Kitu ambacho mara nyingi watu wanafeli Sana ni kuzungumzia GPA kwa elimu ya chuo kikuu.
Chuo kikuu mara nyingi kupata GPA kubwa au ndogo ukiachilia mbali jitihadi na maisha ya msomaji, kunategemea Sana mipango na malengo ya walimu wa chuo husika.
Mara nyingi unaweza kuona Kuna utofauti kati ya chuo kimoja na kikingine kimalengo na mpango kwenye kozi Fulani ambapo mwalimu wa chuo A anaweza kutofautiana na mwalimu wa chuo B katika ufanikishaji. Ukiachilia mbali ufanikishaji Bado unaweza kuona mbinu atakazo zitumia mwalimu wa chuo A na Mwalimu wa chuo B katika kuwapima wanafunzi zinatofautiana kwahyo GPA Bado inakosa haki ya kuhukumu.
Vyuoni wapo baadhi ya walimu kwa makusudi Huwa wanajitengenezea mazingira ya kutaka masomo Yao yaonekane magumu na Hilo ni miongoni mwa mapungufu ya walimu wengi na walimu wengi Huwa wanafanikisha Hilo hasa kwa kuwafundisha na kuwapima wanafunzi nje ya malengo kwa makusudi.
Mfano; LENGO: Mwanafunzi atambue sifa za nchi huru.
Sasa mwalimu mwenye akili akishafundisha na akiamua kuwapima wanafunzi ataweza kutumia swali la wazi lolote kati ya maswali ya fuatayo;
1. Eleza sifa za nchi huru.
2. Taja sifa za nchi huru.
3. Je, unazijua sifa za nchi huru? Kama jibu ni ndio zitaje.
n.k
Sasa ukikutana na mwalimu wa hovyo; LENGO: Mwanafunzi azitambue sifa za nchi huru.
Maswali:
1. Kabla ya mwaka 1961 Tanganyika ilikuwa ikitawaliwa kikoloni. Eleza tofauti zilizopo kabla na baada ya 1961 ukiihusisha Tanganyika.
2. Ukiachilia mbali haki na wajibu, uhuru wa watu, Tanzania ni nchi huru eleza.
n.k
Kwahyo Bado nasisitiza suala la GPA vyuoni kwa % nyingi ni mipango ya walimu.
Kuna watu wanaweza kujituma na kusoma kwa bidii ila Bado wakashindwa kufanya vizuri na wengine wanaweza kuwa na GPA kubwa lakini ukiwa nae kazini unagundua Hana maarifa yanayoendana.
Kwahyo angalau kwa karibu 80% elimu ya chuo kikuu hasa tukihusisha GPA inaweza kuwa na maana endapo upimaji wake utakuwa kama wa shule za msingi na sekondari Yani upimaji uwe wa Jumla kitaifa au kimataifa.
Mwalimu mmoja sio sawa kuamua kuhusu matokeo ya mwanafunzi wa chuo.
Mfano: chuoni Kuna walimu wanaweza kuludia baadhi ya maswali Yale Yale ambayo wameyatumia kuwapima wanafunzi kwenye course work ya 40% kuyauliza kwenye UE ya 60% Sasa Ikiwa mwalimu wa Mwanafunzi A utaratibu wake ukawa tofauti na mwalimu wa Mwanafunzi B itawezekanaje hao wanafunzi kufanana matokeo?
Vyuoni pia kutokana na kwamba mwalimu ndiye mwenye kuamua matokeo upo uwezekano wa mazingira ya RUSHWA.
Ikiwa nahitaji kujua umahili wa muhitimu wa chuo kikuu nitahitaji kuona baadhi ya vitu then vyeti vyake nitaviomba baadaye.
Wakati mwingine tunaweza kusema sifa kubwa kwa elimu ya vyuoni iwe ni kuhitimu. Kwahyo mwanafunzi akigraduate basi tayari awe na sifa stahiki lakini GPA Bado sio ishu za msingi hasa kutokana na ninavyojua.
---------------------