Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Mkuu, nammiss sana huyu mwanamke. Huwa siamini kama kweli alifariki. Huwa ananiijia ndotoni na kupiga stori. Kuna siku niliota tupo sehemu flani hivi. Nikawa namuuliza "mbona niliambiwa umefariki?" We acha tu mkuu.
Au alikufa kwa mawazo ya kumkimbiaa!!!?
Kama unaendelea kumuota jitahd umuombe msamaha humohumo ndotoni.

Inawezekana haja-rest in peace bado
 
Picha ya khumbu ndo kitu pekee kilichomis kwenye hii story na najua mkuu unawasiwasi wadau wataanza
"oooh dem enyewe ndo huyu alikua anamsifiaaa mbona wa kawaidaa sanaaa"" [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hiyo hasa ndo sababu picha ya real khumbu haiwekwiii

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
 
Picha ya khumbu ndo kitu pekee kilichomis kwenye hii story na najua mkuu unawasiwasi wada wataanza "oooh dem enyewe ndo huyu alikua anamsifiaaa mbona wa kawaidaa sanaaa"" [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hiyo hasa ndo sababu picha ya real khumbu haiwekwiii

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
kweli aisee...maana alitufojia picha wadukuzi wakamkosoa...Binafsi naamini Khumbu hakuwa na maajabu yoyote..anaweza kuwa alikuwa mzuri ila sio kama vile ambavyo konda msafi anataka kutuaminisha...The beauty of something is always on the eye of observer...

Hapa bwana Konda msafi inabidi alete picha
 
Bank teller mbona hata darasa la saba anafanya mkuu. Wewe utashindwa kupokea hela za wateja na kuwaandikia slip? By the way huo ulikuwa uongo wake tu. Ukiendelea kusoma utaona nini kilitokea.
Hata hapa tz,zaman advance wengi walikuwa wakimaliza form six hasa wa sayansi walkuwa wanaenda kufanya kaz TRA,Bank na sehemu zingine baadae ndo wanaenda chuo kikuu
 
Nimejaribu kupekua tena uzi mwanzo mwisho labda nitaona picha ya khumbu lakini wapi, mkuu kaza roho fanya hima tafadhali tumuone khumbu achana na maneno ya wakuda, nimeshindwa kabisa kuimagine taswira ya khumbu mawazo yananisukuma kuona picha yake, aisee huwezi amini nimeenda hadi GOOGLE search image kutafuta picha ya khumbu lakini bado roho haitaki. Fanya hima mkuu
 
Inaendelea

Siku ya mazishi niliamua kutokuhudhuria. Nilimpigia simu nikamwambia aniwie radhi sitaweza kuhudhuria kwenye mazishi, aliniuza kwa nini sitaweza, nikamwambia nina test, akaniuliza test gani hiyo siku ya Jumamosi, nikamjibu chuoni kwetu hadi Jumamosi huwa tunafanya test. Kiunyonge akabidi akubaliane na mimi. Kiukweli sikuwa na test wala nini, niliamua tu kutokuhudhuria mazishi. Sababu iliyonifanya kughairi kwenda msibani, sikutaka kukutana na mzazi mwenzie. Sikutaka jamaa anijue. Nilijua siku ya msiba lazima jamaa anijue hata kama sitatambulishwa maana Khumbu lazima zingetokea moments tungekuwa pamoja, mwenyeji wangu alikuwa ni yeye peke yake hivyo lazima tungekuwa pamoja jambo ambalo jamaa angenijua, hivyo jamaa ingeanza kumpa mashaka kumuona mzazi mwenzie yupo beneti na mimi. Khumbuka nilishaambiwa jamaa bado anamhudumia na anaendelea naye.

Baada ya msiba Khumbu alisafiri, tuliendelea kuwasiliana na aliendelea kunilalamikia kwa nini sikuja siku ya mazishi, na mimi niliendelea kusimamia kuwa test ndio ilikuwa sababu.

Baada ya kama mwezi Khumbu alirudi Durban, aliendelea kukaa pale pale kwenye nyumba ya bibi ake na ndugu zake wengine waliokuja kuishi hapo. Maisha yaliendelea, Khumbu aliendelea kutokupatikana kama ilivyokuwa huko nyuma.

Mwaka wangu wa kwanza chuoni kuna module moja sikuisajili, hivyo kila mwaka nilikuwa nabakiwa na module moja ambayo ilipelekea kumaliza chuo mwaka wa nne badala ya mwaka wa tatu. Iko hivi, kila module ina prerequisite yake. Kwa mfano huwezi kusoma economics ya mwaka wa pili kama kuna module ya economics ya mwaka wa kwanza hujaisoma. Kwa hiyo kila mwaka kuna module moja ilikuwa inabaki nyuma. Nilikuja ku-graduate mwaka wanne semester ya kwanza kwa sababu ya somo moja tu tena module moja iliyokuwa inabaki.

Ule mwaka wa nne niliamua kuanza kutafuta kazi kwa sababu nilikuwa nimebakiza somo moja tu tena module moja kugraduate. Hilo somo lilikuwa rahisi sana kwangu, nilikuwa nalimudu bila hata kuingia darasani. Mungu akabariki nikapata kazi shemu moja inaitwa Bloemfontein, ni jiji ambalo liko katikati ya South Africa, province moja inaitwa Free state. Maisha yakabadirika yakawa matamu. Nikawa naenda chuoni kila kunapokuwa na test tu, darasani nikawa siingii tena. Nikawa na mawasiliano ya karibu na wanafunzi wenzangu kuniupdate chochote ambacho kingehitaji uwepo wangu personally. Hivyo siku za test nikawa napanda basi kwenda Durban. Kama test let’s say ni kesho. Leo jioni napanda basi, alfajiri nishafika tayari na kwenda darasani. Baada ya test napanda tena basi kurudi Bloemfontein.

Huko Bloemfontein kuna watoto wa kisutu wakali balaa. Wana maumbo ya kutoa udenda, nadhani kwa South Africa kabila linaloongoza kwa watoto wazuri ni la kisutu likifuatiwa na waxhosa na wazulu. Kuna mmoja nilianza kumdate kunipunguzia machungu ya Khumbu. Mie sinywi pombe wala kuvuta sigara kwa hiyo starehe yangu ilikuwa watoto wa kike tu, na ukizingatia tayari nimeshapata na kazi inayoniingizia kipato ilikuwa full burudani. Nina wasiwasi kama sijaacha mtoto huko Bloemfontein maana huyo mwanamke nilikuwa napiga karibia kila siku.

Nilipopata kazi nikamjulisha Khumbu. Alifurahi sana, tukapanga mipango ili aje Bloemfointein anitembelee.

Itaendelea

8C794W2LXA7 Imethibitishwa. SAMARITAN WATER SOLUTION amepokea 30000.00 tarehe 20210307202059. Nimetuma Mfowetho.
 
kweli aisee...maana alitufojia picha wadukuzi wakamkosoa...Binafsi naamini Khumbu hakuwa na maajabu yoyote..anaweza kuwa alikuwa mzuri ila sio kama vile ambavyo konda msafi anataka kutuaminisha...The beauty of something is always on the eye of observer...

Hapa bwana Konda msafi inabidi alete picha
Huu ndo ukwelii mkuu inawezekana hana maajabu kama konda anavyotuaminisha apaa,,sasa akitupia picha apa dem raia watamdiss sana

Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu KONDA MSAFI kuna mawili, either una kaulofa/Kaufala/kauboya flani hv personal au Ulirogwa na huyo Khumbu, maana hakuna mtu/mwanaume aliye timamu 100% anayeweza kukubali kuendeshwa na mwanamke kiasi hicho kama yaliyokukuta wewe.

That is purely wrong. Tupo hapa kusoma hii story not to judge.
 
Ungeweka picha ya khumbu wale wazee wa chama cha wapiga punyeto ( chaputa) wangeitumia kupigia punyeto zao.

Njia ya kupiga punyeto lazima use na picha ya msichana mwenye makalio/ umbika vizuri kisha unaanza kuvuta hisia.

Chaputa mpoooo.
 
Asante kwa story nzuri kaka Imeni elimisha na kuniburudisha pia [emoji120][emoji120]
 
8C794W2LXA7 Imethibitishwa. SAMARITAN WATER SOLUTION amepokea 30000.00 tarehe 20210307202059. Nimetuma Mfowetho.
safi sana Mkuu kwa kuchangia Samaritan Water Solution kwa ajaili ya Khumbu na Hadithi murua, jamani tusiache changia hata km story haijakugusa, huenda huko mbele akaporomosha nyingine na picha ya Khumbu
 
Sawa mkuu. Kiufupi South africa imejengeka sana kimiundo mbinu. Sijawahi kufika Ulaya au Marekani lakini nimeishi na watu wa hayo mataifa nilipokuwa Johannesburg. Kuna jamaa mmoja ana asili ya kieritrea ila anaishi Canada na ni raia wa Canada tulikuwa tunafanya kazi wote pale kwenye taasis ya kidini, na pia kuna wamerekani tulikuwa nao pale. In fact kuna raia kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya nimefanya nao kazi na wote hao wanasema South Africa haina tofauti na Ulaya au Marekani. Hakuna kitu utakipata Ulaya au Marekani usikipate South Africa. Huyu jamaa mwenye asili ya Eritrea alikuwa mhuni mmoja hivi. Kila weekend tulikuwa tunaenda downtown Johannesburg club au live band. Katika kupiga piga stori naye nilikuwa namwambia dhamira yangu ya kwenda Marekani lakini yeye akawa ananiambia nikae tu South africa, anasema South africa is the best country, sina haja ya kuondoka, kilichopo Marekani ndio kilichopo hapa. Tena alikuwa anasema UK huenda hata ikazidiwa na SA maana huko majengo yao ni ya kizamani ukilinganisha na majengo ya kisasa ya SA. Huyo jamaa ana ndugu zake wa damu Europe hivyo anaijua vizuri europe.
Kwa upande wa maisha, maisha ya South africa ni marahisi kama una elimu. Kwa foreigner kama upo vizuri kwenye masomo ya science na hesabu ukienda SA unakula shavu fasta la kufundisha shule za secondari. Kule kuna upungufu wa walimu wa masomo ya science na hesabu. Kuna rafiki yangu mkameruni tulikutana naye pale kwenye taasis ya dini alikuwa vizuri kwenye hesabu. Yeye alikuwa na degree ya economics. Alipata kazi ya kufundisha hisabati kwenye shule ya serikali Johannesburg. Alianza kufundisha huku pia akaanza kusoma masters. Sasa hivi yuko Marekani anaishi huko. Kaondoka mwaka Juzi South africa. Alisoma mpaka akapata Phd, huwa namuona facebook akitupia picha akila good time in the US. Nadhani alipata kazi kubwa sana huko US iliyomfanya aondoke SA.
Kwa wabongo wanaozamia SA bila kuwa na elimu yoyote wanaishi maisha ya kuunga unga sana. Wanaofanya kazi halali ni wale wanaoamua kuuza matunda na pipi mitaani. Maisha yao ni magumu tu. Wengine ambao hawataki kufanya kazi halali na wanaotaka mafanikio ya haraka ni hao wanaouza unga, waganga wa kienyeji na wezi. Wauza unga wana hela chafu na wanaishi maisha ya kifahari sana. Waganga wa kienyeji nao wanapiga pesa sana (utapeli). Wezi nao wanapata vihela, wanaendesha magari ila huyo mwizi unaweza ukamkuta leo anaendesha gari la kifahari lakini kesho ukamkuta analala nje, amekosa hata hela ya kuchangia chumba. Wabongo wengine ndio hao mabaharia wapanda meli. Wao ni kutembea na vibegi mgongoni na kwenda kunyatia meli ili wazamie. Hao utawakuta wamejaa Durban na port moja inaitwa Richardsbay. Hao ni wachafu hatari. Wanalala parking, wapo standby kudandia meli, sehemu wanazolala ukienda kukaa lazima utoke na chawa.
Ila kwa south Africa Pretoria napapenda napaona ni mzuri ukiwa unarembwa na jakaranda trees na huu ni mtizamo wangu
 
Mkuu KONDA MSAFI kuna mawili, either una kaulofa/Kaufala/kauboya flani hv personal au Ulirogwa na huyo Khumbu, maana hakuna mtu/mwanaume aliye timamu 100% anayeweza kukubali kuendeshwa na mwanamke kiasi hicho kama yaliyokukuta wewe.
Hakuna mkamilifu hata mmoja, na ukiona hayajakukuta shukuru Mungu (kama unaamini yupo) maana ukimpenda mtu unaweza kugeuka mwehu mtaani.
 
Shukrani sana mkuu.
Mkuu nimekufuatilia toka unaanza story ikabidi ni some pia sitory ya pale kwenye family uliokua umepanga hapa bongo kwakweli uko vzr kwenye kusimlia.

Na nilikuwa nashindwa ku koment sababu nilikua bado sio member wa jf. Nikalazimika kutaka msaada wa kuwa member nikakosa msaada kiufupi nilijiongeza nimejiunga tarehe tano mwezi hu.

Nimefulahi kufanikiwa. Sasa nilikuwa najiuliza ivi ili upost episode ilikuwa lazima uwe na bando? Maana Mimi kusoma nilikuwa nasoma bule saizi naaply bule hii ikoje
 
Back
Top Bottom