Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu usiende huko..unataka kutuharibia uzi..introverts hatupendi ligi.Ni kweli tunapata taabu sana kuchangamana na watu wenye IQ ndogo kama maccm
📌Nyie wanawake mnatukataa kwa kusudi tena mnasema hatujui kutongoza
📌Mweka mada hajagusia makundi manne ya watu huko ndo ungeelewa introvert na uongozi upoje... Nitagusia kiasi ktk introvert Kuna makundi mawili pia ya watu melancholic na phlegmatic.. ktk makundi haya mawili ya kiintrovert melancholic anafaa zaidi kuwa kiongozi maana kwanza ndie mtafakariji mkubwa kushinda makundi mengine.. hivyo huyu anaweza kutoa dira ya nini kifanyike au kipi kifatwe.. ktk extrovert pia Kuna aina mbili za watu sanguine na choleric,chorelic in natural kabisa ndio huwa wanapenda kuwa kiongozi! Huyu akiwepo mahali mbawa zake za uongozi hujionyesha ila tatizo lao hawana maamuzi yenye tafakari pana Sana na huwa ni konki yani Kama hutaki toka kama unataka twende.. huyu akiwa anaongoza ndio wale dizaini ya watu wasiotaka mchezo,hana la kulemba atakapotaka kupita yeye ni ama umpishe apite au akukanyage!!.. binafsi nawaona ni viongozi wanaofaa zaidi kwenye maamuzi magumu tofauti na melancholic maana hawa Mambo yao ya taratibu maana inahitaji muda kufikiri vya kutosha,pia wanasikiliza Sana I can say ni demokratic people!.. maana anataka kila mtu amridhishe.. akikaa kwenye uongozi huyu mtafurahia kufokewa si hulka yake,muelewa na wapole lkn ubovu ndio hapo kwenye maamuzi magumu hutumia muda Sana sana.. si wazuri kwenye maamuzi magumu!.. ndio maana huonekana ni dhaifu sometimes na akizinguliwa Sana hujiengua maana as you know introvert ni watu wa kujilaumu Sana!..
So kipi kinafaa.. kinachofaa ni kuwa na kombination ya choleric na melancholic.. ili walau kuziba gapes kadhaa za udhaifu.. melancholic atatoa wazo choleric atawaongoza wengine kulifuata wazo.. lkn hawa wote itafaa zaidi wakiwa wanaelewana kinamna maana Kama melancholic ndo anaongoza halafu choleric yupo chini yake basi melancholic akizubaa anaweza pinduliwa haswa akileta sana u demokrasia!
Ndio maana muda mwengine umekuwa ukisikia mapinduzi yakifanyika hata ktk ngazi za nchi!.. so hii sometimes ukijachunguza utajua ndani yake kuna hizi personality haswa kwa choleric hupenda Sana kuongoza.. we ukisema hapa hapana njia mwenzako anaona njia! Haijalishi mtapita kwa tabu ye anachoangalia mtapita tu!.. melancholic akiona hapana njia atataka kutafuta njia na akiipata mtapita Tena kiwepesi kabisa!..
Ukiweza kujichunguza ukaelewa upo wapi ndugu unaweza kuwa kiongozi Cha muhimu nikujielewa wapi upo imara na wapi haupo imara njia zote hizi zinafaa kuongoza isipokuwa tu ujue muda gani wa kutumia u choleric na ni muda gani wa kutumia u melancholic.. mifano ya viongozi ambao ni choleric ni Idd amin.. kwa upande wa melancholic tulishapata hapa kwetu ni baba wa taifa julias kambarage nyerere.. phlegmatic huwa namuhisi ni jakaya japo sijamchambua vyakutosha sana sina hakika asilimia Mia ila anaonyesha anahizo element za u phlegmatic.. tulienae sahivi sisemi sana ukiangalia tu utajua ni pure choleric..😂 naomba nisiseme Sana..
Moja Kati ya sehemu niliyokuja kumpendea nyerere ni ktk kufanya uamuzi wa Vita Kati yetu na Uganda.. ileweke hivi introvert people haswa melancholic hupenda kutumia logic sana hufanya vitu kwa kujibu haya maswali "how..? When..? Why..? Mengine nimeyasahau ila huwa yapo matano.. ktk vita ya Uganda na tz ile hotuba ya nyerere ukiiangalia inaviashilia hivyo alisema "Nia ya kumpiga tunayo,sababu ya kumpiga tunayo na uwezo wa kumpiga tunao" ukiiangalia hizo kauli unaweza zichukulia juu juu lkn hizo zinaweza kukuongoza hata kwenye kutatua tushida fulani Kama ukiwa muelewa..
Naomba niishie hapo.
[emoji3][emoji3][emoji3]Nyie wanawake mnatukataa kwa kusudi tena mnasema hatujui kutongoza
Mkuu sisi furaha huwa haioneshwi public. Ila kwa watu wetu wa karibu ndio hutujua tukiwa excitedBado nawauliza kuzaliwa Introvet ni kama balaa au
Kwan hakuna intro wenye FURAHA na MAISHA
Duuuh hatari sana aisee. Kumbe haya mambo yako hivi, hata ku-approach warembo ni shidaWalimwengu wananifanya niwe extro baadhi ya nyakati na najisikia mwepesi sana nikiwa hivyo kuliko nikiwa kwenye asili yangu hiyo ya intro
Duuuh naomba kama kuna kitabu au maandishi yanayoelezea haya mambo, nisaidie walau jina ndugu ili walau nijifunze, maana inaonekana kuna siri zimejigichaTarehe 10 ,1,19,28 wote mko kundi moja
Kabisa [emoji3][emoji3][emoji3]Bro naona ulikua muhanga wa VPN
Mie rafiki zangu wananiuliza we mwenzetu una demu kweli?Nyie wanawake mnatukataa kwa kusudi tena mnasema hatujui kutongoza
Hii haihusiani na mtu kuwa domo zege au la. Watu wanashindwa kuelewa maana halisi ya gentleman. Kuna watu mpka leo hii wanaamini ya kwamba mwanaume huwezi kukamilika bila demu na halikadhalika kwa upande wa pili vivyo hivyo. Its just most introverts don't want to rush things when it comes to relationships. We take relationships very seriously. We are vulnerable creatures means we easily get hurt physically and emotionaly. And thats why we would rather spend 3 years alone than being in a dramatic crazy relationship as we don't want to get hurt and thus we would never want to hurt others too.Mie rafiki zangu wananiuliza we mwenzetu una demu kweli?
Hilo swali naulizwa sana wengine wananipa majina domo zege huezi kua na demu.
Mwengine aliwahi kunambia jamaa angu tatizo lako unatafakari sana hata sehem ya kukanyaga mguu unapotembea.
Sipendi sehemu ya watu wengi nikiona watu mara nyingine adi nawakimbia.
Nilipokua mdogo niliwahi kuugua sana hospitali madaktari waliponifanyia vipimo wakawambia wazazi mtoto anafikiri sana anahitaji kurelax nikapelekwa isolation kwa wiki tatu.
Nilizaliwa 10 september.
Kwamba kuna uhusiano kati ya tarehe/mwezi wa kuzaliwa na introverts? Nieleweshe tafadhaliMie rafiki zangu wananiuliza we mwenzetu una demu kweli?
Hilo swali naulizwa sana wengine wananipa majina domo zege huezi kua na demu.
Mwengine aliwahi kunambia jamaa angu tatizo lako unatafakari sana hata sehem ya kukanyaga mguu unapotembea.
Sipendi sehemu ya watu wengi nikiona watu mara nyingine adi nawakimbia.
Nilipokua mdogo niliwahi kuugua sana hospitali madaktari waliponifanyia vipimo wakawambia wazazi mtoto anafikiri sana anahitaji kurelax nikapelekwa isolation kwa wiki tatu.
Nilizaliwa 10 september.
Umetumwaaaintroverts wote wana sifa hizi
- Wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
- Ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
- Wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
- Ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
- Wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
- Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)
Sifa zao nyingine ni pamoja na;
- Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
- Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
- Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
- Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasani si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
- Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
- Wakata tamaa wanapokosolewa.
- Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
Nyinginezo ni;
- Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
- Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo.
- Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
- Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
- Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa).
- Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
- Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana.
- Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe.
- Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
Pia, wanafahamika kwa;
- Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
- Wana busara na hekima nyingi
- Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
- Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
- Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
- Ni kundi la watu wanoridhika haraka
- Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa.
- Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
- Kundi linalopenda amani na utulivu
- Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
- Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu.
Wana sifa nyingi sana, nyinginezo ni;
- Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
- Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
- Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
- Wakati mwingine hupenda kujikataa.
- Ni waaminifu na wasema ukweli
- Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
- Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
- Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
- Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
Kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tamaa mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani].
- Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
- Kwa upande wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua.
Nipo kibaruani nimesoma comment yako mpaka namaliza nikahisi nipo uchi.What???😳
Jamaniiii ha ha hHalafu kwenye mitandao tunajifanya wachangamfu kwa vile hatuonekani nadhani