Jinsi Nilivyotapeliwa Kijinga Sana, Nimejifunza

Mida ya saa 5 asubuhi simu yangu inaita, kuangalia ni namba mpya nikapokea. Hallo, upande wa pili ukaitika, naongea na fulani? (akataja jina langu), nikajibu ndiyo.
Unaongea na huduma kwa wateja kutoka Benki tunafanya maboresho kwenye account yako ya benki, hii namba naoma ndiyo imesajiliwa na huduma za benki, nibeep kwa namba nyingine ambayo haijaungwa na benki nikuelekeze cha kufanya. Nikafanya hivyo.
Alipopiga mara ya pili, akaanza kunipa maelekezo nami nikaanza kufata kila anachoniambia bila hiana.
Cha ajabu nikashangaa inaingia meseji "Umefanikiwa kutuma TZS 998800 kwenda namba 07**********". Nilivyoona hiyo meseji nikashtuka moyo ukalia paaaa nikajisemea tayari nimepigwa. Nikakata simu, nikapigwa na bumbuwazi kwanza kwa dakika kadhaa baadae nikapiga namba hiyo ikawa haipatikani.
Ndiyo nikawa nimetapeliwa hivyo. Inauma sana.
Pole kuwa makini next time. Mjini mipango. Nishawahi kupigiwa simu na watu wa pembejeo back in 2013. Niliwarecord vyema.

Uzuri niliwashtukia simu ya kwanza tu nikawa nawaenjoy....

Ila Protector imeshindwa kujiprotect😀😀😀
 
Mzee mwanzangu acha tu, tena alivyotaja jina langu ndiyo nikaamini kabisa. Lakini kwa sasa nimejifunza kosa kurudia kosa
 
Mkuu kwa nini huweki hiyo namba ya huyo tapeli? Si tueambiwa simu ambazo hazijahakikiwa zimeshafungiwa? Labda wahusika wanaweza kufanya tracing wakampata
 
Mida ya saa 5 asubuhi simu yangu inaita, kuangalia ni namba mpya nikapokea. Hallo, upande wa pili ukaitika, naongea na fulani? (akataja jina langu), nikajibu ndiyo.
Unaongea na huduma kwa wateja kutoka Benki tunafanya maboresho kwenye account yako ya benki, hii namba naoma ndiyo imesajiliwa na huduma za benki, nibeep kwa namba nyingine ambayo haijaungwa na benki nikuelekeze cha kufanya. Nikafanya hivyo.
Alipopiga mara ya pili, akaanza kunipa maelekezo nami nikaanza kufata kila anachoniambia bila hiana.
Cha ajabu nikashangaa inaingia meseji "Umefanikiwa kutuma TZS 998800 kwenda namba 07**********". Nilivyoona hiyo meseji nikashtuka moyo ukalia paaaa nikajisemea tayari nimepigwa. Nikakata simu, nikapigwa na bumbuwazi kwanza kwa dakika kadhaa baadae nikapiga namba hiyo ikawa haipatikani.
Ndiyo nikawa nimetapeliwa hivyo. Inauma sana.
UJINGA + UTAPELI = UMASKINI hapo hakuna wa kumcheka mwenzie maana hata huyo tapeli atarudi kulekule kwenye umaskini maradufu..
 
Hivi bado mnatapeliwa kijinga hivyo na unaona fahari kuja kutangaza ujinga wako humu jf??
Tambua kitu kimoja elimu haina mwisho kuna mtu hajazaliwa au hana ujuzi wa mambo haya akipitia uzi huu atapata maarifa yatakayomwongezea ufahamu kuhusu inshu za utapeli
 
Kila siku Polisi ,Bank na Makampuni ya simu yanatoa taarifa za UTAPELI lakini watu hawajifunzi.

Taarifa za Kibank au Kisimu zinakuwa updated physically na kama kukutaarifu uende utapigiwa na namba 100 tofauti na hapo ni UTAPELI.
 
Back
Top Bottom