Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kabisa mkuu tunapata tabu Sana aisee.!introverts wote wana sifa hizi
- Wana uwezo mkubwa kiakili (high intelligence Quotient)
- Ni wagunduzi wa mambo makubwa ya kisayansi
- Wanamudu vizuri masomo ya sayansi na hesabu
- Ni watu wenye pole pole na wasio na maneno mengi
- Wana hisia kali za upendo na ni kundi linalosadikika kuwa na upendo wa dhati
- Wanawajali sana wenzao hasa wanapokuwa katika shida na matatizo(i.e ndio maana hawa huwa waombaji –wanamaombi wazuri sana kiimani)
Sifa zao nyingine ni pamoja na;
- Wana huruma sana na hawapendi kuona wengine wakionewa
- Wanajitolea kwa haraka na kwa dhati katika mambo ya wengine
- Huondoa uchungu wao kwa machozi (wakiumizwa hulia haraka, hasa kwa upande wa wanawake/wasichana)
- Hawajiamini kwa mambo wanayoyafanya (hata wakiwa darasani si wepesi wa kunyoosha vidole ili kujibu maswali)
- Wanahesabu kushindwa kuliko kufanikiwa (mfano akitaka kuanzisha duka; badala ya kuwaza itakuwaje nikipata faida wanawaza itakuwaje kama duka litaibiwa ama kuungua moto, kwa maswali hayo anajikuta hata anafikia katika uamuzi wa kuahirisha uanzishaji wa mradi huo)
- Wakata tamaa wanapokosolewa.
- Wanapenda sana kutiwa moyo kiuhalisia.
Nyinginezo ni;
- Wanapenda kusoma, kusikiliza, na kusimulia mambo yenye tafakari na uchambuzi wa kina (hawapendi umbea)
- Wanapotoa mawaidha mahubiri ama ushauri wengi(wanaosikiliza) huwa wanaguswa nao na hubadilika haraka kutokana na mawaidha hayo ama ushauri ama mahubiri hayo.
- Hawapendi kuvunja taratibu, sheria za eneo husika.
- Wanapenda usafi na mpangilio mzuri wa vitu vyao
- Ni wa vumilivu sana katika hali mbalimbali (mfano wanapoonewa ama kuumizwa).
- Hawapendi kufuatilia mambo ya wengine pasipo sababu za msingi.
- Ni kundi mojawapo linaloathiriwa sana na magonjwa ya mashinikizo kutokana na kuwa wanawaza sana.
- Ni wagumu wa kusahau na hiyo imewasababishia kuwa wagumu wa kusamehe.
- Wanaumia sana wanapokosea ama kushindwa jambo Fulani
Pia, wanafahamika kwa;
- Wanajeruhika mioyo yao kirahisi (i.e wakiingiwa na pepo wabaya si rahisi kuwatoka kwa sababu ya kutunza uchungu kwa muda mrefu mioyono mwao)
- Wana busara na hekima nyingi
- Ni watu ambao wakiishika imani fulani wanajitahidi kuitimiliza sheria yote.
- Ni wepesi wa kutubia makosa yao na kutubu kwa ajili ya wengine.
- Wana aibu nyingi sana hasa kwa watu wasiowafahamu wala kuzoeana nao
- Ni kundi la watu wanoridhika haraka
- Masikini wengi kiuchumi duniani ni wa kutoka katika kundi hili kutokana na uoga wao wa kuanzisha mambo kwa kuhofia kushindwa.
- Watoto wanaozaliwa katika kundi hili inasadikiwa ni wengi huwa na ndoto za kufanikiwa mapema lakini ni wachache mno ambao huweza kutimiliza ndoto zao kutoka na uoga wa kuanzilisha mambo mapya.
- Kundi linalopenda amani na utulivu
- Wanaogopa sana matatizo, vikwazo na changamoto
- Katika familia baba na mama wakiwa melancolin upo uwezekano mkubwa kwa watoto kuharibika maadili kwa sababu hawa melancolin si wepesi wa kuadhibu.
Wana sifa nyingi sana, nyinginezo ni;
- Mara nyingi hupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
- Hawapendi kumueleza kila mtu mambo yao binafsi
- Ni kundi la watu wenye marafiki wachache
- Wakati mwingine hupenda kujikataa.
- Ni waaminifu na wasema ukweli
- Wanapenda kusaidia wengine kupita hata uwezo wao
- Ni waaminifu sana kwa mambo ya kawaida na yale ya kiimani
- Hawapendi kujionesha mbele ya macho ya watu
- Hawa hawafai kuwa viongozi (si wazuri sana) kwa sababu wanapenda kusikiliza na kutafakari kila wanachoshauriwa hivyo hujikuta kuwa wanayumba kimisimamo. (mfano kama mkurugenzi/mwenyekiti wa eneo Fulani akiwa ni melancolin yafaa sana msaidizi wake awe ni colerick
Kingine kinachowanyima sifa ya kuwa viongozi wazuri ni kutokuwa na uwezo wa kujieleza kwa kujenga hoja zenye ushawishi mkubwa [Musa wa biblia alikuwa ni mmoja ya watu wa kundi hili, alikuwa hajiamini, anakata tamaa mapema, mlalamishi, asiyeweza kujieleza, licha ya kupewa msaidizi na Mungu bado tabia zake zilimuathiri na akajikuta anakosa nchi ya ahadi-Kaanani].
- Wanauhesabu upendo wa dhati kutokana na mambo wanayofanyiwa na sio kuambiwa (wanafurahia sana vitendo kuliko maneno}
- Kwa upande wa wasichana inasemekana kuwa ndio ambao wanasumbuliwa zaidi na maumivu ya hedhi, na kujifungua.
Baki ivo ivo ukitaka kuwa extrovert charge yote inaishaa au hujawahi jaribu ku act as extrovertNaombeni mnipe tricks za kuwa extrovert!
😀😀😀Introvert wengi ndo wanaongoza kupiga puchu
mbona Kuna watu wanasema inawezekana mkuu.!Baki ivo ivo ukitaka kuwa extrovert charge yote inaishaa au hujawahi jaribu ku act as extrovert
Sijakuelewa vizuri emb elezea personality inavyochangiaaYaani huu uzi umenifungua mengi sana. Hata job mie napiga kazi nafanya ma-creativity ila ukijaga msala ni lazima niachiwe na niwe victim. Kumbe personality huchangia
Sijakuelewa vizuri emb elezea personality inavyochangiaaYaani huu uzi umenifungua mengi sana. Hata job mie napiga kazi nafanya ma-creativity ila ukijaga msala ni lazima niachiwe na niwe victim. Kumbe personality huchangia
Mweka mada hajagusia makundi manne ya watu huko ndo ungeelewa introvert na uongozi upoje... Nitagusia kiasi ktk introvert Kuna makundi mawili pia ya watu melancholic na phlegmatic.. ktk makundi haya mawili ya kiintrovert melancholic anafaa zaidi kuwa kiongozi maana kwanza ndie mtafakariji mkubwa kushinda makundi mengine.. hivyo huyu anaweza kutoa dira ya nini kifanyike au kipi kifatwe.. ktk extrovert pia Kuna aina mbili za watu sanguine na choleric,chorelic in natural kabisa ndio huwa wanapenda kuwa kiongozi! Huyu akiwepo mahali mbawa zake za uongozi hujionyesha ila tatizo lao hawana maamuzi yenye tafakari pana Sana na huwa ni konki yani Kama hutaki toka kama unataka twende.. huyu akiwa anaongoza ndio wale dizaini ya watu wasiotaka mchezo,hana la kulemba atakapotaka kupita yeye ni ama umpishe apite au akukanyage!!.. binafsi nawaona ni viongozi wanaofaa zaidi kwenye maamuzi magumu tofauti na melancholic maana hawa Mambo yao ya taratibu maana inahitaji muda kufikiri vya kutosha,pia wanasikiliza Sana I can say ni demokratic people!.. maana anataka kila mtu amridhishe.. akikaa kwenye uongozi huyu mtafurahia kufokewa si hulka yake,muelewa na wapole lkn ubovu ndio hapo kwenye maamuzi magumu hutumia muda Sana sana.. si wazuri kwenye maamuzi magumu!.. ndio maana huonekana ni dhaifu sometimes na akizinguliwa Sana hujiengua maana as you know introvert ni watu wa kujilaumu Sana!..Introvert mie napata tabu sana ktk kufanya maamuzi magumu/seriously uongozi haunifai!!!!!
But vipi nikijengwa kuwa kiongozi nitashindwa kutimiza majukum yangu kwasababu n introvert??
Asante kwa maelezo mazuri lakin ivi KENZY A YOU INTROVERT OR EXTROVERTMweka mada hajagusia makundi manne ya watu huko ndo ungeelewa introvert na uongozi upoje... Nitagusia kiasi ktk introvert Kuna makundi mawili pia ya watu melancholic na phlegmatic.. ktk makundi haya mawili ya kiintrovert melancholic anafaa zaidi kuwa kiongozi maana kwanza ndie mtafakariji mkubwa kushinda makundi mengine.. hivyo huyu anaweza kutoa dira ya nini kifanyike au kipi kifatwe.. ktk extrovert pia Kuna aina mbili za watu sanguine na choleric,chorelic in natural kabisa ndio huwa wanapenda kuwa kiongozi! Huyu akiwepo mahali mbawa zake za uongozi hujionyesha ila tatizo lao hawana maamuzi yenye tafakari pana Sana na huwa ni konki yani Kama hutaki toka kama unataka twende.. huyu akiwa anaongoza ndio wale dizaini ya watu wasiotaka mchezo,hana la kulemba atakapotaka kupita yeye ni ama umpishe apite au akukanyage!!.. binafsi nawaona ni viongozi wanaofaa zaidi kwenye maamuzi magumu tofauti na melancholic maana hawa Mambo yao ya taratibu maana inahitaji muda kufikiri vya kutosha,pia wanasikiliza Sana I can say ni demokratic people!.. maana anataka kila mtu amridhishe.. akikaa kwenye uongozi huyu mtafurahia kufokewa si hulka yake,muelewa na wapole lkn ubovu ndio hapo kwenye maamuzi magumu hutumia muda Sana sana.. si wazuri kwenye maamuzi magumu!.. ndio maana huonekana ni dhaifu sometimes na akizinguliwa Sana hujiengua maana as you know introvert ni watu wa kujilaumu Sana!..
So kipi kinafaa.. kinachofaa ni kuwa na kombination ya choleric na melancholic.. ili walau kuziba gapes kadhaa za udhaifu.. melancholic atatoa wazo choleric atawaongoza wengine kulifuata wazo.. lkn hawa wote itafaa zaidi wakiwa wanaelewana kinamna maana Kama melancholic ndo anaongoza halafu choleric yupo chini yake basi melancholic akizubaa anaweza pinduliwa haswa akileta sana u demokrasia!
Ndio maana muda mwengine umekuwa ukisikia mapinduzi yakifanyika hata ktk ngazi za nchi!.. so hii sometimes ukijachunguza utajua ndani yake kuna hizi personality haswa kwa choleric hupenda Sana kuongoza.. we ukisema hapa hapana njia mwenzako anaona njia! Haijalishi mtapita kwa tabu ye anachoangalia mtapita tu!.. melancholic akiona hapana njia atataka kutafuta njia na akiipata mtapita Tena kiwepesi kabisa!..
Ukiweza kujichunguza ukaelewa upo wapi ndugu unaweza kuwa kiongozi Cha muhimu nikujielewa wapi upo imara na wapi haupo imara njia zote hizi zinafaa kuongoza isipokuwa tu ujue muda gani wa kutumia u choleric na ni muda gani wa kutumia u melancholic.. mifano ya viongozi ambao ni choleric ni Idd amin.. kwa upande wa melancholic tulishapata hapa kwetu ni baba wa taifa julias kambarage nyerere.. phlegmatic huwa namuhisi ni jakaya japo sijamchambua vyakutosha sana sina hakika asilimia Mia ila anaonyesha anahizo element za u phlegmatic.. tulienae sahivi sisemi sana ukiangalia tu utajua ni pure choleric..😂 naomba nisiseme Sana..
Moja Kati ya sehemu niliyokuja kumpendea nyerere ni ktk kufanya uamuzi wa Vita Kati yetu na Uganda.. ileweke hivi introvert people haswa melancholic hupenda kutumia logic sana hufanya vitu kwa kujibu haya maswali "how..? When..? Why..? Mengine nimeyasahau ila huwa yapo matano.. ktk vita ya Uganda na tz ile hotuba ya nyerere ukiiangalia inaviashilia hivyo alisema "Nia ya kumpiga tunayo,sababu ya kumpiga tunayo na uwezo wa kumpiga tunao" ukiiangalia hizo kauli unaweza zichukulia juu juu lkn hizo zinaweza kukuongoza hata kwenye kutatua tushida fulani Kama ukiwa muelewa..
Naomba niishie hapo.
Sawa mkuu umesomekaMates;
Binaadamu tumeumbwa kwa matabaka tofauti tofauti sio wa rangi wala jinsia, katika upande wa Personalites binaadamu yupo katika makundi mabalimbali. Kuna Makundi makuu mawili ya personalities,ambazo ni Extroverts na Introverts. Kwa upande wa introverts dunia kwao si kikwazo au haina kikwazo chochote ambacho kinaweza kuwafanya wasisonge mbele au kupata yale wanayoyahitaji.
Upande wa Introverts mambo ni tofauti sana sana, wao dunia si mahali salama kwa muono wao na inakua ni ngumu sana kwao kupata yale wanayoyahitaji humu duniani. Introverts wanaamini au wanaiona dunia ist the bed of roses na unaweza kuishi na ku-Earn yale unayoyata bila kutumia nguvu kubwa sana ya mwili ila ya akili.
Bahati mbaya dunia haipo hivyo, dunia imejaa michongoma hii inawafanya introverts kuona hawafit kuishi duniani hapa ila ndio wapo sasa inabidi wakubaliane na matokeo.
Kama tunavyoelewa kua Extroverts ni watu Fulani ambao ni waongeaji wazuri na hawana aibu hata kidogo wakitaka kitu watakueleza mojakwamoja ila Introvert ni watu wasio na uwezo wa kujieleza vizuri na wana aibu sana, mara nyingi hutuia muda mwingi katika kufikiri na kutafakari vitu vipya!
Aliyeumba hizi aina kinzani za watu hakua mjinga, alikua na maana kubwa sana kuwaweka pamoja hapa duniani, katika hizi pande mbili kinzani zimeunganishwa na kitu kimoja ambacho ni Kutegemeana katika mazingira. Pande zote mbili zinategemeana mno kwa kiasi kikubwa kwakua introvert wanatumia muda mwingi kufikiria na kutafakari vitu basi hawa walijaliwa Creative and Genius mind!
Ukiangalia maandeleo katika Nyanja ya dunia hii yameletwa na watu ambao ni Introverts. Lakini Introvert person akiungana na extrovert person basi hua wanatengeneza the best duo, Introvert hua anamtumia huyo extrovert kama mdumo wake au nguvu yake huku yeye akitumia akili yake zaidi katika mambo japo maranyingi sana hua extroverts wanawatapeli introverts baada ya muda.
NB, sio kwamba extrovert hua hawana uwezo wa akili no, ila siku zote mtu anayeanza kutafakari maneno wakati wewe uko unaongea muheshimu sana, lakini pia usichanganye introvert na kibuli.
Wapo watu wengi walikua ni introvert wakaungana na extrovert wakatenda mambo makubwa hapa duniani Nitatoa baadhi ya mifano
Mussa
Huyu jamaa alikua nae ni introvert, hana uwezo mzuri sana wa kujieleza ndio maana alipoitwa na Mungu alimuuliza atawezaje kuzungumza nao wakati hawezi kuongea vizuri? Mungu akampatia msaidizi wake amabae ni Aaron, walitengeneza moja ya kolabo bomba hapa duniani nadhani mambo waliyofanya tunayajua na yataendelea kuwepo daima
Tesla
Tesla alikua ni introvert aliyepitiliza, alijua duniani kila mtu ni mwema kama yeye. Alikutana na bwana Thomas Eddison wakafanya kazi pamoja mpaka leo umoja wao ndio unatufanya tunaweza kuchati hapa, bahati mbaya Thomas alimdhurumu tesla ila hakujali kufa maskini alishukuru tu kua akaili yake imeweza kuleta maendeleo duniani.
Mark Zuckenburg
Binafsi hua nikiamuangalia tu mark namuonea huruma tu kwa munekano wake, ni moja kati ya watu amabao wana Innocent face, ukimuangalia tu unamuhurumia. Ni watu wachache sana wenye hiyo haiba yay a kuonekana wanatia huruma. Mark ni introvert maisha yake chuoni alikua sio muongeaji hata ukimuudhi vipi hua anabaki kimya.
Kuna kipindi kama miaka 2 imepita ilitokea mgogoro kwamba mark kaiga ile technology ya kuangalia game in vitual reality. Ikatakiwa alipe pesa, ilimuuma mno ila hakuongea alibaki nalo rohoni. Rafiki yake mkubwa amabae amemsaidia sana kufanikisha facebook kufika hapa ilipo ni Eduardo Sevarin. Eddu alikua muongeaji tu na mtafuta masoko na investors mpaka leo umoja wao huo ndio umeawafikisha hapa mark ni billionea.
David Benioff
Huyu jamaa ni moja kati ya watengenezaji wa tamthiria ya game of thrones, nayeye sio muongeaji kama walivyo introverts wote pia ana aibu mno. Anar rafiki yake waliyekutana nae chuoni anaitwa Daniel Brett Weiss (D.B.Weiss) naye huyu ni moja ya watengenezaji wa tamthiria hii. Ila huyu DB Weiss hana aibu hata kidogo na nimuongeaji sana.
Hata wakiwa kwenye interview maswali yanayomuhu David benioff hua anayjibu yeye the funny thing ni kwamba walipokua wanafanya casting ya actors labda kama kuna actor Fulani ambaye the next season alitakiwa afe David Benioff alikua hawezi kuwaambia eti anaogopa! So aliyekua anafanya kazi hiyo alikua ni DB Weiss tena kwake ilikua rahisi mno.
View attachment 1526082
Issack Newton
Kama kawaida ya introverts wote basi Newton pia hakua na marafiki kabisa alipenda kujifungia ndani ya maabara yake kufanyia tafiti fikra zake na kujipa nafasi ya kufikiri zaidi. Alikua anamsemo wake anasema kwamba “ Plato is my friend, Aristotle is my friend, but my best friend is truth” Lakini naye alikua na rafiki yake ambae alikua ni muongeaji mzuri/Extrovert aliitwa John Locke. Huyu ndio alikua rafiki pekee wa Newton na yeye ndio aliweza kumuelezea vizuri tabia zake za upweke japo baadae walishindwana urafiki wao. Maana Muda mwingi Newton alikua bize.
Albert Eintein
Albert alipohamia Switzerland akaanza kufanya kazi kwenye ofisi za Patent right (haki miliki) ndipo alipoanza kufanyia kazi Hobby yake pendwa ya Kufikiria. Ofisini kwake kulimwezesha kufikiria maana hakua na kazi ngumu, kupitia dirisha lililokua ofisini mwake aliweza kuformulate theory of relativy maana alikua anautafakari mwanga uliokua unaingia ofisini mwake kupitia dirishani….Japo alikua ni mtu mmoja mkimya sana na alikua anaongea kila baaada ya kutafakari sana anachotaka kuongea pia alikua na rafiki yake wa karibu toka zamani ambae wamesaidiana mengi si mwingine ni Michelle Besso. Beso ndio alikua rafiki yake mkubwa na kumuwezesha Albert kufanya mengi makubwa.
Mifano ni mingi sana ya urafiki wa introverts na extrovert, watu maarufu ambao ni Introverts..na wametenda mengi makubwa duniani mfano:
Albert Einstein,Rosa Parks,Bill Gates,Steven Spielberg,Sir Isaac Newton,Eleanor Roosevelt, Mark Zuckerberg,Larry Page,Al Gore,Marissa Mayer, Abraham Lincoln,JK Rowling,Warren Buffett, Mahatma Gandhi,Hillary Clinton, Michael Jordan,Meryl Streep,Elon Musk,Dr. Seuss,Frederic Chopin
Introverts kwakua wao hawawezi kuingiliana vizuri na jamii waliyomo hivyo basi muda wao mwingi hua wanautumia kwenye mitandao ya kijamii. Huku kwenye jamii hawana attention kwa watu so wanachofanya ni kutafuta attention mitandaoni at any cost. Introvertism,Geniusity,Lonelness na Ugonjwa wa akili ni vitu vinavyoenda sambamba. Ukikuta mtu anaandika mapost marefu,anatukana au kuudhi watu mitandaoni usimchukie.
Muhurumie sana maana anakua muhanga wa matatizo niliyoyaainisha hapo juu. Wanafanya kuudhi watu ili nao waonekane kama wanaweza kufanya kitu, wanajitahid kufit in ila bahati mbaya wanatumia approach mbaya ya kuudhi watu.. Introverts ni watu poa sana, wana mioyo mizuri sana na wana akili zenye uwezo mkubwa.
-Vinci
Aisee siamin humu ndan wewe ni msumbufu sana nkajia bonge la extrovertHa ha! In reality Mimi ni introvert ila kwenye key body au daftari ama namna yoyote ya kuandika ni extrovert!.. na huku ndipo introvert wengi tunapopenda kujifichia.
Haha! Humu tu kwasababu yanaonekana maandishi ila nje na hapo! Unaweza sema huyu Jamaa boya fulani hivi..😂 ahsante kwa mitandao nasi tunapunguzia stress zetu..Aisee siamin humu ndan wewe ni msumbufu sana nkajia bonge la extrovert
Uliyosema yote Ni ukweli ila aya hii Ni zaidi ya ukweli ni Mimi mwenyewe kabisa wengi wanatuona Kama viburi nk
Marahupenda kuonesha sura za tabasamu hata kama wapo katika matatizo makubwa
Namjua mwenyewe😅😅
Mie kwa upande wangu tangu nipo mdogo (kuanzia 10yrs) nilikuwa sipendi kuchangamana na wenzangu, nikitoka shule chumbani hadi kufikia wazazi wangu kuichukia tabia yangu, yaani rafiki zangu wakija kunisalimia nipo radhi nivunge nimelala usingizi ili tu waniachie nafasi ya kuwa peke yangu.
Hii tabia niliendelea nayo hadi secondary school, nilikuwa sipendi kitu chaitwa discussion, ni mwendo wa kupiga msuli mwenyewe.
Pia nimekuwa mchaguzi sana wa marafiki, wale wambea, tantalila nyingi hatuivi zaidi ya salamu, sipendi kusikia mtu ananiletea stori za ooh sijui fulani alikuwa anakusema hivi na hivi, akisikia aliache huko huko.
Kuhusu hisia za upendo ninazo sana iwe kwa rafiki ama mpenzi, na kuhusu kusaidia nachukua tatizo la mtu kama la kwangu, hii imepelekea kudhulumiwa sana na watu niliowaamini na kuwasaidia. Huwa naguswa sana.
Sasa sijui nadondokea wapi?
Da'Vinci
Intro inatesa lakini hasa msongo wa mawazo hapo tu ndo pananifanya sometimes nijaribu kuact Kama extro, na nahisi hata wagonjwa wengi wa akili, sonona na magonjwa ya kufanania hayo wengi ni intro's, inafanya kufikia maamuzi ya kujiua sasa hii ni hatari sanaMnatamani kutoka Introvert peranoality kwenda Extrovert modal of personality, Jamani there's no turning back. Ukishakua intro ww ni intro tu huwezi kua extro maana hakuna mtu aliyechagua kuzaliwa intro au extro au aliAdopt kuwa intro or extro kutokana na mazingira aliyopo. Ni kitu tulichozaliwa nacho, huwezi kivua. Unaweza kujaribu kuishi na kutenda kama extro lakini bado utapwaya tu na utakua unarudi Kwenye kundi lako.. there's no middle ground or turning back on this. Jidaie tu na ulichonacho