SIFA ZINGINE NILIZONAKUWA NAZO:
1, Kutongoza ni mtihani, yaani hata kuomba namba ya simu tu ni shida.
Naishia kuwaangalia kwa macho tu. Kuwatongoza labda rafiki zangu wa kike.
2. Nikiwa chuo napenda sana kuwatania washkaji wengine, ila nikitaniwa mimi lazima niumie.
3. Topunye ndio kama starehe yangu tu, nazama kwenye grupu najilipua. Mpaka demu ananiuliza hivi wewe una mpenzi kweli namdanganya ninaye.
4. Nikiwa nachati na mtu au demu tunaongea mpaka ananishangaa hivi huyu ni
The Duke of Cambridge mwenyewe au ni mtu mwingine.
5. Napenda mazingira yawe na mpangilio, nikiona vururuvururu nayapangilia, yaani hata nikirudi home nikikuta papo ovyo napangilia safi.
6. Furaha zangu zipo mitandaoni, nakaa natulia napitiapitia mfano uzi wa vituko mitandaoni basi nafurahi.
7. Sipendi watu wajue sana kuhusu mimi. Ukiniliza unakaa wapi nakupa majibu ya uongo ili nikujatishe tamaa ili usiniulize zaidi kuhusu mimi.
8. Nikiwa shule majamaa wakisema wee unapigaga puta, nakosa raha kabisa, nikionana nao nawakwepa maana naona wananifuatilia.
9. Naweza nikawa na wazo la kufanya kitu kikubwa siku za mbeleni ila akija mtu akiniambia siwezi, mbona flan alishindwa badi na mimi nabadili mawazo.
10. Sipendi kuona mtu anaonewa, kupigwa ana kunyimwa haki yake.
Hata nikiwaona ombaomba natamani kuwasaidia lakini uwezo nakuwa sina.
11. Napenda kukaa na kisasi sana rohoni, mfano mtu nigombane nae basi sitakaa niongee nae hata kusalimiana nae.
12. Nikimkosea mtubnajikuta nasononeka sana why nimemfanyia vile, nikifikiria kumuomba msamaha najikuta nishachelewa.
13. Nikiwa na shida siwezi kuisema, labda nimwambie mtu ninayemuamini sana.
14. Napenda sana kufarijiwa pindi nipatapo tatizo.
15. Napenda kuwasaidia majiran