stormryder
JF-Expert Member
- Mar 23, 2013
- 3,776
- 5,786
CDM walikuwa wanapiga campaign humu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ninachokiona hapa kwa mara ya kwanza Magufuli kama Mwenyekiti anabomoa msingi mzuri uliowekwa na wenyeviti waliopita. Same story waliyoitumia CCM kipindi cha kampeni kuelezea mchakato wa upatikanaji wa Lowasa kugombea urais kwa tiketi ya ukawa kuwa haukuzingatia katiba ndio ikasababisha wapiganaji wa ukweli kwenye siasa za upinzani kujiondoa (Slaa na Lipumba) ndivyo itakavyokuwa hatima ya CCM anayojenga Magufuli na wasaidizi wake. Wanapokewa watu toka upinzani ambao hawana utashi wa kweli zaidi ya maslahi ya matumbo yao na kuwaacha wanachama wao wa siku nyingi. Mchakato wa kuteua wagombea haufuati katiba yao ambayo inaeleza wanachama kupiga kura kumpata mgombea.
Cha kujiuliza hawa wapinzani wanaobomoa upinzani, je watakauwa na nafsi ya kuteuliwa tena mwaka 2020 kwenye chaguzi mkuu au watarudishwa kwa wanachama asili matawini wasurubiwe na watu wenye vinyongo? Inshort naona baadhi yao kupotea kwenye ulingo wa siasa mapema mno. Wengi watatumika kama Bazoka/Big G kisha watatupwa.
Sera za upinzani utazisikia wapi wamezuiliwa kufanya mikutano ya hadharaLakini na wapinzani wajiulize kwa sasa wana sera gani za kuvutia masikio ya wananchi?
Zamani walikuja na sera nzuri sana sijui kwa sasa wamekuaje?
Lakini sasa watakaa kimya? Basi sera waziseme kila mbunge katika jimbo lake.Sera za upinzani utazisikia wapi wamezuiliwa kufanya mikutano ya hadhara
Posho nakupa miye, ulinzi miye, usafiri miye, huduma nyingine zote muhimu nakupa miye....leo hii usimame utangaze mpizani kashinda, utakuwa na "akili" kweli wewe.!Kwa hiyo mnataka mtangazwe washindi bila kushinda?
Ujinga wetu ni kuamini kua kuna uchaguzi ulio huru na wa haki 100%Ujinga wetu ni nini?
Kwa kauli hii tu basi hakuna haja ya kufanya uchaguzi tukapoteza helaPosho nakupa miye, ulinzi miye, usafiri miye, huduma nyingine zote muhimu nakupa miye....leo hii usimame utangaze mpizani kashinda, utakuwa na "akili" kweli wewe.!
Hivi kauli kama hiyo inapotolewa na mkuu wa kaya kwa wale wanaosimamia uchaguzi na kutangaza matokeo, bado tunategemea kuna uchaguzi guru tena hapo? Vituko vyote tunavyoona na kuvisikia kwenye hizi chaguzi za marudio bila shaka ni utekelezwaji wa hiyo kauli kuanzia ngazi za chini hadi juu. "NASIKITIKA KUTANGAZA MAUAJI YA DEMOKRASIA YANAYOENDELEA"
Duh.Kwa hiyo mnataka mtangazwe washindi bila kushinda?
Kwani uongo?Watakuambia hiyo ndio gharama ya demokrasia
UkweliKwani uongo?
Hizo Sera wazitolee wapi ilhali wamepigwa marufuku kufanya mikutano?Lakini na wapinzani wajiulize kwa sasa wana sera gani za kuvutia masikio ya wananchi?
Zamani walikuja na sera nzuri sana sijui kwa sasa wamekuaje?
KWANI CCM IMEWAHI KUSHINDA KWENYE UCHAGUZI GANI? HATA 1992 KWENYE KURA YA MAONI WALICHUKUA MAÖNI YA WACHACHE.HIVYO CCM NI DESTURI YETU KUMCHUKUA MWENYE KURA CHACHE NA KUMTANGAZA MSHINDI.Kwa hiyo mnataka mtangazwe washindi bila kushinda?
UKIONA MWALIMU ANAOGOPA KUCHALENJIWA NA WANF WAKE JUA AKILI YAKE INA UPUPU.Kwa mbano uliopo hizo sera za kuvutia masikio ya wananchi utazisikia wapi? Hakuna mikutano ya hadhara, vyombo vya habari vinadhibitiwa, mitandao inatungiwa sheria kali, kubambikiwa kesi kwa viongozi n.k. n.k. Kifupi tumerudi nyuma kwa hiyo maendeleo tutayasikia kwa wengine.