Jinsi nilivyopata mke, Mwanzo sikumpenda ila sasa nampenda sana

Jinsi nilivyopata mke, Mwanzo sikumpenda ila sasa nampenda sana

Yes bro!! Nimeandika sio kwania ya kupewa sifa kwa kupata mke mwema...

Nimeandika dhumuni kubwa ikiwa kusaidia watu wengine ambao wako kwenye mkwamo kama ulivyosema. Mara nyingi sana watu wanajua nani anafaa kuwa mke mwema ila mara nyingi wenye sifa hizo tunawakataa pengine kwasababu ya elimu, uchumi, family background au mionekano ya nje. Hivi ni vitu ambavyo kwenye ndoa havi saidii, ambao wako kwenye ndoa wananielewa

Kuingia kwenye ndoa na mbwembwe nyingi na kupendana asilimia 100% sio guarantee ya upendo na kudumu kwa ndoa
Kikubwa tu mkuu, asante kwa kutambua sio upendo unafanya ndoa iendelee kuwepo.

Mungu ni mwema atawagusa wanaotafuta, wenzi wao wa maisha.
 
Aisee kumbe Mungu anaweza kukupa mtu ambaye nafsi yako haijamridhia kabisaa? Na akakulazimisha kumpenda kibabe? Huyo Mungu kwakua anauwezo na anatujua zaidi ya tunavyojijua kwanini asitupatie ambaye nafsi zetu zitamridhia?
 
Aisee kumbe Mungu anaweza kukupa mtu ambaye nafsi yako haijamridhia kabisaa? Na akakulazimisha kumpenda kibabe? Huyo Mungu kwakua anauwezo na anatujua zaidi ya tunavyojijua kwanini asitupatie ambaye nafsi zetu zitamridhia?
Kama ukitaka Mungu akupe unachokitaka baadae utajutia kwann alikupa hicho kitu/ huyo mtu. Mungu anakupa unachostahili na kila kitu kipo kwa sababu ukiisha elewa kwann kakileta kwako wala hautasumbuka
 
Hii story ni 'fictional'.

Mungu kuweza kuzungumza nawe kwenye ndoto unahitaji ucha Mungu wa Kinabii ( Sio mwingira type)
Bali kusali na kuomba na kutumaini Muumba ni wajibu, na Yes, utajibiwa maombi ila sio kwa 'manifestation" ya kiasi hiki!
 
Aisee kumbe Mungu anaweza kukupa mtu ambaye nafsi yako haijamridhia kabisaa? Na akakulazimisha kumpenda kibabe? Huyo Mungu kwakua anauwezo na anatujua zaidi ya tunavyojijua kwanini asitupatie ambaye nafsi zetu zitamridhia?
Yesu wakati anakufa msalabani wanafunzi wake walijua tayari kwa upande wao wamefeli. Mwishoni wakati Yesu anafufuka waligundua mtazamo wao ulikua wrong.

Binadamu huwa hatuoni mbali. Yuko anaeona mbali yetu na hata mwisho wetu...

Yule niliempenda mwanzoni alikua na viwango vyake ila hamfikii huyu nilie pewa na Mungu hata nusu... Nilikua wrong sana kwenye chaguo langu
 
Nilikuwa na mchumba wangu ambaye nilimpenda sana. Tulidumu kwenye mahusiano kwa miaka 4. Ujasiri wa kumpenda ulikua mkubwa sababu nilimjua tu baada ya yeye kumaliza kidato cha nne. Mtoto alikua na bikra na jinsi alivyokua mzuri ni kitu ambacho sikutarajia
Ukimtumaini Mungu na kumuomba kwa dhati,hakika hauwezi kukosea katika jambo lolote. Kama binadamu huwa tuna ubishi wetu lakini kama kweli unamwamini Mungu,utasikia sauti yake tu na mwishowe atakupa kilicho sahihi. Hongera sana,Mungu anaishi ndani yako.
 
Amen kubwa,na baraka za Mungu zisiwapungukie.Hongera kwa kutii sauti ya Mungu,naelewa iyo hali ya kusikia sauti ya Mungu,huwa inatupa sitofahamu nyingi na ukikaidi anakujia mpka uelewe.

Natamani Mungu anifunulie ivo wangu maana nliyekuwa nae hamkumpendeza,alinionyesha mara 5 kuwa sio mtu sahihi(AYUBU 33:14-16)na bado nkang'ang'ania,maana hajawahi nikosea,ananiheshimu,ananijali yaani nkaona ni mtu sahihi.Sikuwa na namna zaidi ya kukaa pembeni japo upweke unanitesa kama kijana, bado jamaa anamapenzi na mimi ila nasubiri Mungu atakapopendezwa maana nmechagua Mungu over everything!!Kazi yangu iliyobaki ni kufunga na kuomba Mungu maana anajua naheshimu na nmemsikiliza atanipa tu wakufanana nae.
 
Mkuu asante kwa ushuhuda, maana naamini tunamshinda sheteni kwa shuhuda za maneno yetu.pia naamini kwa ujumbe huu kuna mtu atatoka alipo kwama.

Sifa na utukufu, uweza na nguvu vyote vina yeye alie kupa mke mwema, usiache kutoa sadaka ya shukurani kwa ajili ya mkeo.

Amen
Binafsi amenitia moyo,aya mambo bila kumjua Mungu wataona kama unaongea vitu vya ajabu.
 
Hii story ni 'fictional'.

Mungu kuweza kuzungumza nawe kwenye ndoto unahitaji ucha Mungu wa Kinabii ( Sio mwingira type)
Bali kusali na kuomba na kutumaini Muumba ni wajibu, na Yes, utajibiwa maombi ila sio kwa 'manifestation" ya kiasi hiki!
Inawezekana sana tu,kwa mwanadamu unaona sio rahisi ila kwa Mungu inawezekana.Mungu anafanya vitu kwa watoto wake,Huwezi kumtumikia Mungu afu akakuacha uhaibike.Swala gumu ni kuwa binadamu kusikia sauti ya Mungu na kukubaliana na lile swala.
 
Ni kweli kabisa ndugu. Kumuoa mtu ambae hujamchagua inahitaji uwe na maamuzi magumu sanaml

Nilikuwa na mchumba wangu ambaye nilimpenda sana. Tulidumu kwenye mahusiano kwa miaka 4. Ujasiri wa kumpenda ulikua mkubwa sababu nilimjua tu baada ya yeye kumaliza kidato cha nne. Mtoto alikua na bikra na jinsi alivyokua mzuri ni kitu ambacho sikutarajia

Wakati huo tulikua Arusha, nilihamia Dar katika harakati za kusaka maisha baada ya kumaliza chuo. Tuliishia kuwasiliana tu ila niligundua ni mwanamke mvumilivu sana na mwenye upendo mwingi

Ugumu wa maisha ilinifanya nibadili mtimdo wa maisha. Niliamua kuzikimbia anasa za dunia na kumrudia Mungu. Nilianza kuwa mtu wa sala, kufunga na kuomba kwa bidii sana.

Kwa bidii hiyo Mungu alianza kunifunulia mambo mengi sana ya maisha na maisha yangu kiuchumi,kiroho n.k yalianza kufunguka taratibu. Nilianza kuomba mambo sio yangu hata ya watu wengine nilio wafahamu.

Sikuacha kumwambia Mungu anipe mke mwema pamoja na kwamba nilikua na mchumba wa muda mrefu nilimsihi Mungu mapenzi yake yatimie, si kama nitakavyo mimi ila yeye.

Siku moja niliota ndoto kwamba niko na rafiki yangu na tunaelekea kwa fundi wa suti ya harusi yangu, nilikuta bado fundi hajamaliza kushona na ndio ilikua siku ya harusi, tukaamua kwamba tuwahi kariakoo kutafuta nyingine sababu muda umeisha, wakati tuko njiani kuelekea kariakoo huyo rafiki angu aliniuliza, Bibi harusi ni nani? Na yuko wapi? Nilimjibu mimi mwenyewe simjui ila yuko saloon, twende tukamuome kwanza. Tulienda saloon na tulikuta binti mmoja ambae tulikua tukisali naye tayari amevaa shela na kupambwa vizuri. Nilipo mwona nilijibu, ooh kumbe ni huyu? Basi sawa hamna shida. Ndoto iliishia hapo.

Hii ndoto ilinifedhehesha sana sababu nilijua maana yake na huyu mwanamke nilie muona kwenye ndoto sikua na mazoe nae wala sikumpenda kimapenzi kabisa.

Nilipingana na ndoto hii kwa kuomba ruhusa kazini, nilienda kwa mchumba wangu. Nilienda na kujitambulisha kwa ndugu zake, nilibeba zawadi nyingi sana. Tulikubaliana wiki hiyohiyo nitume washenga kwa miongozo ya mahari na kuanza mchakato wa ndoa haraka iwezekanavyo.

Nilirudi mjini na baada ya siku mbili mchumba alikua hapatikani kwenye simu tena, nilimtafuta ndugu yake lakini majibu yake yalinimaliza. Alisema hapo alipo ana mimba ya mtu mwingine hivyo hatuwezi kuoana na baadae alisema kuna mwanamke amempigia simu akatishia kumuua kama hataachana na mimi. Ninacho jua mm sikua na mahusiano yoyote na mtu yoyote na ndoto ile ilibaki kuwa siri yangu.

Nilienda mkesha wa maombi ya vijana na wakati tunaomba nilisikia sauti kubwa ikisema geuka mtazame mkeo, niligeuka na kumuona yule ambae nilimwona kwenye ndoto. Nilipingana na hili tena na kuuambia moyo wangu HAPANA, hayo pengine yalikua mawenge na uchovu

Baada ya miezi kama miwili nilipigiwa simu na dada mmoja hivi mfanya biashara mkubwa na mcha Mungu Sana, alinambia Mungu amemuonesha maono kwamba kunakitu nilimwomba, akanipa ila sitaki kusikia. Nilimkatalia yule dada. Alinialika nyumbani kwake na nilikuba kumwambia kilichotokea, alisisitiza kwamba nilicho sikia ilikua sauti ya Mungu na hivyo natakiwa kutii.

Wakati huo mchumba wangu wa Arusha alinikataa katakata bila sababu yoyote ya msingi...

Niliamua kumtii Mungu ila kwa kujilazimisha, nilimtafuta binti, na hakusita hata kidogo. Haikuchukua muda tukaanza maandalizi ya ndoa

Mpaka siku ya ndoa nilihisi niko kwenye ndoto, na swali kubwa kwa Mungu lilikua Mungu kwanini unimpe mtu ambaye simpendi? Nitaishi naye vipi? Hisia za mapenzi kama mume na mke hazipo!! Itakuaje? Je, nitampenda lini? Haya maswali yalikua siri ya moyo wangu na Mungu. Nili-fake tabasamu tu lakini moyoni nilijawa na majonzi na maumivu makali.

Nilimuuliza Mungu kwanini hupendi hisia zangu? Na siku ya ndoa niliomba Mungu honeymoon iishe haraka turudi nyumbani.

Siku mpenda mke wangu kabisa, wakati mwingine nilitafuta wine iniondolee mawazo. Niligundua kwamba mke wangu ni mtu wa sala sana, anasali bila kuchoka na kukata tamaa, aligundua kwamba sina hisia kwake lakini hakuacha kuomba.

Kuna mambo alikua akifanya mke wangu yalinivuta sana na kuanza kumtafakari, bidii ya kazi, heshima, mpole, mwaminifu na asiye na makuu. Haya mambo yalinifanya nianze kumpenda mke wangu ghafla. Ghafla nilianza kuona uzuri ambao ulijificha ndani yake ambao kwa jinsi kibinadamu nisingeweza kuuona

Siwezi kuelezea uzuri wake nikamaliza. Leo I feel kama ndio tunachumbiana, kila siku namuona mpya kwangu. Namshukuru Mungu sana kwa kunipa wa kufanana naye.

Mwanzoni sikutambua kusudi la Mungu lilikua nini! Leo nimeona. Mambo mazuri yamefichwa katikati ya changamoto. Mungu akusaidie ujifunze kitu, Amen

Thank you Jesus, thank you LORD!
Mkeo umemkuta bikra pia?
 
Back
Top Bottom