga upepo wa bahari akanisogelea jamaa mmoja mtanashati sana. Akajitambulisha kuwa yeye katoka mtwara amekuja dsm kuonana na Askofu Gamanywa. Pia Mungu anamtumia yeye kufanya miujiza. Nikajua ni wale wale ngoja niendelee kumpotezea muda😂😂😂😂😂.

Basi akaniuliza unaamini Mungu anatenda miujiza nikasema ndio. Akasema leta mkono nikampatia. Akauangalia akaanza kujifanya anatabiri mambo ya familia. Nikawa namwitikia kua anayosema ni kweli tupu. (Alivyo mjinga naye akajiona amenipata). Basi kama kawaida akaja na wapili naye akatabiriwa ila walikua wamoja nilivyowaona. Baadae akasema twende kanisa la jirani tukamalizie maombi. Na kwamba yule aliyetukuta atatangulia, mimi nitakua katikati na yeye atakua nyuma anafanya maombi huku tunaelekea kanisa la jirani.
Huo mpangilio wa kwenda kanisani nikajua ni mtego tosha. Wanataka wanipitishe chocho nikose pa kukimbilia. Ndipo nilipowabadilikia jamaa na kuanza kumpa makavu. Jamaa walikua wapole hao. Nikawatisha naita polisi. Wakaniomba msamaha yaishe.

Funzo. Kama huwezi himili kumsikiliza mtu usiyemjua acha kabisa. Utaibiwa kijinga kisha usingizie ulipumbazwa. Tusipende kupata vitu kwa njia rahisi.
 
Asante katikati ya hii comment kuna hints 'wahanga wengi ni wanawake' na pombe, zinaa, uchafu. Mi naona hivi ni viashiria vya kupenda kukubaliana na linalokuja mbele yako bila kujihoji[kumake sense kwanza]🤔.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…