Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Jinsi mapenzi ya mtoto wa Kizulu Durban South Africa yalivyotaka kunitoa roho

Hakuna mkamilifu hata mmoja, na ukiona hayajakukuta shukuru Mungu (kama unaamini yupo) maana ukimpenda mtu unaweza kugeuka mwehu mtaani.
Huyo anaongea tu. Watu mpaka wanajiua kwa sababu ya mapenzi.
 
Mkuu nimekufuatilia toka unaanza story ikabidi ni some pia sitory ya pale kwenye family uliokua umepanga hapa bongo kwakweli uko vzr kwenye kusimlia.

Na nilikuwa nashindwa ku koment sababu nilikua bado sio member wa jf. Nikalazimika kutaka msaada wa kuwa member nikakosa msaada kiufupi nilijiongeza nimejiunga tarehe tano mwezi hu.

Nimefulahi kufanikiwa. Sasa nilikuwa najiuliza ivi ili upost episode ilikuwa lazima uwe na bando? Maana Mimi kusoma nilikuwa nasoma bule saizi naaply bule hii ikoje
Shukrani mkuu kwa kunifuatilia. Sasa utawezaje kufungua internet bila bando? Sasa labda utuelekeze umewezaje kusoma na kureply bila bando?
 
kufungua internet bila bando? Sasa labda utuelekeze umewezaje kusoma na kuapply bila bando?
Kaka Mimi nimekuwa natumia free basics kwakuwa wewe ni member sio shida download app ya free basics alafu pale utazikuta huduma nyingi utachagua unacho kitaka bila shida yoyote. Picha utaziona kasolo yake huto play video. Ila Mimi kwenye hii jf bado vitu vingi sijavijuwa kwaio naomba kampani yako.
 
Kaka Mimi nimekuwa natumia free basics kwakuwa wewe ni member sio shida download app ya free basics alafu pale utazikuta huduma nyingi utachagua unacho kitaka bila shida yoyote. Picha utaziona kasolo yake huto play video. Ila Mimi kwenye hii jf bado vitu vingi sijavijuwa kwaio naomba kampani yako.
Jalibu hio mku alafu ulete mlejesho tushauliane.
 
Kaka Mimi nimekuwa natumia free basics kwakuwa wewe ni member sio shida download app ya free basics alafu pale utazikuta huduma nyingi utachagua unacho kitaka bila shida yoyote. Picha utaziona kasolo yake huto play video. Ila Mimi kwenye hii jf bado vitu vingi sijavijuwa kwaio naomba kampani yako.
Sawa mkuu.
 
HAPPY WOMEN'S DAY!!!

Hongereni Sana Wanawake wote mliopo kwenye ukurasa huu.

Ninyi ni wanawake wa nguvu na wa thamani sana mbele za Mungu na wanadamu.

Tunawatakia mafanikio mema kwa kila hatua ya maisha yenu.Msirudi nyuma endeleeni kupambana.Tupo pamoja na nyinyi siku zote.Tunawapenda sana.
 
Kaka Mimi nimekuwa natumia free basics kwakuwa wewe ni member sio shida download app ya free basics alafu pale utazikuta huduma nyingi utachagua unacho kitaka bila shida yoyote. Picha utaziona kasolo yake huto play video. Ila Mimi kwenye hii jf bado vitu vingi sijavijuwa kwaio naomba kampani yako.
Internet hakuna huduma ya bure, zote ni lazoma ulipie kwa kulipia bundle ambapo shirika husika hulipia huduma hiyo katika Mkongo wa Taifa.
Huduma km Facebook unaweza kuta unasoma bure lkn Indirect kwa kupitia malipo ya muda wa hewani unapewa bure.
Bure haiwezekani kwani tayari unakuwa registered kwenye line ya simu au IP address au Internet cafe
Kwa sasa JF na www za You Tube utaona ni bure lkn Jamii Media inapata kutoka matangazo madogomado na vyanzo vyao, siku za nyuma JF waliomba kuchangiwa na utapewa Rank kutokana na malipo yako mfano Bronze mpaka Platinum naona kwa sasa wameshazitoa.
Kwa ninavyoelewa jibu ndilo hilo JF kujiunga ni bure hata kupost Hadithi ni bure lkn kwa sh 500/ hutaambulia lolote ni lazima ununue GB kubwa na ndio maana tunaridhia kuichangia SAMARITAN
 
At last, duh uzi na nusu huu! Bonge la story lenye mvuto wa kiaina yake vile, yaani raha ndani, huzuni ndani na mafunzo pia. Shukran konda msafi kwa kuiachia part of your life journey kwa ustadi. Rest easy Khumbu, ulipendwa ila ndio hivyo maisha yalivyo. Sote tu wapita njia.

Salaam toka nchi jirani ✌️
 
Internet hakuna huduma ya bure, zote ni lazoma ulipie kwa kulipia bundle ambapo shirika husika hulipia huduma hiyo katika Mkongo wa Taifa.
Huduma km Facebook unaweza kuta unasoma bure lkn Indirect kwa kupitia malipo ya muda wa hewani unapewa bure.
Bure haiwezekani kwani tayari unakuwa registered kwenye line ya simu au IP address au Internet cafe
Kwa sasa JF na www za You Tube utaona ni bure lkn Jamii Media inapata kutoka matangazo madogomado na vyanzo vyao, siku za nyuma JF waliomba kuchangiwa na utapewa Rank kutokana na malipo yako mfano Bronze mpaka Platinum naona kwa sasa wameshazitoa.
Kwa ninavyoelewa jibu ndilo hilo JF kujiunga ni bure hata kupost Hadithi ni bure lkn kwa sh 500/ hutaambulia lolote ni lazima ununue GB kubwa na ndio maana tunaridhia kuichangia SAMARITAN
Ahsante mku kwa maelezo yako nikweli kwamba bule hakuna ila kwakuwa mtandao husika ndio wanalipia ndipo sisi tuna pata huduma. Ndio maana nimesema kwaza lazima uwe na app ya free basics au Kama vipi kwenye Facebook lite unaipata free basics.
 
Inaendelea

Maisha ya kujitahidi kumtoa Khumbu kichwani yaliendelea. Haikuwa jambo rahisi ila kwa kiasi flani nilifanikiwa maana nilianza kujiona mtu mpya. Nilianza kufurahia maisha na huyu mwanamke wangu wa Bloemfontein huku nikiendelea kuwasiliana na Amina pamoja na huyu wa Sinza. Huyu wa Bloemfontein tulianza kupanga mipango mingi tu ya kimaisha. Alikuwa anaishi township moja inaitwa Tabanju. Tulianza mtindo wa kila siku ya Ijumaa nikitoka kazini tunaenda kukaa kwao mpaka Jumapili jioni ndio tunarudi town nyumbani kwangu. Siku za weekend nilikuwa siendi kazini hivyo weekend nzima tulikuwa tunashinda kwao.

Kama mnakumbuka nimesema huko nyuma kuwa niliajiriwa huku nikiwa bado sijagraduate. Niliendelea kufanya kazi huku mara kwa mara naenda Durban kwa ajili ya tests na assignments zingine. Hatimae nilifanya mtihani wa mwisho wa lile somo moja lililobaki, na 06 September 2012 ilikuwa graduation yangu.

Siku ya graduation nilienda Durban kwa ajili ya hiyo shughuli. Nilipata wazo la kumjulisha Khumbu aje kwenye hii siku muhimu kwangu lakini nilipofikiria kuwa rafiki yangu Sandile na Pontsho wasingenielewa kama ningemwalika huyu mwanamke hilo wazo niliamua kuachana nalo japo nilitamani Khumbu awepo. Sandile na Pontsho nilikuwa nimewajulisha siku ya graduation na waliomba gharama za sherehe ziwe juu yao. Gharama za Joho na suti waliniambia wala nisihofu. Sandile alinipa zawadi ya shati moja zuri sana.

Nilifika Durban siku moja kabla ya graduation. Kesho yake asubuhi nikakutana na Sandile campus ili anipatie joho na suti niweze kutinga kabla ya shughuli ya graduation haijaanza. Nikapiga hiyo suti na kutupia joho kwa juu. Kati ya siku muhimu katika maisha yangu ni hiyo siku nilipovaa hilo joho. Niliona hiyo ilikuwa ishara ya milango ya mafanikio kuanza kufunguka. Nilihisi ndoto yangu ya muda mrefu imetimia. Bongo niliishia form three, niliona kama naota kumaliza elimu ya chuo tena kwenye nchi kama South Africa, niliinua mikono juu na kusema “Asante Mungu”.

Mimi na Sandile tukaanza kuelekea kwenye ukumbi wa graduation nikiwa nimejawa furaha kuu. Nikiwa nawaza sasa nimeingia kwenye ulimwengu wa opportunities. Tukiwa tunaelekea ukumbini tukakutana na rafiki yangu mwingine akiwa na demu wake nao wamekuja kwenye graduation yangu. Kwa kweli nilijiona kama mfalme. Kuzungukwa na watu wanaokupenda na wanaofurahia mafanikio yako ni hisia nzuri sana.

Mgeni rasmi alikuwa mtu maarufu sana kwa South Africa ambaye nisingependa nimtaje. Alitoa speech moja nzuri sana iliyotufanya magraduate wote tuone anything is possible, you can be anything you want. Hapo nikawa napiga picha jinsi maisha yangu yatakavyobadirika, nikawa nafikiria kuwa na mwanamke mrembo, nyumba nzuri ya kuishi kwenye suburb, maisha ya kutoka kila weekend na kwenda kula bata nikiwa na mke wangu mrembo ambaye atanielewa na kufurahia maisha kama tupo peponi. Nikawa najiona naingia boardroom nikiwa kama CEO wa kampuni kubwa, nimepiga suti naendesha mkutano nikiwa nimezungukwa na wafanyakazi.

Ulipigwa wimbo wa taifa wa South Africa, baada ya wimbo ndio shughuli za graduation zikaanza. Mgeni rasmi alikuwa anataja jina la graduate na kwenda mbele kushikana mkono, kupiga picha na kukabidhiwa cheti. Jina la graduate likitajwa ndugu zake wanashangilia na kupiga vigelegele akiwa anaenda kupokea cheti. Hatimae jina langu likatajwa, yalisikika makelele hayo hata sikujua yametoka wapi. Nilitaka kuangalia ni wakina nani hao wanaonishangilia maana nilijua kuna watu wanne tu ndio wamekuja kunipa company ambao ni Sandile, Pontsho, rafiki yangu na demu wake. Ule ukumbi umejengwa kama uwanja wa mpira. Juu wanakaa wageni waalikwa hivyo graduate mnakuwa mmekaa chini, kwa hiyo ukitaka kuwaona wageni waalikwa inabidi utazame juu. Niliposikia yale makelele ya kunishangilia niliona noma kuanza kuangalia juu ilihali naelekea kwa mgeni rasmi kwenda kuchukua cheti na kupiga picha. Nilitamani sana kugeuza shingo niangalie ni watu gani hao wanaonishangilia ila haikuwa rahisi hivyo niliendelea kubaki na shauku yangu mpaka pale shughuli itakapoisha maana watu walikuwa wamejaa hasa, ukumbi ulikuwa umefurika. Huko parking magari yalikuwa yamejaa hadi sehemu ya kupaki ikawa haitoshi. Magari mengine yakawa yamepaki hadi barabarani. Nakumbuka tulipotoka tuliikuta gari moja iliyokuwa imepakiwa barabarani imedondokewa na mti, kioo chote cha mbele kimemwagika na mti umeenda kujikita kwenye siti za mbele. Huyo mweye gari nadhani alilaani sana siku hiyo.

Baada ya hotuba ya mgeni rasmi na shughuli ya graduation kuisha nikawa natoka nje kwenda kukutana na hao wageni wangu waalikwa kwa ajili ya kile walichoniandalia. To my surprise nikamkuta Khumbu yupo pamoja na akina Sandile. Ile kutoka tu nje ghafla namuona Khumbu akinikimbilia na kuja kunivalisha shada la maua. Sikutegemee kumuona Khumbu siku hiyo, na niliamini hajui kama leo ni siku ya graduation yangu na hajui kama nipo Durban. Hapo hapo nikaanza kutokwa na machozi. Sijui yalikuwa ni machozi ya furaha au machozi ya hisia za mapenzi, sielewi. Kulikuwa na watu kama sita hivi. Alikuwa ameongezeka Khumbu na mke wa Sandile. Basi kila mtu ananipa hongera huku Sandile akawa ananipiga picha kwa camera yake ile ya kazi.

Baada ya zoezi la kukumbatiana na kupongezana tukawa tunaelekea parking kwa ajili ya kuondoka na kwenda kupata chakula cha pamoja nilichoandaliwa. Niliingia kwenye gari ya Sandile, Khumbu na wengine wakatumia magari yao. Tulienda mgahawa mmoja unaitwa Nandos, haukuwa mbali sana na pale chuoni. Njia nzima nilikuwa najiuliuza Khumbu kafikaje hapa, nani kamwambia leo ni graduation yangu?

Itaendelea
Mkuu picha haifunguki

Iweke tena
 
Hapana, sijuti kurudi Bongo. Naombea tu JPM aijenge nchi iwe kama SA ili raha za SA tuzipate hapa hapa nyumbani. Nyumbani kuna raha yake ujue. Ukiwa na hela bongo unaenjoy life mara mia kuzidi SA.
Nimekupenda bure. Maedeleo ya watu huja baada ya maendeleo ya vitu. Infrustructure ikiwa imara na watu watajiletea maendeleo si serikali.
 
Sawa mkuu. Kiufupi South africa imejengeka sana kimiundo mbinu. Sijawahi kufika Ulaya au Marekani lakini nimeishi na watu wa hayo mataifa nilipokuwa Johannesburg. Kuna jamaa mmoja ana asili ya kieritrea ila anaishi Canada na ni raia wa Canada tulikuwa tunafanya kazi wote pale kwenye taasis ya kidini, na pia kuna wamerekani tulikuwa nao pale. In fact kuna raia kutoka mataifa mbalimbali ya Ulaya nimefanya nao kazi na wote hao wanasema South Africa haina tofauti na Ulaya au Marekani. Hakuna kitu utakipata Ulaya au Marekani usikipate South Africa. Huyu jamaa mwenye asili ya Eritrea alikuwa mhuni mmoja hivi. Kila weekend tulikuwa tunaenda downtown Johannesburg club au live band. Katika kupiga piga stori naye nilikuwa namwambia dhamira yangu ya kwenda Marekani lakini yeye akawa ananiambia nikae tu South africa, anasema South africa is the best country, sina haja ya kuondoka, kilichopo Marekani ndio kilichopo hapa. Tena alikuwa anasema UK huenda hata ikazidiwa na SA maana huko majengo yao ni ya kizamani ukilinganisha na majengo ya kisasa ya SA. Huyo jamaa ana ndugu zake wa damu Europe hivyo anaijua vizuri europe.
Kwa upande wa maisha, maisha ya South africa ni marahisi kama una elimu. Kwa foreigner kama upo vizuri kwenye masomo ya science na hesabu ukienda SA unakula shavu fasta la kufundisha shule za secondari. Kule kuna upungufu wa walimu wa masomo ya science na hesabu. Kuna rafiki yangu mkameruni tulikutana naye pale kwenye taasis ya dini alikuwa vizuri kwenye hesabu. Yeye alikuwa na degree ya economics. Alipata kazi ya kufundisha hisabati kwenye shule ya serikali Johannesburg. Alianza kufundisha huku pia akaanza kusoma masters. Sasa hivi yuko Marekani anaishi huko. Kaondoka mwaka Juzi South africa. Alisoma mpaka akapata Phd, huwa namuona facebook akitupia picha akila good time in the US. Nadhani alipata kazi kubwa sana huko US iliyomfanya aondoke SA.
Kwa wabongo wanaozamia SA bila kuwa na elimu yoyote wanaishi maisha ya kuunga unga sana. Wanaofanya kazi halali ni wale wanaoamua kuuza matunda na pipi mitaani. Maisha yao ni magumu tu. Wengine ambao hawataki kufanya kazi halali na wanaotaka mafanikio ya haraka ni hao wanaouza unga, waganga wa kienyeji na wezi. Wauza unga wana hela chafu na wanaishi maisha ya kifahari sana. Waganga wa kienyeji nao wanapiga pesa sana (utapeli). Wezi nao wanapata vihela, wanaendesha magari ila huyo mwizi unaweza ukamkuta leo anaendesha gari la kifahari lakini kesho ukamkuta analala nje, amekosa hata hela ya kuchangia chumba. Wabongo wengine ndio hao mabaharia wapanda meli. Wao ni kutembea na vibegi mgongoni na kwenda kunyatia meli ili wazamie. Hao utawakuta wamejaa Durban na port moja inaitwa Richardsbay. Hao ni wachafu hatari. Wanalala parking, wapo standby kudandia meli, sehemu wanazolala ukienda kukaa lazima utoke na chawa.
Dah umenifanya niipende zaidi JF maana siyo mwenyeji Sana humu, Safi Sana mkuu Tupo pamoja hadithi imenifanya nijifunze mambo mengi sana

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Kipindi nipo naye nilikuwa naamini ananipenda lakini kwa sasa baada ya kuwaelewa wanawake vizuri ndio nimezidi kuamini hakika alikuwa ananipenda sana.

Maybe, you were screwing her properly, aliyekuwa mme ya jd anaita kukojoza, ndio maana alikuwa anapewa gari na mtu mwingine lakini bado anakutafuta umkunje.
 
Jamani naomba niikatishe hii stori. Hii stori ni ndefu sana haitaisha leo wala kesho na inanichukulia muda wangu mwingi sana. Ni stori iliyochukua karibia miaka 6, since 2008 hadi 2012, kwa hiyo unaweza kuona ilivyo ndefu. Kwa wale wenye shauku ya kutaka kujua Khumbu yuko wapi kwa sasa, jibu ni kwamba Khumbu alifariki, hatunaye tena duniani. Mwenyezi Mungu aendelee kumuweka mahali pema peponi. I truly miss her and believe one day I will meet her in other worlds of God.
Mimi nilimaliza chuo nikarudi Bongo, nipo Dar nina familia tayari. Kuna uzi mmoja nilishauleta humu mnaweza kuutafuta kuhusu yaliyonipata niliporudi Dar. Asanteni na kwa herini.
Sawa mkuu mimi naomba nikutafute in box
 
Hata hapa tz,zaman advance wengi walikuwa wakimaliza form six hasa wa sayansi walkuwa wanaenda kufanya kaz TRA,Bank na sehemu zingine baadae ndo wanaenda chuo kikuu
Tena Chuo Unasomeshwa, Walikula Maisha Sana Wazee
 
Back
Top Bottom