Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Piteni na huku

 
Nipo siti ya mbele humo[emoji23][emoji106][emoji120][emoji123]
 
Inaendelea

Tulipofika Nandos tukaenda kukaa kwenye kona moja ambayo kumbe Sandile alikuwa yatari kaomba iwe reserved kwa ajili yetu maana tuliikuta tayari meza zimeshaunganishwa na kuna glass zimewekewa maua kwa ndani na kuna cake imewekwa katikati ya meza imeandikwa “Congrats Konda msafi”

Tukaizunguka hiyo meza, mie nikawa nimekaa katikati ya Sandile na Khumbu. Tukiwa tunasubiria chakula tukaanza kutambulishana especially kwa upande wa Khumbu maana sisi watatu tu ndio tulikuwa tunamjua Khumbu wengine wote walikuwa hawamjui. Sandile akaniomba nitoe utambulisho. Nikaanza kumtambulisha mmoja baada ya mwingine. Khumbu alikuwa amekaa pembeni yangu upande wa kushoto, kulia kwangu alikuwa amekaa Sandile. Nilianzia upande wa Sandile nikawa nazunguka kuelekea upande wa Khumbu. Nilipofika upande wa Khumbu nika-pose kwanza kisha nikamwangalia usoni. Nikamwomba ajitambulishe mwenyewe, watu wote wakaanza kucheka, wakaanza kunitania niache ubaguzi, haiwezekani watu wote niwatambulishe halafu nimwambie Khumbu ajitambulishe. Khumbu akiwa anacheka akaingilia kati, akasema atajitambulisha mwenyewe. Akasema I’m Khumbu and I’m the wife of Konda msafi, watu wote wakaanza kushangilia huku wakicheka. Watu wakaanza na utani, wanamtania Khumbu wanacheka yaani ikawa utani na kucheka, kila mtu anaongea lake. Wengine wanatupiga picha mimi na Khumbu. Wengine wanataka nipige nao picha, basi ikawa vurugu tu na stori nyingi.

Baada ya utambulisho nikakata keki na nikaanza kumlisha Khumbu, pia chakula kikaletwa. Nandos wanapika nyama zao kwa mvuke, hawakaangi kwa mafuta kama KFC. Watu wengi South Africa ambao wapo health conscience huwa wanapenda chakula cha Nandos ukilinganisha na migahawa mingine kama KFC, Macdonald au Chicken licken. Kwa hiyo ililetwa nyama choma very jucy, nyama tamu kinoma ya beef, kuku wa kuokwa mlaini na vyakula kibao pamoja na vinywaji. Hakika ilikuwa siku murua sana.

Tukiwa tunaendelea kula nilimwuliza Khumbu amejuaje kama leo ni graduation yangu. Kwanza nilimshukuru kwa ujio wake ila nilitaka kujua amejuaje kama leo ni graduation yangu, na ameonana vipi na akina Sandile? Alichonijibu nilichoka. Akasema kuna mtu tumegraduate naye ambaye ananijua, anakaa huko huko Inanda hivyo alimpa ratiba yote ya graduation ceremony, hivyo alipanga lazima aje anifanyie surprise. Sandile naye akaongezea kuwa wakati MC anatangaza kuelekeza sehemu ya kukaa ya wageni waalikwa, kwenye zile pilikapilika za kupanda juu na kwenda kukaa wakaonana naye hivyo wakamwita na kwenda kukaa sehemu moja. Kwa hiyo yale makelele niliyoyasikia yakipigwa baada ya jina langu kutajwa yeye ndio alikuwa kinara wa kushangilia.

Baada ya kumaliza kula, watu wengine wakaanza kuaga na kuondoka. Na mimi nikawaelezea kuwa sitalala Durban kwa sababu inabidi nirudi Bloemfontein maana nimechukua ruhusa ya siku mbili tu kazini. Watu wote wakaondoka tukabaki mimi na Khumbu, ila nikaenda kwenye gari la sandile kutoa vitu vyangu maana kuna nguo zangu nilikuwa nimeziacha humo.

Tulipobaki wawili nilianza kumwuliza kwa nini hakuja Bloemfontein kipindi nimemtumia nauli. Akasema hilo swali alishajibu na hatapenda nimwulize tena. Of course namjua Khumbu toka zamani huwa hapendi kuulizwa maswali ambayo anajua kabisa majibu yake yatamtia hatiani. Pia nilimwuliza kuhusu ile simu niliyopigiwa ya kufumuliwa kichwa, pia aliendelea kusema alishanijibu na zaidi ya yote hahusiki. Na akaniomba niachane na maswali yatakayochafua hali hewa maana siku ya leo ni siku ya furaha, na hakuja hapa kuniharibia siku bali kusherehekea na mimi. Basi baada ya kuniambia hayo tulianza kupiga stori za mahusiano yetu kipindi cha nyuma na kukumbushana historia ya mapenzi yetu. Mwisho nikamwomba tuondoke wote twende Bloemfontein. Akasema kwa sasa hawezi kuondoka Durban ana mambo yake ya utafutaji hivyo akiondoka yataharibika. Akashauri kama ninataka kuwa karibu naye nitafute kazi Durban. Binafsi niliona kuna shida sehemu, kuna mtu anammiliki, hapa anaongea tu, hata kama nikihamia Durban bado mambo ya kuumizana yatakuwa palepale. Sikutaka hata kuomba mchezo, nilijua nikiomba lazima ataniambia kwa leo haiwezekani labda siku nyingine wakati mie sina muda wa kuendelea kukaa Durban. Nilimwomba tu anipeleke sehemu niliyofikia nikachukue begi langu kisha anipeleke stand nikaangalie usafiri wa kunirudisha Bloemfontein.

Itaendelea
 
Safi sana Konda!
Salaam toka nchi jirani ✌️
 
Du hii sijajua hata iliyopita ni ipi mkuu
 
Amkeni amkeni amkeniiiiii[emoji344][emoji350][emoji344][emoji350][emoji344][emoji350][emoji345][emoji350][emoji350][emoji345][emoji350][emoji344][emoji350][emoji344][emoji350][emoji344][emoji350][emoji350][emoji344][emoji350][emoji344][emoji350][emoji350][emoji344][emoji350][emoji350][emoji344][emoji350][emoji350][emoji344][emoji350][emoji350][emoji350][emoji345][emoji350][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345][emoji350][emoji345]

Khumbu in the air meeen[emoji1783][emoji1783][emoji1783][emoji1783][emoji1783]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…