Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Jinsi polisi walivyonusuru maisha yangu last night

Pambaneni, nimeishi USA na ningeweza baki, ila upweke ulinirudisha, usa palikuwa salama sana kwangu
Ushasema USA. Kule ni mbali ndio maana wengi hatufikirii kwenda kuishi kule.
Hapa Kaburu ni karibu mno na nyumban, na kila mara nikitaka kuja bongo kufanya mambo yangu, naruka mara 1 baada ya wiki 1 au 2 narudia Kaburu kuendelea na maisha.
 
Hiyo nchi kifo nje nje , airport ya dar es salaam kila ndege ya mizigo inapofika lazima uwe na jeneza , mtu amefariki huko
Ni hatari sana mkuu. Ila ndo hivyo mwanaume unapofanikiwa kuwa na jangwa sehemu la kukupatia riziki ya kula na kujiendeleza kidogo, basi haina budi kuipigania sehemu hiyo kwa jasho na damu.

Siku nikitulia nitaleta uzi mwingine ambao pia nilinusurika kuuwawa nikiwa katika mikono ya wauaji wangu, lkn Mungu hakuwapa kibali cha kuniuwa hivyo kujikuta wameshindwa kufikia malengo Yao hao wauaji.
 
Mkuu Mr dundumizi,
Hauna labda mabifu na watu au labda kuna mtu wako wa karibu anKuzunguka?

Ujahisi hivyo?
Nina beef na mzazi mwenzangu ambae ni mzawa, ila sidhani kama yeye anaweza kuandaa mchezo wa aina hii.
Nimeshatoa taarifa kwenye vyombo husika mkuu, so bado tunafuatilia kwa karibu hili tukio la jana ili kuelewa chanzo na sababu zake.
 
Ninaposema mzawa namaanisha ni raia wa hapa hapa.

Tuna beef nae kubwa sana kiasi cha kuiweka ndoa yangu matatani.

Lkn yeye anaishi Pretoria na mimi kwa sasa naishi Johannesburg.
Daaah mkuu pole sana.

Lolote linawezekana huenda akawa anachora ramani yeye, au kama ulivyosema ni wizi tu wa magari au kuna rafiki anaona umemzidi maendeleo yote yanawezekana.

Unaweza hata kuhama sehemu uliyopo current ukamove sehemu nyingine ukajaribu kubadili hata mawasiliano.
Na kuendelea kufanya upelelezi

Pole sana mkuu.
 
Kuna mtu yoyote unamuhisi? Au ushawahi kugombana na mtu huko?
Nina ugomvi mkubwa na mzazi mwenzangu ambae ni mzawa, Ila sifikirii kama yeye anaweza kuandaa mpango huo.

Washkaji wengine ni ile kupishana kauli tu kwa hapa na pale lkn sina uhakika ni nani anaeweza kuandaa mpango huo.

Mungu ni mwema na wa kumshukuru daima.
Daaah mkuu pole sana.

Lolote linawezekana huenda akawa anachora ramani yeye, au kama ulivyosema ni wizi tu wa magari au kuna rafiki anaona umemzidi maendeleo yote yanawezekana.

Unaweza hata kuhama sehemu uliyopo current ukamove sehemu nyingine ukajaribu kubadili hata mawasiliano.
Na kuendelea kufanya upelelezi

Pole sana mkuu.
Hili wazo lako ni zuri sana, maana hata mimi na washkaji wengine including ndugu zangu tulikuwa tunawaza hivi hivi.

Wanasema kunguru muoga hukimbiza bawa lake. Hivyo utanilazima nihame mji huu kabla hayajanikuta ya kunikuta.

Shukran sana mkuu ushauri wako nimeupitisha kwa 100%
 
Hongera kwa kutambua hatari...

Next time jitahidi kuchukua aina yoyote ya ushahidi pia gari yako iwekee Dashboard camera.. na rear camera. Pia weka tinted kali.

Nyumba yako iwekee security nzuri bila kusahau camera.. sometimes unapata ushahidi kwa kufatilia footages za miezi kadhaa nyuma na kumjua/kuwabaini watu wabaya.

Pia ukiwa na mishe zako usiwe mtu wa kutumia njia moja. Yaan njia hiyo hiyo utakayotoka nayo ndio urudi nayo..

Jitahidi uwe mtu wa kubadiri njia mara kwa mara yaan UNPREDICTABLE
 
Back
Top Bottom