Jinsi nilivyougua miaka mingi na kunusurika kifo baada ya kurogewa uchawi wa bundi

Jinsi nilivyougua miaka mingi na kunusurika kifo baada ya kurogewa uchawi wa bundi

Endelea...
Walivyonifikisha Dar shemeji na dada hawakukawia walikaa siku mbili maandalizi yakafanyika nikapelekwa hospital ya binafsi maarufu kama Hindu Mandal ,siku hizi mmezoea kuiita Shree Hindu Mandal hospital maarufu sana kwa kipindi hicho katika jiji la Dar Es Salaam .

Endelea..

Sina kumbukumbu sahihi kwa kipindi hicho maana sasa hivi jiji limejengeka sana nasikia mpaka kuna barabara zinazopisha juu kwa juu,enzi hizo barabara nyingi zilikuwa vumbi hata kariakoo nyumba nyingi zilikuwa za udongo hakukuwa na maghorofa kama kipindi hiki lakini nafikiri hospital hii ilikuwa karibu na mtaa wa India kama unaenda shule ya Zanaki.
 
Endelea...

Shree Hindu Mandal hospitali au tuite tu Hindumandal kama wengine tulivyozoea zamani ilikuwa hospital ya kihindu yenye kila aina ya wataaramu na matibabu yake yalikuwa mazuri wengi waliopeleka wagonjwa wao hospitali hii walijiisi wamepeleka wagonjwa wao sehemu salama sana .

Nilifikishwa hospitalini nikiwa nimebebwa na watu kama wanne asubuhi na mapema mida ya saa 12 ili kuepuka foleni ,baadaye nilipelekwa kwa daktari wa kihindi kwa uchunguzi zaidi.

Dada anaadithia kwamba nililazwa mwezi mzima nikichukuliwa vipimo mbalimbali nakupata matibabu ,lakini hali yangu haikuonyesha kwamba ni mtu ambaye anaweza pona.

Pesa nyingi sana zilimtoka shemeji lakini hakuwa mtu wa kukata tamaa hata pale dada aliposisitiza turudi nyumbani maana hakuna dalili ya kupona shemeji bado hakukubaliana na wazo hilo.

Siku moja wakati shemeji yupo wodini akiniangalia nikiwa kitandani bado katika hali ya koma nisijue nani anayetoka nani anaingia japo macho yana kodoa .Daktari wa kihindi alimuita shemeji na kumuuliza anatokea kijiji gani?shemeji akamjibu natokea Nambalapala- Lindi.

Daktari akamwambia shemeji kwamba mgonjwa wako haonyeshi dalili ya ugonjwa wowote zaidi ya malaria licha ya vipimo vyote tulivyomfanyia ,hivyo nakushauri usiendelee kutumia pesa nyingi kwenye hospital yetu ,unaweza pia ukaenda kuangalia katika upande mwingine au imani zingine iwapo mgonjwa wako atatumia dawa za malaria na kumaliza pasipo kupata nafuu.Ila nasisitiza angalia tiba mbadala huwenda tatizo lipo huko tafuta mganga wa jadi labda inaweza kuleta manufaa kwa mgonjwa wako.

Nilipewa dawa kama sikosei ni sindano za malaria baada ya hapo nilirudishwa nyumbani.

Uzuri mtaani tulikuwa na mama mmoja ambaye ni Daktari wa jeshi la JKT Mgulani alikuwa anaishi karibu na tunapoishi hivyo tukaona hakuna lazima tena kwenda na kurudi hospital kuchoma sindano kila mda wa sindano unapofika .

Maana zamani ulikuwa unaandikiwa sindano labda kutwa mara tatu hvyo hata kama unaishi mbali inabidi ufunge safari hata usiku wa manane ukachome sindano hospitalini kiukweli watu waliteseka sana lakini kipindi hiki huduma za hospitali na zahanati zimekuwa karibu karibu sana.



Itaendelea...
 
Hongera kwa simulizi nzuri mkuu,

Hakikisha hautuachi njiani ghafla[emoji120].
 
Uongo mtupu,kwahiyo wewe unamiaka 60 naa huko Sasa hv??? Maana hii ni story ya mwaka 75 huko 🤣

Babu gani anaandika eti "eti goma likapigwa pale 🤣🤣🤣"
 
Uongo mtupu,kwahiyo wewe unamiaka 60 naa huko Sasa hv??? Maana hii ni story ya mwaka 75 huko [emoji1787]

Babu gani anaandika eti "eti goma likapigwa pale [emoji1787][emoji1787][emoji1787]"
Ujinga mbaya sana

Mbona sijaona cha ajabu. zaidi tu ya mwandishi aandike iwe ndefu kidogo vioamde vifupi fupi vina shusha vibe
 
Uongo mtupu,kwahiyo wewe unamiaka 60 naa huko Sasa hv??? Maana hii ni story ya mwaka 75 huko 🤣

Babu gani anaandika eti "eti goma likapigwa pale 🤣🤣🤣"
Mdio maana watukanaga watu humu mkijua wote mpo sawa humu eti eenh.
Ungenitafuta faragha ningekwambia ID ya mzee wetu Mwinyi ni ipi humu
😂😂😂
 
Yule mwongo pia. Mkuu nenda YouTube tafuta account ya davista mata huto juta
Sasa hivi huyo dada ana miaka kama 75, ina maana ametolewa mwali akiwa na miaka 30 [emoji849]. Kwa kawaida mwali wanatolewa na miaka 13-18

Halafu huu mtindo wa itaendelea mmeutoa wapi? Bongo movie?

Kuna yule jamaa wa "Visa Mikasa vya Kusaka Utajiri", hajaendelea mpaka leo ... Ni Chizi Maarifa sijui
 
Aliyesoma mpaka alipoishia msimuliaji aniambie kama imeisha au itaendelea.
 
Back
Top Bottom