Jinsi nilivyopata mke, Mwanzo sikumpenda ila sasa nampenda sana

Kikubwa tu mkuu, asante kwa kutambua sio upendo unafanya ndoa iendelee kuwepo.

Mungu ni mwema atawagusa wanaotafuta, wenzi wao wa maisha.
 
Aisee kumbe Mungu anaweza kukupa mtu ambaye nafsi yako haijamridhia kabisaa? Na akakulazimisha kumpenda kibabe? Huyo Mungu kwakua anauwezo na anatujua zaidi ya tunavyojijua kwanini asitupatie ambaye nafsi zetu zitamridhia?
 
Kama ukitaka Mungu akupe unachokitaka baadae utajutia kwann alikupa hicho kitu/ huyo mtu. Mungu anakupa unachostahili na kila kitu kipo kwa sababu ukiisha elewa kwann kakileta kwako wala hautasumbuka
 
Hii story ni 'fictional'.

Mungu kuweza kuzungumza nawe kwenye ndoto unahitaji ucha Mungu wa Kinabii ( Sio mwingira type)
Bali kusali na kuomba na kutumaini Muumba ni wajibu, na Yes, utajibiwa maombi ila sio kwa 'manifestation" ya kiasi hiki!
 
Aisee kumbe Mungu anaweza kukupa mtu ambaye nafsi yako haijamridhia kabisaa? Na akakulazimisha kumpenda kibabe? Huyo Mungu kwakua anauwezo na anatujua zaidi ya tunavyojijua kwanini asitupatie ambaye nafsi zetu zitamridhia?
Yesu wakati anakufa msalabani wanafunzi wake walijua tayari kwa upande wao wamefeli. Mwishoni wakati Yesu anafufuka waligundua mtazamo wao ulikua wrong.

Binadamu huwa hatuoni mbali. Yuko anaeona mbali yetu na hata mwisho wetu...

Yule niliempenda mwanzoni alikua na viwango vyake ila hamfikii huyu nilie pewa na Mungu hata nusu... Nilikua wrong sana kwenye chaguo langu
 
Wow hongera Sana mkuu Sifa na utukufu kwa Mungu, Mungu anapenda Sana utii kuliko kitu chochote kile,Ushuhuda wako umenifurahisha Sana Mungu aendelee kuwatunza
Amen. Asante sana
 
Ndoa yenu ina muda gani ?, kama haina muda mrefu basi kuwa mpole maana utarudi mwenyewe kuleta malalamiko alafu wajumbe wakufukulie makaburi ..
 
Ukimtumaini Mungu na kumuomba kwa dhati,hakika hauwezi kukosea katika jambo lolote. Kama binadamu huwa tuna ubishi wetu lakini kama kweli unamwamini Mungu,utasikia sauti yake tu na mwishowe atakupa kilicho sahihi. Hongera sana,Mungu anaishi ndani yako.
 
Amen kubwa,na baraka za Mungu zisiwapungukie.Hongera kwa kutii sauti ya Mungu,naelewa iyo hali ya kusikia sauti ya Mungu,huwa inatupa sitofahamu nyingi na ukikaidi anakujia mpka uelewe.

Natamani Mungu anifunulie ivo wangu maana nliyekuwa nae hamkumpendeza,alinionyesha mara 5 kuwa sio mtu sahihi(AYUBU 33:14-16)na bado nkang'ang'ania,maana hajawahi nikosea,ananiheshimu,ananijali yaani nkaona ni mtu sahihi.Sikuwa na namna zaidi ya kukaa pembeni japo upweke unanitesa kama kijana, bado jamaa anamapenzi na mimi ila nasubiri Mungu atakapopendezwa maana nmechagua Mungu over everything!!Kazi yangu iliyobaki ni kufunga na kuomba Mungu maana anajua naheshimu na nmemsikiliza atanipa tu wakufanana nae.
 
Binafsi amenitia moyo,aya mambo bila kumjua Mungu wataona kama unaongea vitu vya ajabu.
 
Hii story ni 'fictional'.

Mungu kuweza kuzungumza nawe kwenye ndoto unahitaji ucha Mungu wa Kinabii ( Sio mwingira type)
Bali kusali na kuomba na kutumaini Muumba ni wajibu, na Yes, utajibiwa maombi ila sio kwa 'manifestation" ya kiasi hiki!
Inawezekana sana tu,kwa mwanadamu unaona sio rahisi ila kwa Mungu inawezekana.Mungu anafanya vitu kwa watoto wake,Huwezi kumtumikia Mungu afu akakuacha uhaibike.Swala gumu ni kuwa binadamu kusikia sauti ya Mungu na kukubaliana na lile swala.
 
Ni kweli kabisa ndugu. Kumuoa mtu ambae hujamchagua inahitaji uwe na maamuzi magumu sanaml

Mkeo umemkuta bikra pia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…