Hapana mkuu, japo niliwahi kuzaa na msauzi, lkn mke wangu ninaeishi nae huku ni mbongo. Ila tayari tumeshazaa nae watoto wawili, mmoja anaingia darasa la tatu mwakani, na mdogo ataingia la kwanza.
Elimu ya hapa inafaida kubwa kwa nchi yoyote ya Afrika. Hivyo naona bora niendelee kupambana ili kuwapatia watoto wangu elimu bora kwa maisha yao ya baadae.
Pia huyo mtoto niliezaa na mzawa kwa sasa yupo kwenye mikono yangu namsomesha na ashafika la 5. Huyu pamoja na kwamba simtegemei sana kama nitaweza kurudi nae nyumban pale itapobidi kurudi, lkn naona ni damu yangu, siwezi kuacha kumpa haki yake ya msingi kwa ajili ya maisha yake ya baadae hata ntakapokuwa sipo hapa.
Sababu yeye hakupenda au kupanga kujileta mwenyewe dunia, bali ni starehe za sisi wawili (mimi na mama yake) ndio zilizosababisha ujio wake. Hivyo ni lazima nimpambanie kwa ajili ya dreams zake.
Nikiona presha inazidi nitahamia mji mungine, maana nchi hii ni kubwa na kila mji au kila sehemu kuna fursa zake.