Inaendelea
Siku hiyo baada ya boss kunishauri nisiondoke niliendelea kutafakari sana. Nikawa na mawazo yanayogongana. Wazo moja linaniambia nibaki tu niendelee kuishi SA, wazo lingine linaniambia nirudi nyumbani nikaangalie fursa Bongo. Nikawa najipa matumaini kwa elimu niliyoipata South Africa haitakuwa tatizo kupata kazi Bongo, maskini wa Mungu nikawa najipa matumaini kuwa nikifika Bongo lazima nilambe kitengo TRA hahahaha! Usilolijua ni kama usiku wa giza. Niliporudi nilikuta TRA ipo corrupted balaa kwenye kupata kazi. TRA walikuwa wanatangaza nafasi za kazi kwenye tovuti yao, kila nikiapply hata kuitwa tu kwenye interview hakuna. Ikabidi niachane na kazi za TRA, niliona hizi kazi zinamilikiwa na watu kutoka kanda flani.
Haya tuendelee, achana na mambo ya TRA. Nilikata shauri, sitaki ushauri wowote, hata aje nani kuniambia nibaki South Africa sitaki, hapa lazima nirudi Bongo nikaenjoy maisha na dada zangu. Kwanza nishachoka kila siku kuongea kingereza, Kiswahili mpaka nipige simu nyumbani au nikutane na wabongo wenzangu. Aah! mie narudi nyumbani bhana. Nikampigia simu demu wangu wa Bloemfontein, nikamwambia aje kuna jambo nahitaji kumweleza. Maamuzi yote haya niliyachukua siku ilele niliyoongea na boss, kwa hiyo nilipofika nyumbani usiku wake ndio nikaamua liwalo na liwe I’m going home. Nikampigia simu Amina nikamweleza ajiandae kunipokea. Nikampigia simu na mwanamke wa Sinza nikamwambia ajiandae kunipokea. Hapo kila demu anashangilia bonge la bwana anarudi Bongo kuja kunioa hahahahah!
Kesho yake nikaenda ofisini, nikamfuata Boss nikamwambia, boss ushauri wako nimeutafakari lakini nimeona acha nirudi tu nyumbani. Boss akaniangalia kisha akasema “if you are sure of what you are doing it’s okay, no problem”. Ila akaniomba nikae wiki moja ili wapate replacement na niweze kumfanyia hand over ya majukumu.
Jioni nilirudi home nikiwa tayari najiona naenda kuanza maisha mapya Bongo, japo hofu ya maisha mapya ilikuwa inaniijia lakini nilikuwa najipa matumaini kuwa naenda nyumbani kwa wazazi, kwa ndugu na jamaa, kwa watu wanaonijua, na kwa elimu yangu sitakiwi hata kuogopa maisha. Nikikosa kazi Bongo nitarudi South Africa, sijaua.
Yule mwanamke wangu alikuja akiwa na shauku ya kutaka kujua nimemuitia nini. Nikamweleza kuwa nimeamua kurudi nyumbani na tayari nishamjulisha na boss hii dhamira yangu. Ila niliamua kumdangaya kuwa naenda tu nyumbani kusalimia kwa sababu ni miaka mingi imepita sijawaona ndugu zangu hivyo nitarudi. Ila nikirudi SA sitakuja Bloemfontein nitaishia Durban, kwa hiyo asiwe na wasiwasi. Nikirudi nitatafuta kazi Durban kisha atakuwa anakuja kunicheki. Yule demu baada ya kusikia maelezo yangu aliniambia kuwa alijua tu kuwa nitamuacha, yaani hili alilitegemea, na suala la mimi kurudi South Africa ni uongo tu. Mie niliendelea kumsihi aniamini, asiwe na wasiwasi nitarudi. Hakuwa na jinsi ilibidi akubaliane na mimi japo kishingo upande.
Niliendelea kwenda kazini kwa hiyo wiki moja niliyoombwa. Siku ya mwisho pale ofisini boss alinilipa mshahara wa miezi miwili akaniambia mshahara mmoja utanisaidia gharama za usafiri lakini tayari nilikuwa nishafanya booking ya flight kutokea Joburg to Dar. Hiyo siku ilinunuliwa na cake, wafanyakazi wakaitwa kuja kula cake na kuniaga. Ilikuwa ni siku ya huzuni kwangu ila nilikuwa nikifarijika nikifikiria narudi nyumbani.
Ndani ya hiyo wiki nilianza kupiga mnada vitu vyangu vya ndani. Nilianza kuwatafuta wabongo, waburundi na wakongo waliokuwa wanaishi Bloemfontein na kuanza kuwauzia. Kuna baadhi ya vitu havikuweza kupata mteja hivyo tukakubaliana na huyo demu aviuze kisha hela atanitumia. Nikafanya process ya kurudisha nyumba kwa real estate, na siku ya mwisho baada ya kurudisha nyumba nilienda kulala kwa huyu demu wangu. Nikawapigia simu jamaa zangu wa Durban na kuwajulisha nitapitia hapo kuwaaga. Pia nikampigia simu Khumbu nikamjulisha siku flani nitakuwa Durban hivyo ningependa tuonane. Sikumwambia kama naondoka South Africa, nillimjulisha tu kuwa nitakuwepo Durban.
Itaendelea