Inaendelea...
Niliporudi Tanzania niliendelea kuwasiliana na Khumbu zile siku za mwanzo mwanzo lakini baadae nilianza kupunguza mawasiliano maana nilipofika Bongo mambo yalianza kuwa mengi sana. Nilijikuta nimezama kwenye mapenzi ya wanawake wengine. Si mnakumbuka ile thread niliyoileta hapa yenye tittle "Nipo njia panda...?" Amina naye alikuwa ananihitaji, demu wa Sinza naye ndio tupo pamoja, tunapika na kupakua, hivyo Khumbu akawa kama hana tena nafasi kwenye moyo wangu. Nikawa namtafuta hata mara moja baada ya wiki mbili. Kuna siku nilimpigia tuliongea sana na hatimae tukapanga aje Tanzania kutembea, kipindi hicho nilikuwa tayari nimeshapata kazi ila nilikuwa kwenye penzi zito la huyu mwanachuo na nilikuwa na majukumu kama yote. Niliona hata kama angekuja Bongo nisingepata muda wa kuwa naye ile effective maana tayari nilikuwa tayari kwenye commited relationship. Kwa hiyo niliamua kulipotezea ombi lake la kuja Bongo. Kila nikimpigia nilianza kumpiga kalenda nikimwambia subiri kwanza niweke mambo sawa, mambo yakikaa sawa nitakuleta.
Nilikaa kimya kama mwezi mmoja hivi bila kumtafuta. Yeye alikuwa hapigi mimi pekee ndio nilikuwa mtu wa kumpigia.
Siku moja nikaamua acha nimpigie nimjulie hali. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa kazini na kama sikosei ilikuwa 2014. Nilipopiga simu, simu yake ikapokelewa na rafiki yake ambaye tulikuwa tunafahamiana. Alishawahi kuja naye mara nyingi pale workshop, na hata siku ile tulipoenda maeneo ya kwao kipindi cha 2010 FIFA world cup ndio huyo aliyekuja naye pale shopping mall. Pia nilishawahi kwenda kwao mara nyingi tu maana walikuwa majirani. Alipopokea simu nikamsalimia kisha nikamwuliza mbona unapokea simu ya Khumbu, yeye yuko wapi? Akanijibu "Nilikuwa nakutafuta sana nikujulishe Khumbu kafariki" Nikamwuliza "Khumbu kafariki?" Akajibu "ndio Konda msafi Khumbu kafariki, nilikuwa nakutafuta sana nikujulishe, Jumamosi ndio mazishi yake" ...Aisee! Mwili ulikufa ganzi. Nikamwuliza "nini kimemuua?" Akajibu "alibanwa na mbavu, akakimbizwa hospitalini, baada ya muda mfupi akafariki". Nikamwuliza, unasema ulikuwa unanitafuta, ulikuwa unanitafutaje? Akasema nilikuwa naipiga namba yako lakini haitoki. Akaniambia "njoo umzike mpenzi wako". Nikamwambia sidhani kama nitaweza kuwahi mazishi, process za kujiandaa na safari haziwezi kuruhusu kuwahi mazishi.
...Baada ya kumaliza kuongea na huyo rafiki yake nikawapigia simu jamaa zangu wa Durban kuwajulisha habari za kifo cha Khumbu. Jamaa walisikitika sana, wakawa wanasema walikuwa wanakutana naye mara moja moja town wanasalimiana. Wakaniambia niende nikamzike mwanamke wangu. Nikawaambia sitaweza kuja South africa, nikawaomba waende kumzika shemeji yao, na hata kama watashindwa kwenda kumzika nikawaomba waende wakapeleleze nini chanzo cha kifo cha Khumbu maana swala la kusema tu kifua kilimbana haliingia kabisa kichwani. Jamaa wakaniambia watafuatilia na watanijulisha. Kweli baada ya siku chache walinitafuta na kuniambia ni "hakika na kweli Khumbu amefariki".
MWISHO WA STORI YA KHUMBU*