Lakini unasahau kwamba labda Uchumi wa Tanzania karibia wote kwa >85% umeshikikiwa na Waislamu, leo hii Mtanzania yoyote akitafuta kazi private sector hakwepi Uislamu
Ooh! Hapana hujagundua, Waislam sisi tunapata kwa kuangaika sana kuanzia kwenye kuuza maandazi n.k lakini wenzetu wengi huko serikalini wanajichotea Mahela mengi mno na kuyaficha.
Wanatupa data za uongo kuwa sisi ndio matajiri kumbe sikweli. Unaufahamu utajiri wa Edward Lowasa? Marehemu Mfugale? Kijazi, vipi yule mhaya wa Heineken Rugemalila? Prof. Tibaijuka yaani wana mamilion ya dola sema wenzetu wajanja hawasemi katu na hela wameficha huko umangani.
Kikubwa Waislam wengi wanaonekana matajiri kwasababu wali/wanajishughulisha na biashara yaani baada ya kuona mfumo zamani kama uliwakataa wakaanza kuwa wafanyabiashara matokeo yake ikawa heri kwao. Lakini sasa hivi tumejanjaruka na hivi vinafasi vya serikalini jambo ambalo linazolotesha ufanisi wa uchumi bibafsi labda update shimo upige kwelikweli!
Muhimu kuepuka masuala ya udini japokuwa kwenye teuzi huwa haiepukiki kwani inaleta hisia za kipuuzi hata kama aliyeteuliwa hakusaidii chochote.
Mimi muislam ninayejielewa lakini Waislam wenzangu wanaoteuliwa ukiwaendea maofisini wakusaidie wanakupiga danadana tu tena unaweza au unasaidiwa na mkristo tena fresh tu, hapo ndo huwa nashindwa kuelewa udini huwa una nini cha maana; so their appointments have nothing to do with my success!
Kuna Waislam wamenufaika na urafiki wao na Wakristo lakini pia kuna wakristo wamenufaika na urafiki wao na Waislam. Ukikagua viwanda na makampuni mengi ya kiislam utawakuta wako wakristo kibao tena katika nafasi nyeti za HR, IT n.k
Hata Shule kubwa tu kama FEZA, ALMUNTAZIL n.k utawakuta Wakristo kibao tena wakuu wa vitengo wanajinyakulia mishahara minono vivyo hivyo kwa wakristo.
Haya mambo huwa tunayaangalia sisi watu wa chini yaani kajitu kapo kishemundu hakana hata hekari ya mahindi lakini utasikia kanashangilia kuteuliwa boss fulani kisa tu ni dini yake. Upumbavu kama huu unaukuta Afrika hususani Tanzania.
Udini ni sumu, mfano Muislam kama Bashiru Ally aliibuliwa na Magufuli Mkristo kutoka kusiko (Ex nihilo) mpaka kuwa KMK, lakini ukimkuta sehemu utakuta anakwambia Waislam siyo kabisa!
Mtu kama Makonda (natolea mfano) aliibuliwa na Kikwete Muislam kutoka kusiko lakini unaweza kumkuta sehemu anawaponda Waislam na udini.
Nilikaa chini nikagundua kama dini ndo zinaleta mfarakano huu basi hazina maana! Umaana uje kwa kuutanguliza upendo wa ubinadamu wetu ambao Allah alituumba nao.
Wabillah wataufiq!