Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeonja ladha ya vile vipigo mnavyowapa raia shenzi kabisa. Wasimulie askari wenzio ili waache unyama wenu blaaaalifakenIlikuwa siku ya jumamosi tulivu ambapo jiji la Dar es Salaam na Tanzania nzima kwa ujumla macho na akili zao zilikuwa zimeelekezwa wilayani Temeke kushuhudia mtanange wa watani wa jadi, Simba na Yanga wakichiana kugombea ngao ya Jamii.
Mimi na rafiki yangu Dr. Gill Biz na mkewe Hawa, tulikuwa pande za Buguruni tukiburudika na vinywaji laini anga hizo.
Kuna jamaa yetu mwingine Dr. Ally Na, yeye alikuwa Vinginguti, akatupigia simu kuwa amenunua nusu mbuzi hivyo tukamchakate na kumfanya kitoweo.
Basi tukaenda huko kujumuika. Tulipofika huko Mambo yalikuwa mazuri kwelikweli, chupa za kijani na za kahawia zilikuwa zimetamaliki zikitungoja.
Tukala, tukanywa, na tukahamia kwenye bar nyingine huko huko.
Njia ya kwenda huko ilikuwa imejaa vichochoro na kona nyingi, na baada ya dakika 7 tukafika.
Tukakaa huko hadi mida ya saa nne usiku, na tukaamua turudi zetu Makongo Juu tunakoishi.
Tukiwa tunachoronga vichochoro, kwa bahati mbaya tukapotea na tukajikuta tuko katikati ya nyumba ya watu na kuna wanawake wanne wakisukana.
Basi tukawasalimia na kuwaomba msamaha na kuwaomba watuelekeze njia ya kutokea barabara kubwa .
Mmoja kati ya wale wanawake akasema kina baba kwani nyie mnafanya kazi gani?
Wenzangu wakajibu kwamba ni madaktari. Wakaniuliza wee baba Mbona hujitambulishi?
Nikajibu Mimi ni Askari polisi hapo Buguruni.
Basi baada ya hapo, mmoja wa wamama wale akasema "Hapa ni mbali na barabara kubwa na vichochoro ni vingi mtapotea, ngoja nikuitieni kijana awaongozeni njia"
Basi yule mama akatoka na akaenda huko nyuma.
Baada ya dakika tano akarudi yule mama akiwa ameongozana na vijana watatu wenye magongo, na mmoja wao akasema "Yuko wapi huyo polisi?"
Wakanaanza kunipiga, wakaongezeka na wengine wengi kama kumi na nane au ishirini, nikapigwa kikamilifu.
Jamaa zangu wakajaribu kujisaidia na kuwasihi wapigaji wasinipige, lakini haikusaidia kitu. Nilipigwa nikapigika, nikaiva.
Nilipigwa Sana Hadi nikapoteza fahamu. Nikazinduka baada ya siku tatu nikiwa nimelazwa hospitali ya Amana.
Namshukuru sana mwenyezi Mungu kwa kuninusuru na kifo.
Wito wangu kwa Askari Polisi, mkiwa uswahilini hakikisheni mnaficha utambulisho wenu kwa ajili ya usalama wenu.
Umasahau wanavyowasachi watu wakiwakamata ela zote wanachukuaUmeonja ladha ya vile vipigo mnavyowapa raia shenzi kabisa. Wasimulie askari wenzio ili waache unyama wenu blaaaalifaken
Huu wito uliotoa unathibitisha kuwa una akili fupi sana na unapaswa kupigwa tena.Ulipaswa kutoa wito kwa maaskari wenzako kuwa watende haki kwa watu.
Wewe ulipigwa kwa sababu ninyi Askari polisi hamtendi haki kwa jamii na pia hamfanyi kazi zenu kwa mujibu wa sheria.
View attachment 1969330
Kuna siku humu mchangiaji mmoja aliwahi kusema humu chuki inayopandwa na watawala wetu kwa kuwatumia poilisi itakuja kutugharimu naanza kuyaona haya taratibu. Busara hekima ndio njia maridhawa yakuitunza jamii.
Tupewe teabag [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Chai
Chuki tuSwali,
Unadhani ni kwanini ulifanyiwa hivo?
😳Chuki chuki zilizo pandwa zimezaa visasi kwa wananchi!
Wapendeni polisiHadithi yako inatufundisha Nini sisi raia wa huku bupambwa?
SawaChuki chuki zilizo pandwa zimezaa visasi kwa wananchi!