Jinsi Nilivyotapeliwa Kijinga Sana, Nimejifunza

Mida ya saa 5 asubuhi simu yangu inaita, kuangalia ni namba mpya nikapokea. Hallo, upande wa pili ukaitika, naongea na fulani? (akataja jina langu), nikajibu ndiyo.
Unaongea na huduma kwa wateja kutoka Benki tunafanya maboresho kwenye account yako ya benki, hii namba naoma ndiyo imesajiliwa na huduma za benki, nibeep kwa namba nyingine ambayo haijaungwa na benki nikuelekeze cha kufanya. Nikafanya hivyo.
Alipopiga mara ya pili, akaanza kunipa maelekezo nami nikaanza kufata kila anachoniambia bila hiana.
Cha ajabu nikashangaa inaingia meseji "Umefanikiwa kutuma TZS 998800 kwenda namba 07**********". Nilivyoona hiyo meseji nikashtuka moyo ukalia paaaa nikajisemea tayari nimepigwa. Nikakata simu, nikapigwa na bumbuwazi kwanza kwa dakika kadhaa baadae nikapiga namba hiyo ikawa haipatikani.
Ndiyo nikawa nimetapeliwa hivyo. Inauma sana.

Hivi bado mnatapeliwa kijinga hivyo na unaona fahari kuja kutangaza ujinga wako humu jf??
 
Daaah pole sana pesa yenyewe inaanza kama control number, ni makatili sana hao majamaaa
 
Mida ya saa 5 asubuhi simu yangu inaita, kuangalia ni namba mpya nikapokea. Hallo, upande wa pili ukaitika, naongea na fulani? (akataja jina langu), nikajibu ndiyo.
Unaongea na huduma kwa wateja kutoka Benki tunafanya maboresho kwenye account yako ya benki, hii namba naoma ndiyo imesajiliwa na huduma za benki, nibeep kwa namba nyingine ambayo haijaungwa na benki nikuelekeze cha kufanya. Nikafanya hivyo.
Alipopiga mara ya pili, akaanza kunipa maelekezo nami nikaanza kufata kila anachoniambia bila hiana.
Cha ajabu nikashangaa inaingia meseji "Umefanikiwa kutuma TZS 998800 kwenda namba 07**********". Nilivyoona hiyo meseji nikashtuka moyo ukalia paaaa nikajisemea tayari nimepigwa. Nikakata simu, nikapigwa na bumbuwazi kwanza kwa dakika kadhaa baadae nikapiga namba hiyo ikawa haipatikani.
Ndiyo nikawa nimetapeliwa hivyo. Inauma sana.
Watu kama nyie mnatakiwa kupigwa shaba, nchi ina watu wajinga sana wakati huo huo tunasubiria maendeleo. Pathetic
 
Tangu lini watu wa benki wakahitaji password yako tena kwa kupiga simu wewe jamaa umetapeliwa kizembe sana , inaonekana unauzoefu mdogo sana na mambo ya benki anyway ni kheri umejifunza .
Sio kwa ubaya,ila jamaa katapeliwa kizembe sana.
 
MIMI KAMA WIKI MBILI ZILIZOPITA WALINIPIJIA WAKAJIFANYA CUSTOMER CARE NILIWATUKANA SANA..ILA MATUKIO KAMA HAYA NDIO YANAONDOA WATU UJINGA...CUTOMER CARE NI NAMBA MAALUMU KABISA HUWEZI KUONA NAMBA ZA KAWAIDA
 
Kwann usngepga huduma kwa mteja ukazuia muamala au kwenye apps ukafanya reverse mbona mnafanya maisha kua magumu nyie watu
Izo njia zote nilifata mkuu ila nilkuja kugundua kuwa nimekosea muamala baada ya muda kupita hela ikawa imeshatolewa na saiv iyo namba haipatkani tena
 
Back
Top Bottom