Jinsi picha la kurudia chaguzi Tanzania linavyochezwa

Wengine wanatekwa kisha wanalawitiwa huku wakirekodiwa na kutishwa huwa kama hawahami Chadema picha zao ziwekwa.hewani. Tumeingia katika siasa za kishenzi kabisa kuwahi kutokea duniani.
Jiwe anataka kuombewa jamani
 
Ktk hii "orodha ya wanaojiuzuru bila sababu" sijaona jina la yule bwana wa singida aliyetangaza uamuzi wake huko "mbanta" badala ya "umofia" au ni kwa sababu tu yy alitoka yanga kwenda simba(green/yellow to red/white)

Hapa shida naona ni mtu kutoka simba kwenda yanga but siyo yanga kwenda simba.
 
Yaan hii nchi inakera sana huku tunalia serkal haina hera za kulipa wqlimu, na watumishi mbali mbal ila tunatumia mamilion ya tsh kwa kurudia uchaguz wakat mtu kajiuzuru yy mwenyewe bila sababu ya msingi kazi kutubana sisi wajasiliamar wadogo kukutoza kodi kubwa ili wafidie hilo pengo la hera walizotumia ktk uchaguzi
 
Hatutajua maana halisi ya vyama vingi maana walioshika hatamu Pamoja na mashabiki wao wanaamini wapinzani ni maadui (kumbe upinzani ni ushindani) muhimu kila MTZ wa kawaida apambanie maisha yake na familia yake hayo ya wanasiasa si ya kuendekeza utapata presha bure huku wenzako wakineemeka (Siasa za TZ majitaka)
 
Lakini sasa watakaa kimya? Basi sera waziseme kila mbunge katika jimbo lake.
Huko majimboni wanafundishwa kuongea na mkuuuu maana kama ulifuatilia ziara ya kanda ya ziwa ,wabunge wa upinzani walihojiwa pumba zakuwafitinisha na wananchi ila ccm walifagiliwa for nothing
 
Pesa za kuwapandisha watumishi madaraja anasema hamna ila 1.2 billion za kurudia uchaguzi kila mara iko standby.Najuta sana kuzaliwa Tanzania yenye aina hii ya administration/leadership style.

Yaani akitoa tamko kali mnasema anavunja katiba hafati sheria..akifata sheria na katiba mnasema hatoi tamko wala hakemei.

Suala la mtu kuhama chama na uchaguzi kurudiwa ni haki ya kila mtu kisheria na kikatiba. SASA kwanini mnataka rais avunje katiba kwa kukemea???.
Mkiambiwa mnavuta bangi pale ufipa makaburini mnatukana.
 

Wengi wao watafuata njia aliyopitia Alexandre Hleb aliyekuwa mchezaji mahiri wa Arsenal akajiona yuko top akapush transfer to Barcelona. Alipotea ndami ya miaka 2 tu.
 
Ruzuku kwa chadema inapungua taratibuuuu. Kadri wanavyozidi kupungukiwa na wabunge pia hela zao za Ruzuku kama chama nayo inapungua! Mpaka tunafika 2020 chadema wanaweza wasiwe hata na hela za kuendesha kampeni. Poleni sana ndugu zangu wa chadema. Upigaji wa hela za ruzuku unafika ukingoni! Na mwenyekiti anavyoaandamwa ktk biashara zake basi ni tabu tupuuu. Na juzi nasikia wamemkatia umeme ktk hotel yake kule moshi! Eti alikuwa anatumia umeme wa kujiunganishia aka wizi! Slow death hii.
 
Hata pembe za ndovu zilikutwa kwenye meli ya chairman Mbowr
 
Picha liko hivi.mwaka 2015 ccm walijichanganya wakampata mgombea boys, Kwenye uchaguzi wa 2015 Mgombea wa ccm hakushinda.

Ikabidi NEC na KiTENGO walazimishe kumtangaza mgombea was ccm mshindi.

Kwa upinzani ule waliogopa sana.ikabidi KITENGO wakaahidi kumsaidia Huyo jamaa yao kanyaboya.kwa miaka 5 yakwanza mpaka 2020 ndo wanaogoza nchi, yeye yupo kama boya tu. Mtamlaumu Bure kichaa wa watu matatizo yote in kitengo.

KITENGo wakaapa kwanza kuusambaratisha upinzani,has a Cuf na chadema(ukawa)

mipango mingine in pamoja na kuvuruga uchumi, ili watu wakose ukwasi, kuzuia bunge live, kuua( Ben saa8, mawazo), kuteka(Roma, nondo), kuhonga wapinzani vyeo(kitila, Dr slaa nk...), kununua wapinzani( waitara, kalanga)

kitengo wameamua kliangamiza taifa almradi MTU wao atawale bila changamoto ya upinzani, kwa sababu ya uwezo wake mdogo
 
Lakini na wapinzani wajiulize kwa sasa wana sera gani za kuvutia masikio ya wananchi?
Zamani walikuja na sera nzuri sana sijui kwa sasa wamekuaje?
JF imekuwaje..... Sasa hizo sera utazisikia wapi na hakuna amsha amsha za Mikutano,midahalo kama zamani. Unaposema hawana sera za kuvutia nani amewakaririsha? Ningefurahi angalau kama ungekuwa umesoma ilani ya CHADEMA na pia umesoma walau bajeti kivuli ya mwaka huu ndio uje useme wapinzani hawana sera ila hizi tabia za kusema wapinzani hawana sera ilihali hata katiba ya CHADEMA wala ilani ya uchaguzi ama bajeti mbadala hujawahi soma inashusha hadhi ya JF.
 
1. Kuua upinzani siyo kazi rahisi kama wanavyofikiri. Upinzani hautakaa ufe mpaka dunia ya binadamu ifike mwisho wake. Historia ya dunia ipo wazi kuwa hakuna mawazo ya binadamu au mfumo wa kibinadamu uliodumu bila kuangamizwa na kuibuka mawazo na mifumo mbadala iliyo imara zaidi. Tanzania aliyoiongoza Nyerere ni tofauti sana na anayoitawala Jiwe (Magufuli). Hii inatokana na kuongezeka sana kwa uelewa wa watu kuhusu mifumo mbalimbali inayotumika duniani kuanzia Uchina mpaka Amerika. Ni suala la muda tu, elimu ya kujitambua yaani angalau kidato cha nne itakuwa imewafikia asilimia kubwa ya watanzania. Kadiri watu wengi wetu watakavyokuwa na elimu ya kujitambua, ndivyo itakavyokuwa ngumu kuwatawala kwa njia ya kuwalaghai.

2. Kadri mfumo mmoja utakavyopambana kujilazimisha kuwa wa kudumu, ndivyo maangamizi yake yatakavyoharakishwa. Historia zote tangia zama za kale kabisa mpaka hapa majuzi zinatupa mifano iliyo hai ambayo sihitaji kuielezea hapa. Mfumo unapokaribia mwisho wake, ishara za kuangamizwa kwake ili kupisha mfumo mpya huambatana na nguvu kubwa ya kutaka kuendelea kujiimarisha, na mara anguko (Muhumu ni wenye akili kujipanga na kuwa na watu wenye "vision" baada ya anguko). Kusipokuwa na mfumo mpya ulio imara wa kushikiia usukani baada ya anguko, tutaishia kwenye maafa ya muda mrefu sana kama Kongo, Libya, Somalia na kwingineko. Mataifa yenye utambuzi huu, huweka space ya mawazo na mifumo mbadala ili endapo litatokea anguko taifa lisiingie hasara ya maangamizi au instability ya muda mrefu.

3. Binadamu mara nyingi hutafuta uhuru (freedom). Kadiri dunia inavyosogea mbele, binadamu amekuwa ni kiumbe wa kujitafutia uhuru zaidi na sauti zaidi ya namna bora ya kujitawala wenyewe kwa wenyewe, na mara nyingi upinzani huchipua pale mtawala atakapojaribu kupora madaraka ya watu. Pamoja na kiu kubwa ya watawala kutaka kujitwalia madaraka ya kidikteta dhidi ya watu, upinzani huwa mkuu zaidi pale watu wanapohisi mamlaka yao imepokwa. Historia za mapinduzi sehemu nyingi duniani zimechagizwa zaidi na vita ya mamlaka kati ya watawala na watu.

Kwa kuhitimisha, mtazamo wangu ninaiona CCM imedhoofika kwa kiwango kikubwa sana. CCM imekuwa dhaifu hadi inaona wakombozi wao wanapatikana kwenye vyama vya upinzani. Hata wale makada waliokuwa wamejiimarisha kuanzia ngazi za chini kabisa, kwenda wilaya, wajumbe wa NEC kila wilaya na utitiri wa viongozi wamekosa nguvu ya kusema chochote. Chama wameachiwa vichaa wachache wakishirikiana na Lumumba na ikulu. Chama kinaendeshwa na sauti kutoka huko juu kwa akina polepole na wateuliwa wengine wasiokijua kabisa chama na wasiokuwa na "connection" yoyote huku chini. CCM imekufa, kinachotawala ni serikali na na vyombo vyake. Hapa kinachoonekana ni serikali na taasisi zake zote ikiwemo majeshi, msajili wa vyama, tume ya uchaguzi, serikali kuu yote na kushuka chini mpaka pale mkono wa Rais unapoishia, wote wanafanya kazi za CCM.

Yapo makosa mengi yanafanywa na hii serikali ya awamu ya tano. Makosa haya yanaifanya kazi ya kuujenga upinzani mioyoni mwa watu iwe nyepesi. Mfano rahisi sana unapatikana hapahapa kwetu. Kadiri upinzani ulivyokandamizwa huko Zanzibar, ndivyo wananchi walivyozidi kuuamini. Mpaka walipoamua kuuhujumu kabisa kwa kupora ushindi uliokuwa wa wazi kabisa 2015. Uporaji ule uliweka mazingira ya kuvunjika kwa huu muungano siku za usoni kwa amani au kwa shari. Dalili zake zipo wazi sana hata kwa wale wa CCM nao wameshaanza kujiona kuwa koloni tu na hata maamuzi yao mpaka yapate kibali kutoka dodoma. Makosa yaleyale yanajirudia huku Tanganyika. Ipo siku itathibitika wazi kuwa CCM haina uwezo wa kushinda chaguzi huru. Chaguzi zitakuwa na ni kati ya matakwa ya watu au matakwa ya serikali.
 
Pesa za kuwapandisha watumishi madaraja anasema hamna ila 1.2 billion za kurudia uchaguzi kila mara iko standby.Najuta sana kuzaliwa Tanzania yenye aina hii ya administration/leadership style.
Wangekuwa wanahama CCM na kwenda CHADEMA uchaguzi usingerudiwa?? Alipohama Nyalandu kwenda CHADEMA uchaguzi hakurudiwa???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…