flulanga
JF-Expert Member
- Jul 1, 2016
- 4,860
- 6,390
TUTAWAFUNGA JELA AU WATATULIPA MAHELA MENGIHii story bongo movie sasa hivi wataundia sinema au episode
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
TUTAWAFUNGA JELA AU WATATULIPA MAHELA MENGIHii story bongo movie sasa hivi wataundia sinema au episode
Nipo siti ya mbele humo[emoji23][emoji106][emoji120][emoji123]Piteni na huku
Hadithi ya kweli ya maisha yangu
Habarini Wapendwa, Hope mko njema licha hili janga linalo tukumba Mungu ni mwema sana. Leo naomba kushare story ya Maisha yangu Mimi holy holm. Wiki chache zimepita nilileta humu thread ya jinsi nilivyoanza mahusiano ya kimapenzi na jimama na nilihaidi kuwaletea story nyingne ya maisha yangu...www.jamiiforums.com
Na wamlipe jamaaHii story bongo movie sasa hivi wataundia sinema au episode
Na wamlipe jamaaHii story bongo movie sasa hivi wataundia sinema au episode
hauna AIBU /AKILI? jukwaa la MATANGAZO ina mana hujaliona.?TUPATE WADHAMINI KIDOGO
Karibu SafeEye kwa mahitaji ya CCTV CAMERA, Electric Fence, Gate Motor & Video Door Phone .
0716128815
Unasubiri PICHA umeshatoa VOCHANasubiri picha mwenye ma vibe ya kukung'uta siafu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]
Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Safi sana Konda!Inaendelea
Tulipofika Nandos tukaenda kukaa kwenye kona moja ambayo kumbe Sandile alikuwa yatari kaomba iwe reserved kwa ajili yetu maana tuliikuta tayari meza zimeshaunganishwa na kuna glass zimewekewa maua kwa ndani na kuna cake imewekwa katikati ya meza imeandikwa “Congrats Konda msafi”
Tukaizunguka hiyo meza, mie nikawa nimekaa katikati ya Sandile na Khumbu. Tukiwa tunasubiria chakula tukaanza kutambulishana especially kwa upande wa Khumbu maana sisi watatu tu ndio tulikuwa tunamjua Khumbu wengine wote walikuwa hawamjui. Sandile akaniomba nitoe utambulisho. Nikaanza kumtambulisha mmoja baada ya mwingine. Khumbu alikuwa amekaa pembeni yangu upande wa kushoto, kulia kwangu alikuwa amekaa Sandile. Nilianzia upande wa Sandile nikawa nazunguka kuelekea upande wa Khumbu. Nilipofika upande wa Khumbu nika-pose kwanza kisha nikamwangalia usoni. Nikamwomba ajitambulishe mwenyewe, watu wote wakaanza kucheka, wakaanza kunitania niache ubaguzi, haiwezekani watu wote niwatambulishe halafu nimwambie Khumbu ajitambulishe. Khumbu akiwa anacheka akaingilia kati, akasema atajitambulisha mwenyewe. Akasema I’m Khumbu and I’m the wife of Konda msafi, watu wote wakaanza kushangilia huku wakicheka. Watu wakaanza na utani, wanamtania Khumbu wanacheka yaani ikawa utani na kucheka, kila mtu anaongea lake. Wengine wanatupiga picha mimi na Khumbu. Wengine wanataka nipige nao picha, basi ikawa vurugu tu na stori nyingi.
Baada ya utambulisho nikakata keki na nikaanza kumlisha Khumbu, pia chakula kikaletwa. Nandos wanapika nyama zao kwa mvuke, hawakaangi kwa mafuta kama KFC. Watu wengi South Africa ambao wapo health conscience huwa wanapenda chakula cha Nandos ukilinganisha na migahawa mingine kama KFC, Macdonald au Chicken licken. Kwa hiyo ililetwa nyama choma very jucy, nyama tamu kinoma ya beef, kuku wa kuokwa mlaini na vyakula kibao pamoja na vinywaji. Hakika ilikuwa siku murua sana.
Tukiwa tunaendelea kula nilimwuliza Khumbu amejuaje kama leo ni graduation yangu. Kwanza nilimshukuru kwa ujio wake ila nilitaka kujua amejuaje kama leo ni graduation yangu, na ameonana vipi na akina Sandile? Alichonijibu nilichoka. Akasema kuna mtu tumegraduate naye ambaye ananijua, anakaa huko huko Inanda hivyo alimpa ratiba yote ya graduation ceremony, hivyo alipanga lazima aje anifanyie surprise. Sandile naye akaongezea kuwa wakati MC anatangaza kuelekeza sehemu ya kukaa ya wageni waalikwa, kwenye zile pilikapilika za kupanda juu na kwenda kukaa wakaonana naye hivyo wakamwita na kwenda kukaa sehemu moja. Kwa hiyo yale makelele niliyoyasikia yakipigwa baada ya jina langu kutajwa yeye ndio alikuwa kinara wa kushangilia.
Baada ya kumaliza kula, watu wengine wakaanza kuaga na kuondoka. Na mimi nikawaelezea kuwa sitalala Durban kwa sababu inabidi nirudi Bloemfontein maana nimechukua ruhusa ya siku mbili tu kazini. Watu wote wakaondoka tukabaki mimi na Khumbu, ila nikaenda kwenye gari la sandile kutoa vitu vyangu maana kuna nguo zangu nilikuwa nimeziacha humo.
Tulipobaki wawili nilianza kumwuliza kwa nini hakuja Bloemfontein kipindi nimemtumia nauli. Akasema hilo swali alishajibu na hatapenda nimwulize tena. Of course namjua Khumbu toka zamani huwa hapendi kuulizwa maswali ambayo anajua kabisa majibu yake yatamtia hatiani. Pia nilimwuliza kuhusu ile simu niliyopigiwa ya kufumuliwa kichwa, pia aliendelea kusema alishanijibu na zaidi ya yote hahusiki. Na akaniomba niachane na maswali yatakayochafua hali hewa maana siku ya leo ni siku ya furaha, na hakuja hapa kuniharibia siku bali kusherekea na mimi. Basi baada ya kuniambia hayo tulianza kupiga stori za mahusiano yetu kipindi cha nyuma na kukumbushana historia ya mapenzi yetu. Mwisho nikamwomba tuondoke wote twende Bloemfontein. Akasema kwa sasa hawezi kuondoka Durban ana mambo yake ya utafutaji hivyo akiondoka yataharibika. Akashauri kama ninataka kuwa karibu naye nitafute kazi Durban. Binafsi niliona kuna shida sehemu, kuna mtu anammiliki, hapa anaongea tu, hata kama nikihamia Durban bado mambo ya kuumizana yatakuwa palepale. Sikutaka hata kuomba mchezo, nilijua nikiomba lazima ataniambia kwa leo haiwezekani labda siku nyingine wakati mie sina muda wa kuendelea kukaa Durban. Nilimwomba tu anipeleke sehemu niliyofikia nikachukue begi langu kisha anipeleke stand nikaangalie usafiri wa kunirudisha Bloemfontein.
Itaendelea
Du hii sijajua hata iliyopita ni ipi mkuuInaendelea
Maisha ya kujitahidi kumtoa Khumbu kichwani yaliendelea. Haikuwa jambo rahisi ila kwa kiasi flani nilifanikiwa maana nilianza kujiona mtu mpya. Nilianza kufurahia maisha na huyu mwanamke wangu wa Bloemfontein huku nikiendelea kuwasiliana na Amina pamoja na huyu wa Sinza. Huyu wa Bloemfontein tulianza kupanga mipango mingi tu ya kimaisha. Alikuwa anaishi township moja inaitwa Tabanju. Tulianza mtindo wa kila siku ya Ijumaa nikitoka kazini tunaenda kukaa kwao mpaka Jumapili jioni ndio tunarudi town nyumbani kwangu. Siku za weekend nilikuwa siendi kazini hivyo weekend nzima tulikuwa tunashinda kwao.
Kama mnakumbuka nimesema huko nyuma kuwa niliajiriwa huku nikiwa bado sijagraduate. Niliendelea kufanya kazi huku mara kwa mara naenda Durban kwa ajili ya tests na assignments zingine. Hatimae nilifanya mtihani wa mwisho wa lile somo moja lililobaki, na 06 September 2012 ilikuwa graduation yangu.
Siku ya graduation nilienda Durban kwa ajili ya hiyo shughuli. Nilipata wazo la kumjulisha Khumbu aje kwenye hii siku muhimu kwangu lakini nilipofikiria kuwa rafiki yangu Sandile na Pontsho wasingenielewa kama ningemwalika huyu mwanamke hilo wazo niliamua kuachana nalo japo nilitamani Khumbu awepo. Sandile na Pontsho nilikuwa nimewajulisha siku ya graduation na waliomba gharama za sherehe ziwe juu yao. Gharama za Joho na suti waliniambia wala nisihofu. Sandile alinipa zawadi ya shati moja zuri sana.
Nilifika Durban siku moja kabla ya graduation. Kesho yake asubuhi nikakutana na Sandile campus ili anipatie joho na suti niweze kutinga kabla ya shughuli ya graduation haijaanza. Nikapiga hiyo suti na kutupia joho kwa juu. Kati ya siku muhimu katika maisha yangu ni hiyo siku nilipovaa hilo joho. Niliona hiyo ilikuwa ishara ya milango ya mafanikio kuanza kufunguka. Nilihisi ndoto yangu ya muda mrefu imetimia. Bongo niliishia form three, niliona kama naota kumaliza elimu ya chuo tena kwenye nchi kama South Africa, niliinua mikono juu na kusema “Asante Mungu”.
Mimi na Sandile tukaanza kuelekea kwenye ukumbi wa graduation nikiwa nimejawa furaha kuu. Nikiwa nawaza sasa nimeingia kwenye ulimwengu wa opportunities. Tukiwa tunaelekea ukumbini tukakutana na rafiki yangu mwingine akiwa na demu wake nao wamekuja kwenye graduation yangu. Kwa kweli nilijiona kama mfalme. Kuzungukwa na watu wanaokupenda na wanaofurahia mafanikio yako ni hisia nzuri sana.
Mgeni rasmi alikuwa mtu maarufu sana kwa South Africa ambaye nisingependa nimtaje. Alitoa speech moja nzuri sana iliyotufanya magraduate wote tuone anything is possible, you can be anything you want. Hapo nikawa napiga picha jinsi maisha yangu yatakavyobadirika, nikawa nafikiria kuwa na mwanamke mrembo, nyumba nzuri ya kuishi kwenye suburb, maisha ya kutoka kila weekend na kwenda kula bata nikiwa na mke wangu mrembo ambaye atanielewa na kufurahia maisha kama tupo peponi. Nikawa najiona naingia boardroom nikiwa kama CEO wa kampuni kubwa, nimepiga suti naendesha mkutano nikiwa nimezungukwa na wafanyakazi.
Ulipigwa wimbo wa taifa wa South Africa, baada ya wimbo ndio shughuli za graduation zikaanza. Mgeni rasmi alikuwa anataja jina la graduate na kwenda mbele kushikana mkono, kupiga picha na kukabidhiwa cheti. Jina la graduate likitajwa ndugu zake wanashangilia na kupiga vigelegele akiwa anaenda kupokea cheti. Hatimae jina langu likatajwa, yalisikika makelele hayo hata sikujua yametoka wapi. Nilitaka kuangalia ni wakina nani hao wanaonishangilia maana nilijua kuna watu wanne tu ndio wamekuja kunipa company ambao ni Sandile, Pontsho, rafiki yangu na demu wake. Ule ukumbi umejengwa kama uwanja wa mpira. Juu wanakaa wageni waalikwa hivyo graduate mnakuwa mmekaa chini, kwa hiyo ukitaka kuwaona wageni waalikwa inabidi utazame juu. Niliposikia yale makelele ya kunishangilia niliona noma kuanza kuangalia juu ilihali naelekea kwa mgeni rasmi kwenda kuchukua cheti na kupiga picha. Nilitamani sana kugeuza shingo niangalie ni watu gani hao wanaonishangilia ila haikuwa rahisi hivyo niliendelea kubaki na shauku yangu mpaka pale shughuli itakapoisha maana watu walikuwa wamejaa hasa, ukumbi ulikuwa umefurika. Huko parking magari yalikuwa yamejaa hadi sehemu ya kupaki ikawa haitoshi. Magari mengine yakawa yamepaki hadi barabarani. Nakumbuka tulipotoka tuliikuta gari moja iliyokuwa imepakiwa barabarani imedondokewa na mti, kioo chote cha mbele kimemwagika na mti umeenda kujikita kwenye siti za mbele. Huyo mweye gari nadhani alilaani sana siku hiyo.
Baada ya hotuba ya mgeni rasmi na shughuli ya graduation kuisha nikawa natoka nje kwenda kukutana na hao wageni wangu waalikwa kwa ajili ya kile walichoniandalia. To my surprise nikamkuta Khumbu yupo pamoja na akina Sandile. Ile kutoka tu nje ghafla namuona Khumbu akinikimbilia na kuja kunivalisha shada la maua. Sikutegemee kumuona Khumbu siku hiyo, na niliamini hajui kama leo ni siku ya graduation yangu na hajui kama nipo Durban. Hapo hapo nikaanza kutokwa na machozi. Sijui yalikuwa ni machozi ya furaha au machozi ya hisia za mapenzi, sielewi. Kulikuwa na watu kama sita hivi. Alikuwa ameongezeka Khumbu na mke wa Sandile. Basi kila mtu ananipa hongera huku Sandile akawa ananipiga picha kwa camera yake ile ya kazi.
Baada ya zoezi la kukumbatiana na kupongezana tukawa tunaelekea parking kwa ajili ya kuondoka na kwenda kupata chakula cha pamoja nilichoandaliwa. Niliingia kwenye gari ya Sandile, Khumbu na wengine wakatumia magari yao. Tulienda mgahawa mmoja unaitwa Nandos, haukuwa mbali sana na pale chuoni. Njia nzima nilikuwa najiuliuza Khumbu kafikaje hapa, nani kamwambia leo ni graduation yangu?
Itaendelea
Mkuu hongera sana.Photo
Ndiyo Khumbu au [emoji95][emoji111]Photo
Ni yeye ni yeye (kwa sauti ya tid)Photo
Hongera Sana mheshimiwa rais JPMPhoto
Duh, kifaa bombastic hataree fire! 👌Photo