Jinsi Nilivyotapeliwa Kijinga Sana, Nimejifunza

Jinsi Nilivyotapeliwa Kijinga Sana, Nimejifunza

Protector

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2019
Posts
422
Reaction score
893
Mida ya saa 5 asubuhi simu yangu inaita, kuangalia ni namba mpya nikapokea. Hallo, upande wa pili ukaitika, naongea na fulani? (akataja jina langu), nikajibu ndiyo.

Unaongea na huduma kwa wateja kutoka Benki tunafanya maboresho kwenye account yako ya benki, hii namba naoma ndiyo imesajiliwa na huduma za benki, nibeep kwa namba nyingine ambayo haijaungwa na benki nikuelekeze cha kufanya. Nikafanya hivyo.

Alipopiga mara ya pili, akaanza kunipa maelekezo nami nikaanza kufata kila anachoniambia bila hiana.
Cha ajabu nikashangaa inaingia meseji "Umefanikiwa kutuma TZS 998800 kwenda namba 07**********". Nilivyoona hiyo meseji nikashtuka moyo ukalia paaaa nikajisemea tayari nimepigwa. Nikakata simu, nikapigwa na bumbuwazi kwanza kwa dakika kadhaa baadae nikapiga namba hiyo ikawa haipatikani.

Ndiyo nikawa nimetapeliwa hivyo. Inauma sana.
 
Back
Top Bottom