Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jamani naomba niikatishe hii stori. Hii stori ni ndefu sana haitaisha leo wala kesho na inanichukulia muda wangu mwingi sana. Ni stori iliyochukua karibia miaka 6, since 2008 hadi 2012, kwa hiyo unaweza kuona ilivyo ndefu. Kwa wale wenye shauku ya kutaka kujua Khumbu yuko wapi kwa sasa, jibu ni kwamba Khumbu alifariki, hatunaye tena duniani. Mwenyezi Mungu aendelee kumuweka mahali pema peponi. I truly miss her and believe one day I will meet her in other worlds of God.
Mimi nilimaliza chuo nikarudi Bongo, nipo Dar nina familia tayari. Kuna uzi mmoja nilishauleta humu mnaweza kuutafuta kuhusu yaliyonipata niliporudi Dar. Asanteni na kwa herini.
Daah umetuacha juu kwa juu
 
Shukrani mkuu kwa appreciation. Tupo pamoja. Hii stori niliileta kwa hiari yangu na nitaimaliza kwa hiari yangu. Tulikotoka ni mbali, mwisho wa safari umekaribia, yamebaki matukio mawili tu kulingana na muainisho niliouweka pale mwanzo kabisa wa hii stori. Tuvumiliane tu ndugu zangu, tupo ukingoni.
umesema vema kabisa lakini dear bas do not make promises za kumaliza siku flani maana unatupa expectations mwisho wa siku zinadisapoint mi nashauri kausha tu hata kama miaka ukija shusha yote iishe sio unasema jtano na jtano unakuja na sound kiubinadam hata kama ni mali yako na hiyari yako inakera hadhira iliyokusudiwa mkuu mbaya zaidi tunakuona unareply yani ni kama unamdai mtu af mnaenda mgahawani anaagiza supu chapati mbili...good job upo vizuri
 
Khumbu atamzidi huyu kuku wa kienyeji kwa utamu kweli. Wanapakaa babycare, wanabana nywele hawatii dawa, kutwa nzima na kanga hata akienda benki, ciakula chao ni mihogo na miguu ya kuku, kupiga mswaki mpaka akumbushwe na mama yake ila denda lake tamu kinyamaaa.

Hawavaagi bra ila chuchu konzi. Ushawahi kukutana na hizi type kitandani? Hautojutia kumlamba ni watamu mnoooo. UNABISHA?
View attachment 1710472
Wanakuaga watamu ila wanatoaga kaharufu flan kanakinaisha sana
 
Konda msafi kisha nitumia story yoteee pm tena inamengi zaidiii ya haya anayowapa... ila mpaka umtumie hela ya vocha

Ubahili wenu mtachelewa sanaaa
 
Duh kuna story nyingi sana humu JF hasa siku hizi kwa jinsi tulivyobanwa na TCRA hakuna siasa wala majukwaa yetu watu wazima
Ila story ya Mchepuko alivyoenda mletea fujo Mke wa jamaa imenigusa sana na hata mm nitaleta mnisaidie hii michepuko balaa
WA KWANGU kaniletea fujo na kazaa mtoto na mfunga buti mmoja analinda kiwanda jirani na nalipompangia chumba, kumbe mm nikiwa na wife yeye anaingiza, usiku mm zamu yangu mchana, siku tukagongana, akanidanganya ni wa chumba cha pili kwa shoga yake, hapo cumbani anapenda kuangalia tamthilia tu, basi alipotoka nikamwambia mbona mchafumchafu analalalindoni chini, akamtete mtu namna hiyo nisimdharau, kwani bibie chumnba cha pili anamsifu kuwa ligwaride analipatia si mchovumchovu (nikajua ni mm ninayesembwa viwili chali tena na condom)

Basi akajifungua mtoto kadi jina langu du miezi mtoto hatufanani nikabinywa sikio na shoga niliyeambiwa wa mfunga buti sio wako huyo, kuangalia mapigo yangu na ndomu mimba imeingiaje, nikamkatalia, fujofujo mpaka kwa wife na mama yangu,
nikaomba Dawati la jinsia POLISI tupime DNA, basi yule mfunga buti kusikia

Wazee na mm nimechoka, usiku sana ngoja nipumzike nitaendelea baada ya konda msafi
[emoji1787] 😀 [emoji23] [emoji7] [emoji1787] [emoji1787][emoji23][emoji56][emoji16] usiku mwema raha ya JF

Ikawaje mzee [emoji23][emoji23][emoji23]

Nipo interested kujua iliishaje hiyo issue.
 
Shukrani mkuu kwa appreciation. Tupo pamoja. Hii stori niliileta kwa hiari yangu na nitaimaliza kwa hiari yangu. Tulikotoka ni mbali, mwisho wa safari umekaribia, yamebaki matukio mawili tu kulingana na muainisho niliouweka pale mwanzo kabisa wa hii stori. Tuvumiliane tu ndugu zangu, tupo ukingoni.
Konda naomba nikukumbushe umesahau na tukio la 3 (Picha ya Khumbu)....😂
 
Ikawaje mzee [emoji23][emoji23][emoji23]
Nipo interested kujua iliishaje hiyo issue.
Premij ni vituko sana huyo Binti ni Mnyambwa anaishi na Mama yake nyumba ya vyumba vi3 majirani wamenieleza hakatai mtu ni anawapanga hasa, usiku kwa mchana na hata wakigongana hawagombani kabisa, Mama anawapangua wanaondoka km yupo aliyewahi, ndio anayeendelea kula mzigo.
Nilitumia Kikao cha Mtaa ili nipate kibali cha kwenda Dawati la Jinsia POLISI, basi mfungabuti akaniwahi POLISI kuwa mtoto ni wake ila wanibane nitoe matumizi wala wasiniruhusu nikawapime DNA wote wanne, hapo nikagonga ukuta
sasa mtoto amekua funga buti alishaachishwa kazi kwa ajili ya ulevi na alikuwa na mke, mke akamkimbia mfunga buti
sasa huyu mchepuko wangu naye akamkataa, jina nimeambiwa anatumia la mfunga buti ila shule kaandikisha ubini wangu, juzi ananiambia hata akifa kwa ukimwi au Corona nikachukue mtoto.
yaani naogopa Mungu ameninusuru ila nashindwa kumuacha kwani kaumbika kuliko Khumbu yeye ana asili ya unyambwa na ututsi baba yake ni hawa madereva wa Malori Rwanda, waliokuwa wanapark malori vituo km Kintiku ndipo Mama akabeba mimba.
Kweli Bint ana vituko kwani kwa umbo mwembaba shingo ndefu nyuma kajazia hivyo ni mwepesi na popote anajikunja na anakupea iwe ndani ya gari, iwe mlingotini wima km miti porini iwe ile chuma mb. uchochoroni, tatizo alitaka atambulike kwetu wakati mtoto sifanani nae kabisa na DNA hataki
Ngoja niishie hapo kwanza nimpishe mleta Mada konda msafi
 
Endelea tu mkuu. Mie ya kwangu nitaimalizia nikipata utulivu. Endelea kutuhabarisha hili sakata mkuu.
 
Matukio yote nayasummarise hapa angalau nitoe lawama maana mnavyonishambulia si kitoto.

Baada ya Khumbu kuja na huo mkoko mpya nikamwuliza ameupataje. Akasema kanunua kwa mkopo. ...Baadae kupitia kwa yule demu wa mshikaji niliyewaambia alihamia, alinipa siri ya huo mkoko mpya wa Khumbu. Aliniambia hiyo ndinga kanununuliwa na Mayor wa Durban. Khumbe hata ile habari ya kuniambia kuwa kapata kazi bank hatutakuwa tunaonana mara kwa mara ilikuwa uongo tu. Alitengeneza mazingira ya mimi kutokuwa namuhitaji kila mara ili Mayor akimuhitaji awe anapatikana. Yaani mimi aniweke kando ili awe huru na Mayor. Hivyo hizo story za kuwa busy na kazi ilikuwa za uongo.

Siku niliyotaka kuingia mikononi mwa police:

Wale jamaa walianza kufungia mzigo humu ndani tulimokuwa tunaishi. Lile gheto la kule mwanzo ulikokuwa unafungiwa mzigo waliacha kulitumia. Hivyo mzigo ukaanza kupimwa humo humo getoni tunapoishi. Binafsi kukaa kwenye nyumba na hayo makitu kilikuwa ni kitu ambacho nilikuwa sikitaki kabisa. Baada ya mambo kuanza kufungiwa humo nikaanza mchakato wa kuhama maana niliona hapa naenda kuhatarisha maisha yangu ya chuo. Nilijua tu kuna siku tutavamiwa humu.

Kufunga hayo madude wanatumia hii mifuko ya plastic tuliyokuwa tunaiita ya rambo. Sasa kwenye kufunga lazima kuwe na vipande vipande vya hiyo miplastic kwenye kukatakata. Na hivyo viplastic ukikutwa navyo hata kama hawajakuta mzigo umekwisha maana wazee wanavijua hivyo vipande vya plastic huwa vinasababishwa na nini.
Sasa hawa jamaa kila wakifunga walikuwa wanavizoa tu hivyo vipande na kuvikusanya na kuviweka kwenye makabati. Walikuwa wanasubiria mpaka yawe mengi ndio wakatupe. Kitendo cha kuishi na hivyo vipande vya plastic kilikuwa kinaninyima amani kabisa, halafu ukiwaangalia hawa masela hata hawajali kabisa. Nilichokuwa nafanya ilikuwa kila asubuhi nikiwa naenda chuo navishindilia kwenye begi naenda kuvitupa mbele ya safari ili angalau tukivamiwa wasikute ushahidi wowote. Maana hawa jamaa zangu walikuwa hawajali kabisa.

Sasa siku moja ilikuwa Jumapili, na sikuwa na mpango wa kwenda kokote. Mule ndani kulikuwa na hivyo vipande vya viplastic. Nikaamua acha nikavitupe ili nishinde home kwa amani. Nikawa nimevishindilia kwenye begi langu la shule. Ila kama Mungu tu ameniambia, Konda msafi be careful. Japo nilikuwa natoka mara moja kwenda kuvitupa, niliamua kuvaa kama vile naenda mbali. Yaani sikutaka kutoka let's say nimevaa bukta na vest kwa sababu najua natoka mara moja na kurudi. Nilivaa nguo kama naenda mjini au chuo. Nikachukua kabisa na kitambulisho changu cha chuo. Nikaweka begi mgongoni, nikatoka ndani, nikashusha ngazi na kuanza kuelekea getini nikiwa na rimoti ya geti. Ile kufungua geti tu nakutoka nje ya geti, mara pah! Kipira cha wazee kimepiga break miguuni kwangu, dah! Roho ikalipuka pah! Nikasema hapa nimekwisha. Wakisema tu fungua hicho kibegi tuone ndani kuna nini nimekwisha. Nikawa naona sasa shule ndio imefikia mwisho. Kipira kimesimama miguuni kwangu. Walikuwa askari weusi. Wakashusha kioo cha gari upande niliokuwepo wakaniambia nisogee karibu. Nikasogea, jamaa walikuwa wawili, kama nilivyosema wote weusi wapo kwenye uniform. Nikawa najitahidi nisionyeshe wasiwasi wowote. Wakaniuliza, unakaa humu ndani? Maana nilikuwa ndio nimetoka tu hapo getini. Nikasema ndio nakaa humu. Wakaniuliza tena, humo kwenye begi kuna nini, nikasema kuna vitabu vya dini, naelekea kanisani kufundisha kipindi cha dini kwa ajili ya watoto. Halafu kile kitambulisho cha chuo nilikuwa nimeking'iniza kifuani. Wakaniuliza wewe ni mwanafunzi, nikasema ndio, nikawapa kile kitambulisho wakakiangalia harafu wakanirudishia. Kisha wakasema tulikuwa tunakusalimia tu, wahi kanisani ukamtumikie Mungu. Wakakanyaga mafuta wakasepa, dah! Aisee! Kwanza nilifikiria sijui nirudi ndani nisiendelee kwenda kuyatupa haya madude. Nikaona acha niendelee na safari ya kwenda kuyatupa maana wasije wakageuka wakaniona tena narudi ndani nikawapa wasiwasi, mbona huyu kasema anaenda kanisani halafu amerudi ndani tena? Basi nikaanza kutembea fasta, hapo naangalia kona yoyote nitakayokutana nayo nipige, nipotee kabisa kwenye hiyo barabara. Kona tu ya kwanza nilipoipata nikaikamata, nikatembea mbele kidogo tu, nikafungua begi na kuyatoa hayo madude fasta na kuyatupa. Nikatembea mbele kabisa huko kuzunguka ili nirudi nyumbani kutokea upande mwingine.

Itaendelea jamani.... nilisema nitasummarise ila nashindwa kusummarise. Huko mbele acha nijifunze kusummarise.
Ok, Ngoja nisome sasa, Sema si ungeiwekea Link kule juu kwenye ule Muendelezo au?
 
Back
Top Bottom