Jinsi Project ya Mbingu mpya na Nchi mpya itakavyotengenezwa na itakavyofanikiwa

Umeongea kinadharia sana

Umeongea ni kama vile una hadithia movie, yaani kama umeahaona sasa unatuambia ilivyokuwa ili hali ni mambo yanayotarajiwa kuwepo

Hayo ni mawazo yako huenda ikawa hivyo au ikawa tofauti kabisa na unavyosema

Kuishi sayari ni moja ya ndoto kubwa ya Elon Musk kama anavyosema yeye mwenyewe lakini itachukua muda mrefu mno. Tena muda mrefu zaidi kama matajiri wenzake hawatoungana nae kukamilisha hilo lengo

Project ya kuprint chakula ipo na tangu ianze kufanyiwa kazi miaka mingi sana nyuma wamefanikiwa kuprint sahani moja tu na ni Burger

Na hawaprint kama unavyoona una print karatasi na hawatumii mashine za 3D kiongozi hapo uliongea chai

Wanatumia mchanganyiko maalumu wa kemikali wanazozijua wao, procedure tofauti na unavyo print kama ulivyoongea kwa lugha rahisi

MARS HAIWEZI KUWA MBINGU MPYA KWASABABU

1. kwenye dini zote inaaminika mbinguni kutakuwa na mito ya maziwa na asali. Kama tu maji kupatikana ni ishu sembuse wataweza kutengeneza flow ya maziwa iwe kama mto? Kama wataweza itawachukua miaka mingi sana zaidi ya unavyofikiria.
 
nimemaanisha ulivyosema wanaproject za kupandikiza cell kwenye miili ya watu ili wawe immortal..
Kaongea chai huyo

Mwili mzima wa binadamu umeundwa na seli. Kila kitu unachojua wewe kiumeundwa na seli

Damu, ubongo, mifupa, nyama, nywele. Kila kitu kimeundwa na seli ndo maana cell is the central part of a living thing

Sasa unaposema mtu anapandikizwa cell, anapandikizwaje? Ikiwa mwili umeundwa na cell? Ingekuwa hivyo hata wale wanaoongezewa damu wangekuwa wanaishi watu wawili kwenye mwili mmoja.

Mtu anaumwa figo, anatolewa figo yake iliyoharibika inachukuliwa figo ya mtu mwengine anawekewa. Lakini hatuoni watu wawili wakiishi kwenye mwili mmoja eti kisa figo ya huyu (ambayo figo pia imeundwa na cell) kapandikizwa mwengine

Specific cell kwa pamoja zinaunda tissue, specific tissues kwa pamoja zinaunda an organ, different organs zinaunda system, different systems ndo zinaunda organism ambae ni ndo aidha binadamu au kiumbe hai

Mfano wa cell ni bone cell, stem cell, blood cells, musle cells nk

Mfano wa tissues ni epithelial tissue, muscle tissue, nervous tissue, na connective tissue

Mfano wa organs ni moyo, figo, mapafu, nk

Mfano system (mfumo) ni mfumo wa upumuaji, mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, nervous system, endocrine system

Alafu organism ndo binadamu sasa

HUU MTIRIRIKO UPO HIVYO HATA KWA VIUMBE WENGINE
 
mkuu umemwaga madini ya kutosha, shukran..
 
Waganga waseme neno basi"Yesu" ni nan mbona wanamuogopa sana wenda kuna siri nyingine hatujua
 
Huu uzi ni wa kijinga tu. Hii ni kufuru kwa Mungu
 
Laiti mngejua maana ya mbingu mpya na nchi mpya.

Acha mengine tubakie nayo mioyoni maana hamna imani ya kutosha hata mkiambiwa maana yake hamtasadiki.
 
Inawezekana maana harakati za kina Elon ni busy sana
 
Punguzeni kula makande
 
sasa hii stori ina akili kubwa ipi mkuu? Yani kusimulia vitu ulivyosikia nayo ni akili kubwa? Hizi fiction tu, maisha Mars hayawezekaniki.
Kwann? Mbona watu wanakaa hewani uko pasipo na oxygen miezi na miezi? Na curiosity ipo kule inapiga picha ina maana kunafikika.
 
Huu uzi ni wa kijinga tu. Hii ni kufuru kwa Mungu
Hallelujah mwerevu karibu katika thread ya wajinga uungane nasi
Mbingu ileeeeeee
Mwaka 2500 watakua mbingu ya mars wakila biryani lililopikwa Kwa umeme uliozalishwa na Nuclear power!

Enjoy!
😁😁😁
 
[emoji28] hako kaujanja ka kutishia watu kifo mnakapenda. Kwa taarifa yako kitu chochote ambacho mtu anakawambia utaona baada ya kufa ni uongo mtupu
Kwanini? Kwani wewe ulishakufa ukaufahamu ukweli? Yoyote anayeongelea maisha baada ya kifo ni imani tu. Hakuna ushahidi. Including you.
 
Kwann? Mbona watu wanakaa hewani uko pasipo na oxygen miezi na miezi? Na curiosity ipo kule inapiga picha ina maana kunafikika.
acha kuwajibu mapimbi Hao akili zao ni visoda Wewe muulize watu waliwezaje kujenga international space station na wanafanya kazi Huko kitu ambacho Babu Yao kinjeketile ngwale hajawahi hata kukifikiria na ukirudi ukamwambie atakuona wazimu watu wataishije nje ya Dunia Huko sehemu ambayo ukikaa unaizoom Dunia Kwa mbali?
Watu Wana macho lakini hawaoni Wana akili ila hazichaji Wala hawaangalii vitu for future wakila makande na kunywa gongo wanaona maisha ndio haya haya!
Afrika bwana Raha sanaaaa!
😁😁😁😁
 
Kama sio kizazi hiki basi kizazi kijacho ila usihitimishe kuwa haiwezekani. Mwanzoni hata sayari hazikujulikana sasa hivi zinafikika.
 
Kutokujua yanayoendelea mkuu.. hapa watu hawajui kuwa sasa hivi kuna binadamu wanajaribu kupasua mwamba mkubwa huko anga za mbali kama majaribio ikitokea kuna mwamba ukaielekea dunia basi yasitokee yaliyowahi kutokea. HAWAJUI YAFANYIKAYO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…