oscar classic
JF-Expert Member
- Mar 21, 2020
- 731
- 1,367
Siyo kumbu !!kudadekiKumbu kama kumbu
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Siyo kumbu !!kudadekiKumbu kama kumbu
Dumelang ✔Daaa!! umenikumbusha, misele yangu paleeee! Lady Blandy ndani ya Bloemfotein.karibu mno na kingdom of Lesotho huko Maseru mole nilikuwa natinga kila week end.
Palee!! mitaa ya Kubhtsoana.western maseru, Hapita.quachasnake. Qeen Mamhato loool bin Duuu!!!
ndo zilikuwa mitaa zangu mpaka nikajua kisotho ni patamu usipime.
Na kweli bana wale wamechongwa utadhani si watu. Halafu haikuwa rahisi kujua mimi siyo Msotho. Tulifanana sana.
tukikutana na wenyeji Njiani hawanisalimii kiinge no. wananisalimia
"Dumela" hujwang" uswakae! basi naiitikia kiulainiii!!! Hawakujua mie mbongo. Kwa mbongo
Zile kugha ni rahisi tu ukitaka.
Sasa nakuuliza Mkuu baba pale Blomfotein kuna chuo cha medicine je nita mudu maisha ya kusoma na kufanya vibarua nikajaribu? Hali ikoje kwa hilo mkuu tafadhali nakuomba.
Ntate moruti✔af majina yao km ya kiswahili tu . Mpho, lebhu.tatho, matabho, Tante mughuti (baba mchungaji)
Unaona sasa ntate kikurya ni tata)
Ng'wana allaa=mwana alia.
Tuliza ng'wana=tuliza mtoto yaani rahisi haiitaji umakini saana kuijua
Mkuu nijibu baba shulee ya medicine huko Bloemfotein vipi?
Je unajua chochote nikajinoe?
Ok, Kumbe uzi unaendeleaInaendelea
Tulipofika Nandos tukaenda kukaa kwenye kona moja ambayo kumbe Sandile alikuwa yatari kaomba iwe reserved kwa ajili yetu maana tuliikuta tayari meza zimeshaunganishwa na kuna glass zimewekewa maua kwa ndani na kuna cake imewekwa katikati ya meza imeandikwa “Congrats Konda msafi”
Tukaizunguka hiyo meza, mie nikawa nimekaa katikati ya Sandile na Khumbu. Tukiwa tunasubiria chakula tukaanza kutambulishana especially kwa upande wa Khumbu maana sisi watatu tu ndio tulikuwa tunamjua Khumbu wengine wote walikuwa hawamjui. Sandile akaniomba nitoe utambulisho. Nikaanza kumtambulisha mmoja baada ya mwingine. Khumbu alikuwa amekaa pembeni yangu upande wa kushoto, kulia kwangu alikuwa amekaa Sandile. Nilianzia upande wa Sandile nikawa nazunguka kuelekea upande wa Khumbu. Nilipofika upande wa Khumbu nika-pose kwanza kisha nikamwangalia usoni. Nikamwomba ajitambulishe mwenyewe, watu wote wakaanza kucheka, wakaanza kunitania niache ubaguzi, haiwezekani watu wote niwatambulishe halafu nimwambie Khumbu ajitambulishe. Khumbu akiwa anacheka akaingilia kati, akasema atajitambulisha mwenyewe. Akasema I’m Khumbu and I’m the wife of Konda msafi, watu wote wakaanza kushangilia huku wakicheka. Watu wakaanza na utani, wanamtania Khumbu wanacheka yaani ikawa utani na kucheka, kila mtu anaongea lake. Wengine wanatupiga picha mimi na Khumbu. Wengine wanataka nipige nao picha, basi ikawa vurugu tu na stori nyingi.
Baada ya utambulisho nikakata keki na nikaanza kumlisha Khumbu, pia chakula kikaletwa. Nandos wanapika nyama zao kwa mvuke, hawakaangi kwa mafuta kama KFC. Watu wengi South Africa ambao wapo health conscience huwa wanapenda chakula cha Nandos ukilinganisha na migahawa mingine kama KFC, Macdonald au Chicken licken. Kwa hiyo ililetwa nyama choma very jucy, nyama tamu kinoma ya beef, kuku wa kuokwa mlaini na vyakula kibao pamoja na vinywaji. Hakika ilikuwa siku murua sana.
Tukiwa tunaendelea kula nilimwuliza Khumbu amejuaje kama leo ni graduation yangu. Kwanza nilimshukuru kwa ujio wake ila nilitaka kujua amejuaje kama leo ni graduation yangu, na ameonana vipi na akina Sandile? Alichonijibu nilichoka. Akasema kuna mtu tumegraduate naye ambaye ananijua, anakaa huko huko Inanda hivyo alimpa ratiba yote ya graduation ceremony, hivyo alipanga lazima aje anifanyie surprise. Sandile naye akaongezea kuwa wakati MC anatangaza kuelekeza sehemu ya kukaa ya wageni waalikwa, kwenye zile pilikapilika za kupanda juu na kwenda kukaa wakaonana naye hivyo wakamwita na kwenda kukaa sehemu moja. Kwa hiyo yale makelele niliyoyasikia yakipigwa baada ya jina langu kutajwa yeye ndio alikuwa kinara wa kushangilia.
Baada ya kumaliza kula, watu wengine wakaanza kuaga na kuondoka. Na mimi nikawaelezea kuwa sitalala Durban kwa sababu inabidi nirudi Bloemfontein maana nimechukua ruhusa ya siku mbili tu kazini. Watu wote wakaondoka tukabaki mimi na Khumbu, ila nikaenda kwenye gari la sandile kutoa vitu vyangu maana kuna nguo zangu nilikuwa nimeziacha humo.
Tulipobaki wawili nilianza kumwuliza kwa nini hakuja Bloemfontein kipindi nimemtumia nauli. Akasema hilo swali alishajibu na hatapenda nimwulize tena. Of course namjua Khumbu toka zamani huwa hapendi kuulizwa maswali ambayo anajua kabisa majibu yake yatamtia hatiani. Pia nilimwuliza kuhusu ile simu niliyopigiwa ya kufumuliwa kichwa, pia aliendelea kusema alishanijibu na zaidi ya yote hahusiki. Na akaniomba niachane na maswali yatakayochafua hali hewa maana siku ya leo ni siku ya furaha, na hakuja hapa kuniharibia siku bali kusherehekea na mimi. Basi baada ya kuniambia hayo tulianza kupiga stori za mahusiano yetu kipindi cha nyuma na kukumbushana historia ya mapenzi yetu. Mwisho nikamwomba tuondoke wote twende Bloemfontein. Akasema kwa sasa hawezi kuondoka Durban ana mambo yake ya utafutaji hivyo akiondoka yataharibika. Akashauri kama ninataka kuwa karibu naye nitafute kazi Durban. Binafsi niliona kuna shida sehemu, kuna mtu anammiliki, hapa anaongea tu, hata kama nikihamia Durban bado mambo ya kuumizana yatakuwa palepale. Sikutaka hata kuomba mchezo, nilijua nikiomba lazima ataniambia kwa leo haiwezekani labda siku nyingine wakati mie sina muda wa kuendelea kukaa Durban. Nilimwomba tu anipeleke sehemu niliyofikia nikachukue begi langu kisha anipeleke stand nikaangalie usafiri wa kunirudisha Bloemfontein.
Itaendelea
Hahahahaha, Zilizala la Picha Feki ya KhumbuStori haijaisha ndugu yangu. Nasubiri kwanza upepo wa picha fake ya Khumbu upite ili tuendelee. Si unaona kulivyochafuka humu na picha fake ya Khumbu.
1.Africa Dzonga=Africa kusini lugha shangani/vendaMimi naomba ufafanuzi wa maneno haya mawili yana maana gani kiswahili au ni misemo tu :-
1.Dizonga
2.Mzansi
Khumbulani=kumbukeni.
hujwang ngwaneso? Huswaakae!! Wenna!! Oyiooo! Uko njemaDumelang ✔
Dumela ❌
Ntate moruti✔
Tante mughuti ❌
Wasotho wako njema sana
Nalog off
weye nae kwa nini hukumpiga limbwata la dharula lile la kiumeni kiumeni? Uliumia breee!!Inaendelea
Khumbu alinipeleka nilikofikia kuchukua vitu vyangu kisha akanipeleka stand kuangalia usafiri wa kunirudisha Bloemfontein. Katika mizunguko yote hiyo niliweza kunoticekuwa Khumbu bado alikuwa ananipenda ila ni kama alikuwa na commitment flani hivi zinanamfanya kuwa na wakati mgumu kunisikiliza kila ninachomwambia, maana kuna kipindi alikuwa kama anazama kwenye lindi la mawazo hivi, halafu nikiwa namweleza ni jinsi gani anayafanya maisha yangu kuwa magumu kimahusiano nilikuwa namuona kama mtu anayejutia hivi. Kulikuwa na zile moments ukimya unatawala halafu mkija kuangalia unaona kama kila mtu machozi yanamlengalenga. Aliponifikisha stand, nikashuka na yeye akashuka, tukaagana kwa kukumbatiana, sikuweza kuongea chochote maana kitendo cha kumkumbatia na kuushika mwili wake kilinifanya niingiwe na huzuni sana, nilimsikia tu akitamka maneno mawili “I’m sorry” na akaanza kujitoa mikononi mwangu, nilikuwa nimemkumbatia kuzungusha mikono yangu kiunoni kwake mpaka ikakutana, kwa hiyo akawa anaishika kwa kuiachanisha ili niweze kumuachia. Baada ya kujitoa mikononi mwangu akaingia garini akaondoka. Niliendelea kusimama pale nikimwangalia mpaka alipojichanganya kwenye magari mengine ndio nikaondoka hilo eneo.
Njiani nikiwa kwenye basi nilianza kufikiria vitu vingi sana vya kimaisha. Mojawapo nilianza kufikiria je nieendelee kuishi Bloemfontein nijenge maisha na huyu mwanamke wa Bloemfontein? Je nirudi Durban nikatafute kazi huko ili niweze kuwa karibu na Khumbu? Je nirudi Tanzania nikamthaminishe Amina na yule demu wa Sinza kisha atakayelipa zaidi nije naye South Africa? Baada ya hii graduation je niendelee kuishi South Africa yaani nijichanganye kabisa hapa niachane na mawazo ya kurudi Tanzania yaani hapa Sauzi yawe ndio maisha yangu permanent? Je nirudi Tanzania nikatafute kazi, nikaishi tu nyumbani huenda nikaishi kwa furaha zaidi? Maswali yalikuwa mengi na sikujua lipi niamue.
Baada ya graduation niliendelea na kazi huku nikiwa na huyu mwanamke wa Bloemfontein. Pia niliendelea kuwasiliana na Amina na huyu wa Sinza. Huyu wa Sinza alikuwa na sauti moja amazing. Kipindi naonana naye alikuwa mzuri sana ila kwa kuwa ilikuwa ishapita miaka mingi nilikuwa na wasiwasi kama bado ni mrembo maana wanawake huwa wanabadirika haraka sana, miaka sita kwa wanawake ni miaka mingi sana. Amina alikuwa ananitumia picha na alionekana bado analipa sana tu ila huyu wa Sinza kila nikimwomba anitumie picha alikuwa anadai nije nimuone mwenyewe kwa macho yangu ila kwa maoni yeke yeye ni mrembo wa haja. Huyu wa Sinza kitendo cha kukataa kunitumia picha kilianza kunitia wasiwasi hivyo nikaamua kutuma mtu kwenda kukutana naye ili anipe feedback. Kuna mdogo wangu alikuwa anasoma chuo flani nikampigia simu nikamwomba akamcheki huyu demu. Nikampa namba ya huyo demu na pia nikampigia simu huyo demu nikamwambia shemeji yako nimemwomba aje akusalimie ili mjuane pia apajue unapoishi ili hata kama kuna shida yoyote iwe rahisi kupatikana kwako. Demu akakubali. Dogo akaenda kumcheki na baada ya kumcheki akanipigia simu kunijulisha matokeo. Dogo akaniambia demu ni wa kawaida sana hana maajabu yoyote. Kama ni wa kula na kusepa fresh ila kama unataka kufanya naye maisha na kwa jinsi ninavyokujua unapenda kula vilivyo bora huyo hajafikia viwango vyako. Hiyo ilikuwa tathimini ya dogo. Dah! nikawa najiuliza labda huyu dogo ana jambo lake tu. Mbona demu alikuwa kifaa hivi enzi hizo, iweje awe mbovu tena? Nikasema huyu dogo anazingua, acha niendelee na mchakato wa kuwa naye karibu huyu demu. After all nishatumia gharama za kupiga simu karibia kila siku hivyo hata kama atakuwa halipi acha angalau nikafidie gharama zangu kwa kumla. Hivyo maisha ya kuendelea kuwasiliana na wote hawa wawili yaliendelea hadi niliporudi Tanzania.
Kadri siku zilivyokuwa zinasonga ndivyo nilivyozidi kupata moto wa kurudi nyumbani. Picha za Amina na Sauti ya demu wa Sinza zilikuwa zinanipa matumaini mapya ya kimapenzi. Huyu wa Sinza alikuwa na sauti nzuri hatari, nikiwa naongea naye nilikuwa hadi dushe linasimama. Amina naye hivyo hivyo, picha zilikuwa zinanichangaya sana.
Siku moja usiku mwezi wa 10, 2012nikakata shauri la kurudi nyumbani. Niliamka usiku wa manane, nikachukua diary yangu nikaandika tarehe ya hiyo siku nikasema hii tarehe ndio tarehe niliyokata shauri na kuamua kurudi Bongo.
Kesho yake asubuhi nilipofika ofisini nikamfuata Boss wa kampuni, ni mmoja wa madirectors, nikamwambia “Leo naacha kazi”. Aliniangalia akwa kama anashangaa, akasema nirudie tena nilichokisema, nikarudia tena “Leo naacha kazi” nilimuona kama kaduwaa. Alikuwa ana kikombe cha kahawa mkononi akakiweka kwenye mezani kisha akaniuliza vipi unaumwa? Umechanganyikiwa? Nikamjibu siumwi wala sijachanganyikiwa. Nimeamua tu niache kazi, nimeamua kurudi nyumbani. I miss home. Akasema wewe Konda msafi unacheza na maisha. Unarudi Tanzania kufanya nini? Akaanza kunipa ushauri, nakumbuka kuna maneno nayakumbuka mpaka leo aliniambia, alisema “All these achievements I have I never got them in one day I have acquired them in years. If you serve God, God will take care of you” . Akaniomba jioni baada ya kazi nisiondoke ili tupate muda wa kuzungumza zaidi. Jioni baada ya kazi nikaenda ofisini kwake. Jamaa alinishauri mambo mengi sana ya kimaisha. Akawa ananiambia sio jambo la kushangaza kama siku moja ataniona namiliki kampuni yangu hapa South Africa kama nitakuwa na nidhamu ya kazi. Pale kwenye kampuni nilikuwa nadili na suppliers wa materials na payroll. Auditor wa kampuni alikuwa Ernst and Young kwa hiyo queries zote za auditor kuhusu suppliers na payroll nilikuwa nazi-attend. Kila mwisho wa mwezi nilikuwa napelekwa na dereva wa kampuni kwa auditor. Suppliers wakipiga simu kuulizia malipo yao mimi ndio nilikuwa nadili nao au mimi kuwapigia simu kama kuna mzigo una shida au umechelewa kufika. Kuhakikisha materials yamepokelewa na kampuni ilikuwa ni kazi yangu, invoice za suppliers lazima nizihakiki kabla ya malipo. Jamaa akawa ananiambia hatashangaa siku moja akiniona nimeshakuwa Chartered Accountant kama nitavumilia, na akasema ataniunganisha na CAs ili wanipe muongozo jinsi ya kufika hapo. Kiufupi jamaa alianza kunipa elimu ya maisha mpaka nikaghairi maamuzi yangu.
Itaendelea
ungemsaidia hata yeye asife kifalaweye nae kwa nini hukumpiga limbwata la dharula lile la kiumeni kiumeni? Uliumia breee!!
Libwata la kiumeni likoje?weye nae kwa nini hukumpiga limbwata la dharula lile la kiumeni kiumeni? Uliumia breee!!
Hebu fafanua kidogo hapa.ungemsaidia hata yeye asife kifala
Sawa mkuu tupo pamoja. Nina imani kuna cha kujifunza kupitia hii stori.Daahh mzee tangu nianze kuisoma sijachoka dar R I p khumbu
Vipi kwaio mlipo agana pale stand mpaka unaondoka SA hamkuona tena? Je ulipoondoka SA ulihudhulia msiba wa Khumbu?Hebu fafanua kidogo hapa.
Mzee nmejikuta natamani niwe wewe bonge la moment kwenye maishaSawa mkuu tupo pamoja. Nina imani kuna cha kujifunza kupitia hii stori.
Siku nilipoondoka tulionana na tuliagana. Kuhusu msiba nitaelezea kwa kirefu maana stori bado haijaisha.Vipi kwaio mlipo agana pale stand mpaka unaondoka SA hamkuona tena? Je ulipoondoka SA ulihudhulia msiba wa Khumbu?