Kitu kilichomuumiza ni Mabeste kuanza kuongea kwamba sababu ya wao kuachana ni pesa. Kaongea kwenye media.
Mama wa watu imebidi atoke hewani akaelezea jinsi alivyomlea jamaa toka mwanzo mpaka wanaachana, hadi mahari alijilipia.
Ugonjwa aliokuwa anaumwa inasemekana kwamba chanzo ni familia ya Mabeste, maana mara zote Mabeste alikuwa akiwatuhumu nyumbani kwao na haelewani na wazazi wake kabla hata hajakutana na Lisa.
Idea ya kukusanya michango kwa ajili ya matibabu ni ya Lisa, na hata kuendesha accounts za Mabeste yeye ndiye alikuwa anafanya hivyo, ile concert yeye ndiye aliyeplan na kuanza kufatilia kila kitu.
Ukiweza kupata muda wa kumsikia utaelewa, na bahati mbaya kwa Mabeste, Lisa alifikia sehemu akaanza kurekodi kila walichokuwa wanazozana au kujadili.