Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Are you clean, huna bifu na hao jamaa, kuna sehemu umeingilia maslahi ya watu, au mmedhurimiana??Kama walikuwa wanashida na gari, they want bother, watatafuta nyingine, kama walikuwa wanakutafuta wewe personally kuwa makini - watakurudia tena....Ongea na huyo mwenzako pia..isije kuwa yeye ndo alikua target....kama kuna issue mmezingua sort it out..
 
Nasikia cape town nafuu sana kwa uhalifu...au Pretoria
 
Wakuu mkipata pesa Tanzania ni salama Kuna matukio madogo madogo
 
Aisee pole sana. SA si salama sana. Jumapili iliyopita nimekutana na mzee mmoja( Baba N) kutoka maeneo ya Kigogo aliniambia kuwa watoto wake wako South na anafurahia sana. Lakini nikiwaza matukio ya huko kwa kweli yataka moyo sana. Maana ni mra nyingi tunapigiwa simu tuchangie pesa ya kusafirisha mwili. Angalia jinsi ya kujilinda.
 
Shukran sana kwa ushauri mkuu. Binafsi sina tatizo na mtu, na mwana anasema yeye hanaga ugomvi na mtu (japo moyo wa mtu msitu)

Nafikiria kuhama mji kwanza nikaanze maisha kwengine kabla hayajanikuta makubwa.
 
Nasikia cape town nafuu sana kwa uhalifu...au Pretoria
Cape pia hakufai, yan baada ya jobeg cape inafuatia kwa uhalifu maana nimeshaishi nikaamua kuondoka mwenyewe.

Pretoria ni pazuri mno na kuna usalama wa kutosha maana ni capital city ya nchi.

Na Pretoria ndio nilipoishi muda mrefu na kukutana na huyo mzazi mwenzangu. Ila niliamua kupahama kwa sababu yake hasa baada ya kuoa mke kutoka nyumbani.

Kuna maeneo mengi tu ambayo mtu unaweza kwenda kujichimbia na kuanza maisha. Ila kama mtu una familia basi inahitaji kujipanga kiasi.
 
Wakuu mkipata pesa Tanzania ni salama Kuna matukio madogo madogo
Yah ni kweli mkuu. Mimi huku sijalowea, huwa nakuja mara kwa mara nyumbani na namshukuru Mungu nimeshajenga vibanda vyangu kwa ajili ya wanangu. Na pia nimewekeza kwenye mambo fulani.

Kinachoniweka huku sasa hivi ni mishe mishe zangu fulani za kimaisha, na elimu bora kwa ajili ya watoto wangu.
 
Rudini bongo
 
Kuna unafuu Kwa wanaoishi Sandton?
 
Asante mkuu. Huku kuna matukio ya kuuwawa kwa kuwindwa na maadui zako, kuuwawa baada ya kuibiwa na kuuwawa kwa wale vijana wanaoleta usela mavi bila kujua kuwa wanaemletea usela mavi amejiandaaje kujibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…