A
Anonymous
Guest
Naandika waraka huu kwa masikitiko makubwa nikiwakilisha sauti za vijana wengi ambao wanapitia mateso na unyanyasaji ndani ya kampuni ya utoaji mikopo iitwayo Orbit Microfinance Services inayofanya shughuli zake Zanzibar.
Kampuni hii imekuwa ikiendesha utaratibu wa kuajiri vijana unaoambatana na vitendo vya kikatili na kinyume na sheria za kazi kama ifuatavyo:
Kampuni hii imekuwa ikiendesha utaratibu wa kuajiri vijana unaoambatana na vitendo vya kikatili na kinyume na sheria za kazi kama ifuatavyo:
- Kushikilia Vyeti vya Elimu Kinyume cha Sheria: Waajiriwa wanalazimishwa kukabidhi vyeti vyao halisi (Original) vya Kidato cha Nne kama dhamana ya ajira. Kampuni inakataa kurudisha vyeti hivi wanapodaiwa, na hatujui wanavitumia kwa shughuli gani.
- Unyanyasaji (Kupigwa): Wafanyakazi wanapokuwa kazini wanakumbana na vitendo vya kupigwa na kudhalilishwa na viongozi wa kampuni hiyo.
- Kubambikiziwa Kesi na Utapeli: Kampuni inatumia mbinu ya kuwabambikizia wafanyakazi makosa na kuwatishia kuwafunga gerezani kwa madai kuwa wana uwezo wa kutoa hongo kwa mamlaka. Kupitia vitisho hivi, wanawakamua vijana pesa nyingi sana isivyo halali.