Hapo hakuna cha utapeli, naona kuna mambo makuu mawili...
1.Tamaa ya utajiri wa haraka
-Kwa mara ya kwanza tu kujihusisha na uwekezaji wa hisa ,ukaamua kununua za Millioni 2,ambazo kwa kipato chako inaonekana hiyo hela ni kubwa.
2.Kukosa elimu
Kwa maelezo yako ,inaonesha wazi haukuwa na elimu ya kutosha na mpaka bado hauna elimu ya kutosha kuhusiana na hisa.
Kilichokuchanganya ni kuskia neno IPO,,,ambapo
- ni kawaida katika IPO bei za hisa kuwa juu....
- Ulinunuaje hisa bila kupata elimu ya Sekta ya Nishati hasa katika makampuni ya utafiti wa mafuta.
- Ulinunuaje bila kufuatilia financial statements za kampuni husika.?
- Kampuni ya utafiti wa mafuta huwa inaingiza hasara always, unapewaje gawio? Hiyo ni dunia nzima.
Ukiona elimu gharama, jaribu ujinga....