Jinsi mitumba inavyotuunganisha na watu tusiowapenda!

Jinsi mitumba inavyotuunganisha na watu tusiowapenda!

Asubuhi ya leo wakati navua raba nilipotoka mazoezini, ghafla lilinijia wazo la ni nani alikuwa anaivaa raba hiyo kabla haijaletwa Tanzania kama mtumba?

Nikaanza kuangalia jinsi mitumba ilivyotawala maisha ya Watanzania kwa kiasi kikubwa Sana. Lakini huwa tunajiuliza hiyo mitumba ilikotoka ilikuwa inatumiwa na nani?

Kwa mfano magari ingawa hatupendi sana kuyaita mitumba, badala yake tunayaita "Used" lakini ukweli wa mambo na yenyewe pia ni mitumba.

Unaweza kuwa unachukia watu wenye tabia ya ushoga, lakini una hakika mitumba unayotumia hakuna ambao ulikuwa unatumiwa na shoga kabla ya wewe kuununua?

Ipo mitumba toka kwa wezi, majambazi, makahaba, watu wa dini tofauti na sisi, wabaguzi, wauwaji, wafungwa, wabakaji, matapeli na lundo jingine kubwa sana la watu tusiowapenda.

Unapotumia mtumba jua kuwa inawezekana kabisa kabla ya kuletwa Tanzania huko ulikotoka ulikuwa unatumiwa na mtu/watu usiowapenda kabisa.
Unapoenda lodge unaweza lala katika kitanda ambacho mkeo aliliwa hapo, shoga alipakuliwa hapo so don't stress yourself kwa vitu vidogo vidogo
 
Kwani mkuu wewe unajua aliyelima chakula unachokula Kila siku ni mtu wa aina gani?

Hata hizi nguo mpya unazonunua unajua ni nani katengeneza?

Ni muhimu tu kutumia Imani Yako ya kidini kuombea vyote katika maisha yako.

Jambo BAYA ni uliloshuhudia wewe mwenyewe...
 
Mtoa mada sijui akili zako zipoje,umekuja kutangaza ushoga ama? Kwani ukienda mgahawani huwezi kula chakula kilichopikwa na Shoga? Hiyo suti mpya unayovaa je haijashonwa na Shoga? Chumba ulichopanga hajawahi kupanga kahaba kabla yako? au mwizi? au yeyote yule usiyempenda? Usihukumu usije ukahukumiwa.
Umemuelewa mleta uzi alichomaanisha au haujasoma na kuelewa?
 
Ila ushoga haujawahi kukubalika tokea enzi hizo hadi leo na ndio maana inatumika jitihada kutaka kufanya ushoga uonekane ni kitu cha kawaida tu kama vyengine.
Kweli kabisa, hata haya maandiko ya wanaojifanya wanautetea ni mojawapo ya jitihada zao.
Kwa kifupi haukubaliki mto jamii.
 
Ni watawala wenye ufinyu wa mawazo utakuta waipigia upatu tusitishe kuchukua mitumba.

Mitumba tunahitaji sana hasa nchi zetu za huku kusini, mtumba high grade unatufanya na sisi tuonekane watu mwana, sasa wee unataka kunivalisha libatiki mkono mmoja mnene mwingine mwembamba mimi ili iweje, unicheke!

mitumba ya aina hizi miaka mia itapita bado watanzania wengi hawataweza kutengeneza au kununua nguo dizaini yake ikiwa mpya.

-Kuna mtumba wa sindilia grade one

- kuna mtumba wa nguo za watoto, cotton

- mtumba wa viatu

- mtumba mabegi

- mtumba bidhaaa za ngozi
 
Back
Top Bottom