Tatizo lilianzia mwaka 2003, Rais wa wakati huo, George Bush alisain 'American dream' iliyojumuisha ndoto ya kila Mmarekani awe na nyumba. Masharti yalilegezwa na watu wengi walikopesheka, nyumba nyingi zikajengwa(Biashara ya makazi ililipa sana watu wakawekeza zaidi) na watu kununua kwa mkopo.
Mwaka 2007/08 watu wengi wakashindwa kuendelea kulipa hii mikopo kwa sababu ilitolewa kwa sera kuliko kupima uwezo wao wa kulipa. Kwa kawaida ukishindwa kulipa benki hurudi sokoni na kuuza ili kufidia deni. Wafilisi wakaenda sokoni kwa pamoja, nyumba zikawa nyingi sana sokoni na kawaida vitu vikizidi kuliko uhitaji huwa vinashuka bei, Marekani ikashuhudia anguko kali la bei kwenye sekta ya nyumba na bado zikawa haziuziki kwa urahisi.
Hii ikaleta 'panic' na soko la nyumba likafeli rasmi, kumbuka mzunguko mkubwa wa pesa umeshikiliwa na sekta ya makazi. Mabenki na 'hedge funds' vikaathirika pakubwa. Mwaka 2008 Lehman brothers akadondoka ikiwa ni anguko kubwa zaidi kwenye sekta ya fedha Marekani.
Nchi zilizoendelea mabenki ni muhimu sana kwenye uchumi, kuyumba kwao kukapelekea sekta nyingi kukwama. Watu wakaacha kufanya manunuzi wakilinda walichonacho na wengine wakashindwa kukopa ili kufanya manunuzi. Uzalishaji ukapungua na ajira zikapotea. Mzunguko wa mchakato huu ukapelekea mdororo wa uchumi ukiwa mkubwa zaidi baada ya mdororo uliosababishwa na vita kuu ya pili ya dunia.
Imani yangu umepata mwanga kilichotokea.