Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Mambele ni wapi mkuu? Kama ni "ng'ambo" utakuwa umekosea kwa sababu kila siku kuna nyuzi za watu wengi wanaotamani kwenda huko na kuna za wanaokiri kuwa hawajawahi kwenda na hawana mpango huo maishani mwao. Si rahisi kwa kila mwana JF kuwa "mambele"
Au sio
Pumba tupu
 
Nina kisa changu pia ila sitapenda kukiunganisha hapa lakini kitakuwa na title kama Yako ila pole na hongera kwa kuwaza haraka kujibanza kwa polisi SA ni hatari sana
Asante mkuu, hakika dunia ina mengi, ila kama hayajakukuta kamwe hauwezi kuelewa.

Pole kwa yaliokukuta japo bado haujayaweka wazi hapa.
 
Asante kwa kunisaidia mkuu. Watu wengi wanafikiri kwamba mtu ambae tayari ushapambana kujipanga unaweza kutoka tu sehemu hivi hivi kuja kuanza moja nyumbani.

Ni afadhali wengine wameshauri nihame mji, wazo ambalo hata mimi mwenyewe nilikuwa nalo.
 
Kwanza napenda kutumia nafasi huu kushukuru kwa niaba yangu na ya wenzangu kuhusu madhila yanayotukuta hapa.

Pili tukiachana na zile fujo zao dhidi ya wageni, mauaji ya hapa huwa hayachagui utaifa wa mtu. Yanaweza kutokea kwa mtu yeyote, kibaya uwe umeotewa tu na majambazi, au mmegombana na mtu na akachukua uamuzi wa kukuuwa ghafla, au watu fulan wapewe deal la kukutafuta ili wakumalize (hili tumeona mpaka wasanii wao wenyewe wanauwawa)

Kuhusu rangi nyingine mfano wazungu ni vigumu sana wao kuuwawa kwa sababu wengi wao wanatembea na silaha za kujilinda, lkn pia hawana ushirikiano sana na watu weusi hivyo inakuwa ngumu mtu kuwaingia kichwa kichwa cause hawezi kujua yeye au mwenzake wa pemben amebeba nini ndani ya gari au suruali yake.
 
Pale nyumbani Tanzania Kuna amani na upendo mwingi sanaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…