Mweka mada hajagusia makundi manne ya watu huko ndo ungeelewa introvert na uongozi upoje... Nitagusia kiasi ktk introvert Kuna makundi mawili pia ya watu melancholic na phlegmatic.. ktk makundi haya mawili ya kiintrovert melancholic anafaa zaidi kuwa kiongozi maana kwanza ndie mtafakariji mkubwa kushinda makundi mengine.. hivyo huyu anaweza kutoa dira ya nini kifanyike au kipi kifatwe.. ktk extrovert pia Kuna aina mbili za watu sanguine na choleric,chorelic in natural kabisa ndio huwa wanapenda kuwa kiongozi! Huyu akiwepo mahali mbawa zake za uongozi hujionyesha ila tatizo lao hawana maamuzi yenye tafakari pana Sana na huwa ni konki yani Kama hutaki toka kama unataka twende.. huyu akiwa anaongoza ndio wale dizaini ya watu wasiotaka mchezo,hana la kulemba atakapotaka kupita yeye ni ama umpishe apite au akukanyage!!.. binafsi nawaona ni viongozi wanaofaa zaidi kwenye maamuzi magumu tofauti na melancholic maana hawa Mambo yao ya taratibu maana inahitaji muda kufikiri vya kutosha,pia wanasikiliza Sana I can say ni demokratic people!.. maana anataka kila mtu amridhishe.. akikaa kwenye uongozi huyu mtafurahia kufokewa si hulka yake,muelewa na wapole lkn ubovu ndio hapo kwenye maamuzi magumu hutumia muda Sana sana.. si wazuri kwenye maamuzi magumu!.. ndio maana huonekana ni dhaifu sometimes na akizinguliwa Sana hujiengua maana as you know introvert ni watu wa kujilaumu Sana!..
So kipi kinafaa.. kinachofaa ni kuwa na kombination ya choleric na melancholic.. ili walau kuziba gapes kadhaa za udhaifu.. melancholic atatoa wazo choleric atawaongoza wengine kulifuata wazo.. lkn hawa wote itafaa zaidi wakiwa wanaelewana kinamna maana Kama melancholic ndo anaongoza halafu choleric yupo chini yake basi melancholic akizubaa anaweza pinduliwa haswa akileta sana u demokrasia!
Ndio maana muda mwengine umekuwa ukisikia mapinduzi yakifanyika hata ktk ngazi za nchi!.. so hii sometimes ukijachunguza utajua ndani yake kuna hizi personality haswa kwa choleric hupenda Sana kuongoza.. we ukisema hapa hapana njia mwenzako anaona njia! Haijalishi mtapita kwa tabu ye anachoangalia mtapita tu!.. melancholic akiona hapana njia atataka kutafuta njia na akiipata mtapita Tena kiwepesi kabisa!..
Ukiweza kujichunguza ukaelewa upo wapi ndugu unaweza kuwa kiongozi Cha muhimu nikujielewa wapi upo imara na wapi haupo imara njia zote hizi zinafaa kuongoza isipokuwa tu ujue muda gani wa kutumia u choleric na ni muda gani wa kutumia u melancholic.. mifano ya viongozi ambao ni choleric ni Idd amin.. kwa upande wa melancholic tulishapata hapa kwetu ni baba wa taifa julias kambarage nyerere.. phlegmatic huwa namuhisi ni jakaya japo sijamchambua vyakutosha sana sina hakika asilimia Mia ila anaonyesha anahizo element za u phlegmatic.. tulienae sahivi sisemi sana ukiangalia tu utajua ni pure choleric..[emoji23] naomba nisiseme Sana..
Moja Kati ya sehemu niliyokuja kumpendea nyerere ni ktk kufanya uamuzi wa Vita Kati yetu na Uganda.. ileweke hivi introvert people haswa melancholic hupenda kutumia logic sana hufanya vitu kwa kujibu haya maswali "how..? When..? Why..? Mengine nimeyasahau ila huwa yapo matano.. ktk vita ya Uganda na tz ile hotuba ya nyerere ukiiangalia inaviashilia hivyo alisema "Nia ya kumpiga tunayo,sababu ya kumpiga tunayo na uwezo wa kumpiga tunao" ukiiangalia hizo kauli unaweza zichukulia juu juu lkn hizo zinaweza kukuongoza hata kwenye kutatua tushida fulani Kama ukiwa muelewa..
Naomba niishie hapo.