Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Leo nipo free nitatupia episode nyingine moja.
Amina mkuu!
76541.jpg
 
Huyo Dada wa Sinza na Amina nao Wana story yao katika uzi mwingine kabla ya huu Kaka. So ukiwasoma ndo utaelewa kwenye huo uzi mwingine
Hapana mkuu. Kwenye huo uzi hao watoto ni tofauti na Amina na huyu wa Sinza.
 
Inaendelea

Siku hiyo baada ya boss kunishauri nisiondoke niliendelea kutafakari sana. Nikawa na mawazo yanayogongana. Wazo moja linaniambia nibaki tu niendelee kuishi SA, wazo lingine linaniambia nirudi nyumbani nikaangalie fursa Bongo. Nikawa najipa matumaini kwa elimu niliyoipata South Africa haitakuwa tatizo kupata kazi Bongo, maskini wa Mungu nikawa najipa matumaini kuwa nikifika Bongo lazima nilambe kitengo TRA hahahaha! Usilolijua ni kama usiku wa giza. Niliporudi nilikuta TRA ipo corrupted balaa kwenye kupata kazi. TRA walikuwa wanatangaza nafasi za kazi kwenye tovuti yao, kila nikiapply hata kuitwa tu kwenye interview hakuna. Ikabidi niachane na kazi za TRA, niliona hizi kazi zinamilikiwa na watu kutoka kanda flani.

Haya tuendelee, achana na mambo ya TRA. Nilikata shauri, sitaki ushauri wowote, hata aje nani kuniambia nibaki South Africa sitaki, hapa lazima nirudi Bongo nikaenjoy maisha na dada zangu. Kwanza nishachoka kila siku kuongea kingereza, Kiswahili mpaka nipige simu nyumbani au nikutane na wabongo wenzangu. Aah! mie narudi nyumbani bhana. Nikampigia simu demu wangu wa Bloemfontein, nikamwambia aje kuna jambo nahitaji kumweleza. Maamuzi yote haya niliyachukua siku ilele niliyoongea na boss, kwa hiyo nilipofika nyumbani usiku wake ndio nikaamua liwalo na liwe I’m going home. Nikampigia simu Amina nikamweleza ajiandae kunipokea. Nikampigia simu na mwanamke wa Sinza nikamwambia ajiandae kunipokea. Hapo kila demu anashangilia bonge la bwana anarudi Bongo kuja kunioa hahahahah!

Kesho yake nikaenda ofisini, nikamfuata Boss nikamwambia, boss ushauri wako nimeutafakari lakini nimeona acha nirudi tu nyumbani. Boss akaniangalia kisha akasema “if you are sure of what you are doing it’s okay, no problem”. Ila akaniomba nikae wiki moja ili wapate replacement na niweze kumfanyia hand over ya majukumu.

Jioni nilirudi home nikiwa tayari najiona naenda kuanza maisha mapya Bongo, japo hofu ya maisha mapya ilikuwa inaniijia lakini nilikuwa najipa matumaini kuwa naenda nyumbani kwa wazazi, kwa ndugu na jamaa, kwa watu wanaonijua, na kwa elimu yangu sitakiwi hata kuogopa maisha. Nikikosa kazi Bongo nitarudi South Africa, sijaua.

Yule mwanamke wangu alikuja akiwa na shauku ya kutaka kujua nimemuitia nini. Nikamweleza kuwa nimeamua kurudi nyumbani na tayari nishamjulisha na boss hii dhamira yangu. Ila niliamua kumdangaya kuwa naenda tu nyumbani kusalimia kwa sababu ni miaka mingi imepita sijawaona ndugu zangu hivyo nitarudi. Ila nikirudi SA sitakuja Bloemfontein nitaishia Durban, kwa hiyo asiwe na wasiwasi. Nikirudi nitatafuta kazi Durban kisha atakuwa anakuja kunicheki. Yule demu baada ya kusikia maelezo yangu aliniambia kuwa alijua tu kuwa nitamuacha, yaani hili alilitegemea, na suala la mimi kurudi South Africa ni uongo tu. Mie niliendelea kumsihi aniamini, asiwe na wasiwasi nitarudi. Hakuwa na jinsi ilibidi akubaliane na mimi japo kishingo upande.

Niliendelea kwenda kazini kwa hiyo wiki moja niliyoombwa. Siku ya mwisho pale ofisini boss alinilipa mshahara wa miezi miwili akaniambia mshahara mmoja utanisaidia gharama za usafiri lakini tayari nilikuwa nishafanya booking ya flight kutokea Joburg to Dar. Hiyo siku ilinunuliwa na cake, wafanyakazi wakaitwa kuja kula cake na kuniaga. Ilikuwa ni siku ya huzuni kwangu ila nilikuwa nikifarijika nikifikiria narudi nyumbani.

Ndani ya hiyo wiki nilianza kupiga mnada vitu vyangu vya ndani. Nilianza kuwatafuta wabongo, waburundi na wakongo waliokuwa wanaishi Bloemfontein na kuanza kuwauzia. Kuna baadhi ya vitu havikuweza kupata mteja hivyo tukakubaliana na huyo demu aviuze kisha hela atanitumia. Nikafanya process ya kurudisha nyumba kwa real estate, na siku ya mwisho baada ya kurudisha nyumba nilienda kulala kwa huyu demu wangu. Nikawapigia simu jamaa zangu wa Durban na kuwajulisha nitapitia hapo kuwaaga. Pia nikampigia simu Khumbu nikamjulisha siku flani nitakuwa Durban hivyo ningependa tuonane. Sikumwambia kama naondoka South Africa, nillimjulisha tu kuwa nitakuwepo Durban.

Itaendelea
 
Hiyo ni page ya kwanza na ya pili ya academic records. Mnaweza mkaona performance ilivyobadirika ya mwaka wa kwanza ukilinganisha na miaka iliyofuatia kabla Khumbu hajanichanganya na miaka iliyofuatia baada ya Khumbu kunichanganya. Masomo ya mwaka wa kwanza yameandikwa I, wa pili II na wa tatu III. Na hicho kingine ni ile siku niliyoaindika kwenye diary kuwa narudi Bongo.
 

Attachments

  • Academic.jpeg
    Academic.jpeg
    26.2 KB · Views: 95
  • Academic2.jpeg
    Academic2.jpeg
    25.2 KB · Views: 95
  • Diary.jpeg
    Diary.jpeg
    19.5 KB · Views: 95
Hiyo ni page ya kwanza na ya pili ya academic records. Mnaweza mkaona performance ilivyobadirika ya mwaka wa kwanza ukilinganisha na miaka iliyofuatia kabla Khumbu hajanichanganya na miaka iliyofuatia baada ya Khumbu kunichanganya. Masomo ya mwaka wa kwanza yamaendikwa I, wa pili II na wa tatu III. Na hicho kingine ni ile siku niliyoaindika kwenye diary kuwa narudi Bongo.
gud mkuu...ila tuwekee na picha ya khumbu...
 
Let's goooo sasa tupo ktk huzuni mode ,itakua hawa vijana wa Tz amina na mwenzie walikua wanakuchomea dawa hahaha
Hapana ulikuwa tu ule mzuka wa kwamba narudi Bongo naenda kukutana na warembo wa nyumbani. Pia nilikuwa sijarudi muda mrefu sana hivyo zile feelings za kumiss home mixer na mateso ya Khumbu basi ikawa ni sababu tosha kabisa ya kuondoka huko.
 
Uzi nimeuanza leo leo na nimejitahid mpaka hapa ulipofikia,nikupongeze mwandishi kwa uandishi wako mzuri na pia kujitahid kujibu maswali ya wasomaji kwakwel wewe ni tofauti na waandishi wengine wenye tabia ya kuutelekeza nyuzi zao,
Achana na watu ambao wao kila kitu wanakosoa tushawazoea,m hata ukikaa wiki siwazi maana najua kadhia iliyopo kwenye kuchapa story ndefu kiasi hiki
 
Hiyo ni page ya kwanza na ya pili ya academic records. Mnaweza mkaona performance ilivyobadirika ya mwaka wa kwanza ukilinganisha na miaka iliyofuatia kabla Khumbu hajanichanganya na miaka iliyofuatia baada ya Khumbu kunichanganya. Masomo ya mwaka wa kwanza yamaendikwa I, wa pili II na wa tatu III. Na hicho kingine ni ile siku niliyoaindika kwenye diary kuwa narudi Bongo.
binafsi napenda mtu anaeandika mambo yake katika diary. ni usmart fulan upstairs.
hivi konda since then hujawahi rudi tena south Africa?
au nitulize niendelee kula mtori nyama ziko chini.
nadhani pia kitisho cha kuuawa south kilikua ya sababu pia ya kukushawishi kurud bongo.
 
binafsi napenda mtu anaeandika mambo yake katika diary. ni usmart fulan upstairs.
hivi konda since then hujawahi rudi tena south Africa?
au nitulize niendelee kula mtori nyama ziko chini.
nadhani pia kitisho cha kuuawa south kilikua ya sababu pia ya kukushawishi kurud bongo.
Endelea kunywa mtori nyama utazikuta chini mkuu.
 
Ndugu wasomaji nimewasiliana na Konda msafi amenambia ameacha utoto.Amesema muendelee kuwa watulivu na kesho atatupia episode nyingine.Ni bandika bandua had amalize...
 
Back
Top Bottom