Jinsi mitumba inavyotuunganisha na watu tusiowapenda!

Jinsi mitumba inavyotuunganisha na watu tusiowapenda!

Hiyo mitumba unajua kuwa huwa inatolewa bure Ila MTU mweusi akiikusanya analeta anauza
Usijidanganye kwa marekani soko la mitumba la Africa mashariki linawaingizia dola zaidi ya million 250 kwa mwaka ndo maana waking'aka sana pale Africa mashariki ilipopanga kujizuia mitumba
 
Mitumba upande wa nguo zinazoletwa Africa kwanza mitumba imechoka , imechakaa michafu

Ndo tunaleta ili tuvae ni umasikini tu.

Kukuta nguo ya mtumba ya maana ni Nada Sana.

Tukubali kuwa sisi ni dark country
Mbona inakuja kwa grades mkuu? Ukitaka yale marapurapu pia utapata. Lakini ipo mitumba Grade 1 inayozipiku zile nguo za madukani aka redi-medi.
 
Mbona inakuja kwa grades mkuu? Ukitaka yale marapurapu pia utapata. Lakini ipo mitumba Grade 1 inayozipiku zile nguo za madukani aka redi-medi.

Kitu ambacho MTU ameshavaa hadi akaona hakifai akaamua kukitoa donation then wewe unasema ni kizuri !!

Umasikini hamna grade au nini huwezi kusema nguo ya mtumba iwe nzuri kuzidi ya dukani is impossible
 
Inabidi kupigwa marufuku mitumba.

Nguo za mitumba nimevaa Ila sio nguo ni umasikini tu
AaaaaDokta; Hututakii mema broo. Hebu siku moja hapa Tz. nenda mnadani uone jinsi mitumba ya nguo na viatu inavyong'ang'aniwa na wadau.
 
Kitu ambacho MTU ameshavaa hadi akaona hakifai akaamua kukitoa donation then wewe unasema ni kizuri !!

Umasikini hamna grade au nini huwezi kusema nguo ya mtumba iwe nzuri kuzidi ya dukani is impossible
Mitumba ni jina lakini ndani ya mitumba hiyo zipo nguo au hata viatu ambavyo havijatumika labda vilitumika tu wakati mtu huyo alikuwa anajaribisha dukani.
Baadhi ya mitumba e.g ile ya Grade 1 ni nguo au viatu vilivyokaa dukani kwa muda mrefu na havinunuliki tena unaweza kusema kwa kibongbongo vimedoda. Havijatumika kabisa yan.
 
Napenda sana uzungumziwe, ila sio kinafikiii.
Mtazamo wangu, naukubali na kuuelewa sana ushoga.
Ushoga ulikuwepo toka enzi na enzi na utaendelea kuwepo daima dumu. Mtu esp.wale WANAFIKI, Kuukubali au Kuukataa Ushoga hakubadilishi chochote. Kwa mantiki hiyo; mkuu coca uko vizuri. Wanaoupigia kelele ukiwauliza jambo hilo limekuhusu vipi hawana majibu toshelezi. (Samahani lakini hili ni nje ya mada)
 
Unaweza kuwa unachukia watu wenye tabia ya ushoga, lakini una hakika mitumba unayotumia hakuna ambao ulikuwa unatumiwa na shoga kabla ya wewe kuununua?
Ulivyoanza hivi nikapata wasiwasi na maswali ulilenga nini
 
Asubuhi ya leo wakati navua raba nilipotoka mazoezini, ghafla lilinijia wazo la ni nani alikuwa anaivaa raba hiyo kabla haijaletwa Tanzania kama mtumba?

Nikaanza kuangalia jinsi mitumba ilivyotawala maisha ya Watanzania kwa kiasi kikubwa Sana. Lakini huwa tunajiuliza hiyo mitumba ilikotoka ilikuwa inatumiwa na nani?

Kwa mfano magari ingawa hatupendi sana kuyaita mitumba, badala yake tunayaita "Used" lakini ukweli wa mambo na yenyewe pia ni mitumba.

Unaweza kuwa unachukia watu wenye tabia ya ushoga, lakini una hakika mitumba unayotumia hakuna ambao ulikuwa unatumiwa na shoga kabla ya wewe kuununua?

Ipo mitumba toka kwa wezi, majambazi, makahaba, watu wa dini tofauti na sisi, wabaguzi, wauwaji, wafungwa, wabakaji, matapeli na lundo jingine kubwa sana la watu tusiowapenda.

Unapotumia mtumba jua kuwa inawezekana kabisa kabla ya kuletwa Tanzania huko ulikotoka ulikuwa unatumiwa na mtu/watu usiowapenda kabisa.
Piga mitumba tuu,hata yale magwanda ya chadema nasikia ni mitumba toka ubelgiji,ni kweli?
 
Back
Top Bottom